NAITAFUTA FURAHA YANGU SEHEMU YA 01 | BongoLife

NAITAFUTA FURAHA YANGU SEHEMU YA 01

NAITAFUTA FURAHA YANGU


BY mogy shine
No.0621302436
Mahali__dar
****************


Kila kukicha ama siku inapoanza kila mmoja wetu ,hutamani siku iwe ya furaha na anacho kifanya basi kifanikiwe kama alivyokipanga,hamna anae penda sura yake iwe ya majonzi,simanzi ama karaha. Hii story ina mambo mengi yenye ujumbe tele na inatupelekea kujifunza kutokana na makosa na namna ya kuitafuta furaha yetu hasa inapokosekana ndani ya mioyo yetu ama ndani ya familia.ni nani anaitafuta furaha yake
Basi nawaalika tuungane kwa pamoja tufuatilie kisa hiki tujifunze na kuelemika na tuweze kumjua ni nani anaitafuta furaha kwa nini furaha yake ilipotea STORY ZA MOGY SHINE TZ,kila kitu kitajieleza jina la story
***kabla sijaanza storyy niwashukuru wote mlionitakia heri ya kuzaliwa ,nilijisikia faraja ,siku pata hata wasaa wa kujibu comment zenu kutokana kubanwa na shughuli ndogo ndogo,
Nawashukuruni sana sana wadau wangu wa nguvu,mungu awabariki*****
NAITAFUTA FURAHA YANGU.
Ni usiku wa manane ndani ya familia ya bwana Ally ,simu yake iliita diliiiii diliiiii. Akiwa amelala na mke wake rahma ,basi ally alifunua shuka na kunyanyua mkono wake hadi kwenye meza ndogo iliyoko chumbani karibu na kitanda,
Macho yake yakiwa yamejaa usingizi aliyapikicha ili aweze kuangalia ni nani amepiga simu usiku huo wa manane.mke wake rahma(mama adinani ,nae aliamka baada ya kusikia mlio wa ile simu ya mme wake.
Oooooh!!!/akiwa anahema kwa usingizi mzito ,aliuliza kwa sauti iliyojaa usingizi "mme wangu ni nani huyo anapiga simu sasa hivi usiku huu au uliweka alamu?. Ally alishusha pumzi na kumwonesha mke wake ile simu na kumwambia " mke wangu naona mlinzi wa dukani ananipigia simu.
Rahma "oooh haya mpokelee huenda kuna tatizo limemkumba,ndipo mme aliitikia na kubofya kitufe cha kijani kisha aliweka simu sikioni .
Hallow" ndio sauti aliyoanza nayo
Bosi naomba uwahi hapa dukani kwako moto umewaka na umeteketeza kila kitu dukani majirani na watu wa eneo hili wamejitokeza kunisaidia kuuzima lakin moto bado unendelea kuwaka."ni maelezo aliyoyatoa mlinzi
Moto umesababishwa na nini?ally aliuliza huku akitupa shuka na kuteremka kitandani."mlinzi alijibu "boss sijui tatizo ni nini kisha simu ikakatwa.
Ally ,alivaa suruali yake haraka na tisheti kubwa ," mme wangu waenda wapi mbona wavaa nguo?,mke wake aliuliza "
Mke wangu inuka twende duka letu la magomeni limeungua moto,basi rahma nae alivaa nguo upesi ,kisha walibeba funguo ya piki piki .Ili waweze kwenda dukani kushuhudia huo moto umesababishwa na nini.
Ally pamoja na mke wake makazi yao yalikuwa tabata bima ,maisha yao ndio kwanza yalikuwa yameanza ,walikuwa na nyumba ndogo yenye viumba vitatu na sebule.walikua na piki piki moja ambayo walikuwa wanaitumia kwa ajili ya kwenda dukani kwao.
Ally aliwasha piki piki ili aweze kwenda magomeni mapipa liliko duka lao ,ile ally anawasha piki piki mtoto wao adinani aliamka na kuchungulia dirishani kisha akaita baba "mnaenda wapi sahizi usiku hivi?
mama alidakia " mwanangu tunaenda magomeni sasa hivi tumepigiwa simu na kuambiwa duka limeungua ,adinani aliuliza
"Nini chanzo cha moto huo?,mwanangu wewe lala baki na akina mudrick pamoja na nusra sisi ngoja tukaangalie nikitu gani kimetokea tukirudi tutakueleza.baba alijibu.
Adinani alifunga dirisha na kuwatakia safari njema,basi aliwasha piki piki kisha walianza safari kuelekea magomeni.
Walitoka nyumbani na kuingia bara bara ya lami ndipo waliona gari nyeusi imepaki ikiwa inawasha taa nyekundu ,tu.
Ally hakutilia sana manani ile gari aliendelea na safari yake huku ameshikilia usukani vilivyo wa piki piki yake.wakiwa barabarani kwa nyuma ile gari ambayo ilikuwa imepakiwa ilianza kuwafuatilia kwa nyuma.
Ally hakuwaza sana maana jiji la dar es salam watu wanatembea masaa yote barabarani. Ndani ya ile gari alikuwepo juma akiwa na rafiki yake kelvin
Kelvin aaliuliza " juma hii piki piki ndio ya ally ama hawa watu wengine.juma aliitizama na kusema ni yakwake yupo na mke wake sasa tunatakiwa tumalize kazi kwa mara moja.
Kelvin aliuliza andaa pesa yangu upesi namaliza kazi "juma alitoa bahasha na kumpa kelvin kisha akamwambia " pesa yako hii hapa fanya kazi asaivi.
Wakat huo ally na mke wake walifika relini ile wanataka kuingia barabara kubwa ,ndipo iLe gari iliongeza spidi na kuwagonga puuuu masikin ally na mke wake walidondoka kwenye lami puu
Ile hari ilirudi nyuma kisha dereva alikanyaga mafuta na kuwapitia juu ally pamoja na mke wake kisha gari walichocheagia na kuondoka eneo la tukio.nimpango wa juma na sijui dhamira yake yakufaNya vile
Ally na mke wake kwa pamoja walipoteza maisha huku miili yao ikuwa imevunjwa vunnjwa kila mahali,mama adinani alipasuka kichwa huku ally tair ya gari ilimpitia maeneo ya kifuani.
Ni simu tu ndio ilidonokea mbali
Kwakuwa ulikuwa ni usiku sana bara bara ilikuwa nyeupe ,hivyo gari iliyowagonga hamna mtu aliyeweza kuwaona.duka likateketea lote huku ally na mke wake wakapoteza maisha.
Mlinzi aliendelea kumpigia boss wake simu ,lakin simu haikupokelewa ndipo watu walitokea kwenye hio ajali na kutoa msaada,waliwafunika marehemu kisha walipiga simu polisi.
Jeshi la usalama barabarani waliweza kufika na kupima tukio ,wakiwa wanafanya vipimo ndipo walisikia simu inaita.
Kila mmoja aliangalia chini na kuweza kuiona alisema "jaman askari simu ya marehemu hii hapa na wanapigiwa na mlinzi wao.
Askari ilibidi apokee ile simu.haloo,ndipo alikutana na sauti ya mlinzi akiongea kwa masikitiko " bosi bado hujafika duka lako lote limeteketea na moto kila bidhaa imeungua.askari alisikiliza kisha akauliza duka la bosi wako liko wapi maana bosi wako amepata ajali nahisi ndio alikuwa anakuja huko.
Mlinzi aliuliza kwa mshangao bosi kapata ajali?
Ndio amepata ajali askari alimjibu basi mlinzi aliweza kuwaelekeza mahali duka lilipo
Askari aliweza kufika na kushuhudia jinsi duka lilivyoungua
Lilikuwa duka kubwa lenye bidhaa ndogo ndogo za nyumbani ,lote limeteketea.
Wakati huo miili ya ally na mke wake ilibebwa na kwenda kuhifadhiwahosp
italin,ndipo mlinzi alihojiwa mahali marehemu ally na mkewe walikokuwaa wanaishi,mlinzi aliwapeleka nyumbani
Tayari pashapambazuka ,saa kumi na mbili ndipo askari wawili waliweza kufika nyumbani kwa ally walikuta mlango umefugwa ndipo waligonga.alifungua mtoto wao adinani akiwa anajiandaa ili aende shule.mlinzi alisema "askari hapa ndipo nyumba yake na huyu ni mtoto wake.
Askari alitikisa kichwa kisha akamuuliza adinani.wewe ndio mtoto wa ally,adinani alijibu ndio mimi ni mtoto wake,ila kama mnamtafuta baba hayupo pamoja na mama walienda magomeni tangu saa nane usiku.
Askari alimwangalia adinani na kuwaza ataanzaje kumweleza kuwa mama yake na baba wamepata ajali na kufariki ,vile vile duka limeungua lote.
Askari wakiwa wamesimama ndipo rafiki yake mkubwa ally na alikuwa anamwamini sana huku wameeshiriki vitu vingi kwa pamoja kama kujenga nyumba walikuwa wakisaidiana alikuwa si mwingine bali ni "juma".
Huyu juma ndio alimpa pesa kelvin kisha kelivin akawagonga ally na mke wake.hadi kupelekea kupoteza maisha.
Juma alifika na kuuliza swali la kinafiki sana " aliita adinani baba yako yupo? Nataka aniazime piki piki yake niende mwenge mara moja.masikini adinani akiwa hajui kitu chochote ,alijibu "baba hayupo toka saa nane usiku alienda dukani kwake magomeni alisema kuna dharura imetokea bado hajarudi.juma alitabasamu kisha akajisemea moyoni " sio baba hajarudi na hatorudi milele kisha akasema
Sawa adinani miee narudi nyumbani.basi juma aliondoka zake
Huku askari alimwangalia adinani ambae anaonekanika ana miaka kumi na saba alimuuliza "hapa mnaishi na nani?
Adinani alimwanglia askari kisha akamwambia baba,mama na wadogo zangu wawili
Kabla askari hajauliza ama kumweleza adinani kuwa baba na mama wamepoteza maisha ndipo " mudrick,na nusra nao wakaamka askarii aliwaangalia ni watoto wadogo mmoja miaka mitano mwingine mitatu
Mara rafiki yake mama adinani alisikika akilia kwa uchungu huku akisema mama adinani kwanini umefariki mapema,naa hawa watoto wako nani atawalea kwanini mmefariki mapema ,mama adinani jamani nini kimewasibu mbona mmeondoka mapema?
Hakika rafiki rake marehemu alilia nakugara gara chini
Ndipo adinani,mudrick nanusra waliuliza kwa pamoja mama na baba wamefariki kisha wote wakamwangalia askari kwa mshangao
JE NINI KITAENDELEA?

COMMENTS

BLOGGER

VISA NA MIKASA $type=THREE

Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,171,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,212,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,126,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,7,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : NAITAFUTA FURAHA YANGU SEHEMU YA 01
NAITAFUTA FURAHA YANGU SEHEMU YA 01
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/04/naitafuta-furaha-yangu-sehemu-ya-01.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/04/naitafuta-furaha-yangu-sehemu-ya-01.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content