Iklan Billboard 970x250

MPENZI WANGU ANAWASILIANA NA EX WAKE

MPENZI WANGU ANAWASILIANA NA EX WAKE

mume akiwasiliana na ex-wife

Naomba mnishauri

Mie nina uhusiano na kaka mmoja ambae ana mambo yafuatayo:-

1.kabla yangu alizaa na mdada mmoja (hawakufunga ndoa) wana mtoto mwenye mwaka 1 lakini wametengana

2.Kila siku lazima aende kusalimia huko na anakaa hata zaidi ya masaa matatu.

3.Najua wazazi lazima wawasiliane lakini mwanamke anadiriki kupiga hata usiku au alfajiri japo nimekataza lakini naona mume hakemei.

4.Kuna mdada mwingine ana mimba yake walikwenda wote clinic na wanawasiliana japo nakemea.Nikimuuliza  mume umri wa mimba anasema hajui wakati walikwenda wote clinic.

5.Usiku wa kuamkia leo huyo mwenye mtoto alipiga cm saa 5 hivi usiku akasema mtoto ana homa...mie nikachukia nikamwambia kama vp aende hukohuko nimewachoka maana haoneshi nidhamu.

6.Sometimes anachat na ma-x wake.

Kifupi nimechoka hata kama tulikuwa tuna lengo la kuingia uchumba nataka nimwambie kila mtu aendelee na maisha yake maana mwenzenu presha siziwezi.

Nitakuwa nimekosea?


Related Posts
SHARE
Subscribe to get free updates

Related Posts

Maoni 5

 1. Jibu fupi na lamsingi, hakufai! Mungu hawezi kuja kukutamkia kuwa huyu mtarajiwa wako hakufai, ila atakuonesha kupitia matendo yake sasa wewe ndo utachagua kujutia baadaye au kuwa huru mapema! Hakufai huyo!

  JibuFuta
 2. AsiyejulikanaAprili 10, 2019

  Matty: Achana naye huyo hana msimamo bado atakusumbua sana kama utaendelea naye , bora ambaye anafanya kwa heshima bila wewe kujua huyo hapana

  JibuFuta
 3. Huyo sio mwanaume wa ubavu wako maana anatahixi

  1.sio mwaminifu

  2.hana msimamo na ndio maana ameshindwa kulinda heshima yako kwa hao wanawake wengine.

  3.anaonekana ni mpenda vya nje sanaa kifupi hajatulia.maana hawezi kuwa na mwanamke mwenye mtoto wa umri wa mwaka then hapohapo awe na mwingine mjamzito.na wakati huohuo yupona wewe...

  JibuFuta
 4. Achana nae faster, huyo sio mchumba wala mume, asikupe nuksi. Kaza roho mana yawezekana kajaa moyoni mwako, piga teke la maana.  Fyuuuu zake

  JibuFuta
 5. Hahahahaha...... Najiuliza maswali mengi Sana.

  1. Unampenda?

  *Kama unapenda funga nae Ndoa*!  2. Anakupenda?

  *Kama anakupenda pendaneni*!  3. Anakutimizia mahitaji?

  *Kama anakutimizia Wewe komaa nae*!  4. Akienda anamaliza hukohuko akirudi hakupi?

  *Kama anakupa, komaa nae siku moja ataelewa*!  5. Anaweza kazi vizuri kitandani?

  *Kuwapata siku hizi wanaoweza ni Bahati, komaa nae usije tafuta wa kukutia shombo la shahawa*!  6. Yeye huwa anawaanza?

  *Kama wanamuanza wenyewe mwenyewe ni Wewe, na ana nafasi NNE za wake wa kuoa, acha kujitia majununi*!  7. Aliwahi kuoa?

  *Kama hajawahi Wewe na yeye wote wazinifu tu, Tulieni mtubie wote mbadilike*!  8. Wale watoto unafikiri ni wake?

  *Kisheria sio wake ila anafanya ihsani tu, acha kujitetua*  9. Wewe una mwanaume mwingine?

  *Kama huna, kubali kubaki uolewe,kuliko kumwacha Nawewe utaingia kwa wanawake zake wengine,hiyo nafasi ikichukuliwa na mwingine*  10. Unajua sifa ya Mapenzi?

  *Kuanza,kustawi,kukomaa afu kuzeeka,kuchoka na kufa*!

  Pia huwa yanachipua.  Yadhibiti tu.  *Sikushauri kumwacha kama unampenda*!  Naitwa Bibi

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Use [video]youtube-video-link[/video] to insert video in comment
Use [img]image-link[/img] to insert image in comment

Post Central Advertising