KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI) SEHEMU YA 05 | BongoLife

$hide=mobile

KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI) SEHEMU YA 05

KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI)

SEHEMU YA TANO

STORY NA Mbogo Edgar.

ILIPOISHIA SEHEMU YA NNE, “braza kama nina kufananisha hivi?” aliongea yule tingo akimtazama kwaumakini Lukas, “ujanifananisha ndugu yangu nimimi” alisema Lukas, akiamini kuwa walejamaa akiwaeleza ukweli ita kuwa salama yake, sasa walishanza kimtelemko cha mto wa luhuhila kuelekea chandaluha, “mh! Devi, unajuwa huyu jamaa ndio yule jambazi anae tafutwa” alisema yule Tingo kwa kuhamaki, ENDELEA ..........
“ata mimi nimemwona, lakini ..... wacha tumsaidie tu!” alisema yule dereva, akionyesha wasi wasi, “sikilizeni ndugu zangu, mimi siyo jambazi, ila polisi wanataka kunipa kesi..” alisema Lukas kwa sauti tulivu sana, lakini yule Tingo akamkatisha kwa kupaza sauti, “wana kupa kesi kivipi?, hacha uongo bwana, nyie ndio wauwaji wakubwa” Lukas akaona huyu jamaa amechachamaa, akamtazama dereva ambae nae alikuwa ana mtazama, “sikiliza ndugu yangu mimi siyo jambazi, ila nime shuhudia polisi wenyewe wakiwauwa wenzao, na kuiba pale hifadhi...” hapo wote wawili wakacheka kwanguvu, “unaona Devi, huyu mjinga kweli, yani anaona uongo huo ndio utaeleweka” alisema kwa zarau Tingo, ambae alimtazama dereva wake, na kumshauri jambo, “Devi huu ni msala bola tumshushe hapo juu, maana tukikatwa na polisi tutaonekana na sisi ni majambazi” alisema Tingo, lakini dereva akaonekana kuwa na utu kidogo, “pale ni porini, wacha tukamshushie karibu na mshangano” alishauri suka, akimaanisha wakamshushe kwenye kijiji kinachofwata, lakini Tingo akukubari, “bwana heee! huyu jambazi, ataogopaje msitu” alisema yule tingo wakati huo walikuwa wana pandisha taratibu mlima wa chandaluha, wakati huo huo likawapita gari la polisi, lililo beba askari kama sita nyuma yake, huku mmoja wa saba pamoja na dereva wakiwa mbele, mapigo ya moyo ya kijana huyu yaka lipuka, kwa mstuko wa uoga, “ok! jamani, mimi nashukia hapo juu, ila mkibahatika kusikia mwisho wa hili, mtajuwa nilikuwa naongea nini, pia nawaomba mkihojiwa na polisi, msiwaambie kama nime waambia kuwa wao ndio walio fanya tukio la NMC” alisema Lukas, akionekana kubadiri mawazo yake, lakini yule Tingo alionekana kuto kukubaliana na maneno ya Lukas, “bwanae sema tusi waambie kama tume kushusha hapa, ila usitudanyaje chochote, tena wale polisi watakuwa wanakufwata wewe” alisema tingo alie onekana kuchukia sana majambazi kama huyu bwana Lukas, pasipo kujuwa kuwa amzaniae ndie, kumbe siye,
Nikweli baada ya kumaliza kilima dereva akasimamisha gari pembeni ya barabara, na bwana Lukas aka shuka, mala moja na kutokomea polini, akijuwa kuwa lazima wale polisi watarudii baada ya kumkosa kwenye dala dala, na alihofia kuwa wataelezwa kuwa, alionekana akipanda kwenye lile Nissan diesel, hivyo lazima wata rudi mala moja kulisimamisha gari hili, na wakimkosa lazima yule Tingo ata sema walipo mshusha, hivyo alizama porini, na kusogea mbali kidogo, sehemu ambayo aliamini kuwa ata wakianza kumfwatilia lazima ataweza kuwakimbia, lakini alichagua sehemu ambayo ilimwezesha kutazama barabarani, maana kwambali aliliona gari la polisi lile lile, likirudi kwa speed kali.
 “unajuwa Devi awa watu sio wa kuwazowea kabisa, unge shangaa ana tuteka njiani” alisema Tingo huku safari inaendelea, ni baada ya kumshusha Lukas, “ange tutekaje wakati akuwa na silaha yoyote, alijibu yule suka, huku akiendesha gari taratibu kabisa, “haa bwana ee, mimi nawachukia tu majambazi, ata kama akuwa na bunduki” alijibu tingo kwa chuki ya wazi kabisa, “lakini kama unge msikiliza vizuri yule jamaa inawezekana akawa anaongea ukweli” alisema Devi, na kupigwa vikali na tingo wake, “mnafiki yule mshenzi, afadhari polisi haooo! wana kuja, simamisha gari tuwaambie tulipo mwacha yule mshenzi, wanaweza kutupatia fedha” alisema Tingo, huku wote wawili wakilitazama gari la polisi lililokuwa lina kuja kwa speed,  “mi sisimami naona moyo wangu unasita” alisema Devi, akionyesha kweli alimaanisha alichosema, lakini aikuwa hivyo ilimlzimu kusimama, maana polisi awa wali mwashia taa, kama ishara ya kusimama, huku wakilijaza gari kati kati ya barabara, na kuiziba ubande mmoja, Devi akaliweka gari pembeni ya barabara, “vipi, wame juwa kama tulimbeba au?” alIuliza Devi kwa sauti iliyojaa mashaka, “yani mimi siwafichi nawaeleza mpaka tulipo mshushia” alisema yule tingo kwa shahuku, huku wakimtazama polisi mmoja alie kuwa amekaa seat ya mbele ya gari hilo la polisi, akishuka na kuwafwata, kwenye gari lao, sambamba na polisi wengine watatu, toka nyuma ya gari, 
“wote shukeni chini, hasibaki ata mtu mmoja” alisema sajent Idd kibabu, kwa sauti kavu ya kipolisi, huku ameikunja sura yake ikionyesha hapakuwa na utani wala ubembelezana, ni baada tu ya kuliifikia gari lao, tena bila ata salamu, bwana Devi na Tingo wake, wakiwa wamejaa wasi wasi wasi, wakafungua Milango ya lile gari, vichwa vyao vikiwa na wasi wasi na maswali mengi, “kwani sisi ndio waharifu?” alijiuliza Tingo, lakini kabla awaja shuka waka stuka wakidakwa juu juu na polisi, kisha kuvutiwa chini, kama wahalifu, “fanyeni haraka, mnatuchelewesha nyie wajinga”, huku tingo akifikia kwa kuanguka chini, “piga magoti haraka” alisema mmoja wa askari wale, huku sajent Kibabu akitazama kwenye gari, nikama alitarajia kumwona Lukas akishuka, “mwenzenu yupo wapi nyie wapumbavu?” aliuliza sajaent Idd Kibabu, hapo kauri zika gongana, maana wote wawili, yani Devi na Tingo wake waliongea kwa moja, wakati devi anasema tupo sisi wawilitu”, hukuTingo alisema, “tume mshusha hapo nyuma” wakati huo polisi mmoja akapanda kwenye lile gari, na kutazama kama kuna alie bakia, mle ndani ya gari, “kweli hakuna mtu afande” alisema yule polisi alie ingia ndani ya gari, hapo Sajenti akaamlisha kuwa lile gari lisachiwe lote mpaka kwenye body, yani nyuma sehemu ya kubebea mizigo, huku akiamlisha askari wengine wakimbilie kule walikosema wamemshusha Lukas, lakini licha ya kuvuruga vichaka vyote na kujaribu kutafuta nyayo, awakuona mtu, wala dalili ya mtu yoyote, wakati huo Devi na tingo wake, bado walikuwa wame pigishwa magoti, huku polisi mmoja akiwa amesimama karibu yao na bunduki yake mkononi,
