Iklan Billboard 970x250

Mume alitaka kuowa mke wa pili kwa siri

Mume alitaka kuowa mke wa pili kwa siri

Jamaa alitaka kuowa mke wa pili kwa siri. Akakubaliana na watu wa upande wa mke harusi itakua siku ya ijumaa. Mke wa kwanza akapata khabari za huo mpango basi ilipo fika siku ya alkhamisi akampikia mumuwe chakula cha usiku kizuri kisha wakalala. Mume alipo amka akavaa kanzu yake na kujifukiza udi. Mke akamuuliza unakwenda wapi? Mume akajibu nakwenda kuswali ijumaa. Mke akamwambia  keti utue leo ni jumapili. Juzi nilikutilia dawa ya kulala kwenye chakula ukalala siku tatu. Na siku nyengine nikisikia wenda kuowa wallahi nitakutilia dawa ukiamka tena ni siku ya kiama!


不不不不不不不不不

Related Posts
SHARE
Subscribe to get free updates

Related Posts

Chapisha Maoni

Post Central Advertising