NI KUFURU KWA NINI VIJANA WA MJINI HAWAFANIKIWI?

ELIMU UNAYO NDIO UNAISHI VIPI NA WATU UNAKUTA MTU UNA KAZI AFU DHARAU NYINGI KANA KWAMBA DUNIA YOTE INAKULA KWAKO NI HIVI ELIMU,KAZI,NYUMBA,SIJUI MASHAMBA NI YAKO NA FAMILIA YAKO KUWA MAKINI MAISHA NI SARAKASI JAPO UNABARIKIWA KILA SIKU HUWA NAJIULIZA SANA KWANINI NYIE WATUMISHI WA UMMA MKIJA MTAANI MNAKAA MIAKA 3 MNAKUFA TATIZO NN ILI HALI UNAPOKEA MALIPO YA MILIONI 30 KWA MWEZI UTAFITI UNAONESHA WAAJIRIWA WENGI WANAONGOZA KUFA NI STRESS TUPUUU MAISHA NI WW KILA MTU PESA ANAZO TUMEZIDIANA NDIO MAANA UKIFILISIKA WANAKUCHEKA TU  WENGI SUALA LA KULIMA TUNAIGA TU KISA FULANI ANALIMA KILIMO NOUMA OHOOO USIKURUPUKE KAMA HUWEZI KULIMA ENDELEA KUAJIRIWA TU NDUGU YANGU HUKU UTALIA KILIMO NI KIPAJIIIIIIII USIENDELEE KULAMBANA MIGUU NA WATU WASIO NA MSAADA KWAKO AU kukutambia maisha yake acha nae NDIO MAANA WATZ WENGI WANA STRESS UNAJUA KWAMBA 🤣 90% YA WATANZANIA WANAISHI MAISHA YA KUUNGA UNGA NI 7% TU WANAISHI MAISHA YA KIFAHARI KABSA 3% HAWA NI WALE OHOO KUKU NIMECHOKA MM KULA YAANI HAWA 3% NI KUFURU KWA NINI VIJANA WA MJINI HAWAFANIKIWI?. 


Inawezekana na wewe umekuwa ukijiuliza swali hili lililokuwa likinitatiza kila siku kwamba kwa nini vijana wengi wanaoishi mjini huwa hawafanikiwi kama wale wanaotoka vijijini na kuja mjini? Hili ni jambo linalowatesa watu wengi, wengine wamekuwa wakilalamika kwamba kwa nini fulani ametoka kijijini, kaja mjini kafanikiwa na wakati wao ni maborn town lakini bado wamepigika kitaa.

Nimefanya uchunguzi, nimezungumza na vijana wengi na nimefanikiwa kupata baadhi ya majibu ambayo leo hii ningependa kuzungumza nawe, labda tushauriane mawili-matatu, kama kuna hatua za kuchukua, basi uchukue ili na wewe ufike pale unapotakiwa kufika.

Kumbuka kwamba mimi pia nilizaliwa kijijini, nikakulia huko, nikaondoka na kuja Dar es Salaam ambapo sikuwa na ndugu, mvua zilikuwa zangu na jua lilikuwa langu. Sikuwa na pa kwenda, katika kituo cha mabasi ya mkoani (KISUTU) hapo zamani ndipo nilipokuwa nikilala.

Niliumwa sana na mbu, lakini katika hayo yote, sikujuta, maumivu niliyosikia nilijipa moyo kwamba kuna siku yangekoma, kweli, leo unapozungumza watu waliyoyabadilisha maisha yao kutoka kijijini na kuja mjini, basi mtoto wa mkulima, mimi pia nitakuwepo kwenye orodha hiyo.

Hebu ngoja nikwambie kwa nini vijana wengi wa mjini hawafanikiwi kirahisi.


KUJISHTUKIA

Mjini kuna ajira nyingi kuliko vijijini ambapo ajira yao ni moja tu, kulima. Vijana wengi waliozaliwa mjini huwa hawafanikiwi kirahisi kwa kuwa wanajishtukia. Leo unaweza ukamwambia kijana wa mjini auze sabuni kwa kutembeza, lakini anaogopa, anamuonea aibu mtu fulani atamuona, lakini biashara hiyohiyo, mtu kutoka kijijini anafanikiwa na mwisho wa siku anaachwa kijana wa mjini akilalamika.

