DHANA YA NDOA NA MAISHA YA MAFANIKIO | BongoLife

$hide=mobile

DHANA YA NDOA NA MAISHA YA MAFANIKIO

*Mr HUNDRED INSPIRATION 🇹🇿*

    *"MBIU YA USHINDI 🎷* "

 *{ WINNING IS SIMPLY A MINDSET}* 

 *_📚Somo LA Weekend Hii📚_* 

SOMO 📚 ; *" DHANA YA NDOA NA MAISHA YA MAFANIKIO - Sehem ya Pili"*

 *MALENGO BAADA YA KUJIFUNZA SOMO HILI*

👉🏿 Kujua Mke/Mme Aliye Umbwa Kwa Ajili Yako {Mwenza Wako Halali}.

👉🏿 Kujua Uhusiano Uliopo Kati Ya Ndoa Na Mafanikio Ya Mtu.

*SOMO LILILO PITA.*

     Week Iliyopita Tulijifunza Sehem Ya Kwanza Ya Somo Letu Hili.Ambapo Tulijifunza Maswali Ya Msingi Ya Mtu Kuji Uliza Kabla Haja Amua Kuingia Kwenye Ndoa Ambayo Ni Nikwanini Unaitaji Kuoa/Kuolewa Pili Ainagani Ya Mwanamke/Mwanaume Unamuitaji Na Kwa Nini Huyo Si Mwingine,Tatu Lini Unaitaji Kuoa Na Kwa Nini Mda Huo Na Si mwingine,Pia kweli Tano Kuhusu Ndoa Ambazo Wengi Hawazijui,Pia Tuka Jifunza Sababu Za Kwanini Watu Huoa Ambazo Ni Zaupotevuni Si Sababu Sahihi Kwa Wao Kuoa/Kuolewa.Na Kubwa Tulijifunza Makosa Makubwa Ma 4 Wanayo Fanya Watu Wakati Wa Kuchagua Mwenza Wa Maisha Yao.Kosa La Kwanza Hukubali Kuchagukiwa Mke/Mme,Kosa La Pili Huyumbishwa Na Maumbile,Rangi Na Pesa,Kosa La 3 Huoa/Kuolewa Kabla Ya Ndoa,Kosa La 4 Hukubali Kudanganyika Wakati wa Uchumba Wao.

*SASA ENDELEA.* 

     Moja Kati Ya Swali Kubwa Ambalo Pengine Utakuwa Umewahi Jiuliza Kwenye Maisha Yako Ni *"Nitajuaje Mme/Mke Aliye Umbwa Kwa Ajili Yangu?"*.Katika Somo La Week Hii Nina Imani Pasi Na Shaka Utaenda Kupata Jawabu La Swali Hili.Kama Nilivo Eleza Katika Somo Lililo Pita Kwamba Usipo Jua Namna Ya Kumpata Mwenza Sahihi Basi Fahama Fika Utaoa/Kuolewa Na Mme Wa Mtu Na Swala La Amani Na Furaha Kwako Utasikia kwa Wenzio.

 _*VIASHIRIA VYA KUJUA MKE/MME ULIYEUMBIWA*_

 *1. Kunakuwa Na Sababu Ya Msingi Ya Kukutanishwa Nae Kwenye Maisha Yako.*

     Nikisema Hivi Namaanisha Mkeo/Mmeo Hutakutana Nae Bahati Mbaya,NO Bali Kuna Kuwa Na Kiunganishi Chenye Mashiko. *_Mfano_* Unasafiri Kutoka Mbeya Kuja Dar Ukawa Umekaa Siti Moja Na Mtu Ambaye Kwa BAHATI Mbaya Ni Mgonjwa Sana Na Hakusafiri Na Mtu Sasa Kwa Sababu We Ndo Ukonae Karibu Unajikuta Unavaa Wajibu Wa Ndgu Na Kumpeleka Hospital Na Unajikuta Unalala Ili Umwangalie Kwa Sababu Hana Ndgu Mwengine Ww Unayafanya Haya Kwa Ubinadam Tu Baada Ya Yote Una Ondoka Zako Bila Kutarajia Kulipwa Na Baadae Unakuja Kukutana Nae Bila Kutarajia.Watu Wengi Huja Kujikuta Walisaidia Waume/ Wake Zao Kwa Njia Kama Hizi.

Mfano Mwengine - Mpo Kanisani Mchungaji Ana Tangaza Kuna Mtoto Kaokotwa Tunaomba Mtu Yoyote Ajitolee Kumlea Huyu Mtoto Kama Mwanae Siku Zote.Unajikuta Unajaa Huruma Una Nyanyuka Baada Ya Wewe Kunyanyuka Mchungaji Ana Sema Ataye Saidiana Kuleana Na Huyu Kaka Wewe Kama Binti Una Inuka.Ninapo Sema Sababu Ya Msingi Ya Kukutanishwa Ndo Kama Hivi.Hivo Mna Jikuta Kwa Sababu Ya Kulea Mnakuwa Karibu Na Kuzoeana Na Hatimaye Mna Endana Na Kuoana.

Mfano Wa 3 wa Sababu Ya Msingi Ya Kukutanishwa Na Mwenza Wa Kweli.Wewe Ni Kijana Unaye Penda Sana Kushiriki Mashindano Ya Kisayansi Na Katika Shindano La Wana Sayansi Nchini Kwako Mka Jikuta Wawili tu Ndo Mme Shinda na Kupata Bahati Ya Ww Na Mwenzio Kupata Nafasi Ya Kwenda Kusoma Miaka 5 Denmark Chuo Kimoja.Huko Kutokana Na Kutoka Nchi Moja,Kupenda Kitu Kimoja,Kuishi Karibu Uhusiano Una Imarika Na Hatimaye Mnaingia Kwenye Mahusiano na Baadae Ndoa.Hizi Ndo Sababu Zenye Mashiko.Sio Umepanda Daladala Umemwona Mdada Mrembo Unamwomba Namba Mnakuwa Wapenzi Na Mna Oana Ndoa Hizi Huvunjika Mapema Sana.

 *2. Yeye Atakupenda Vile Ulivo.*

     Ndgu Yangu Ikiwa Ume Oa/Olewa Na Mtu Ambaye Kila Baada Ya Mda Flani Anataja Kasolo Yako Huenda Ukawa Ume Oa/Olewa Na Mme Wa Mtu.Mwenza Halali Atakupenda Vile Ulivo Na Atajivunia Kuwa Na Ww Siku Zote Licha Ya Kwamba Anajua Unamadhaifu Eiza Ya Viungo Au Tabia.Kama Ameumbwa Kwa Ajili Yako Basi Aliumbwa Kustaimili Madhaifu Uliyo Nayo.Hivo Kama Leo Una Kilema Au Udhaifu Wa Tabia Flani Kuwa Na Amani Hivo Havita Zuia Kupata Mwenza Mzuri wa Maisha Yako.Siku Moja Nilikuwa ITV kwenye Mada Iliyo Husu Waremavu Ambapo Ali Alikwa Rais Wa Walemavu Nchini Na Ali Ongozana Na Mkewe.Nili Shangaa Kuona Mke wa Yule Rais Akijiona Fahari Sana Kuwa Na Mme wake Licha Ya Mumewe Kuwa Kipofu Yangu Utotoni Na Yule Mwanamke Alikuwa Mzuri Tu Bila Kasoro.Nilipata Funzo Hapa.

