KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI) SEHEMU YA02

KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI)

SEHEMU YA PILI

STORY NA Mbogo Edgar.

ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA, hapo Lukas akajuwa kuwa swala hili halikuwa na chembe ya mambo ya kijeshi, wala utani, ila huu ni uvamizi wa watu ambao wamejifanya kuvaa mavazi ya polisi, yani hivyo ndivyo alivyo amini Lukasa, hivyo akaona kuwa ule mkanda anao record ni chanzo kizuri cha kuwakamata majambazi hawa, Lukas aliendelea kuchukuwa tukio pasipo kujuwa kuwa anajiingiza kwenye matatizo, na ukichukulia mahali hapa palikuwa mbali na makazi ya wananchi, itaendelea saa tatu usiku usiku. ENDELEA..........
Akiwa anatetemeka kwa uoga, Lukas aliejibanza kwenye uambaza wa ukuta wa moja ya majengo makubwa pale NMC, alishuhudia wale askari wengine wanne waliobakia, wakitaaruki na kuanza kutimua mbio, kila mmoja na upande wake, lakini aikuwasaidia, maana wale askari saba waliotumia vyema SMG zao, zilizo kooa na kutema vitu maka miali ya moto, hapo Lukas alie endelea kuchukuwa tukio lile, alishuhudia wale askari wanne wakiangua chini, kama vifurushi vya pamba, ukweli Lukas akuelewa maana ya tukio hili, la kuogofya, maana ukiachiia kuwa ni mala yake ya kwanza kuona mtu akipigwa risasi, pia kilicho mchanganya ni kwamba, walikuwa ni polisi kwa polisi, ambapo aliwaona wale polisi saba wakickuwa mikebe ya risasi kwenye gari na kuiweka kwenye bunduki za wale walio wauwa na kukuchukuwa ile mikebe ya risasi za bandia.
Lukasi Benjamin, aka mwona mmoja kati ya wale polisi saba, akilisogelea lango kubwa la Benk ya hifadhi ya rasimali vitu, na kuufyetulia risasi sehemu ya kufuri, la mlango huo mzito wa chuma, kisha aka litoa kufuri, na kujaribu kulivuta lile lago kubwa la chuma, hapo Lukas akawaona mlango wa kushoto wa lile gari aina ya Land Rover one ten, ukifunguliwa akashuka mmtu mmoja alie valia koti jeusi refu mpaka magotini, na kofia pana sana ya duara, kipindikile walikuwa wanaita Kanda bongo man, Lukas aliendelea kuchukuwa tukio lile, ambalo bado alikuwa anahisi kuwa ni maiizo, kutokna na mambo aliyo kuwa anashuhudia, akamwona yule mtu ambae mwili wake ulionekana mpana na ulii tanguliwa na kitambi, akisogea pale mlangoni, akatazama kwa sekunde kadhaa kisha akazama ndani, akifwatiwa na askari wa tano, wawili wakibakia nje ya jengo lile, mmoja akatazama upande wa kushoto, mmoja kulia, nikama walikuwa wanatazama kama kutatokea mtu yoyote kuja eneo lile, muda mfupi baadae wakaonekana wale askari walio ingia ndani wakitoka na mabox yachuma, haraka haraka, wakiwa wameyabeba kwa kwa kusaidizana, wawili wawili, na kwenda kuyapakiza kwenye gari, kisha kurudia tena ndani na kuchukuwa mengine, hapo Lukas akatamani kuona vizuri yale mabox, ndipo lipoizoom ile video camera yake, Naam sasa aliweza kuona mabox ya shaba, yanayo ng’aa yakiwa yanapakizwa kwenye gari, huku watu hao wakionekana vizuri kabisa kwenye Camera ya bwana Lukas, kihasi cha kuwatambua kwa sura zao, endapo ungetazama vizuri kwenye screen ya video.
Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana, kilicho tumia dakika zisizo zidi tatu, tayari walikuwa wamesha maliza, ata yule jamaa alie valia koti refu jeusi, alitoka mle ndani ya jengo la benk ya hifadhi, alafu wote waka ingia kwenye gari na kuondoka zao, huku Lukas akiendelea kuwa chukuwa na video camera yake, lakini walipo ikamata barabara kuu, akawaona polisi wale wakikata kona kuelekea kushoto, upande wa magharibi mwa mkoa wa Ruvuma, wakiacha kuelekea kulia, yani songea mjini, hapo ndipo tatizo lilipo anzia, maana wakati wana kata kona ndipo walipoonekana wakisimama ghafla, na kushuka kwenye gari, ikonyesha kuna kitu walikiona, Lukas akujuwa kwanini watu hao wame simama ghafla, hivyo aka waza kwenda kushuhudia, hapo Lukas kwa umakini mkubwa sana, aka zunguka upande ule ili ajionee kilicho wasimamisha wale wauwaji waliovalia mavazi ya kipolisi, lakini safari hii alipitia kwenye vichaka virefu, akiwa na Camera yake mkononi, baada ya kupata sehemu nzuri ya kujibanza, ikiwa ni mita kama 50 toka pale lilipo simama gari, aliweza kuwaona wale polisi wakiisogelea baiskeli yake iliyokuwa kiambazani nakulifungua begi, ambalo alikuwa ameliacha juu ya kitako cha baiskel, wakatoa camera, akaona mmoja wao akipeleka camera na begi kwa yule jamaa, aliekaa mbele ya gari, alie onekana kuwa ndie mkubwa wao, sijuwi alimweleza nini yule askari, maana ghafla yule askari akaonyesha ishala kwa wenzie, kuwa wazunguke lile eneo na kulipekuwa, maana kuna dalili ya kuwepo mtu eno lile, hapo Lukas akajuwa akukuwa na usalama kwake, maana aliwaona wale jamaa alio wahisi kuwa siyo askari, kama wanavyo onekana, wakianza kuzagaa eneo lile kutafuta kitu flani, nasiyo kitu kingine ni yeye mwenyewe ndie anae tafutwa, na mbaya zaidi aliona jamaa wawili wakija upande aliokuwa yeye, 
kitendo bila kungoja ushahuri, Lukas akaifungua ile Camera yake, na kutoa tape record iliyo kuwepo ndani yake, na kuishika vyema mkononi, akiibana kwanguvu sana, akiiacha ile camera pale chini, na pasipo kujari nyaraka zake zilizopo kwenye begi alilo liacha kwenye baiskeli, pamoja na kitambulisho chake, bwana Lukas akaanza kuondoka taratibu na kwa kunyata, akizama porini,  “jamani ebu njooni huku muone hii” Lukas alisikia mmoja wa wale jamaa, akiwaambia wenzie, hapo akawaona wengine wawili wakisogea pale alipoiacha camera yake ya video, wakiwa na yule mmoja alie kuwa na huyu alie ongea jumla waka wanne, akawaona wana itazama ile video camera yake, atakuwa maeneo aya aya” aliongea mmoja wao, akiwasha tochi na kumulika mulika eneo lile, huku akielekeza mwanga wa tochi upande alipo Lukas, mwingine akapaza sauti, “jamani njooni huku atajuwa maeneo haya, apatikane auwawe mala moja” hapo kijana Lukas akaona mahali hapa siyo pakushangaa, maana kwa aliwaona wale jamaa wote saba wakikusanyika na kuanza kuzagaa eneo lile wakija upande alipo kuwepo yeye, huku mianga ya tochi kitangulia, japo aikuwa ime mlenga mpja moja kwa moja, ila kijana Lukas alijawa na uoga mkubwa sana hivyo akujiuliza mala mbili, Lukas akachomoka kwa mbio za hajabu, mbio zilizo wagutua wale wale jamaa ambao wakujiuliza mala mbili, wakaanza kufytua risasi, kuelekea upande ambao Lukas Benjamin, alikuwa ana kimbilia, kwa lugha nyepesi risasi zilimfwata Lukas, ambapo zililindima mpaka zilip koma zenyewe, zikimaanisha zimeisha kwenye magazine, (mikebe yake), ndipo wale jamaa ambao kimtazamo ungesema ni askari wapolipo kimbilia ukufwata uelekeo aliokimbilia Lukas, huku mmoja wao akitumia torch kuangazaia mapori na vichaka, “jamani naona damu” alisema yule mwenye torch, na wenzie wakaenda kuangalia pale alipoonyesha mwenzao, “inaonye tumemtandika risasi, eu mtafuteni tuupate huo mkanda, maana akiufikisha sehemu nyingine tume umbuka” alisema mmoja wao huku wakitawanyika, na kuendelea kumtafuta kijana Lukas, kwa kufwata mchilizi ya damu,
Yote kwa yote wale jamaa licha ya kuona damu ambazo walizi fwatilia, lakini awakuweza kumwona kijana Lukas, ata alama ya damu ilipo koma, Lukas  akuonekana. ******
Usiku huo huo mjini Mbeya, katika chuo cha usimamizi wa fedha, ndani ya chumba kimoja kati ya vyumba vingi vya bweni la Uhuru, moja ya bweni kati ya mabweni mengi ya chuo hiki kikubwa, katika ukanda wa nyanda za juu kusini na mikoa ya kusini kwa ujumla, alionekana kijana mmoja, alie jilaza juu ya kitanda kimoja cha juu, kati ya vitanda vinne vilivyomo ndani ya chumba kile, kwa maana ya dubble deck, kijana huyu tofauti na wenzie watatu walio kuwepo mle ndani, alioneka kuwa na mawazo mengi sana usiku ule, kihasi cha kuto kujiunga na wenzie hao, waliokuwa wanapiga porojo, kwa sauti kubwa na kusababisha kelele ndani ya chumba kile, na gumzo ilo liliusu umalizaji wa mitihani ya mwisho ya chuo, na safari watakazo zifanya kuelekea makwao, baada ya mahafari yakayoanza kesho sanne, 
“sijuwi kwanini huyu demu anitoki kichwani?” alijiuliza kijana huyu, alikuwa bado amejilaza kwenye kitanda chake, nikweli huyu kijana alikuwa anawaza juu ya binti mrembo sana pale shuleni, ambae kila mmoja ana mfahamu binti huyo, siyo kwa uzuri wake tu!, ila pia kwa ubora wake katika masomo, na na jinsi binti huyo alivyo jitunzia heshima pale chuoni, maana hakuwa na kashfa yoyote pale chuoni ata mtaani, kwa muda wote, wa miaka mitatu aliyo kuwepo pale chuoni, japo wanaume wengi wakila aina, wana chuo wenzake, wakufunzi, ata watu wa mtaani, walijaribu kumfukuzia mwanamke huyo, wakitumia vishawishi vya fedha, lakini mwanamke huyu akuonekana kushawishika ata kidogo, unajuwa kwanini mdau?, sababu huyu binti ni mtoto wa tajiri Anderson, akuwa na shida ya fedha ndogo ndogo, na mbaya zaidi alikuwa ana mchumba wake, mtoto watajiri mwenzao ambae ni family friend, yani Erasto Richard Misago, wa huko huko mkoa wa Ruvuma, huyu binti anaitwa Monalisa Anderson, binti wa miaka 22, “khaaa! niujinga huu, yani miaka yote hii, na muwaza mschana mmoja tu!” alisema kijana huyu ambae bado alikuwa kitandani, unaweza kujiuliza kwa nini kijana huyu ana muwaza Monalisa, na utashangaa nikikuambia kuwa kijana huyu licha ya kuumia moyo wake kwamuda mrefu, akiliwaza penzi la Monalisa, lakini toka alipo kutana na Monalisa kwa mala nyingine hapa shuleni, miaka mitatu iliyopita, hakuwai kumtongoza tena, na hii ni kutokana na mambo yaliyowai kutokea zamani, yani miaka kumi na moja iliyopita, na haikutokea ata kusimama nae angalau kwa dakika ata moja, zaidi ya kusalimiana, kama watu wanao fahamiana toka utotoni, huku wanapishana.