Baada ya kuangaika kwa dakika kadhaa, mala akarudi Sajenti akiongozana na bahadhi ya askari walioenda kumsaka Lukas, “nyie lazima mnajuwa kila kitu kinacho muhusu huyu jambazi” alisema Kibabu kwa sauti kavu ya kuogofya, huku akiiwa kazia macho wakina Devid, “afande ni kweli tulimpa lift yule jambazi, ila mwanzo hatukumjua kama ni jambazi” alisema Devid, kwa sauti ya kushawishi kuwa awakuwa njia moja na jambazi Lukas, “kwanini mlimshusha, au mliamua kumsaidia ili atukwepe, baada yakuona tumewapita?” aliuliza Idd kibabu, kwasauti ile ile kavu, akionyesha kuwa hakuwa anatania, hapo Tingo aka kurupusha mdomo wake na kuanza kuongea, “hapana hatukumshusha kwa aajili awakimbie, ila tuliogopa kumpa lift, maana alianza kuongea uongo, eti anasema kuwa yeye ajafanya ujambazi, anaushahidi wa video kwamba ni polisi wenye ndio mlio fanya uajambazi” hapo sasa, sajent Kibabu akaonekana kustushwa na kauri ya Tingo,
Pia kauli hiyo ya tingo ilimstua kila mmoja, mahali pale, siyo polisi peke yao, ata Devi nae alistuka sana, kwa ulopokaji wa mwenzie, hapo devi akainua usowake nakumtazama yule polisi kiongozi, yani sajent Kibabu, akamwona akiwa amewakodolea macho, kama vile, anatafakari jambo flani, alifanya vile kwa sekunde kadhaa, kisha akageuka na kuwatazama wenzake, “mmoja awatazame awa, wengine ni fwateni” alisema sajent babu huku anaanza kutembea, kuelekea kwenye gari lao, akifwatiwa na askari watano, huku mmoja akiwa amesimama karibu ya hawa vijana wawili, ambao walikuwa ndio kwanza wanaanza safari yao, akiwaonyeshea bunduki yake sub machine gun, “kwanini uwezi kutuliza mdomo wako, hizo nyingine siri za kwao wenyewe” alilahumu Devi, kwa sauti ya kunong’ona, akiwa ame sogeza mdomo kwake karibu na sikio la Tingo wake, wakiwa wamepiga magoti karibu karibu, “bola hivi bwana, kwani yule ni ndugu yetu” alisema tingo, pasipo kuelewa Devi alikuwa anamaanisha nini, “subiri uone faida ya ulopokaji wako” alisema devi ambae alihisi vibaya, juu ya kile kikao cha sajenti Idd, na askari wake, 
nikweli japo Devi akusikia kilicho jadiliwa na polisi wale waliosogea pembeni kidogo, lakini ukweli ni kwamba, polisi wale walikuwa wana jadiliana kuhusu usalama wa siri yao, maana ata awaha vijana wawili tayari walisha juwa kuwa nipolisi ndio waliofanya tukio la NMC, lakini mwisho wa mjadala ni kwamba, polisi awa waliokosa uaminifu kwa serkali wanayo itumikia, waliamua kuwa vijana hawa wawili, wauwawe, kwa usalama wa siri yao. ******
 Mida hii Kanal Kisona alikuwa ndani ya ofisi ya mkuu wa upelelezi mkoa, akiongea na mkuu wakitengo hicho, bwana Manase Kingarame, akiwa na hoja mbili, ni baada ya kuriport kwa brigedia Fransis Haule, ambae alimtuma aende kuongea na uongozi wa polisi mkoa, asa kitengo hiki cha upelelezi, kama ifwatavyo, kwanza ni kitendo cha kuiendesha opareshen kwenye eneo la jeshi bila taarifa yoyote, ambapo bwana Kingarame akajibu kuwa, ilikuwa ni dharula, na walipanga kutoa taarifa baadae, “lakini uoni kuwa nikitendo cha hatari sana, kufanya tukio kama hilo kwenye eneo lajeshi, pasipo kuujulisha uongozi wa jeshi?” aliuliza bwana Kisona, baada ya kuona majibu ya bwana Kingalame ni mepesi sana, “unazani kwa umakini mlio nao, nmaweza kuwashambulia polisi mchana kama kama huu, eti mmeshindwa kuwatambua?” aliuliza Kamanda Kingarame, kwa sauti