GIRLS AND BOYS SIKIENI HII | BongoLife

$hide=mobile

GIRLS AND BOYS SIKIENI HII

Fikiria umeanza kuwasiliana na mwanaume/mwanamke kwenye mitandao.
Mara ya kwanza ukahisi ni kawaida na hakuna cha zaidi.
Ni rafiki tu.
Mkaanza kuwasiliana usiku na mchana.
Akakufanya utabasamu, akakuleta karibu zaidi.
Akakupa nafasi kubwa katika maisha yake.
Kampani ikazidi, mkawasiliana zaidi.
Siku zikakatika, mkazidi kuwasiliana, akataka kukutana nawe uso kwa uso kwa mara ya kwanza.
Hatimaye mkakutana, mkakumbatiana, mkaenda sehemu mbalimbali, mkawa marafiki wa karibu.
Ukajisikia huru, ukamwambia Mungu kwamba huyu ndiye niliyekuwa nikimtaka.
Halafu usiku mmoja akakwambia “Unajua kwamba nakupenda, si ndiyo?”
Ukashtuka.
Ukajifanya hukumsikia.
Ukamuona akianza kuwa na huzuni.
Halafu na wewe ukamwambia unampenda.
Mkaendelea kukutana zaidi na zaidi.
Mkapiga sana selfie, mkaenda kwenye bembea, mkanunuliana sana koni na zawadi huku mkienda kutazama muvi pamoja.
Mwisho akakwambia uwe mpenzi wake.
UKAMKUBALIA.
Miezi ikakatika, mapenzi yakanoga, kila mmoja akajaribu kumuonyeshea mwenzake kwamba alimpenda mwenzake zaidi ya mwenzake.
Vikwazo vikaja, mkashikana na kuvishinda.
Popote pale mlipokoseana, mkasameheana.
Baada ya hapo, hisia za kimapenzi zikaanza kutoweka.
Majaribu yakaja.
Ukajikuta ukiwa katika mikono ya mtu mwingine.
Hakutaka kukuacha japokuwa alijua kinachoendelea.
Ila kwa sababu hisia juu yake zilipotea, ukamsukumia mbali.
Alichokuwa akikihitaji ni kukupa penzi alilokuwa nalo kwako.
Akakulilia.
Akakufuata sana.
Lakini ikaonekana una furaha mno na mwingine.
Ukapiga naye picha, ukaziweka mitandaoni.
Akaziona.
Akaumia.
Akalia usiku kucha.
Machozi yakawa sehemu ya maisha yake.
Akaona bora akuache japokuwa hakutaka iwe hivyo.
Akaanza kujiweka mbali nawe.
Baadaye akaanza kukufuata tena.
Ukachanganyikiwa.
Ila ukampuuza.
Ukajifanya upo bize na mtu mwingine.
Hakukata tamaa ila mwili wake ukachoka kukufuata.
Akakuacha.
Ukawa na furaha na mtu mwingine.
Ukweli ni kwamba aliumia.
Ila USIKU mmoja.
Ukagundua kwamba umemkumbuka.
Ukakumbuka jinsi mlivyokuwa.
Ukatamani kumpigia simu.
Kumtumia meseji.
Ukaogopa kwa kujua aliondoka.
Hukujua kama angeweza kuwa peke yake kipindi chote tangu umuache.
Unatamani ufanye jambo fulani.
Ila ukaogopa.
Unampenda, si ndiyo?
Ukajidanganya hujali, ila ukweli ni kwamba unajali.
Hisia zikawa kumbukumbu
Siku zikazidi kwenda mbele, bado ukakumbuka mlivyokuwa kipindi cha nyuma.
Mipango yote mliyopanga.
Ila kwa sasa...hakuna tena hilo.
Mipango imekwenda...hata yeye amekwenda.
Ukabaki ukilia, ukahuzunika usiku na mchana.
Haukula, haukulala, furaha ikapotea kwa sababu yake.
Ulichobaki nacho ni kumbukumbu juu yake.
USIRUDIE MAKUSA.
Kumbuka majaribu yapo kwa ajili yetu kutujaribu.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : GIRLS AND BOYS SIKIENI HII
GIRLS AND BOYS SIKIENI HII
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/girls-and-boys-sikieni-hii.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/girls-and-boys-sikieni-hii.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy