Iklan Billboard 970x250

MWANAMKE LITAMBUE HILI

MWANAMKE LITAMBUE HILI

_*Idadi kubwa ya wanaume bado hawajatimiza ndoto zao, wanatamani sana kupata wanawake watakaowaunga mkono na kuwafikisha katika ndoto zao.*_


_*Ila ukweli unaoumiza ni kwamba wanawake hawataki wanaume hao walio mbioni kuzifatia ndoto zao bali wanahitaji wanaume ambao wameshatimiza ndoto zao.*_


_*Ajabu ilioje wanawake wanasahau kuwa katika kila mwanaume mwenye mafanikio nyuma yake kuna Mwanamke aliesimama imara kumfikisha hapo alipo.*_


_*Unaweza kuwa unalalamika kuwa huna bahati sababu kila mwanamme anakuacha bila ya kufunga ndoa na wewe licha ya uzuri wa sura na umbo lako:*_


_*Tambua maamuzi yako ndio maumivu yako na huenda umenyimwa hekima, unapaparika na kijana mtanashati kisa elimu yake, kazi yake, mali zake na mara kwa mara anakutoa out na kukupa zawadi hii na ile, lakini unambeza kijana ambae si msomi, hana kazi nzuri, ila Ni mtu wa ibada tena unamuona si lolote si chochote.*_


_*Jiulize! Huyu sharobaro wako sixpack zaidi ya kukupeleka club, kukufanyia shopping, na kukupa hela ya matumizi Ni kipi cha maana zaidi ya ndoa alichokufanyia kinachokufanya uwe na furaha kuwa nae?*_


_*Unategemea nini zaidi ya kukugeuza kama chapati akichoka anakutosa anamtafuta mwengine asie na akili wala maarifa kama ulivyo wewe!!*_


_*Umefika wakati sasa wanawake mjitambue, maisha ya starehe yana mwisho wake, umri wako hausimami kukusubiri wewe uwe tayari ili wende sambamba na wewe.*_


_*Jiulize uliingia kwenye kamari ya mapenzi ukiwa na miaka 15 hadi sasa umeshaonja pingili ngapi na umefaidika na kipi?*_


_*Ukisubiri muda uwe tayari kwa ajili yako unachelewa sana.*_


_*Zinduka mdogo wangu, using'ang'anie kuolewa na tajiri au msomi, mwenzio huwezi jua maskini wa leo ndio tajiri wa kesho.*_


*Chagua wako uanze nae mbio za maisha.*

Related Posts
SHARE
Subscribe to get free updates

Related Posts

Chapisha Maoni

Post Central Advertising