KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI) SEHEMU YA 03

KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI)

SEHEMU YA TATU

STORY NA Mbogo Edgar

ILIPOISHIA SEHEMU YA PILI, tuna msaka mtuhumiwa mmoja, alie fahamika kwa jina la Lukas Benjamin, ambae alidondosha kitambulisho chake, katika eneo la tukio, wakati wa mapambano na polisi walio uwawa” hapo Lukas mapigo yake ya moyo yakalipuka kwa kihoro, akainamisha kichwa chini, licha ya kuwa baridi ilikuwa kari sana, lakini cha hajabu Lukas alianza kutokwa na jasho, endelea ...........
“kwa yoyote ambae anamfahamu kijana huyo, atoe taarifa kituo cha polisi cha karibu, picha zake zitabandikwa kila sehemu” iliendelea kusisitiza sauti hiyo kwenye redio, sauti ya kamanda Manase Kingarame, nakuzidi kumchanganya zaidi kijana Lukas, lakini akajipa moyo kuwa endapo atafanikiwa kufikisha tape ile, basi takuwa salama yake, “kwahakika hatuta kuwa na msamaha na yeyote alie usika na tukio hilli la kinyama” ukweli sauti ya kamanda Kingarame, ilizidi kumtia uoga kijana huyu mpiga picha, 
“mabanda mawili wakushuka” alitangaza kondakta, hapo Lukas aka pata wazo la haraka sana, kuwa ni muhimu ashuke kwenye dala dala, kabla waja mstukia, “shusha” alisema Lukas na dala dala lika simamishwa pembeni mwa barabara, hapo kijana Lukas akashuka toka kwenye dala dala, kisha gari ilo lika endelea na safari, Lukas aka anza kutembea kurudi alikotoka, huku akitafakari maneno ya mkuu wa kitengo cha upepelezi, lakini aka pata wazo, akiamini kuwa ni zuri zaidi, ni kwenda kituo cha polisi  cha pale bomba mbili, aombe kuonana ongea na mkuu huyo wa upelelezi, ilimweleze kuwa ana ushaidi wa tukio la jana usiku na kwamba yeye siyo muuwaji wala jambazi, ila alipanga kuto kumkabidhi mtu yoyote zaidi ya yule kamanda wa upelelezi aliekuwa anaongea kwenye radio, *******
Ndani ya viunga vya chuo cha biashara cha Mbeya, walionekana wanafunzi wakiwa wanaelekea kwenye ukumbi wa chakula, ili wakapate kifungua kinywa, na kisha kwenda kwenye ukumbi wa mikutano kuanza mahafari ya kumaliza mafunzo yao, lakini ndani ya chumba cha kina Monalisa, kwenye bweni la Mapinduzi, alikuwepo Monalisa binti mrembo sana, ambae leo alionekana kuwa mrembo mala dufu, ambae nae alikuwa mmoja wa wahitimu, na sasa alikuwa peke yake, ndani ya chumba hicho, akitoa bahadhi ya vitu vidogo vidogo toka kwenye begi kubwa, na kuviweka kwenye kijibegi kidogo cha mgongoni, Monalisa alionekana akiweka vitu vyake kwa umakini mkubwa sana, ikiwa pamoja na kuzikjagua fedha zilizo kuwepo ndani ya kile kijibegi kidogo, alimaliza kupanga vitu vyake, akibakiza suluali nyeusi ya jinsi, na tishet moja jeusi zuri, na viatu vyenye visigino virefu, vya mchumio, lakini wakati anataka kufunga begi lake akaona uona ule mfuko wa kaki, akauchukuwa ule mfuko na kuutazama kwa sekunde kadhaa, kama alivyo fanya jana, ila leo alitabasamu muda wote alipokuwa ana utazama ule mfuko mdogo wakaki, Monalisa aka ufungua ule mfuko, na kuingiza mkono ndani yake, ili kutoa kilichomo, “we! Mona, unajitabasamulia peke yako?” Monalisa alistuliwa na sauti ya mtu ambae kiukweli uingiaji wake mle ndani Mona akuwa na taalifa nao, mana alistuka huku akiutoa mkono ndani ya mfuko akisitisha zoezi la kutoa kilichomo, na kugeuka nyuma, kumtazama muongeaji, “stella umenistua” alisema Mona huku, ana ukunja ule mfuko na kuuweka kwenye kijibegi chake cha mgongoni, “vipi Mona bado tu nilikuwa nakungoja twende kwenye chai?” aliuliza stella, “yani Stella sijuwi kwa nini, kila nikifikilia kurudi nyumbani inanijia picha ya kuolewa tu, basi mwenzio nakosa ata hamu ya kula” alisema Monalisa, kwa sauti flani hivi ya unyonge, huku akifunga begi lake, “mh! sasa Mona kwani tatizo nini, miaka 22 inatosha kuolewa, isitoshe mtu mwenyewe mnafhamiana toka utotoni” alisema Stella huku akikaa pembeni ya Monalisa, alie kuwa anamalizia kuweka sawa vitu vyake, “Stella ni vigumu sana, kuolewa na mtu ambae umesha shuhudia mambo yake mengi sana, ametembea mpaka narafiki zangu wa karibu tukiwa shule, tena wengine nilikuwa namtongozea mimi mwenyewe, alafu leo nikaolewe nae inakuja kweli?” hapo wote wakatulia kwa dakika kadhaa, kama walikuwa wanawaza jambo flani, kisha Stella akasema “lakini Mona, hiyo si ilikuwa ya utotoni?” Mona akacheka kidogo, kicheko ambacho kilionyesha wazi binti huyu anakumbukumbu chungu za mchumba wake, maana nikama alicheka kwa kuguna, “Stella, hivi nikikuambia kuwa, mwaka jana nilimkuta ana fanya mapenzi na dada wao wakazi, utania mbia ni mambo ya utotoni?” alisema Monalisa ambae kwasimulizi hiyo, nikama alikuwa katika wakati mgumu sana, hapo