flani ambayo Kisona alitaafsiri kuwa ni kejeri, “unazani kila anae vaa gwanda la polisi au jeshi, anafanya kazi ya serikali?” kauli hiyo ilimstua kidogo bwana Kingarame, ambae alitazama kushoto na kulia, ungezani kuwa alikuwa akitazama kama kuna mtu mwingine mle ofisini, alie sikia lile swali, “kwahiyo unamaanisha nini kijana?” aliuliza Kingarame, kwa hasira, na pasipo kumwachia Joseph, nafasi ya kujibu, Kingarame akaongeza, “umamaanisha kuwa tunafanya kazi kinume na sheria?” aliuliza Kingarame, kwa sauti iliyoonyesha hasira iliyo changanyika na wasi wasi, kwambali, “sija sema hivyo labda wewe useme” aliongea Kisona kwa namna flani ya utani wakuchukiza, kwa ASP Kingarame, “kijana unajuwa usijifanye unamaneno mengi, unajuwa kuwa nimepewa report kuwa umewazuwia vijana wangu wasifanye kazi yao, ya kumkamata mwalifu” aliongea hayo bwana Kingarame, akizania kuwa inatosha kumdhibiti na kumlegeza Kisona, asiendelee kuongea maneno mazito yaliyo mchukiza, lakini kamanda Kingarame akashangaa kumwona Kisona anatabasamu, “labda umekosea kusema, ni kuwa niliwazuwia kuuwa, na maumizi mabaya ya risasi za serikali, na siyo kwamba nilizuwia askari wako, kumkamata mwalifu, alafu kumbuka kuwa huu ni ujumbe wa brigedia kamanda, hivyo majibu yako ni muhumu sana” hapo Kingarame aka tabasamu kibishi, yani kwa kujilazimisha, kisha mtazama Kisona, “wewe bado mdogo sana bwana Kisona, uwezi kujuwa sisi wakubwa tunavyo fanya kazi” alisema Kingarame kwa dharau, kisha akaongezea, “ongea jingine kama unalo” hapo Manase Kingarame akatulia kidogo kmusikiliza kama, “jingine kamanda ni hilo la matumizi ya risasi, zilizo nunuliwa kwa fedha ya wananchi” alisema Joseph Kisona, huku akimtazama bwana Kingarame, “kwa hiyo unataka nifanyaje?” swali hilo lilionyesha kuwa Kingaame amechoshwa na maneno ya Kisona, “ongea na vijana wako, watumie vizuri risasi, maana inashangaza kuona polisi sana walio fuzu mafunzo yao, wakielekeza bunduki zao kwa mtu mmoja, ambae hana siraha yoyote mkononi mwake” alisema Kisona kwa namna flani ambayo ilimstua sana bwana Kingarame, “ok! bwana Kingarame, nakutakia msako mwema wa huyo bwana Lukas” alisema Kisona, huku anainuka na kutoka nje ya ofisi,
 Kingarame baada ya kumwona Kisona ametoka, akashusha pumzi kwa nguvu na kumgonga ngumi mezani kwanguvu, “unajifanya unatafuta sifa siyo, upati kitu mnjinga mkubwa” ********
 Akiwa kichakani bwana Lukas, yani umbali wa mita kama miatatu hivi, toka bara barani, aliweza kuona tukio zima la kusimamishwa kwa wale vijana wawili walio mshusha toka kwenye gari lao, wakiwa wamesimamishwa na polisi, na kupigishwa magoti, akaombea wasije kuongea kama alivyo wasimulia juu ya yeye kuwa na ushahidi wa mkanda wa video watukio la jana usiku pale NMC, maana awata kuwa salama,
