Iklan Billboard 970x250

MAPISHI YA KUPIKA KACHORI

MAPISHI YA KUPIKA KACHORI

KACHORI


KACHORI

MAHITAJI YA KUPIKA KACHORI

 • Viazi 1/2 kilo
 • Kotmiri ilokatwa katwa
 • Pilipili ya kijani 1 ilokatwa ndogo ndogo
 • Chumvi
 • Garam Masala kjk 1 cha chai
 • Manjano ya unga 1/2 kjk cha chai 
 • Sukari kjk 1 cha chai
 • Tangawizi na kitunguu saumu kilichopondwa kjk 1 cha chai
 • Mchanganyiko wa kuchomea : 
 • Unga wa dengu gramu.
 • Hamira ya soda/chapa ya maandazi kidogo .
 • Maji
 • Mafuta ya kukaangia

JINSI YA KUPIKA KACHORI


 1. Kosha na chemsha viazi
 2. Vikiwiva menya na uviponde kisha weka pilipili, kotmiri, Garam Masala, sukari, tangawizi na kitunguu saumu, chumvi na kamulia ndimu kisha changanya.
 3. Mchanganyiko wa viazi utakuwa tayari. 
 4. Tengeneza maumbo ya mipira
 5. MCHANGANYIKO WA UNGA:
 6. Anza kwa kuweka unga wa dengu kwenye bakuli, kisha weka hamira ya soda na chumvi , changanya vizuri kisha weka maji kidogo 
 7. Tengeneza uji mzito kisha engeza maji uwe mwepesi kiasi
 8. Weka mafuta jikoni yakipata moto chovya kachori kwenye mchanganyiko wa unga na uzikaange mpaka ziwe na rangi nzuri
 9. Andaa kuliwa kwa chatine.


Related Posts
SHARE
Subscribe to get free updates

Related Posts

Chapisha Maoni

Post Central Advertising