   Na Labla Nikwambie Tu Mpendwa,Hakuna Mke/Mme Utaye Mpata Asiye Na Kasoro/Mapungufu,Ikiwa Utampata Mwenye Elim Atakuwa Bize Sana Na Kazi Kuliko Kuwa na Ww,Na Ukimpata Mwenye Pesa ni Dhaili Atakuwa Na Dharau Hasa Kama Hamkuchuma Nae,Ukimpata Handsome/Beautiful Basi Atakuwa Anang'ang'aniwa Na Wengi Kutokana Na Mvuto wake Hivo Kwako Itakuwa Stress Na Mwisho Ukimpata Mwenye Upendo Wa Dhati Basi Utakuta Hana Maisha Mazur.Hivo Basi Ukiwa Ume Mpenda Mtu Na Anamapungufu Flani Usisite Kuoa/Kuolewa Nae Maana Kupitia Upendo Utamtengeneza Vile Utakavo Ikiwemo Kutafuta Pesa Na Kumbadili Tabia Mbaya Alizonazo.

*3. YEYE NI WEWE*

       Hiki Ni Kiashiria Kikubwa Sana Cha Kujua Mme/Mke wako Halali.Ukiona Uko Na Mwenza Ambaye Mna Tofauti Ngingi Basi Jua Ume Oa/Olewa Na Mme Wa Mwenzio.Kama Ni Mwenza Halali Wako Basi Vitu Vingi Sana Mtafanana.Mfano Ni Rahisi Sana Kufanana Vipaji {Kumbuka Nilisema Mke/Mme Huletwa Kwa Kusudi Linalo Fanana}.Mfano Mzuri Ni Anko Zumo Na Mkewe Wote Ni Waigizaji Wachekeshaji.Mfano Mwengine Ndgu Nelson Mandela Na Wini Mandela Wote Walikuwa Wanaharakati Wakubwa Wa Afrika.

     Pia Ninapo Sema Yeye Ni wewe Nina Maana Mna Endana Sana Kuanzia Vitu Mnavyo Penda (Chakula),Hobbies, Pia Tabia,Kubwa Zaidi Hata Malengo Yenu Duniani Yanakuwa Hayana Tofauti.Kama Maandiko Matakatifu Yasemavyo Mwanamke Katoka Kwenye Ubavu wa Mwanaume Yaani Ni Mwili Mmoja Basi Akiumizwa Mkeo/Mmeo Kiwango Kile Kile Cha Maumivu Apatacho Mwenza Wako Ndicho Utacho Pata Na Ww Na Hii Ndo Tafsiri Ya Yeye Ni Wewe.Nimekuwa Nikiona Wanaume Waki wakataza Wake Zao Kufanya Mambo Flani Hatakama Ni Ya kujenga Hii Hutokana Na Wanaume Wao Hawafanyi Hiko Kitu Ila Ukifanya Kitu Ambacho Mumeo Anafanya/Anapenda Hawezi Kukukataza Badala Yake Atakupa Sana Sapoti Tafsiri Yake Ni Nini *Ni Ngumu Sana Kwa Mwanamke Kutimiza Ndoto Alizo Nazo Ikiwa Aliolewa Na Mme Wa Mtu Kwa Sababu Ndoto Zao Zita Kinzana.* *_Olewa Na Mumeo Achana Na Mme Wa Mtu_*.

 *4. Aina Ya Hadithi Anazo Kuletea Mkiwa Pamoja.*

     Ikiwa Uko Na Mwenza Yeye Mda Wote Anawaza Kukwambia Mambo Ya Kufanya Mapenzi Tu Huna Mtu Hapo.Mme/Mke Aliye Umbwa Kwa Ajili Yako Mda Wowote Atao Kuwa Na Wewe Kiwango Kikubwa Cha Stori Zake Kwako Zitakuwa Zinagusa Maisha Yenu Kwenye Ndoa.Kama Na Wewe Ni Miongoni Mwa Wale Wenye Mpenzi Ambaye Hajawahi Kuku Uliza Maswala Ya Watoto Wenu Mkizaa,Au Haulizi Mara Kwa Mara Maswala Ya Harusi Yenu Ndgu Hapo Unapoteza Mda.Mme/Mke Halali Kwako Hata Kabla Ya Kuingia Kwenye Ndoa Mkiwa Kwenye Uhusiano wa Mapenzi Atakuuliza Sana Kuhusu Harusi,Watoto Na Hata Eneo La Kuishi Baada Ya Ndoa.Maswali Kama Haya *KATU KATU* Mtu Aliye Kutamani Kukuchezea,Hawezi Kukuuliza Kwa Sababu Yeye Ana Malengo Ya Mda Mfupi Kwako.