Kijana huyu anaitwa Edgar Eric Mbogo, wenzie walipenda sana kumwita dubble E, asa kwa kipaji chake cha uchoraji na kucheza mpira wa kikapu, kijana huyu mwenye miaka 22, ni mtoto wa bwana Eric Mbogo, mwanajeshi mtaafu wa jeshi la ulinzi, Edgar licha ya kuwa maarufu pale shuleni na kushobokewa na wanafunzi wenzake wakike, kutokana na umahili wake katika uchoraji wa michoro mbali mbali, na uchezaji wa mpira wakikapu, akiwa firist five, (list ya kwanza) katika timu ya shule, sifa nyingine ya kijana huyu, ni kwamba alikuwa mcheshi kwa kila mtu, lakini usiku waleo alkhamis alionekana kuwa mwenye mawazo mengi sana juu Monalisa, Edgar alikumbuka zaidi ya miaka kumi na mbili iliyopita, kipindi hicho walikuwa wanakaa pamoja mtaa wa seed farm A, jirani jirani kabisa na wakina Monalisa, au Mona kama wengi walivyo kuwa wana muita, kipindi hicho walikuwa darasa la nne, shule ya msingi matogoro, wawili awa walikuwa marafiki waubwa sana katika michezo ya utotoni, mpaka michezo ya pamoja ilipo koma, kipindi cha likizo ya mwezi wa sita, huku Edgar akijiona ndio sababu ya wakina Monalisa kuhama seed farm, na ndio mwisho wa urafiki wao, nasiyo tu kupoteza urafiki na Monalisa, pia tukio hilo lilimwachia Edgar kilema cha kushindwa kutongoza mwanamke, yeyote, ambae ni mzuri, japo kichwani kwake alikili kuwa akuwai kuona mschana wa kumfikia Monalisa, kwa sifa tabia na uwezo alionao, “jamani mbona leo simsikii Edgar, au anaumwa?” aliuliza mwanafunzi mwenzao mmoja, kati ya wale watatu waliokuwa wanaongea ndani ya kile chumba.****** 
Wakati Edgar ana waza hayo, usiku huo huo, ndani ya maji maji hotel, katika kati ya mji wa songea, ndani ya chumba kimoja tulivu na cha gharama kubwa, alionekana kijana mmoja mmoja mtanashati, akiwa na binti mmoja mrembo, alie valia sale za wahudumu wa hotel ile ya maji maji, ambzo ni kisketi kifupi cheusi, na shati jeupe lililo kuwa limesha funguliwa vishikizo vyote, na kuachia wazi sehemu yote ya mbele, yani kuanzia tumboni mpaka kifuani, ata manyonyo ya liyo anza kulegea ya mwanamke huyu, yalionekana wazi, mrembo huyu mhudumu ambae nywele zake alikuwa ameweka lelax, alikuwa amekaa kwenye mapaja ya kijana huyo mtanashati, (yani amepakatwa) aliekuwa amkaa kwenye kochi lenye mapilow, manene na mazuri, (kipindi hicho yalikuwa ndio makochi ya kisasa) wawili awa walikuwa wakinyinyana ndimi zao, huku mkono wa kijana mtanashati ukichezea manyonyo ya mschana huyu, huku mezani ilionekana chupa ya pombe kali, na grass mbili zenye pombe nusu kila moja wapo, na pembeni ya chupa hiyo kulikwa na paketi la sigara na kiberiti, wakati wawili awa wanaendelea na kupea juice hiyo yapekee, mala yule mwanamke akajitoa mdomoni kwa kijana mtanashati, “inamaana akija huyo mchumba wako, ndio utani acha?” aliuliza yule mwanamke kwa sauti flani ya kunyongea, yule kijana mtanashati akatabasamu kidogo, huku anainua grass mezani, na kuisogeza mdomoni, aka piga funda moja ngumu, kisha akarudisha grass mezani, “Happy usiwe na wasi wasi, yeye ana muda wake na wewe una muda wako” alisema yule kijana mtanashati, huku ana peleka tena mkono kwenye ziwa la huyu dada anae itwa Happy, ambae alitabasamu kidogo, “mh! unasema tu! lakini kipya akinyemi” alisema Happy huku ana inuka toka kwenye mapaja ya kijana mtanashati na kusimama, pembeni kidogo, 