wote wakatulia tena, na baada sekunde chache, Monalisa aka mtazama Stella, na kujitabasamulisha, tena tabsamu la kinyonge hivi, “lakini sawa, kipindi hicho hakuwa mchumba wangu, na pia wazazi wangu watafurahi sana, nikiolewa nae, sababu wazazi wetu ni marafiki, pia baba na mama walitaka kuona naolewa na mtu wanae mwamini” alisema Monalisa huku akiinuka na kuliweka begi lake vizuri, hapo Stela akatabasamu kidogo, “lakini raha, kuolewa na mtu unae mfahamu vizuri” alisema Stellah, kwa sauti flani tulivu iiyo onyesha kutamani kitu kama kile kimtokee yeye, “lakini upande mwingine, kuna magumu sana,” alisema Monalisa, akiweka kituo kidogo, huku Stella akitega masikio kwa umakini, “ujuwe kabla ya kuambiwa na mama kuwa Erasto ndio ata kuwa mchumba wangu, nilikuwa namchukia sana Erasto” lisema Monalisa, akiweka kituo kama mwanzo, “kwanini sasa, au kutembea na dada yao wakazi?” aliuliza Stella kwa mshangao, “hapana, sababu alikuwa mmbea sana, sikuzote hakutaka ni simame na mvulana yoyote, akiniona tu! alikuwa ana kimbilia kwa mama yangu kumweleza” alisema Monalisa huku akijiweka sawa, na kujitazama kama amevaa vizuri, “labda alikuwa ana mlinda mke wake mtarajiwa” alisema Stella kisha wote wakacheka, lakini ukweli amenikosesha kitu ambaacho sizani kama nita futa chuki yangu juu yake” alisema Monalisa, kisha kikapita kimya kidogo, huku kila mmoja akijiweka sawa, si unajuwa mambo ya wanawake, tena warembo kama hawa, “kwahiyo  Mona, unataka kuniambia ujawai kupenda mvulana yoyote toka umezaliwa?” aliuliza Stella, ambae kiukweli ndie rafiki yake mkubwa sana pale chuoni, Monalisa alicheka kidogo,  huku anaongoza nje, ya chumba chao akifwatiwa na Stella, “mh, sijuwi nisemeje, ila kweli unabakia kuwa, utakijuwa unacho kipenda baada ya kukikosa” alisema Monalisa kisha akaachia kicheko kikubwa sana, akisaidiwa na rafiki yake Stella, ambae akuwa ameleewa maana ya maneno ya Monalisa, “nazani unaweza kwenda kunywa chai na vitumbua, maana umechangamka sasa” alisema Stella na Monalisa akaunga mkono, maana alikuwa anpenda sana vitumbua, nao waka elekea messi, kujiunga na wanafunzi wenzao kupata chai, ****** 
Lukas alifika kituo cha polisi, ambapo alimkuta polisi mmoja wakike wakiwa counter, polisi yule wakike akuwa na kazi nyingi, zaidi alikuwa ameinamia meza kubwa ya pale mapokezi, huku mbele yake watu wawili, raia, walionekana kusimama mbele yake, inaonyesha alikuwa ana anaandika maelezo flani, kwenye daftari kubwa, lakini bwana Lukas kabla ajafanya lolote, macho yake yaka tua kwenye ukuta wa kituo kile, eneo la matangazo, na ndipo alipo ona karatasi lenye picha, aka litazama vizuri, ile picha ilikuwa ni picha yake, ikiambatanishwa na maandishi makubwa sana, JAMBAZI SUGU ANATAFUTWA, NA POLISI, huku tangazo ilo liki sisitiza kwa kutaja jina lake na namba za simu simu, (kipindi hicho Kampuni simu ya taifa) Lukas alipo tazama vizuri akagundua kuwa ile picha aikuwa moja, zilikuwa zaidi ya sita,
Hapo kijana huyu aka tazama kushoto na kulia, kama kuna mtu mwingine alikuwa ana mtazama, akuona mtu zaidi aliona makaratasi yenye picha zake, yakiwa yame bandikwa kwenye nguzo za umeme, hapo Lukas aka tazama ndani ya kituo cha polisi, akaona yule polisi wakike, akiwa busy na raia wake wawili, Lukas aka ona ita kuwa ngumu sana kujieleza kwa huyu polisi wakike, kutokana na jamo hili tayai kufikia  kwenye hatua kubwa, hivyo akaokota kijiti chini, na kujiandika zile namba kwenye sehemu ya mkono wake, siyo kiganjani, kwa kujikwangua kwangua, (lakini bila kujichubua) kisha akaondoka zake akipanga akatafute kibanda cha kupigia simu, ili apige zile namba, za kwenye tangazo la kutafutwa kwake, lakini bada ya kutoka pale kituoni, akiwa amekiacha kama mita hamsini tu, akaliona gari la polisi likija nyuma yake, usawa wa kituo cha polisi, kwa kasi ya hajabu sana, Lukas alilitambua lile gari kuwa lime fanana kwa kihasi kikubwa sana kama lile la jana usiku, japo magari haya nimengi sana hapa mkoani, lakini sijuwi kwa nini hili lilimstua sana Lukas, pengina kwakujuwa amesha julikana kuwa ni yeye ndie aliekuwepo kule NMC, usiku ule, na mbaya zaidi atakama wale jamaa wauwaji siyo polisi, lakini pia ilisha tolewa tangazo kuwa yeye ni jambazi,