   Pia Ikiwa Una Mpenzi Ambaye Mda Mwingi Anawaza Ngono Tuu Hapo Huna Mme Au Anawaza Umpe Pesa Huyo Sio Mke.Mmeo Halali Kwanza Hatakuwa Na Haraka Na Wewe Ya Kufanya Mapenzi Kwa Sababu Anajua Wewe Upo Tu Hapa Ndo Tunapata Msemo Usemao *"Kuku wangu Manati Ya Nini"* Ikiwa Kuku Wako Huta Mvutia Manati Uta Msubiri Aingie Bandani".Ndivyo Kwenye Ndoa Ilivo.Pia Mmeo Halali Atakuonea Huruma Kufanya Mapenzi Hasa Kabla Ya Ndoa Maana Anajua Fika Ni Hatari Kwa Afya Yako,Mme Halisi Kwa Ajili Yako Atakuwa Ana Huruma Sana kwako.Pia Ukiona Uko Na Mpenzi Ambaye Anaomba Omba Hela Huyo Sio Mkeo Halali,Sisemi Dada Zangu Msiombe Pesa Kwa Wapenzi Wenu Lahasha Ila Mna Omba Kwa Ajili Ya Nini Hapa Ndo Penye Tatizo,Usiwe Unaomba Pesa Ili Ubadili Wigi Au Uongeze Nguo Sina Tatizo Kwa Wale Dada Zangu Wanao Omba Pesa Kuongeza Mtaji Au Anaumwa Anaomba Pesa Ya Dawa { Uwena Sababu Ya Msingi Na Yalazima Kuomba Pesa}.Kitendo Cha Ww Kuomba Pesa Kama Ume Olewa Ni Kumlazimisha Mwanaume Aanze Kuumia Mpaka Aanze Kufikiria Malipo Ambapo Utaitajika Umpe Penzi { Wanawake Wengi Hujiuza Bila Wao Kujua}.

    Mme/Mke Aliye Umbwa Kwa Ajili Yako Mkiwa Pamoja Ataitaji Zaidi Kujua Undani Wako,Wa Familia Na Hata Ukoo.Wakati Mwengine Atakuuliza Hata Maswali Ambayo Ww Utayaona Kama Hayana Maana Mfano Maswali Kuhusu Ulivo Kuwa Mtoto,Maswali Kuhusu Ndugu Zako Kama Majina Ya Babu zako Na Wanapo Ishi Majina Ya Shangazi zako Hii Utokana Na Ukweli Kwamba Kuwajua Ndugu Zako Ni Kujijua Yeye Maana Mke Na Mme Ni Mwili Mmoja Haina Hii Ya Maswali Kwa Aliye Kutamani Kwa Kufanya Mapenzi Tu Hawezi Kuuliza.Pia Maswali Kama Unataka Tuwe Na Watoto Wangapi Na Tuwape Majina Gani?,Una Tamani Harusi Yetu Ifungiwe Wapi?,Na Kubwa Zaidi Utaona Anapenda Sana Kukaa Na Mama Yako,Shangazi Zako Na Hupenda Kuwazungumzia Hawa Kwako.Ukiona Mwanamke/Mwanaume Wa Namna Hii Basi Andaa Pete Ya Pingu za Maisha.