 Lukas alishuhudia wale polisi, ambao kila dakika zilivyo pita ndipo alipo zidi kupata uakika kuwa ndio wale aliowaona usiku NMC, wakijikusanya na kujadiliana jambo, ni baada ya kumaliza kulikagua gari lile lamizigo, kikao akikutumia muda mrefu akawa shuhudia wale polisi wakiwa funga kamba mikononi, na miguuni, wale vijana wawili, huku wakiwatandika makofi mawili matatu, pia wali waliwaziba midomo yao, kwa vipande vya mashati yao waliyo yachana pale pale, baada yahapo, waka wapakiza nyuma ya gari lao la mizigo, yani Nissan Diesel, pamoja na askari polisi wanne, akiwepo sajenti Kibabu, na mmoja akaingia upande wa dereva wa gari hilo, huku polisi wawili walio bakia, wakiingia kwenye gari lao dogo, yani land rover 110, kisha wakaanza kuondoka kuelekea mjini,
 Lukas licha ya kuakikisha tayari adui zake wamesha ondoka, alitulia pale kichani aki waza jambo la kufanya, ili kujiondoa na mkasa huu wa kutisha, ambao alitamani iwe ndoto, na kwamba akiamka asubuhi iwe imekweisha, na yeye yupo salama, maana alijuwa kulipoti katika kituo chochote cha polisi, ndani ya mkoa huu wa Ruvuma, nisawa na kujiingiza mwenyewe kwenye kifo, maana mpaka sasa alisha gundua ni kwamba, lengo la polisi hawa ni kupata tape aliyo nayo, na kumpoteza kabisa, yani kum uwa kabisa, iliwafute ushaidi watukio lao kule NMC, la kuwauwa wenzao na kupola mari, ambazo mpaka sasa ajajuwa thamani yake,
 Baada ya kuwaza kwa dakika kadhaa, Lukas akawakaumbuka wale wanajeshi, wajeshi la ulinzi, alio waona pale nyumbani kwake, kabla haja vamiwa tena na polisi na kumshambulia kwa risasi, akaona kulikuwa na uelekeo wa yeye kupata msaada, toka kwa kwa wanajeshi wale, kama alivyoona wakati ule, na ukweli ni kwamba, alimkumbuka yule kamanda alie kuwa na wale askari pale nyumbani kwake, anaitwa Joseph Kisona, alimfahamu siku zilizo pita, kwenye mkasa wa kifo mkononi sehemu ya kwanza, kipindi kamanda huyu kijana, alipo jizolea sifa baada yakuonyesha uwezo mkubwa sana, wa kimapigano, na kulimaliza kundi kubwa la wahasi, wa hiumbi, “tatizo ni kwamba, nita mfikiaje?” ilo ndilo swali alilo jiuliza Lukas, ambae baada ya kuwaza chakufanya, akaona ni vyema asafiri nje ya mkoa, akiwa na malengo mawili, moja ikiwa ni kwenda makao makuu ya polisi huko dar es salaam, huku akipanga njia yapili kuwa endapo atafanikiwa kupata kambi lolote la jeshi la ulinzi, aombe mawasiliano na kamanda Joseph Kisona, ili amweleze ukweli juu ya kutafutwa kwake, na kuusishwa na ujambazi,
 Lukas baada ya kupata jibu hilo akaona jitokeze barabarani, ili atafute usafiri wa kumtoa nje ya mkoa wa Ruvuma, Lukas alitembea pembeni ya barabara, huku akiwa makini sana, akitazama nyuma kuakikisha akuna gari la polisi litakalo mkuta, akutembea sana kijana Lukas, akabahatika kupata lift, ya gari aina ya Datsun wagon, ambalo lilikuwa linaelekea Mbeya, ndani ya gari alikuwa mtu mmoja tu, alie jitambulisha kwa jina la Said Mtutuma, ambae ni fundi na dereva mzoefu, bahati nzuri Said akuonyesha kumtambua Lukas kuwa ndie mtu ambae habari zake zimetapakaa huko mjini, kuwa anatafutwa kwakosa la ujambazi na mauwaji, ilikuwa saa saba na robo, ******
