Iklan Billboard 970x250

TIPS ZA JIKONI NYUMBANI

TIPS ZA JIKONI NYUMBANI

HIZI HAPA TIPS 10 ZA JIKONI 

1⃣ Ukimarinate nyama au samaki kwa viungo( vitunguu saum, tangawizi, masala) ongeza mafuta kidogo na mtindi vjk viwili inalainika na kunoga


2⃣ Ukikosa vanila unaweza saga Ganda la limao bichi kuleta harufu nzuri kwenye keki au chapati maji


Ukitaka kupika mboga ya karanga, saga karanga kisha tumia maziwa kukorogea karanga badala ya maji inanoga sana
3⃣ Chapat ukiógeza kdg nazi ya unga na ukakandia maziwa chapati inakuwa zaid ya nzuri


4⃣ Ukitaka chips au ndiz ziwe nzuri, chemsha kdg dk 5 ipua zichuje maji then weka kwenye freezer. Ukitaka kukaanga toa pasha mafuta choma usisubiri zitoke barafu, utastaajab radha yake


5⃣ Ukiunguza wali penyeza mapande makubwa ya pilipili hoho ndani ya wali huwa inaondoa kabisa harufu ya kuungua


6⃣ Ukiona mafuta yamekuwa mengi kwenye supu au mchuzi tumia mkate wa siles kupitisha juu kufyonza


7⃣ Ukitaka maharage yawe na rojo zuri,baada ya kubandika tia mafuta ya kupikia yaivie pamoja


8⃣ Ukitengeneza juice ya rosela au ubuyu unaweza weka mchaichai pale unapochemsha juice inavutia sana


Chapati ikilala ukitaka kuipasha iwe lain ichove kwenye maji baridi na kuitoa then pasha kwenye frypan bila mafuta..itakuwa kama umepika leo


9⃣ Ukipika matembele ukiweka tangawiz na pilipili manga yanakuwa matamu balaa


🔟 Juice ya parachichi weka ndimu au limao utaipenda


♦ Ukitaka samaki wabichi wasivurugike au kung'ang'ania wkt wa kukaanga. Wapake unga wa ngano wakolee halafu kaanga ni watamu mno


♦ Ukitaka kubadili pishi la wali weka kitungú maji, saumu na iliki kdg wkt wa kuchemsha maji then yachuje halafu pika wali wako unanukia balaa


♦ Kama unatumia gesi kupikia wali, jaribu tumia maji ya baridi kupikia mchele unanoga hasa


♦ Ukitaka utumbo uive haraka weka limao pekee bila chumvi kwa yatke maji ya kwanza.


USIWE MCHOYO WA MAARIFA WATUMIE NA WENZAKO
Related Posts
SHARE
Subscribe to get free updates

Related Posts

Maoni 1

Chapisha Maoni

Use [video]youtube-video-link[/video] to insert video in comment
Use [img]image-link[/img] to insert image in comment

Post Central Advertising