 *5.Lini Mme Kutana - Time Factor.*

    kipindi Gani Umekutana Na Mwenza Wako Ni Kigezo Tosha Cha Wewe Kujua Huyo Ni Mwenza Wa Kweli Au Laah.Ikiwa Ume Mpata Mwenza Mkiwa Sekondari Kutokana Na Mda Kuwa Sio Sahihi Basi Anaweza Akawa Sio Mwenza Sahihi Na Hapa Tunapata Msemo Unao Sema *"Maamuzi Sahihi Kwa Wakati Usio Sahihi Yanakuwa Sio Sahihi"*.Swali Lako Kwangu Laweza Kuwa Ntajuaje Mda Sahihi wa Kuoa/Kuolewa Umefika.Mda Sahihi Wa Wewe Kuingia Kwenye Ndoa Ni Ule Mda Ambapo Wewe Ume Jitosheleza.Nikisema Ume Jitosheleza Nina Maana Kwa Msichana Maumbile Yako Yawe Tayali Kupokea Hata Mtoto, Kwa Mwanaume Unapo Owa Jiulize Je kwa Mda Huo Uki Ingia Kwenye Ndoa Ndoa Haitayumba Kwa Namna Yoyote Ile?.Je Ume Komaa Kiakiri Pia Uchumi Wako Una Uwezo Wa Kutunza Familia Au Unataka Uwe Omba Omba.

   Muda Sahihi Wa Wewe Kuoa Si Kumaliza Masomo na Kupata Kazi Yenye Mshahara Mzuri Kama Wengi Wanavo Amini Kwamba Ndo Mda Ume Fika.Nakukumbusha Tena Mda Sahihi Wa Wewe Kupata Mke/Mme Ni Pale Utapo Gundua Kusudi La wewe Kuwepo Duniani Maana Dhana Ya Mke/Mme Ni Usaidizi Hivo Huwezi Leta Msaidizi Ikiwa Hujui Anakuja Kukusaidia Kazi Gani {Rejea Somo Langu La Namna Ya Kugundua Kusudi La Kuja Duniani}.Wakati Unaingia Kwenye Ndoa Uwe Vyema Ki Akiri,Kiroho,Kimwili Na Kiuchumi Ili Kusudi Usije Kimbia Familia Kwa Kuona Ndoa Mzigo.

 *6. HUWA RAHISI KUUTEKA MOYO WAKE.*

      Nikwambie Tu Mke/Mme Aliye Umbwa Kwa Ajili Yako Katu Hawezi Kukusumbua Mda Mrefu Wakati Wa Kumtongoza Mambo Huwa Kitonga Sanaa Na Hii Utokana Na Ukweli Kuwa Kulikuwa Na Sababu Ya Msingi Ya Wewe Kukutana Nae {Rejea Hoja Yetu Ya Kwanza Hapo Juu Ili Uelewe Vzr Hili}. Huwa Ninacheka Sana Unakuta Mtu Mpaka Anaenda Kwa Mganga 😂😂😂 Ili Apendwe,Mpendwa Una Nunua Maumivu Kwa Mganga,Au Unakuta Mtu Anakataliwa Mpaka Ana Jinyonga 😂😂😂 Sinaga Utaratubu Wa Kucheka Kwenye Masomo Yangu Ila Hawa watu Wanayumba Sana Au Unakuta Mtu Ana Tumia Pesa Nyingi Sana Kumwaminisha Mwenza Wake Na Mwisho Wasiku Ha Aminiki Tu,Nikwambie Tu Mke/Mmeo Hata Kupenda Kwa Sababu Ya Unacho Mfanyia Bali Hatakuwa Na Sababu Ya Kukupenda Kwa Sababu Wewe Ndo Umeumbwa Kwa Ajili Yake Atajikutaga Tu,Unajua Unapo Umpenda Mtu Kwa Sababu Endapo Sababu Hiyo Ikiondoka Basi Huta Mpenda,Hivo Mpende Mtu Bila Sababu.

   Na Katu Usimkubalie Mtu Kuwa Mapenzi Wako Eti Kwa Sababu Tu Kakusumbua Sana Au Una Mwonea Huruma Atajinyonga Itakula Kwako Mpendwa.Ukiona Una Tumia Nguvu Nyingi Kuuteka Moto Wa Mtu Flani Basi Huenda Una Lazimisha Kuoa/Kuolewa Na Mme Wa Mtu Kuwa Makini sana.Siamini Sana Mwenza Aliye Umbwa Kwa Ajili Yako Utateseka Sana Kumpata Siamini Katika Hili Na Kama Ikiwa Hivi Basi Huwa Nadra Sana Kutokea.Na Wakati Mwengine Mnajikuta Mme Ingia Kwenye Mapenzi Bila Hata Kusema Neno "Nakupenda Naomba Uwe Mapenzi Wangu" Badala Ya Maneno Matendo Ndo Huongea.