“kipya kivipi, wakati namfahamu miaka na miaka, toka tukiwa wadogo” alisema yule kijana mtanashati, huku ana chukuwa paketi la sigara mezanina kuitoa moja, kisha akarudhisa mezani, akibakia na sigara moja aliyoipeleka mdomoni, kisha akachukuwa kiberiti pale pale mezani, “mh! wakati uliniambia kuwa mwanamke mwenyewe bikira” alisema Happy huku ana livua lile shati, ikionyesha kuwa atoenda tena kuhudumia, “nikweli, lakini bikira yake ndio nini, tena kumvesha pete siyo ndio kulala nae, yani tumekubaliana mpaka tufunge ndoa” alisema kijana yule mtanashati, huku ana washa sigara, hapo Happy alicheka kidogo, “hahahahahaha!, ila nyi wana ume mnatufanya sie wajinga sana, wakati bibi harushi amekutunzia bikira yake, wewe una faidi uchi tu!” alisema Happy huku ana malizia kuvua sketi yake, na kubakia na chupi, nikweli huyu mhudumu akuwa ana mpango wa kurudi kazini, sababu siku zote mpenzi wake huyu anapokuja, uwa anaongea na manage wa hotel hii, akimpatia na fedha kidogo, ili amwachie wakafanye yao, kitu ambacho Happy alikuwa akijuwi nikwamba, kijana huyu alikuwa anafanya hivyo, katika bar nyingi alizo kuwa anaenda, na alikuwa ana mwanamke karibu kila bar kubwa hapa mjini, Huyu anaitwa Erasto Richard, bwana harusi mtarajiwa, ndie mchumba wa Monalisa Anderson,***** 
wakati Erasto ana kula raha na binti Happy ndani maji maji hotel, binti mrembo Monalisa Anderson alikuwa ndani ya chumba, kimoja cha bweni la mapinduzi, pamoja na wascha wenzie watatu, wakiongea mawili matatu, kila mmoja akiwa na shughuli zake, “Mona wenzio tukipata gari kesho naondoka” alisema Stella rafiki mkubwa wa Monalisa, akiwa anamalizia kufunga begi lake, na kuliweka kwenye kabati la kuifadhia mabegi, “mi wenzio sipendi kulala njiani, tungeondoka wote mkaniache makambako” alijibu Monalisa ambae pia alikuwa ana iweka vizuri uniform yake, ambayo ataitumia kesho, kwenye mahafari ya kumaliza chuo, “ila wewe ingekuwa vizuri ungeenda kulala makambako, sababu kesho kutwa mapema unaingia songea, kwaajili ya ile sherehe yako” alishauri Stella, ambae sasa alikuwa anapanda kwenye kitanda chake, hapo Monalisa akatulia kidogo, kama kunakitu alikuwa anawaza, kisha aka inua kichwa kutazama vitanda vya juu, yani aliwatazama wale wengine wawili, ambao walikuwa busy wana soma vitabu vya simulizi, toka kwa mwandishi, E. Mbogo, wa hadithi za mbogo Edgar, kisha akatabu kidogo, kama vile alijilazimisha, hapo Stella akahisi jambo, jambo ambalo uwa analihisi kila siku kwa mwenzie kuhusiana na huyo mchumba wake ambae anatarajia kuveshwa nae pete ya uchumba, siku chache zijazo,
Monalisa alimaliza kuweka nguo zake kwenye kining’inizo, (hanger) na kulisogelea bag lake kubwa la nguo lililo lala kitandani, likiwa wazi, huku ndani yake likionekana kuwa, limepangwa vizuri sana, tayari kwa safari, Mona lisa akaingiza mkono wake ndani ya begi hilo, akiupenyeza kwenye mfuko wa pembeni, akaibuka na mfuko wa karatasi ngumu ya kaki, ambayo nikama ndani yake kulikuwa na kitu laini, aka utazama ule mfuko kwa dakika kadhaa, kama vile anajishuri, afungue au asiufungue, baada ya kuwaza kwa dakika chache aka ishia kutabasamu huku akiurudisha ule mfuko kwenye begi lake, kisha aka chukuwa kibegi kidogo cha mgongoni, chenye kila dalili ya kuwa ni kibegi  cha kike, chenye rangi ya pink, ambacho ndani yake ilionyesha akukuwa na kitu kikubwa, kabla haja fungua kile kibegi chake, ambacho kama ni matumizi ya shule ungesema ni cha mtoto wa darasa la kwanza, kwa ukubwa wake, Monalisa aligeuza shingo yake na kuwatazama wenzie, aka gongana macho na Stella, “wewe ujalala tu” alisema Monalisa, binti amba urembo wake una wafanya ata waschana wenzie watamani kuwa kama yeye, “nita lala je wakati rafiki yangu bado ujalala?” alitania Stella, huku akimtazama Monalisa alie ghaili kufungua kile kibegi cha mgongoni chenye mikanda mirefu, aka kirudisha kwenye begi kubwa na kulifunga, “ndio basi tena, maana kutembeleana hapo kwa bahati mbaya” alisema Monalisa, akimaanisha baada ya kumaliza chuo, huku ananyayua begi lake na kuli weka kwenye makabati ya kuifadhia mabegi, “tutaonana tu mwaya, kwanza nitakuja kwenye harusi yako” hapo nika Stella alifanya makusudi, ili kuthibitisha jibu la swali lake, akamwona Monalisa akisimama na kutazama chini kwa sekunde kadhaa, kama anawaza jambo flani *******
Saa nane usiku, pembezoni kabisa mwa barabara kuu iendayo ya makambako, maeneo ya bombambili, alionekana kijana Lukas akitembea kwa haraka, huku akiwa amejishilia kwenye bega, sehemu ambayo ilionekana ikiwa inavuja damu, ambazo zilianza kukauka, huku kwenye kiganja cha mkono huo ulio umia akionekana kuufumba kwanguvu, akiikamana ile tape ya video aliyo ipiga kule NMC, huku akinusulika kuuwawa na watu wale walio valia sale za jeshi la polisi, na wakitumia gari la polisi,
Lukas Benjamin alitembea huku akionekana kuwa na wasi wasi  mkubwa sana, maana alitembea huku mala kwa mala, akitazama kushoto, kulia na nyuma, kuona kama kuna mtu au gari, ambali lina mfwata, asa akilinge maadui zake, ambapo huko alikotoka aliliona gari lao mala kadhaa, likizulula mitaani ni wazi lilikuwa lina msaka yeye, sasa kijana huyu ambae toka kule luhuwiko, alitembea kwa kujificha sana, mpaka alipo fika hapa bombambili, alitembea kwenye barabara, hii kubwa iendayo mikoa ya iringa mbeya, mrogoro na dar es salaam, na baada ya mwendo wa mita nia mbili aka chepuka upande wa kulia na kuzama mtaani, akizidi kutokomea, akielekea upande wa milima wa chandamali, huku mala kwa mala akitazama kilekiji mkanda kidogo cha video, alicho kitoa kwenye video Camera yake, huku wazo lake likiwa ni kukipeleka kituo cha polisi kesho mapema sana, ilikuwezesha polisi waweze kuwakamata wale majambazi, 
Lukas alitembea kwa mwendo wa dakika kumi na tano, sasa alikuwa amekaribia kuumaliza mtaa wa bombambili, akiwa amefikia kwenye safu ya nyumba za mwisho kabisa, za mtaa huu, zilizo paka na msitu wa mlima wa chandamali, uliopo ndani ya mipaka ya eneo la jeshi la ulinzi, hapo Lukas aka tembea kwenye safu ya nyumba zile za mwisho za mtaa ule, mpaka alipo ifikia nyumba moja ndogo ya vyumba viwili,  aka anza kujipapasa mfukoni, hapo akaachia zinga latusi languoni, nikwamba funguo za nyumba ile alikuwa ameziweka kwenye lile begi alilo liacha kule NMC, hapo Lukas akalishika kufuri na kulitazama kidogo, kisha akaliacha na kuzunguka nyuma ya nyumba yake, ambako akuchelewa akarudi akiwa amebeba kipisi cha nondo, ambacho alitumia kutenganishia lile kufuri,
Akiwa ndani ya chumba kimoja wapo cha ile nyumba, Lukasi akiwa amewasha taa ya kandiri, alijifanyia huduma ya kwanza, ikiwa ni kujisaafisha kidonda, kilicho sababishwa na mkwaluzo wa risasi, moja, kati ya nyIngi zilizo mkosa kosa kule NMC, hiyo moja ikimjeruhi begani, baada ya lisaa limoja kijana huyu alimaliza kujifanyia matibabu, ikiwa na kufunga kile kidonda kwa vitambaa, vilivyo patikana baada ya kuchana moja ya shati lake, na ndipo alipo jilaza kitandani, huku akiwaaza juu ya hatima yake, endapo wale jamaa wata mtambua kuwa ni yeye, na kuamua kumfwatilia, wazo jema aliona ni kwenda kutoa taalifa kituo cha polisi kesho mapema sana,***** 
Wakati yeye bwana Lukas akiwaza hayo, usku ule ule, mtaa wa mahenge A, ndani ya nyumba moja kubwa sana ya kifafahari, yalionekana magari kadhaa ya kifahari, kipindi hicho, pamoja na gari la polisi, yakiwa nje ya uwanja wa nyumba ile kubwa iliyo zungukwa na ukuta mkubwa sana, huku vijana kdhaa walio valia sale za jeshi la polisi, wakionekana pale nje karibu ya lile gari la polisi, “kazi nzuri sana tumeifanya, lakini tatizo ni huyu bwana Lukas Benjamin, lazima tufanye jambo, na kuipata ile tape kisha kummaliza kabisa, kwa kufuta ushahidi” ilisikika sauti toka ndani ya nyumba hiyo, “lakini mkuu, hapo inabidi kwanza tumpe kesi yeye, ili itusaidie kumwanga miza kilahisi, maana wengi watajuwa kuwa ni mmoja wa majambazi alie usika na mauwaji yale” alishauri mwingine, na wote waliokuwa mle ndani wakaunga mkono, wakipanga kesho kufanya kazi hiyo na kueneza propagander juu ya kijana Lukas, ili aonekane kuwa ndie alie fanya mauwaji kule NMC, ushaidi ukiwa ni bahadhi ya vifaha na vitamburisho vyake vilivyo kutwa eneo la tukio.********
Ijumaa asubuhi, Kijana Lukas aliamka mapema sana, lakini alichelewa kutoka nyumbani kwake, alitoka saa mbili, akiwa na kipochi chake kidogo alicho funga kiunoni, ambacho ndani yake kulikuwa na, fedha elfu kumi na tano, na  kile kimkanda cha video, kijana Lukas akiwa amevalia suluali ya kitambaa, na tisheti, huku chini akivalia raba, alitembea taratibu, akijikaza asisikie maumivu ya bega lake lililo jerhuiwa na risasi, ambalo aliamini kuwa, baada ya kuifikisha ile tape kituo cha polisi, angeweza kwenda kutibiwa, maana angeweza kupata PF 3,
Kijana Lukas alipanda daladala kwenye kituo cha daladala  cha sanga one, safari ya kuelekea kituo mjini ikaanza, maana lengo lake ni kupeleka, kwenye kituo cha polisi wilaya, ndani ya dala dala watu walikuwa wengi, kihasi cha wengine kusimama, mmoja kati ya watu waliosimama ni Lukas, ambae alijitaidi kuvumilia maumivu ya bega, yaliyo sababishwa na mminyano wa mle ndani ya dala dala, zikiambatana na sauti za malalamiko ya abiria, kila mmoja akimshutumu mwenzie kuwa ana mbana, kelele hizo ziliwafanya watu washindwe kusikiliza ata redio ya mle ndani ya dala dala, “jamani ebu sikilizeni kwanza” alisema mtu mmoja, mle ndani ya dala dala, habiria wote wakaa kimya, huku dereva akiongeza sauti ya redio, “majambazi hao awakuishia kupola mari na fedha peke yake, ila wame uwa askari wetu watano” hapo Kijana Lukas akajuwa mala moja kuwa, lina zungumziwa,  nilile tukio la NMC jana usiku, hapo Lukas akajuwa kuwa msaada wake unaitajika haraka sana, akasikia ile sauti inaendelea “mpaka sasa kutokana na tukio hilo la mauwaji ya askari wetu na upolaji wa mari katika hifadhi ya mari za wananchi, tuna msaka mtuhumiwa mmoja, alie fahamika kwa jina la Lukas Benjamin, ambae alidondosha kitambulisho chake, katika eneo la tukio, wakati wa mapambano na polisi walio uwawa” hapo Lukas mapigo yake ya moyo yakalipuka kwa kihoro, akainamisha kichwa chini, licha ya kuwa baridi ilikuwa kari sana, lakini cha hajabu Lukas alianza kutokwa na jasho, itaendelea ........ ili kujuwa kilicho mtokea kijana Lukas, endelea kufwatilia mkasa huu hapa hapa Hadithi ZA MBOGO EDGAR
DONASI VIA PAYPAL Help make a donation if the article feels useful. Donations will be used to renew the domain https://www.bongolives.com/. thanks.
Machapisho Mapya Machapisho Mapya Machapisho ya Zamani Machapisho ya Zamani

Machapisho mengine

Maoni

Chapisha Maoni