Iklan Billboard 970x250

VITU AMBAVYO VINAKERA WANAUME WENGI

VITU AMBAVYO VINAKERA WANAUME WENGI

Moja ya vitu ambavyo vinakera wanaume wengi ni kurudi nyumbani, unataka kuingia ndani unakuta mlangoni kumejaa wanawake, sijui majirani sijui mashoga zake mkeo wanapiga stori.


Wengine wametandika na mkeka kabisa wanaongea kana bila wasiwasi wowote. Yaani ili kuingia ndani nilazima upite katikati yao. Unaingia ndani, labda mke alikupokea au hata hakukupokea lakini anatoka nnje kuendeleea na mazungumzo.


Lakini pia umewahi kurudi nyumbani, umeamua ukapumzike mara hodi, mara sijui naomba hiki, mara kile mara kile. Hamkai mkapumua washakuja kuangalia TV, sijui kuna tamthilia.


TV yako lakini huwezi hata kuangalia kwa uhuru, shoga yake kashikilia romoti. Mwisho wa wiki ndiyo kabisa, rafiki zake ni kujazana hapo nyumbani, wengine washenzi kabisa wanaingia na jikoni kupika.


Yaani wanajifanya kupendana sana (Wale ambao wanashona na sare kabisa) wanakuja wanakaa wanapiga stori, kupika na kucheka kila saa! Mwanaume unaamua tu kulala ndani au kujifanya una ubize kzaini.


Ndiyo hicho kitu kinakera sana, mwanamke punguza marafiki wa namna hiyo, utawapunguza kwa wewe kuacha kwenda kwao mara kwa mara, utawapunguza kwa wewe kutowaendekeza kuzoea nyumba yako.


Wao ni majirani tu, si sehemu ya ndoa yako, acha kuwafanya kama sehemu ya nyumba yako, mumeo anakwazika, labda hajawahi kukuambia anajifanya kufurahia lakini anachukia na inamkera sana. Sasa ni wajibu wako kuhakikisha kua hilo halitokei!


Hembu waambie marafiki zako, huu ni muda wa mume wangu, weekend ni kwaajili ya mume. Mume akufurahie afurahie kuwa na wewe awe na muda wa kuongea na wewe na si marafiki zako.


Sasa wewe waendekleze hao marafiki, siku mume akikuchoka na hata kumchukua mmmoja woa ndiyo unaanza kulialia wakati ulishatengeneza mwenyewe mazingira ya kuibiwa. Weka mipaka kati yako na marafiki zako!

vitu ambavyo vinakera wanaume wengi

SHARE
Subscribe to get free updates

Related Posts

There is no other posts in this category.

Chapisha Maoni

Post Central Advertising