 Mama wa mrembo Monalisa, akiwa na na mama mkwe mwenza walikuwa mjini wana fanya manunuzi kwaajili ya sherehe, itakayo fanyika kesho jioni nyumbani kwakina Monalisa, ikiwa nisiku peke kwa watoto wa wamama awa wawili, kuveshana pete za uchumba, kama ahadi ya wawili hao kukubaliana kuwa wachumba, na kwamba tarehe ya ndoa ipangwe, kilicho wa stua wakina mama hawa ni baada ya kuiona picha ya kijana mpiga picha, walie mwalika kwaajili ya kupiga picha kwenye sherehe hiyo ya vijana wao, tukio hilo lili wastua sana wakina mama hawa, “inamaana jana alipotoka nyumbani alipitia kuiba NMC?” aliuliza mama Monalisa, “ndugu yangu, ata mimwenyewe nimeishiwa nguvu, yani hawa vijana siyo waaminifu kabisa” alisema mama Erasto, “lakini wasije wakawa wanamsingizia kijana wawatu, mbona aelekei kuwa ni jambazi kijana wawatu” alisema mama Monalisa, kwa sauti ya kuto kuamini kweli, alafu hasubuhi niliwasikia wakitangaza redioni, kumbe huyu mpiga picha aitwa Lukas aliongea mama Erasto, wakiwa wameikodolea macho picha ya kutafutwa kwa Lukas, iliyobandikwa kwenye moja ya ukuta wa majengo ya hapa mjini ***** 
Sajent Kibabu alishuka toka kwenye gari kubwa yani Nissan Diesel huku ana jifuta damu mkononi mwake, akitumia kitambaa kilicho patikana kwenye shati la Tingo wa Devi, lililo simama kwenye viunga vya jengo dogo la kituo cha polisi bombambili, likitanguliwa na land Rover 110, la polisi, baada ya kumaliza kujifuta damu mikononi, aka rushia kile kipande cha kitambaa nyuma ya lile gari, nakuingia kwenye jengo la kituo hicho, akiwaacha wenzie kwenye gari, Kibabu akaenda moja kwa moja mpaka mapokezi, ambapo alimkuta yule polisi wakike, ambae sasa hakuwa peke yake, alikauwa na polisi wengine wawili wakiume, na raia kadhaa wenye shida zao mbali mbali, Kibabu aka mwendea yule polisi wakike, ambae baada ya kumwona aka msalimia salamu ya kijeshi, wakaingia ofisini, kisha yule skari wakike akamweleza kuwa, tayari ile miili ya wakina mama wawili, wamesha ipeleka hospital ya mkoa, kuiifadhi, “ok! naomba nipishe kidogo niongee nasimu” alisema sajenti kibabu, nayule askari wa kike aka mpisha, nae aka bonyeza namba za  simu, na dakika chache baadae akaanza kuongea, kwa sauti ya chini akimweleza mkuu wake bwana Kingarame, jinsi mambo yalivyo kuwa na kwamba, mpaka sasa wamesha wauwa vijana wawili walio pewa siri na Lukas, “ok! hao washenzi wame uliwa na huyu jambazi, na nyie njooni haraka ofisini kwangu tujadiriane” ndivyo alivyo maliza Kingarame *******
 Mzee Mbogo mida hii alikuwa ndani ya gari lake, Land rover 109, station wagon, yani lile la kuzibwa kte, wengi uwa wanaita milango mitano, alielekea mjini kumfwata mke wake kwa mwendo wa taratibu, huku anasikiliza redio ya kwenye gari lake, huku anawaza juu ya mwanae Edgar, ambae ni mwanae wapekee, na hajamwangusha katika swala la elimu, “habari zilizo tufikia hivi punde, nikwamba yule jambazi bwana Lukas Benjamini, ameendelea kuwakimbia polisi, na kufanya mauwaji mengine ya watu wanne, wakiwepo, wakinamama wawili waliokuwa wana kata kuni, ndani ya pori la mlima wa chandamali, na dereva mmoja na tingo wake, waliokuwa safarini kuelekea dar es salaam” ilikuwa ni habari ambayo ilimwondoa mzee Edgar, toka kwenye mawazo ya kumkumbuka mwanae Edgar, na vituko vyake vya zamani, “kamanda wa upelelezi mkoa wa Ruvuma, ametoawito kwa wananchi yoyote atake mwona au kupata habari ya jambazi hilo, atoe taalifa kwenye kituo cha karibu cha polisi” iliendelea hiyo habari, ambayo aikuwa ngeni kwa bwana Mbogo, ila ilikuwa ni mwendelezo tu wa habari za toka leo asubuhi.