Lukas akujiuliza mala mbili, aka litazama jengo moja dogo mbele yake, akaona ni hatua kama tano tu! ana lifikia, aka fanya hivyo kwa hatua za haraka sana, na kujibaza upenuni mwakile kibanda, akatulia kwa sekunde kadhaa, akisikilizia mlio wa gari, ambalo alilisikia likisimama kituo cha polisi, hapo Lukas aka chungulia kidogo kule kituoni, akaona lile gari la polisi likiwa limesimama pale kituoni, huku askari polisi sita wenye bunduki zao aina ya SMG mabegani mwao, wakiwa nyuma yagari, na baada ya sekunde chache akamwona askari polisi mwingine ana tokea ndani ya kituo cha polisi, na kuingia kwenye gari, kisha gari likaondoka kwa speed na kurudi lilipo tokea, hapo Lukas aka tulia kidogo akijaribu kukumbuka jambo, maana jana aliwaona watu hawa wakiwa saba, kama alivyo waona leo, kwahiyo inawezekana polisi hawa ndio wale wale waliofanya mauwaji kwa wenzao, hapo Lukas akatambua kuwa anatakaiwa kuwa makini sana, hivyo kinacho takiwa apate sehemu salama atakayo piga simu kwa kamanda kingarame, na sehemu hiyo ni stationary kwa mteja wake mmoja wakike, anae itwa Faraja, ambae mala nyingi uwa anapiga picha kwake. ******
Katika jengo kubwa sana la polisi mkoa, kwenye chumba cha mikutano, walionekana makamanda wakuu wa polisi mkoa, wakijadiri jambo, lililo onyesha kuwaumiza kichwa vyao, huku wakitembezeana picha moja kubwa ya rangi, yenye sura ya kijana Lukas, “hii ni ahibu kubwa sana, kwa jeshi letu” alisema RPC, kwasauti kavu iliyo jaa hasira na majonzi, “inawezekanaje vijanawetu washindwe ata kujibu mapigo” aliendelea kuongea mkuu huyu wa polisi mkoa, kwa sauti ile ile ya ghadhab, kisha aka mtazama mkuu wa upelelezi mkoa wa Ruvuma, bwana Manase Kingarame, “RCO, nataka huyo mtu apatikane mala moja, aijalishi akiwa hai au ame kufa, hizo mali alizo iba siyo tatizo, muhimu ni yeye apatikane” alisema RPC kwa sauti ya amri, yenye machungu makubwa, na hasira kali sana, “RCO, tumia askari na silaha tulizo nazo, ili umpate huyo mhalifu” alisema tena RPC, kwa msisitizo, hapo hapo OC FFU, aliekuwa ameishika ile picha ya Lukas, akaomba kuchangia jambo katika swala lile, akaruhusiwa, “bahati nzuri ni kwamba, huyu kijana, anafahamika sana, aliwai kupiga picha kwenye kipaimara cha kijana wangu” alisema mkubwa yule wa FFU, na bahadhi ya wenzake waka kubaliana nae, kuwa yule kijana nilikwe mpiga picha na ni mharufu sana pale mjini, “ila uwezi hamini kabisa kama huyu kijana anaweza weza kushiriki ujambazi” alisema Staff office, huku akichukuwa karatasi lenye picha ya Lukas na kuitazama, huku bahadhi yao wakionyesha kushangazwa na ushirki wa kijana Lukas kwenye ujambazi, “ok! tutawanyike, tukaendelee na majukumu, ila endapo RCO ata itaji msaada wowote toka ktk kitengo chochote, asaidiwe haraka sana, ilikuweza kufanikisha msako huu” alisema RPC, na kuinuka kisha akatoka nje ya chumba cha mikutano, *******
Monalisa na Stella, walitembea taratibu kuelekea kwenye jengo la chakula, yani messi, mala kama kuna kitu Stella akakumbuka, “Mona unajuwa jana Denis alimiambia amepata usafiri, tunaondoka saa tisa, unaonaje tuondoke pamoja tuka kuache Makambako?” Denis ni mpenzi wa Stella, pale chuoni, wana kaa pamoja dar es salaam, hapo Mona alitulia kidogo, akionekana kuwaza jambo, sasa walikuwa wamekaribia kwenye lango la kuingilia messi, ukumbi wa chakula, “ok! tutaangalia, maana ata tiketi bado sijakata” alijibu Monalisa huku wanaingia ndani ya jengo hilo, kama kawaida ndani walionekana watu kibao, yani mwanachuo, ambao waligeuza shingo zao kumtazama Monalisa, kiasi cha binti huyu kutazama chini kwa kuona nishai, alafu akatembea haraka mpaka kwenye meza moja iliyo kuwa na mtu mmoja, ambae alikuwa ameinamia shani yake na kikombe cha chai, huku viti vitatu vikiwa wazi, yeye na Stella wakaa, wakisubiri wale wadada wanao hudumia waje kuwa hudumia, maana hapa chuoni chakula ni kujitegemea, yani mwana chuo alitakiwa kujinunulia chakula,
Ukweli ni kwamba Monalisa akuwai kuzowea macho ya watu, japo akuwai kupishana na mvulana au mwanaume yoyte, asigeuka mala mbili kumtazama, kutokana na jinsi mwanamke huyu alivyo pendelewa uzuri wa hasiri, “habari dada Mona, utakunywa chai na nini? au vitumbua kama kawaida yako” tayari mhudumu mmoja alikuwa amesha fika, Monalisa alicheka kidogo, “haya niletee chai na vitumbua” alisema Monalisa huku akiinua macho kutazama, wenye sahani ya yule mtu walie mkuta pale walipokaa, akastuka kidogo, akainua uso wake, kutazama mtu huyu, hapo akajikuta ana toa macho ya mshangao,  “na mimi leo niletee kama Mona, ata sijuwi kwanini anapenda sana vitumbua” alisema Stella, huku ana mtazama Monalisa, “eti Mona kwanini una penda sana vitumbua?” aliuliza Stella, lakini akastuka kuona mwenzie akiwa amemkazia macho mtu walie mkuta, pale walipo kuja kukaa, na yeye Stella aka geuza shingo kumtazama yule mwanachuo mwenzao, kisha akashusha macho mezani, kwenye sahani ya yule mwanafunzi, kulikuwa na kitumbua kimoja kizima, na kingine nusu, wote pamoja na yule mwanafunzi wakiume waka tabasamu.