*UHUSIANO KATI YA NDOA NA MAFANIKIO YA MTU.*

     Ipo Siri Kubwa Sana Katika Ndoa,Wengi Hudharau Ndoa Kwa Sababu Hawajui Ina Uhusiano Wa Moja Kwa Moja Na Mafanikio Yao.Ukweli Ni kwamba Uwepo Wa Mme Au Mke Ni Kwa Ajili Ya Usaidizi Si Tu Kufanya Mapenzi Na Kuzaa Watoto Hizi Ni Kazi Za Ziada.Hivo Kiwango Cha Mafanikio Yako Kita Tegemeana Sana Na Chaguo La Maisha Yako Ulilo Lipata.Na Nikwambie Tu Ni Mwenza Wako Halali Tu Ndo Ataye Elewa Malengo Yako,Kuolewa Na Mwenza Wa Mwenzio Kutamfanya Kukupinga Maana Atakuwa Haelewi Na Hapendezwi.Ndoto za Wanawake Wengi Zimekufa Baada Ya Kuolewa Na Wanaume Ambao Hawakupangiwa.

     Iko Hivi Ikiwa Mke Anapenda Sana Kuwa Karibu Na Watoto yatima Hata Mume wake Atakuwa Mwenye Roho Ya Namna Hiyo Mwisho Wa Siku Watu Kama Hawa Huanzisha Kituo Cha Malezi Kwa Yatima Lakini Ukiwa Na Mme Ambaye Anaona Kusaidia Yatima Kama Mzigo Ndoto Yako Itayeyuka Mara Moja.Katu Huwezi Fanikiwa Kwenywe Ndoto Zako Ikiwa Mda Wote Una Stress Kutokana Na Mke/Mme wako.Maana Wapo Watu Ambao Baada Tu Yakuoa Walipoteza Furaha Na Wanashindwa Kutoka Katika Kifungo Hiko Maana Ndoa Ni Kifungo.Ukiwa Utaoa/Kuolewa Na Mme Halali Basi Utapata Faraja,Ushauri Na Hata Fedha Katika Kile Unacho Fanya Kwa Sababu Mwenza Wako Nae Anakipenda.Wapo Watu Baada Tu Yakuingia Kwenye Ndoa Maisha Yao Yamebadirika Kuanzia Uchumi Mpaka Wengine Kiroho Na Kuishi Maisha Ya Furaha.Watu Wengi Huzaa Watoto Ambao Sio Wao Kwa Sababu Ya Kuolewa/Kuoa Na Mwenza Wa Mtu Mwishoe Watoto Huwa Wasumbufu Wasio Tii Na Hapa Ndo Unakuta Baba Anakuwa Hapendi Watoto Aliye Wazaa Mwenyewe Mwishoe Watoto Wanapoteza Mwelekeo Wa Maisha Kwa Sababu Ya Kukosa Malezi Ya Wazazi Halali.Kuwa Makini!!.

 _*MWISHO NA KWA UMUHIM.*_ 

    Wakati Mwengine Mungu Huweka Mafanikio Ya Mtu Kwa Mme/Mke Wako Ili Idhiirishe Umuhim Wa Ndoa.

 _Kabla Sija Maliza Nikukumbushe Mambo Haya Kwa Mara Nyingine._ 

👉🏿 Faham Fika Hakuna Siri Ya Kuwa Na Amani Na Upendo Kwenye Ndoa Na Familia Yako Nje Na Kuoa/Olewa Na Mme Wako Uliye Pangiwa Na Mungu.