 Taalifa hiyo aikumfikia bwana mbogo peke yake, pia ilimfikia bwana Joseph Kisona, ambae alikuwa ofisini kwake anajiandaa kwenda ofisini kwa mkuu wake, kutoa report juu ya safari yake, ya ofisini kwa mkuu wa upelelezi mkoa, ukweli mwenendo wa matukio hayo, ulimpa mashaka sana, bwana Kisona, maana pale porini  chandamali alishuhudia kwa macho yake kuwa walioshambulia ni polisi, na siyo yule kina Lukas, ambae zaidi ya pochi aliyo ining’iniza kiunoni, akuwa na silaha yoyote, “sasa yule kijana amewezaje kuuwa wakinamama wasio na hatia, wakati hakuwa na silaha yoyote?”alijiuliza Joseph Kisona, ****** 
gari aina ya Dutsun likiwa limetembea umbali wakilomita kumi, toka chandalua, lilisha fika maeneo ya Mlilayoyo, huku muda wote wa safari wawili hawa yani lukkas na Mtutuma wakiwa kimya wana sikiliza redio iliyo kuwa ina toa taarifa ya tukio la jambazi sugu, ambalo linaendeleza mauwaji, ndani ya mji wa Songea, “ngoja kwanza ninunue sigara kidogo maana tukitoka hapa mpaka maadaba ndio tunakuta maduka tena” alisema Said Mtutuma huku akisimamisha gari pembeni, kisha akashuka, na kuelekea dukani, sasa basi wakati Mtutuma ana kiwa dukani, Lukas akakumbuka kuwa akuwa amekula toka jana, akaona bora atumie nafasi hii kununua japo biskuti na juice, apooze njaa, kijana huyu mwenye bahati mbaya, akiwa anaamini kuwa huku kijijini awakuwa wamepata taarifa ya kutafutwa kwake, kwamaana ya matangazo ya piicha aka shuka, toka kwenye gari na kuelekea dukani,  nikweli hakukuwa na dalili ya kuwepo kwa picha zake zilizo badikwa, kama kule mjini, Lukas alienda kwenye lile duka alilo ingia mtutuma na kununua biskuti na juice, kisha wote kwa pamoja waka rudi kwenye gari, “utani samehe kidogo ndugu yangu, maana napenda sasna kuvuta sigara” alisema Mtutuma huku akiondoa gari na kuwasha sigara, kwa kutumia kichomeo (heat) ya kwenye gari, “usiwe na shaka ndugu yangu, tujari tufike salama tu” alisema Lukas akiwa anaanza kufungua juice yake na pact ya juice, tayari kupunguza njaa, akiona kuwa tayari amesha uacha mji wa songea na sasa yupo salama, 
Ukweli mawazo ya Lukas hayakuwa sahihi, maana akujuwa kuwa, kuna mtu mmoja, ambae muda mfupi uliopita, alikuwa amepandanae kwenye dala dala moja, ni lile la mshangano, kabla haja shuka na kupanda kwenye gari kubwa la mizigo lakina Devid, na baaada ya Lukas kushuka mda mfupi baadae, polisi walikuja na kulisimamisha gari lile, wakimtafuta kijana huyu, ambae ata yeye alisha sikia habari zake, kuwa ni jambazi sugu, nabaadae kusikia kuwa ame wauwa wale jamaa waliompa lifti, 
 Sasa basi baada ya kuwa amemwona tena kijana huyu, akiwa anaingia kwenye Dutsun, akaona afanye juhudi za kulitahalifu jeshi la polisi, ukweli simu kipindi hiki zilikuwa ni zakampuni ya simu ya serikari pekee, kwa hiyo kijana huyu, baada ya kuulizia sehemu ambayo anaweza kupata simu akaelezwa kuwa aende kwenye kituo cha afya cha mlilayoyo, akatimua mbio kuelekea huko, ... vipi kuhusu Edgar na Monalisa, tuungane jioni kujuwa kinachioendelea....... endelea kufwatilia mkasa huu hapa hapa Hadithi ZA MBOGO EDGAR

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,179,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,213,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,131,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,243,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,10,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI) SEHEMU YA 05
KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI) SEHEMU YA 05
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/05/kifo-mkononi-bikira-ya-bibi-harusi_81.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/05/kifo-mkononi-bikira-ya-bibi-harusi_81.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content