Huyu alikuwa Edgar Eric Mbogo, kumbuka kuwa licha ya kuwa wawili hawa walikuwa wanafahamiana toka utotoni, lakini awa kuwa na ukaribu sana asa kwa maisha yao ya hapa chuoni, kwa kuthibitisha ilo, katika miaka mi tatu waliyo kuwepo hapa  chuoni, leo ndio wame kaa meza moja, yani kwa ukaribu zaidi, ukaribu ambao waliwai kukaa zaidi ya miaka kumi na mbili iliyoita, “Edgar mambo?” alisalimia Monalisa, huku akiachia tabasamu, nakumshangaza Stella, siyo kwa kusalamia, ila ni hili tabasamu, ambalo lilionyesha kuwa watu awa wana fahamiana sana, tena kwa ukaribu zaidi, “poa hongera kwa kumaliza chuo” alisema Edgar, akijitaidi kukwepesha macho yake yasikutane na macho ya mrembo Monalisa, “asante Hongera na wewe” alijibu Mona, kisha kikafwata kimya, kimya kilicho  dumu kwa dakika nzima, mpaka chai yao ilipoletwa, na wakina Mona kuanza kunywa, lakini Edgar alikuwa amesha maliza kunywa chai, akainuka, “Edgar, nikuongeze vitumbua, au umekula vingi sana?” aliuliza Monalisa kwa sauti flani ya utani, iliyo mfanya Edgar acheke kidogo, “nabakiza nafasi ya nyumbani” alisema Edgar, na kumfanya Monalisa achekezaidi, nikama kunajambo alikumbuka, Edgar akuendelea kubakia maali pale, akaondoka zake, akiwaacha wakina Monalisa na Stella, wakiwa bado wanacheka, “kwani Mona mna fahamiana na huyu mkaka?” aliuliza Stella, wakiwa wanaendelea kunywa chai, “ndio, nimesomanae shule ya msingi” alisema Monalisa, na kumshangaza Stella, “haaa! sasa mbona mlikuwa manaishi kama amjuwani?” aliuliza Stella kwa mshangao, Monalisa akuijibu kitu ila alitabasamu tu!, “yani mwenzio nampenda huyu kaka, ana juwa kuchora, alafu anacheza vizuri baskert” alisema Stella kwa sauti ya chini, na kumfanya Monalisa aendelee kutabasamu, bila kujibu kitu, “yani ningejuwa mapema, ningekuambia uniunganishe nae” aliendelea kusema Stella, lakini hapo Monalisa aka inua uso wake na kumtazama Stella kwa mshangao, “alafu Denis unge mwachia nani?” aliuliza Monalisa, akiwa bado anamtazama Stella, “kwani kuwa karibu ndio kuwa wapenzi?” aliuliza Stella, akijaribu kuweka saawa hisia za Monalisa, “mama yangu aliniambia, kuwa ukiwa karibu na mwanaume, una mshawishi akutongoze, saa unazani ungeweza kujizuwia?” aliuliza Monalisa huku akiendelea kunywa chai, Stella akakaa kimya, na kuendelea kunywa chai, huku Stella akijihisi kuwa ameongea swala ambalo, alikumpendeza Monalisa, maana ni la kihuni sana,
“Mona usije uka sahau kuniwekea kadi ya mwaliko, lazima nije kwenye harusi yako” aliongea Stella akijaribu kuamisha mada, hapo Monalisa akainamisha kichwa chini, na kuonekana kama anawaza jambo flani, ********
Saa tatu asubuhi Lukas alikuwa kwenye sehemu ambayo palikuwa na maduka machache, sana kama matatu hivi, ata watu walikuwa ni wachache eneo lile, aka ongoza moja kwamoja kwenye duka mmoja la vifaha vya maofisi ni na mashuleni, yani stationary, ukweli nikwamba mpaka mida hii karibu kila sehemu picha zake zilikuwa zime bandikwa, “we Lukas jamani kwa nini umefanya ujinga kama huo?” aliuliza binti mmoja alie kuwepo mbele ya counter ya duka lile, kwa sauti ya mshangao, na huruma, mala tu baada ya Lukas kuingia ndani ya stationary hiyo, akionyesha kuwa amesha sikia habari ya Lukas kutafutwa na polisi kwatuhuma za ujambazi, “sikia Faraja, muda huu siyo wa maswali, kinacho takiwa nijitaidi kufikisha ushahidi huu kwa Wausika, ndipo nitakuwa salama” alisema Lukas huku akichukuwa peni na karatasi na kuanza kuandika namba za simu, ambazo zilikuwa kwenye mkono wake, “nipigie hii namba” alisema Lukas na kumpatia yule dada ile karatasi, nae aka ipokea na kuanza kubonyeza namba kama zilivyo andikwa na Lukas, “sasa imekuwaje wakakuusisha na tukio hili?” aliuliza Fraja huku akiweka mkonga wasimu sikioni, “Faraja, nitakusimulia kila kitu, ngoja kwanza ni kamilishe nia yangu ya kuonana na RCO, nikzubaa nita uwawa.....” kabla haja maliza kuongea bwana Lukas, akamsikia Faraja akiongea na simu, “shikamoo.......... sijambao....., kuna mtu anataka kuongea na wewe” alisema Faraja kwa sauti ya uoga kidogo, nazani nibaada ya kuongea na mtu asie tarajia, aka mtazama Lukas, kwa macho yakama ana taka kumsuta, kisha akampatia simu, akiwa ameziba mkonga wa simu, ile sehemu ya kuongelea, “mkubwa wa polisi” alinong’oneza Lukas, Lukas akapokea mkonga wa simu na kuweka sikioni, “hallow shikamoo mzee” alisalimia Lukas kwa sauti iliyomezwa na hofu kubwa, kiasi cha kusindwa kumiliki pumzi nzito zilizo jaa kifuani kwake, na kusikilizia jibu la upande wapili, “marahaba ungaongea na SSP Manase kingarame, nani mwengu?” ilikuwa sauti nzito na kavu ya upande wapili wasimu, hapo Lukas akaaachia tabasamu la matumaini, akijuwa kuwa ukombozi umepatikana, “naitwa Lukas Benjamin, yule mtu mnae mtafuta” alisema Lukas, akijuwa kuwa sasa amepata usalama, “ok! kijana, unataka nini, na kwa nini utaki kujisaliisha?” aliuliza kamanda Kingarame, “mzee mimi siyo jambazi, nimekupigia ili tukutane nikukabidhi ushahidi, nina mkanda wa video unao onyesha tukio zima” alisema Lukas kwa kujiamini, huku faraja akimsikiliza kwa umakini kabisa,