👉🏿 Kabla Hujaoa/Kuolewa Julize Maswali Yafwatayo Je Niwakati Sahihi Wa Mimi Kuingia Ndoani?,Je Sababu Yangu Ni Sahihi Ya Mimi Kuoa/Kuolewa,Je Mwenza Huyu Atanifaa Kweli Mm,Wazazi Na Ndugu Zangu,.Je Mwenza Huyu Hata Nikiondoka Duniani Anauwezo Wa Kutunza Familia?,Na Kigezo Ulicho Kitumia Kumchagua Mwenza Wako Kina Maana Kwenye Ndoto Zako na Mwisho Jiulize _*Je Mwenza Huyu Ni Rafiki Kwa Kusudi Langu Hapa Duniani?*_.

👉🏿 Ikiwa Shinikizo La Ww Kuoa Limetoka Nje { Maumbile,Pesa,Magari Rangi} Usioe Ila Ikiwa Shinikizo Limetoka Ndani Yaani Moyoni Basi Oa/Olewa.

👉🏿 Ndoa Ni Ya Watu Wa 2 Katu Usilazimishwe Wala Kusikiliza Watu Wanampenda Nani Ndo Wewe Uoe/Uolewe Nae Usije Oa Mke wa Mwenzio.Mke/Mme Wako Atakuja Wakati Sahihi Na Unao Faa Hata chelewa Wala Kuwahi Daima Kuwa Mpole Maana Huta Mleta Wewe Bali Atakuja Mwenyewe Na Katu Usitafute Mke/Mme Utakosea!!.

 *WEEK IJAYO*

        Week Ijayo Tuta Jifunza Namna Ya Kuwekeza Katika Wazo Ulilo Nalo Mpaka Lizae Mafanikio.Kumbuka Maendeleo Yoyote Inayo Yaona Duniani Hutokana Na Wazo Ambapo Huwekezwa Na Kuzaa Matunda.Changamoto Kubwa Huja Pale Unapo Kuwa Na Mawazo Mengi Na Hujui Ni Wazo Lipi Litafaa Kwa Wakati Huo Ili Uwekeze Kwalo Lilete Faida.Nazungumzia Wazo Kwa Ujumla Liwe Na Kisiasa,Biashara Au Kiteknolojia.Kubwa Tuta jifunza Namna Ya Kuunda Wazo,Then Namna Ya Kuwekeza Katika Hilo Wazo Sambamba Na Namna Ya Kuambukiza Watu Waelewe Wazo Lako Ili Wakupe Ushirikiano Na Msaada.Nikwambie Tu Kati Ya Mawazo Mengi Uliyonayo Kichwani Litalo Kutoa Kwenye Maisha Ni Moja Tu,Je Unajua Namna Ya Kutambua Wazo Hilo Kati Ya Hayo Mengi Uliyonayo?.Tukutane Weekend Ijayo.Kama Utaitaji Ushauri Zaidi Kuhusu Uchumba/Ndoa Nitafute.

🖋_*Waweza Nitafuta Tujifunze Kwa Pamoja Au Kwa Lolote Bila Ghalama Yoyote Kwa Mawasiliano Yangu Na Kama Ulikosa Sehem Zilizo Pita Za Mafunzo Uta Patiwa*_

   ðŸ–‹ *"KUMBUKA Masomo Haya Yana Kujia Kila Week End J'pili"!!."* 
        *"SAMBAZA KWA WATU WENGI NDGU JAMAA NA MARAFIKI KWA UPENDO NAO WAJIFUNZE NAWE UTA BARIKIWA.AMENI!!."* 
 *Aluta Continue !!* 
 *Mawasiliano* 
 +255 744126640
 +255 658503737
Email - mrhundredinspiration@gmail.com
 *FROM* 
          *Mr HUNDRED*
      *{UDSM STUDENT}* 
    *"BECOMING A LEGEND"*

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : DHANA YA NDOA NA MAISHA YA MAFANIKIO
DHANA YA NDOA NA MAISHA YA MAFANIKIO
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/06/dhana-ya-ndoa-na-maisha-ya-mafanikio.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/06/dhana-ya-ndoa-na-maisha-ya-mafanikio.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy