Iklan Billboard 970x250

MAPISHI YA KUPIKA BHAJIYA ZA KUNDE

MAPISHI YA KUPIKA BHAJIYA ZA KUNDE

BHAJIYA ZA KUNDE

BHAJIYA ZA KUNDE

Leo tutapika bhajiya za kunde karibuni 

MAHITAJI YA KUPIKA BHAJIYA ZA KUNDE
 • Vikombe 2 kunde
 • Kitunguu maji 1 kikubwa
 • Pilipili kichaa 2 
 • Vijiko 2 vya chakula maji ya limao (ukipenda)
 • Kijiko 1 cha chai baking powder
 • Vijiko 1½ vya chai tangawizi
 • ¼ kikombe majani ya giligilani
 • Chumvi kwa kuonja
 • Mafuta ya kukaangia

JINSI YA KUPIKA BHAJIYA ZA KUNDE

 1. Katakata kitunguu maji, pilipili kichaa na majani ya giligilani; twanga tangawizi. Weka pembeni
 2. Weka kunde na maji ya limao kwenye mashine ya kusagia chakula au blender. Unaweza pia kutumia mashine ya mkono ukipenda au kutwanga kwenye kinu. (hakikisha mashine yako ina nguvu ya kutosha kusaga kunde). Saga ila isilainike sana kwanza. (endapo itakuwa ngumu kusaga ongeza maji kiasi)⤵⤵⤵
 3. Ongeza kitunguu maji, pilipili kichaa, tangawizi na majani ya giligilani kwenye mchanganyiko, saga kwa sekunde kama 20. Hakikisha vitunguu na majani ya giligilani hayasagiki kabisa. Weka mchanganyiko kwenye bakuli kubwa. Ongeza chumvi na baking powder, changanya vizuri
 4. Funika bakuli, acha viungo vikolee kwenye friji kwa lisaa 1 hadi 2
 5. Zikiiva toa weka katika chujio la bati zichuje mafuta au weka katika tissue kisha weka katika chombo kizuri hata mlaji kimvutie sio vyombo vyapambwa kabatini mume anaandaliwa sahani yenye MAPENGO Haipendezi ⤵⤵⤵⤵

SHARE
Subscribe to get free updates

Related Posts

There is no other posts in this category.

Chapisha Maoni

Post Central Advertising