Hapo Lukas akasikia sauti ya mstuko ya kamanda kingarame, “he! unasema mkanda wa video?” aliuliza Kingarame, “ndio mzee wangu niambie kama hupo hapo ofini kwako, nikuletee, au nielekeze niipelekewapi?” aliongea tena Lukas kwa kujiamini, “vipi kuna mtu yeyote ana juwa kama unao huo mkanda wa video?” aliuliza Kingarame kwa sauti ya chini kana kwamba akutaka mtu mwingine asikie, yani kule alikokuwepo, “hapana mzee, zaidi najitaiadi kuwakwepa polisi, maana wananitafuta sana”alisema Lukas ambae kwa sasa alionekana kuwa mwenye amani kubwa moyoni, “sikia kijana kwa ni sasa hupo wapi?” aliuliza Kingarame akionekana kuhamasika kwa ile tahalifa, “nipo bomba mbili” alijibu Lukas, “sawa nenda kwenye bara bara ya juu, ya mlima wa chandamali, kisha nisubiri hapo, usi mwambie mtu yoyote”,
Hivyo ndivyo walivyo kubaliana wawili hawa, huku Lukas akipata matumaini makubwa juu ya usalama wake, asa baaada ya kuambiwa asimwambie mtu yoyote, akatoka pale kwa Faraja, akiahidi kuja kumsimulia kilakitu, endapo ata rudi toka chandamali, pasipo kujuwa kuwaw pengine ule ndio ulikuwa mwisho wao wa kuonana, Faraja alimsindikiza kwa macho kijana huyu alie pendezwa sana na upigaji wake picha, na uaminifu katika ahadi zake za uletaji wa picha, ukiachilia wengine ambao mala nyingi utoa sababu nyingi za kuungua kwa picha, Lukas alitoka nje ya ofisi ya Faraja, na kuelekea upande wa mlima chandamali, na ndiko anakokaa yeye, ****** 
Mida hii ndani ya kambi moja kubwa sana la jeshi la ulinzi, pembezoni kidogo ya mji wa songea, jirani kabisa na mlima wa chandamali, katika ofisi moja nyeti sana ya Jeshi la ulinzi, kati ya ofisi nyingi zilizo pakana na msitu ulio zunguka mlima wa chandamali, alionekana jamaa moja alie valia magwanda ya jeshi, yale ya kivita, ya ni combat dress, huku akipita badhi ya report za saa ishilini na nne, katika kupitia kwake makaratasi yale, alionekana kuvutiwa na report moja, “copral Katembo ebu njoo mala moja” aliita kamanda huyu mwenye cheo cha canal, mlango wa ofisi ukafunguliwa akaingia kijana mmoja alie valia kama yeye, mwenye mwili ulio jengeka vyema, akiwa na alama ya vii mbili begani kwake, yani kopral, akapiga salut, akiwa mguu sawa mbele ya meza kubwa, “hivi Katembo, hili tukio la NMC, mmejaribu kulifwatilia kujuwa limeishia wapi?”, liuliza yule kanali ambae kwenye kifua chake, kuna name tag, yaani kiambatanishi jina, kilichoandikwa J.N Kisona, “atuja fwatilia afande sababu swala lipo chini ya polisi mkoa” alijibu yule askari jeshi mwenye cheo cha koplo, hapo yule kanali akatulia kidogo akilitazama kwa uamakini lile karatasi lenye kuonyesha tukio la NMC jana usiku, “lakini mlijaribu kuipitia vizuri hii report, nakujiuliza kinachoendelea?” aliuliza yule Kanal ambae ukitazama kwenye mfuko wake wa kusoto wa lile vazi la kijeshi, inaonyesha jina lake ni Kisona, hapo koplo Katembo aka stuka kidogo, maana huyu mkubwa wake akitilia shaka jambo, ujuwe kuna mashaka kweli, “tumeipitia afande, kwani kuna tatizo lolote?” aliuliza Katembo huku ana sogelea meza ya mkubwa wake, “ebu tazama kwanza, polisi watano wenye silaha, wame uwawa, sehemu moja” alisema kanal Kisona, kwa sauti iliyotilia mashaka, huku akiendelea kuongea tena, “Polosi, walishindwa kutumia silaha zao, ambazo zime kutwa eneo la tukio, alafu atakama majambazi walishindwa kubeba bunduki za poli hao, sasa alishindwa kuchukua ata risasi?” aliuliza kanal Kisona kwa sauti ya mashaka, huku ana tabasamu, hapo Kplo Katembo na yeye akaanza kuhisi jambo juu ya swala hili, 
Huyu anaitwa Kanali Joseph Kisona, (soma sehemu ya kwanza ya KIFO MKONONI (UTANI WA BIBI) ***** 
Lukas alifika mapema sehemu ya ahadi, ilikuwa imesha timia saa nne kasoro, ukweli msitu huu wa chandamai ni msitu mdogo sana, ulio zunguka mlima huu mdogo, wenye historia kubwa sana mkoa Ruvuma na Tanzania kwa ujumla, sasa Lukas alikuwa amesima kati kati, akiugawa msitu wa chandamali, kwenye njia inayo katiza msitu huo, pembezoni mwa mlima huu, huku pande zote, huki zungukwa na miti iliyo shona vyema, kuonyesha kuwa jeshi la ulinzi lipo imara kuulinda msitu huu, watu wasikate miti hovyo, zaidi ya kuokota zile zilizo kauka kwa matumizi ya kuni, Lukas akatazama kushoto na kulia, akuona mtu yoyote, akaamua kutulia kidogo ili kumsubiri kamanda Kingarame, aje ampatiae ushaidi wa tape ile ya video, na yeye kujitoa kwenye tuhuma za mauwaji na ujambazi.
Lakini wakati anaendelea kusubiri pale polini, bwana Lukas, kuna vitu vika mjia kichwani na kumshangaza kidogo, ni kutokana na mambo mawili, moja kitendo cha Kamanda Kingarame kuongea kwa kustuka stuka, na yachini, baada ya yeye kujitambulisha, na kumweleza kuwa anaushaidi watukio zima, kitu cha pili, ni kitendo cha kumweleza wakutane kule porini, kwanini asinge kuja pale pale stationary, hayo yote alijumlisha na wale askari saba walio kuja pale kituo cha polisi bombambili, wakiwa kwenye gari la polisi, ilizidi kumjia picha kuwa watu wale ndio alio waona jana usiku NMC, hapo Kijana Lukas akapata wazo la kujificha, ili atazame kama ata kuja mwenyewe Kamanda Kingarame peke yake, au watakuja wale askari saba, aua atakuja nao.
Lakini alisha chelewa sabababu, wakati anajiandaa kuingia msituni, akaliona gari la polisi, likija speed kali, kufwata usawa alipo yeye, na nyuma yagari hilo, kulikuwa na kuna askari ambao kwa haraka haraka alishindwa kupata idadi yao, lakini akuitaji mkalimani kumweleza kuwa, gari lile ndilo lililo kuja pale kituo cha polisi, na sasa lilikuwa mita chache toka alipo kuwepo, hapo kitendo bila kuchelewa Lukas aka cmoka mbio kuingia polini, na kukimbia mita kadhaa, kwenye vichaka virefu usawa wa shingo aua kifua, na kwenda kujibanza kwenye jiwe moja lililo zungukwa na naysi ndefu, akiakikisha anapata nafasi ya kutazama kule njiani,  ambapo ilimwezesha kuwasoma wale polisi, ili ajuwe kama ni wema kwake, au ndio wale majambazi,
Akiwa pale alipojificha, bwana Lukas aliliona gari la polisi, likisimama kwa blak za ghafla, na wale haskari waka shuka haraka toka kwenye gari hilo, wakiruka na bunduki zao mkononi,  nakunza kuja mbio mbio upande alipojificha yeye, ikionyesha wazi walishamwona wakati anaingia polini, hapo Lukas akatulia kwenye mficho yake, akiofia kufanya kosa kama la jana, kule NMC alipo kulupuka na kuonyesha maficho yake, na kusababisha aambulie risasi ya bega, wazo lake lili saidia maana aliwaona wale polisi, waki zangaa ovyo ovyo eneo lile, huku wakonyesha kuwa walikuwa tayari kufyeka chochote kitacho jitokeza mbele yao, “kumbukeni huyu mtu lazima apatikane kwanza, ndipo tumnyongelee mbali, maana amethibitisha mwenyewe kuwa ile tape anayo” aliongea mwenzao alie onekana ndie mtoa amri, begani kwake akiwa na alama ya vii tatu, yani cheo cha sajenti, Lukas akahisi mwili mzima ukimsisimka, baada ya kusikia neno kunyongwa, na mbaya zaidi inaonyesha kuwa hawa jamaa wana taalifa yote kama alivyo itoa kwa kamanda kingarame hapo Lukas akawachungulia wale askari, akawaona wanaendelea kuzagaa, wakipekua vichaka,  huku mmoja wao akionekana kuelekea pale alipo jibanza Lukas, hapo Lukas akajuwa amesha naswa, maana yule askari polisi, alikuwa amekaribia kabisa pale alipo,
Lukas akapiga mahesabu mepesi, yani hiki ongeza hiki jibu lake kile, akaokota kipande cha jiwe na kulirusha upande wa kushoto wa yule askari, na kweli kilicho fwata yule askari aligeuka mzima mzima kutazama lilipo tuwa jiwe, ikiwa ni atua kama kumi hivi toka alipo yule askari, Lukas akuchelewa, aka mrukia yule askari na kumpiga kikumbo kikubwa sana, kiasi cha yule askari kuanguka chini akiachia bunduki yake, huku akipiga ukelele mkubwa, ulio wastua wenzake, kama lilivyo lengo la Lukas, ni kutafuta njia ya kujiokoa, Lukas akaitazama ile bunduki ya yule askari polisi, iliyo dondokea mita mbili mbele yake, bunduki ambayo licha ya kutoweza kuitumia, pia bwana Lukas akuwai ata kuishika mikononi mwake, hapo akiwa ana jilahumu kwa kujiona mjanja kipindi kile wana fundisha mgambo kijijini kwao, kakola huko tabora, akatimua mbio kwa nguvu sana, akipandisha kilimani, huku ghafla milindimo ya risasi ikisikika nyuma yake, na ukweli ni kwamba aikuwa bahati yake, maana risasi moja ilimpata kwenye paja la mguu wake wa kushoto, na kumfanya aanze kukimbia kwa kujikongoja, akijuwa muda wowote maadui zake wana mkamata, maana ukimbiaji wake ulikuwa ni wataratibu, tofauti na mwanzo.
Lakini aikuwa hivyo, maana alisikia kelele za yule alie onekana kuwa ni kiongozi wake, akipaza sauti, “acha kupiga risasi nyie wajinga” kweli mapigo yakakoma, na uzuri wake wakati wana piga risasi akuna polisi aliekuwa ana mkimbiza Lukas, wakiofia kufyetuliwa na wenzao, hivyo Lukas alisha fika mbali, “mme sahau kuwa tupo kwenye eneo la jeshi, tena bila kuwajulisha, ebu rudini kwenye gari haraka, tuka mzungukie kwa mbele” hapo wale polisi walio ongozwa na polisi sajent Idd Kibabu, waka ondoka haraka kuwai kwenye gari lao na kuondoka kabisa eneo lile, wakimwacha Lukas ana tokomea mlimani, huku ana vuta mguu wake wakushoto, ulio chalazwa risasi, pasipo kujuwa kuwa wale polisi walikuwa wana zunguka upande wapili wa mlima hule, yani kule aliko kuwa anaelekea yeye, *******
Joseph Kisona na Koplo Katembo, wakiwa ndani ya ofisi yao wakijadiri report ya uvamizi na mauwaji ya NMC, walisikia mlindimo wa risasi, ambao mala nyingi kwa maeneo ya mjini kama yale usikika wakati wa shabaha, hapo wote wawili kama waliambizana, yani bila kuongea neno, wakatoka nje ya ofisi haraka sana, nakujiunga nawenzao kadhaa, waliokuwa wanatazama upande wa mlimani, kulikotokea milio ya risasi, akiwepo brigedia Fransis  Haule, “Kisona hivi kuna zoezi lina endelea huko juu?” aliuliza brigedia Haule, huku akimtazama Joseph Kisona, wakati huo ulisikia mlio wagari, walio utambua kuwa ni wa land rover 110, likiondoka kwa mvumo mkubwa sana, likionyesha lilikuwa katika speed kali sana, “hakuna taharifa ya zoezi afande, nazani nibola nika angalie” alijibu Kisona, kisha akatazama kushoto na kulia, akamwona mwanajeshi mmoja mwenye nyota mbili, “leutinent (lutein) niletee walinzi watatu wenye bunduki na risasi haraka” alisema Kisona huku ana rudi ndani ya ofisi yake, na kuvuta mtoto wa meza, (wengine wanaita drow) akachukuwa bastora na kuikagua kama ina risasi, kisha akatoka nje, ambako alimkuta brigedia Fransis Haule, akiwa bado amesimama pamoja na kundi la askari, wakiendelea kutazama kule mlimani, japo akuona kitu kutokana na msitu ulio wazinga mbele yao, 
