FANYA HAYA KWA MUME WAKO.

1. Muite kwa jina lake la utani.

2. Muache atumie mamlaka yake kama
kichwa cha nyumba.

3. Usimcheke akiwa ameumizwa na
jambo fulani.

4. Kaa kimya pale anapokuwa na hasira.
Unaweza ukaenda kumuomba msamaha
na kumueleza kwanini ulimkosea pale
hasira zinapokua zimemuisha.

5. Kuwa na haraka ya kuomba msamaha
pale unapokosea, sisitiza juu ya msamaha na mbusu pale
anapokusamehe.

6. Ongelea mazuri yake na yeye kabla
ndugu, jamaa na marafiki hawajafanya
hivyo.

7. Waheshimu wazazi wake.

8. Msisitize kuhusu kwenda kuwasalimia
wazazi wake na kuwapelekea chochote.
Na afanye hvyo na kwa wazazi wako pia.

9. Msuprise kwa chakula akipendacho,
hasa kipindi kile anapokuwa na msongo
wa mawazo. Na kamwe usimcheleweshee chakula chake.

10. Usiruhusu dada wa kazi amhudumie
chakula mume wako ukiwa nyumbani.

11. Mkaribishe kwa kumkumbatia
anapotoka kwenye mihangaiko yake.
Msaidie mizigo aliyokuja nayo au hata begi.

12. Tabasamu pale unapomtizama, vaa
vizuri na jipendezeshe kwa ajili ya mumeo.

13. Mpigie simu na umwambie kwamba
unampenda na umemkumbuka

14. Muamshe asubuhi na umpe romance
kiasi kwamba ifike hatua ya kuhitaji, mpe
na hata jishughulisha na wanawake
wengine siku hiyo.

15. Kamwe usithubutu kutamka kuwa
hakuridhishi na tendo la ndoa. Tafuta njia muafaka ya kufikisha ujumbe wako.

16. Mwambie ni kiasi gani una bahati
kuwa nae kama mume wako.

17. Mkumbatie tu bila sababu yoyote ile.

18. Mshukuru Allah kwa kukupa ubavu wako na usingizi/kitulizo chako
 katika maisha yako.

19. Kumbuka kumuombea na kumkabidhi
mikononi mwa Allah.

20. Tengenezeni utaratibu wa familia
nzima kumshukuru Allah kwa pamoja.

Mungu abariki ndoa yako.

 Mlio single Mkapate wapenzi wenye mapenzi ya
kweli leo na daima.
Na wasio serious na mahusiano
wanaokupotezea muda wako wajikatae
kwako mapema ili wasikuzibie nafasi.

Comments

Use [video]youtube-video-link[/video] to insert video in comment
Use [img]image-link[/img] to insert image in comment