Iklan Billboard 970x250

MAPISHI YA KUPIKA VILEJA VYA CHOCOLATE NA VANILLA

MAPISHI YA KUPIKA VILEJA VYA CHOCOLATE NA VANILLA

VILEJA VYA CHOCOLATE NA VANILLA:

VILEJA VYA CHOCOLATE NA VANILLA

MAHITAJI YA KUPIKA VILEJA VYA CHOCOLATE NA VANILLA

  • 🔸Unga wa ngano vikombe 3
  • 🔸Baking soda 1/2 kijiko cha chai
  • 🔸Chumvi 1/4 kijiko cha chai
  • 🔸Siagi kikombe 1 
  • 🔸Sukari nyeupe vikombe 2
  • 🔸Mayai 2, yalopigwa 
  • 🔸Vanilla kijiko 1 cha chai 
  • 🔸Unga wa cocoa(cocoa powder) 1/4 kikombe 

JINSI YA KUPIKA VILEJA VYA CHOCOLATE NA VANILLA

1. Changanya unga pamoja na  baking soda na chumvi. Weka pembeni.

2. Piga siagi na sukari kwa kutumia mchapo au mwiko hadi mchanganyiko uwe mweupe

3. Tia mayai na vanilla kisha piga tena vizuri kuchanganya. 

4.  Tia unga kidogo kidogo ukiwa wachanganya hadi ujikusanye na kufanya donge, gawa nusu kwa nusu

5. Katika donge moja tia cocoa (choco primo) kisha changanya vizuri upate donge la chocolate

6. Sukuma donge lako la vanilla kufanya umbo pembe nne ,weka pembeni, kisha sukuma donge lako la chocolate umbo pembe nne pia. 

(kama unga unakusumbua unalainika tia katik fridge kwa muda wa nusu saa kisha sukuma) 

7. Bebanisha zote mbili ukianza na wa vanilla chini wa chocolate juu kisha sokota kufanya log (kama wakunja busati) kisha zungusha katika plastic na tia katika fridge hadi uwe set (kuwa mgumu) 

8. Washa oven joto 180°C. Funika tray lako la kuokea kwa karatasi ya kuokea au zungusha kwa foil

(unaweza pia paka tray yako mafuta kisha nyunyiza unga) 

9. Toa unga wako katika fridge kisha kata slices kwa kutumia kisu kikali,  Panga katika tray na hakikisha unaacha nafasi kila baada ya kimoja. 

10.  Weka kwa muda wa dk 10-15 ziwe set vizuri na kupata rangi pembezoni na chini kwa mbali 

11. Epua kisha wacha zipoe kabisa katik tray.

Related Posts
SHARE
Subscribe to get free updates

Related Posts

Chapisha Maoni

Post Central Advertising