Sekunde chache baadae walioneakana askari watatu wenye bunduki aina ya SMG mikononi mwao, wakiongozana na yule lutein, ambae baada ya kufika alipiga salute, “tayari afande, askari wapo tayari, na kila mmoja ana risasi thelathini” hapo Kisona aka watazama wale askari kwa zamu, kisha aka waambia, “askari wote miguu sawa” nao waka nayua miguu na kukanyaga kwanguvu, wakiwa wamefunga miguu, kisha akawaambia tena, “onyesha silaha kwa ukaguzi” wale askari watatu waka toa mikebe ya risasi (magazine) kwenye bunduki zao na kukoki bunduki zao, kisha wakatulia,  hapo kanal Kisona, kamanda alie pata cheo baada ya kulitokomeza kundi la wahasi, akaanza kutembea kwa kila askari wale watatu, akikagua binduki zao, mpaka lipo wamaliza, kisha aka rudi alipokuwa mwanzo na kusema, “kaa sawa” nao waka weka magazine zao kwenye bunduki na kukaa sawa, hapo Kisona aka sema “tulia” kisha akageuka kijeshi, kutazama upande alipo kuwa brigedia, akapiga salute huku watu wote waliokuwepo eneo lile wakiwa wametulia bila kutikisika, kasolo brigedia peke yake “afande nipo tayari, naomba kibari chako kwenda kuangalia kilicho tokea mlimani” alisema kisona, hapo birigedia alie kuwa ameitikia salute ya kisona kwa kupiga salute, akasema “kibari kimetolewa, kama kuna msaada utaitajika tujulishe malamoja kwa ishara ya kivita” hapo Kisona akapiga salute nyingine, iliyo jibiwa na birgedia zito, kisha aka ligeukia kundi lake, la askari watatu, “nifwate mimi” alisema Joseph Kisona huku akiongoza kuelekea ndani ya msitu, ******
Mida hii Erasto Richard Misago au bwana harusi mtarajiwa, alikuwa ndani ya jumba lao kubwa la kifahari, lililopambwa na vitu vya thamani huko Luhuwiko, amekaa kwenye kiti mbele ya meza kubwa, kwenye ukumbi wa chakula, (dianing room), akitazama chai na vitumbua, vilivyokuwepo mezani, kama unge mwona, ungezani kuwa anatazama udongo au kitu cha ovyo pale mezani, “wewe mtoto, mbona auli, unakitazama tu chakula?” aliuliza mama Erasto mke wa bwana Richard, aliekuwa anatokea chumbani kwake, akiwa amevalia mavazi yaliyo ashilia kuwa alikuwa anamtoko flani, huku akiweka hear ring, masikioni mwake, “naona aipandi kabisa, alafu haya mavitumbua ndio kabisaaa” alijibu Erasto, kwa sauti ya kichovu sana, ikiashilia bado anauchoovu wa jana usiku, na ukizingatia, amerudi asubuhi hii, “mipombe hiyo ya usiku kucha, subiri uoe, ukamsumbue Mona, kukuandalia supu kila asubuhi” alisema mama Erasto, huku ana pekua kutafuta funguo za gari, “Mwanaaa” aliita mama Erasto, “abee mama” aliitikia dada wakazi kwa sauti yenye rafudhi ya kimakonde, huku anakuja mbio sebuleni, na kusimama akimtazama boss mama wake, aliekuwa bado anatafuta funguo za gari, “ebu pasha ile nyama jikoni kisha umwekee huyu mlevi supu” alisema mama Erasto, na binti Mwanaheri alikimbilia jikoni, kufanya alicho agizwa, akimwacha mama Erasto anaendelea kuchambua vitu juu ya fliji kutafuta funguo za gari, alipozipata aka mtazama mwanae, “mimi na mpitia mama Mona tunaenda mjini, na wewe usisahahu kwenda kununua zawadi za mchumba wako, pia upitie pete pale sonara” alisema mama Erasto kisha akataka kutoka nje, lakini kama kuna kitu alikumbuka, akamtazama tena mwanae, “alafu uwe makini na matembzi yako, si umesikia ujambazi uliotokea hapo NMC jana usiku?” alisema mama Erasto, kisha pasipo kusubiri jibu la mwanae akaondoka zake,
Erastor alisikiliza mpaka alipo sikia mlio wagari, aina ya Suzuki, umetoweka ndipo aka inuka toka kwenye kiti, na kwenda jikoni, ambako alikmkuta mwanaheri binti wa kimakonde, mwenue umri wama miaka kumi na nane, akiwa ana endelea na upashaji wa mboga kwenye jiko la umeme, akamtazama maeneo ya mgongo huku akishusha macho mpaka kwenye makalio, yalio jaa kahasi, huku gauni lake jepesi  kuu kuu, likionyesha wazi, kuwa binti huyu akuwa amevaa nguo ya ndani, maana muda wote gauni ilikuwa ainazama na kunasa katikati ya makalio, zamani walikuwa wanasema deki ina kula mkanda, ila ukweli ni kwamba Erasto anaijuwa vyema tabia ya Mwanaheri, ambae ana miezi sita tu! tokaanze kazi hapa kwao kitokea Nanyamba huko mtwara, juu ya uvaaji wa nguo hito yandani Erasto, alimtazama Mwana kwa sekunde kadhaa, mpaka binti huyu alipo geuka na kumtazama Erasto huku akitabasamu, “mbona una nitazama sana, wakati sikuhizi umenisusa?” alisema yule binti wakazi, kwa sauti yenye rafudhi ya kimakonde, Erasto akatabasamu kidogo, “kwani umetamani?” aliuliza Erasto kwa sauti iliyoambatana na mikwaluzo ya hang over, “hiiiii! hapana sijatamani, lakini ukitaka sikunyimi”  alisema Mwanaheri, huku anacheka cheka, hapo Erasto akachekelea kidogo, “poa ngoja nile kwanza” alisema Erasto, kisha akarudi sebuleni na kuwasha tv, kisha akajilaza juu yakochi, akitazama music, Erastor mwenyetabia ya kutembea na wafanya kazi wandani mwao, alikuwa amerudi nyumbani masaa mawili yaliyo pita, akitokea maji maji hotel, alikuwa amelala leo na mpenzi wake Happy, anae fanyia kazi hotelini hapo, “lakini Mwana ana vino flani hivi, wacha nika mgonge kabla sijaenda kutafuta zawadi za Mona” aliwaza bwana harusi mtarajiwa. *****
Baada ya kupanda mlima mpaka kileleni, huku akindamwana na maumivu makali sana yaki mchamanda, kwenye mguu, ulio kuwa una vuja damu maeneo ya paja, yaki msahaulisha yale maumivu yakwenye bega, Lukas akasikaka na kutazama pende zote nne, akiuna mji mzima wa sogea, na vitongoji vyake, unaweza kusema nikama alikuwa ana tazama google map, kwa njia ya settlite, Lukas aliweza kuona gari la polisi likielekea barabara kuu na mwisho kukata kona kulia na kuikamata barabara hiyo ienday mikoa ya iringa na mbeya, aliendelea kulitazama lile gari lililo endambele na ukata tena kulia likiuzunguka mlima, “hawa majambazi wakubwa, alafu wanajifanya  polisi” alisema Lukas, kwa sauti iliyo ambatana na maumivu makali yaliyo mkabili, huku ana badili uelekeo na kushuka ubavuni mwamlima huo, akilenga upande wa bombambili, sehemu ilipo nyumba yake, ****
Seed farm ya mwaka 1997 ilikuwa na nyumba chache sana, zilizo kuwa zina kaliwa na wenyeji, huku maeneo mengi yakitawaliwa na vichaka mapori ya wastani na nyumba chache zilizo kuwa zina jengwa, na pembezoni mwa mtaa huu wa seed farm upande wa luhuhila, ndipo nyumba ya mzee Mbogo ilipo, tokea asubuhi ya leo mzee Mbogo alikuwa mwenye pilika pilika nyingi sana, ukiachilia kuliandaa gari lake, aina ya land rover 109, alilo linunua baada ya kustaafu utumishi ndani ya jeshi la ulinzi, malanyingi ukiona hivyo, ujuwe kuwa kuna safari itafanyika hivi karibuni,
Sasa mzee Mbogo alikuwa ndani ya chumba kimoja kikubwa, chenye makolokolo mengi sana, yaliyo jaa, pamoja vitu vingi vilivyo tandwa na vumbi na buhibuhi, kuonyeshakuwa chumba hiki uwa akingaliwi mala kwamala, mzee huyu mwenye mwili wenye nguvu, kutokana na mazoezi aliyo kuwa ana yafanya toka kipindi akiwa jeshini, na kila siku asubuhi, alitazama kwenye ukuta za chumba kile, ambazo zilionekana zikiwa zimening’iniza vitu mbali mbali, pamoja na bunduki kadhaa za kuwindia, aka tazama akizunguzusha macho, mpaka alipo gota kwenye silaha moja yakizamani, kama zile nyingine zote, lakini hii ilikuwa ni aina ya hunting sniper rifle, Eric Mbogo aliitazama kidogo ile bunduki kisha aka tabasamu huku anaiendea ile bunduki na kuichukuwa, ilikuwa ime tapakaa vumbi jingi na buhibuhi, akaikoki kwanguvu sana, nayo ikajikoki na toa vumbi jingi, lililo twanyika mle ndani, kama vile kuna mtu amekung’uta fuko la unga, 
“kho! kho! kho! baba Eddy bwana, uta niua na hilo vumbi” ilikuwa sauti ya mke wake, iliyo sababishia mzee Mbogo ajuwe kuwa mke wake, alikuwa ameingia humu ndani ya chumba hiki, bila tahalifa yoyote, “hooo! kumbe cha kimbelembele ume ingia” alisema baba Edgar, huku anacheka kidogo, na kugeuka kumtazama mke wake, alie kuwa amevalia gauni zuri la kitenge, akionyesha kuwa alikuwa na mtoko, “unazani utani, utaniuwa mwenzio bwana” alilalamika mama Edgar, huku akimsogelea mume wake, “kwahiyo umeshindwa kunisubiri nikupeleke? maana naona kama tayari umesha jiandaa” aliuliza baba Edgar akiwa bado ameshikilia bunduki, “nimeona bola ni tangulie nikazunguke madukani, alafu wewe utani kuta pale maduka mapya, karibu na kwa sonara, mtaa wa Zanzibar, nitakuwa nimesha nunua kila kitu” alisema mama Edgar, ambae uso wake ulitawaliwa na tabasamu languvu, muda wote, “ok! basi acha mimi nifanye mambo yangu taratibu, mpaka mida ya saa saba ndio nitaanza kuja, maana nataka Edgar akija kesho, apumzike kwanza, alafu keshokutwa jumapili, tuelekee” alisema baba Edgar, akimanisha kuwa ilikuwa ni safari ya kwenda kuwinda, 
Kamanda mstaafu Eric Mbogo, akaagana na mke wake, ambae leo hii aliamua kwenda mjini ununua maitaji ya familia yake, pamoja na vitu flani flani, kwaajili ya kumpongeza mwanae Edgar, alie maliza chuo, akiwa ndie mtu wakwanza kuitimu helimu hiyo katika ukoo mzima. (pengine ni utani)
Mle store alibakia baba Edgar peke yake, ambae aliishika na kuitazama sana ile Hunting Sniper Rifle, huku tabasamu likianza kujijenga taratibu usoni mwake, kufwatia picha iliyo mjia ikiwa ni kama kumbukumbu flani, ya miaka mingi iliyopita, wakati Edgar alipo kuwa anaanza kuelewa kuitumia bunduki ile, baada ya mze huyu kumfundisha kwa muda mrefu, mzee Mbogo alizidi kukumbuka siku moja, jinsi mwane alivyo mwonyesha mahajabu ya ulengaji wa shabaha, ni baada ya kuwapiga swala watatu, waliokuwa wana kimbia pamoja, akitumia risasi tatu, kwa risasi moja swala mmoja, walio kuwa katika mwendo, wenyewe wanaita, fire in movement, “safari hii kijana, nataka unionyeshe kuwa hupo vizuri zaidi kwenye urengaji” alijisemea mzee Mbogo, huku ana iweka mezani ile bunduki ya uwindaji, na kuanza kuifungua kifaha kimoja baada ya kingine, moyoni alijivunia wazo lake la kumkeep busy mwanae huyu, akizamilia kumwepusha na majanga ya watoto wa kike, asa baaada ya kusababisha mtafaluku mkubwa sana, miaka yanyuma, kwa jirani yake bwana Anderson, itaendelea KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI)

Mle store alibakia baba Edgar peke yake, ambae aliishika na kuitazama sana ile Hunting Sniper Rifle, huku tabasamu likianza kujijenga taratibu usoni mwake, kufwatia picha iliyo mjia ikiwa ni kama kumbukumbu flani, ya miaka mingi iliyopita, wakati Edgar alipo kuwa anaanza kuelewa kuitumia bunduki ile, baada ya mze huyu kumfundisha kwa muda mrefu, mzee Mbogo alizidi kukumbuka siku moja, jinsi mwane alivyo mwonyesha mahajabu ya ulengaji wa shabaha, ni baada ya kuwapiga swala watatu, waliokuwa wana kimbia pamoja, akitumia risasi tatu, kwa risasi moja swala mmoja, walio kuwa katika mwendo, wenyewe wanaita, fire in movement, “safari hii kijana, nataka unionyeshe kuwa hupo vizuri zaidi kwenye urengaji” alijisemea mzee Mbogo, huku ana iweka mezani ile bunduki ya uwindaji, na kuanza kuifungua kifaha kimoja baada ya kingine, moyoni alijivunia wazo lake la kumkeep busy mwanae huyu, akizamilia kumwepusha na majanga ya watoto wa kike, asa baaada ya kusababisha mtafaluku mkubwa sana, miaka yanyuma, kwa jirani yake bwana Anderson, itaendelea baadae...., endelea kufwatilia mkasa huu hapa hapa Hadithi ZA MBOGO EDGAR ..., endelea kufwatilia mkasa huu hapa hapa Hadithi ZA MBOGO EDGAR
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni