JIHAZARI NA WIZI WA KUPITIA SIMU BANKING

Mtu alinipigia simu akaniambia alikuwa akifanya usajili mtandaoni na kwa makosa aliweka namba yangu kimakosa kwa ile website aliyokua akijisajili, anadai kwamba namba yangu ni sawa na namba yake na kwamba zimetofautiana kidogo tu hivyo anaomba password iliyoingia kwenye simu yangu ambayo mimi kwa kweli niliona imeingia ktk msg na ilikua ni 6310.

Alikuwa anaomba kwangu nimpe password iliyotumwa kwenye simu yangu ili apate kumaliza usajili wake. Nilimwambia anipigie simu na namba anayodai ilikuwa inafanana na yangu ili nipate kuthibitisha madai yake, aliniambia hakuwa na pesa katika line hiyo.

Nilipitia mtandaoni ili zaidi janja yake, na nikagundua kwamba alikuwa akijaribu kubadilisha neno la siri ktk sim banking yangu ili aniibie pesa. Nilivyofungua email yangu ya yahoo nikaona msg ikionyesha kuwa mimi nataka nibadili password yangu nikagundua ni udanganyifu, huyu ni hacker wa akaunti na pia 419er. Ikawa sikumpa tena ile password iliyoingia  kwenye simu yangu, ambayo angeweza kuitumia ili kubadilisha upya akaunti yangu ya benki ya simbanking / ya programu ya simu.

Tafadhali hebu tuwe makini na tuchukue tahadhari. Wadanganyifu wanagundua njia mpya kila siku.

Hii ni njia mpya ya kuwadanganya watu ...

Shiriki ili kusaidia wengine.


_ * Ninajali ............ pls tahadhari * _nimetuma kama nilivyopokea.


* PLS SHARE MAELEZO haya NA MENGINE.

⬆Nimeituma hii msg baada ya kuiona ina umuhimu mkubwa sana, ili kuepusha watu wasiibiwe.

Comments

Use [video]youtube-video-link[/video] to insert video in comment
Use [img]image-link[/img] to insert image in comment