Unapoamua kutafuta maisha, usiogope kuchekwa, usiogope kudharaulika. Najua wengi hawataki kubezwa wanapofanya biashara za kutembeza pipi au nyingine, lakini kumbukeni kwamba hata matajiri wakubwa mnaowaona katika Tanzania hii, wameanzia hukohuko, kwenye biashara ndogo, zikakua na kuanzisha kubwa.


STAREHE

Hii nayo ni sababu mojawapo. Vijana wengi wa mjini, baada ya kupata fedha kidogo, wanachokifikiria ni starehe tu. Kijana wa mjini yupo radhi atumie hata elfu hamsini kwa usiku mmoja tu na wakati kiasi anachoingiza ni kidogo.

Kabla ya kufanya matumizi makubwa, hebu jiulize, je kuna umuhimu wa kufanya hivyo? Kama unataka kwenda sehemu kula bata kwa hamsini hiyo, hebu jiulize, je usipokwenda siku hiyo, utakufa? Je usipotumia kiasi hicho cha fedha maisha yatakwisha? Je utachekwa? Kama jibu lako ni hapa, basi achana nalo, acha fedha zako ziwe akiba na zikusaidie hapo baadaye.

Unapoanza starehe, kunywa pombe kupindukia, huwezi kufanikiwa, kila siku utakuwa mtu wa kulalamika. Nafurahi kumuona kijana akiendesha gari, lakini wakati anaendesha gari, nafurahi zaidi kumuona akiwa na biashara inayomuingizia kipato kikubwa.

Huwa sifurahii kumuona kijana akiendesha gari, huku mafuta akitumia mshahara wake. Mtu kama huyu kufanikiwa ni vigumu, acha mshahara ufanye mambo mengine, gari ni gharama, wakati mwingine linaharibika, linahitaji vifaa vya gharama, je mshahara ndiyo utakaotumika tu? Na kama ndiyo, je fedha za matumizi na kufanyia mambo mengine zitatoka wapi?


KUJISAHAU

Ndiyo! Wengine wanajisahau. Kama leo mtu akafanya kitu kikamuingizia laki moja, basi kesho hawezi kufanya kitu kama hicho, atakwambia mpaka fedha hizo ziishe kwanza. Hivi umekwishajiuliza kwa nini makonda wengi wa daladala hawafanikiwi?

Wengi wanapata fedha nyingi, kwa siku konda anaweza kupata hata shilingi elfu thelathini mpaka hamsini, kweli mtu wa namna hiyo hawezi kufanikiwa? Kuna mtu anafanya kazi kwa mshahara wa laki mbili, na anafanikiwa, kwa nini mtu kama konda hafanikiwi?

Nimewahi kukutana na makonda wengi, kauli zao ni kwamba wanapata fedha kila siku, leo akipata elfu hamsini, kesho inaingia nyingine sasa kwa nini niiweke hii ya leo? Ukisikiliza sababu zao unaweza kuona zina mashiko lakini hazina mashiko yoyote.

Mchukulie mtu kama Mengi au matajiri wengine, wanaingiza kiasi gani? Mbona wanajua kuweka akiba na huwasikii wakisema leo imeingia hii, nitumie yote kwa kuwa kesho itaingia nyingine? Ni lazima fedha tunazozipata tuziweke matumizi sahihi na tusijisahau kwa kujipa moyo kwamba kesho itaingia nyingine.

Kama tukipambana, tukiingiza fedha na kufanyia vitu vya msingi, tusiporidhika, tusipojisahau basi hii Tanzania itakuwa na mabilionea wengi sana na kila kijana atakuwa na maisha mazuri.


KUKOSA UBUNIFU

Kuna wengine wanapata fedha lakini wanapofungua biashara, wanakosa ubunifu. Kabla ya kufungua biashara fulani ni lazima uangalie je ukiifungua biashara hiyo sehemu fulani, utapata wateja? Je biashara hiyo inahitajika mahali hapo?

Huwezi kufungua baa sehemu yenye vijiwe vya wahuni, watu wataogopa kuja kwa kuwa wanaogopa kukabwa! Huwezi kufungua duka sehemu isiyokuwa na nyumba zaidi ya kumi, unapoamua kufungua biashara, ni lazima uangalie sehemu na kisha ufanye ubunifu.

Hapo ndipo ambapo vijana wengi wamekuwa wakifeli, wengine wanaamua kuanzisha biashara ya mandazi sehemu ambayo kuna wauzaji wengi wa mandazi, je unapotaka kuanzisha biashara hiyo sehemu kama hiyo, unaweza kufanya ubunifu?

Kama unaweza, fanya ila kama hauwezi, achana nayo. Jirani anauza mandazi, na wewe hapa unaanzisha biashara ya mandazi, unahisi utaweza kupata wateja? Ni lazima ufanye ubunifu, yaani kama mtu anauza mandazi, angalia udhaifu wake, kama mandazi yake ni ya kawaida, yako yaweke hiriki, yako yafanye yawe makubwa, huo ndiyo ubunifu.

Kama unataka kuanzisha biashara ya chipsi, angalia udhaifu wa mwenzako. Yeye anauza chipsi bila mishikaki, wewe weka na mishikaki, kama anauza chipsi bila samaki, wewe weka na samaki. Siyo yeye hana samaki, na wewe huna, yeye hata soseji, na wewe huna, yeye hana mishikaki, na wewe huna, ni lazima ufanye ubunifu.

Sasa vijana wengi wa mjini wamekosa vitu hivyo na mbaya zaidi wengi wao hawataki kushaurika. Hili linawakosti sana na ndiyo maana wengi huanzisha biashara na kuanguka chini.

Kwa leo acha niishie hapa, natumaini vijana wa mjini mtafanyia kazi yale machache niliyoshauri.

Asanteni.


@MtonyoShambani 🌱🌱 kuajiriwa ni utumwa kabisa!!!!!!!!!!!!!!

 .

Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hujui ufanyie nini) hivyo umeona uukabidhi ujuzi wako kwa wenye "akili na uwezo" wa kuupangia matumizi ya huo ujuzi wako.


Ndio maana licha ya kwamba elimu ni yako wewe, maarifa ni yako wewe, vyeti ni vyako wewe; na kazi unafanya wewe; lakini hao waliokuajiri ndio wanakuamulia kiasi gani wakulipe! Si hivyo tu bali pia wanao uhuru wa kukupiga mkwara, kukutishia na hata kukufukuza muda wowote (utakapowakosea, watakapojisikia ama watakapokuchoka)! Nini nakwambia? Kama umeajiriwa, usiridhike wala usibweteke na mshahara pekee kwa 100%, hebu jiongeze aiseee, una uwezo wa kuzalisha zaidi sambamba na mshahara (waliojisikia) kukulipa.


Usiufunge uchumi wako kwenye gereza la ajira, fikiria zaidi ya ajira maana hao waliokuajiri nakuthibitishia HAKUNA mwenye mpango mzuri na "future" yako, zaidi sana wanaihujumu "future" yako!


Nimemaliza! USHAURI WANGU ANZA KUAJIRIWA KAMA MUWEKEZAJI TU ILI UJIAJIRI NA KUAJIRI WENGINE.


We nuna weee, kasirika weee, vimba weee mpaka upasuke, lakini kidonge hicho kimeze japo kichungu, ndiyo dawa tena utafanyaje, ila mwisho wa siku uwe na JIONI NJEMA ili ukawaze na kuwazua vizuri.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,151,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,203,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,114,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,12,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,208,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,40,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : NI KUFURU KWA NINI VIJANA WA MJINI HAWAFANIKIWI?
NI KUFURU KWA NINI VIJANA WA MJINI HAWAFANIKIWI?
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/04/ni-kufuru-kwa-nini-vijana-wa-mjini.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/04/ni-kufuru-kwa-nini-vijana-wa-mjini.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content