MAMBO NUMBER 5 - YALIYONIKUTA OMAN - SEHEMU YA 01

SIMULIZI YA KWELI.

YALIYONIKUTA OMAN 

MWANDISHI: ALLY KATALAMBULA. 


SEHEMU YA 01


ILIKUWA ni mara ya kwanza katika maisha yangu kupanda ndege. Licha ya kuwa na wasiwasi juu ya maisha ninayokwenda kuishi katika nchi ngeni ya Kiarabu, nchi yenye utamaduni na sheria tofuati na nchi yangu, hilo halikunifanya kutoona fahari kuwa ndani ya Fly Emirates Airlines iliyokuwa ikikata mawingu kwa kasi ya ajabu.


Nikiwa nimeketi katika siti ya dirishani ndani ya ndege hiyo kubwa. Niliyatupa macho nje, kupitia dirisha dogo ndani ya dege hilo. Niliona tupo katikati ya mawingu meupe yaliyozagaa katika anga na kuleta taswira kama shamba la pamba lililomea.

Nilijisikia raha isiyoelezeka. 


Masikioni mwangu nilikuwa nimevaa visikilizio, nikisikiliza muziki mzuri wa Craig David uitwao ‘Walking Away’ uliokuwa unatokea kwenye ipod yangu kupitia kwenye visikilizo hivyo vya masikioni. 


Sikumbuki tulitumia muda gani kusafiri angani, ninachokumbuka baada ya muda mrefu kupita sauti ya mhudumu wa ndege kupitia spika zilizokuwa ndani ya ndege ilisema:


“We are about to land, all passangers of fly Emirates Airlines, wake up and make sure your belt is close” 

Sauti laini ya kike ilisikika, aliongea kwa kimombo akimaanisha abiria tunatakiwa kufunga mikanda kwani ndege inakaribia kutua.

Ni sauti hiyo ndiyo iliyonistua, nikaangalia saa yangu ya mkononi ikanionyesha ilikuwa ni saa mbili usiku, nilifunga mkanda kama tulivyotakiwa, kisha nikatulia kwenye kiti, mapigo ya moyo yalianza kwenda kasi, hofu ikanijaa moyoni mwangu.


Maneno niliyoambiwa na mama kabla ya kupanda ndege hiyo yakijirudia akilini mwangu.


“Wasichana wanaokwenda kufanya kazi Oman, mara nyingi baadhi yao wanabakwa, wanamwagiwa maji ya moto, na hata kuuawa, kubwa kuliko vyote nchi ile inasheria kali dhidi ya makosa mbalimbali. ” 

Sauti ya mama yangu ilikuwa ikijirudia akilini mwangu mara kadhaa tangu mwanzo wa safari hiyo. 


Taswira ya mandhali ya kijiji cha Makose huko mkoani Tanga ilinijia kichwani, na wakati taswira ya kijiji inapita ubongoni mwangu ilikwenda sanjari na picha halisi ya maisha yangu nikiwa miongoni mwa wenyeji wa kijiji hicho kinachokaliwa zaidi na wakazi wa makabila ya Wasambaa na wapare waliojipenyeza wakitokea mikoa ya Arusha na Kilimanjaro. 


Baada ya kumaliza kidato cha nne nilikuwa miongoni mwa wanafunzi wachache waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwenye Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa iliyoko jijini Dar.


Zilikuwa ni nyakati za furaha maishani mwangu pengine kuliko nyakati nyingine zozote, lakini ni nyakati hizohizo furaha yangu iligeuka na kuwa majonzi yasiyoweza kusahaulika kichwani mwangu.

Ilikuwa ni pale wazazi wangu niliponieleza hawawezi kunisomesha kwa kuwa hawakuwa na uwezo huo, tena mbaya zaidii nikiwa mbali na nyumbani. 


“Hutuwezi kumudu gharama za kukusomesha mwanangu. Shule uliyofaulia ni shule ya kutwa. Hii inamaana kwamba, upangishiwe chumba, na upate huduma kama mwanamfunzi. Hiyo ni mbali na ada, sizungumzii nauli na mambo mengine ya shule...


Jambo baya zaidi, jiji la Dar lina sifa kuwa na gharama kubwa ya maisha.”

Sikubishana na ukweli wa maneno yale. Alichokisema mama kilikuwa sahihi kabisa, familia yangu ilinuka ufukara, mara kadhaa nilikuwa nikishuhudia tukishinda na kulalia uji usiyokuwa na sukari. 


Siyo mara moja kuchekwa nikiwa shuleni, lilikuwa ni jambo la kawaida kudharauliwa, hata kutengwa kwa kuvaa nguo za kuchanikachanika kiasi cha kutoa picha kamili ya kiwango cha ufukara ulionizingira.


Wala halikuwa jambo la kushangaza kuacha kwenda shule na kufanya vibarua kwenye mashamba ya wanakijiji, pesa kidogo iliyoipatikana ndiyo ilitumika kwa kula, kununulia madaftari na sare za shule.


Niliishi maisha ya kifukara tangu nazaliwa hadi nilipokuwa binti. Nikiwa msichana mrembo wa miaka 21 nilikuwa ni mtu mwenye ndoto na matarajio makubwa sana kama vijana wengine. 


Nilisumbuliwa na wanaume wakware pale kijijini na baadhi yao, walitumia umasikini wangu kama njia rahisi ya kunipata. Ajabu nilikuwa na misimamo isiyoyumba. Niliamini mwanaume pekee atakayeujua mwili wangu ni yule atakayekuwa mume wangu. Kwa kweli nilikuwa ni mwanamke mwenye matarajio makubwa sana, lakini ndoto zote zilizimishwa na ufukara ulionizingira.

*


Niliyakumbuka hayo nikiwa nimetulia ndani ya ndege iliyotarajiwa kutua dakika chache katika nchi ya Oman. Nilitokwa na jasho lililotokana na hofu huku nikihisi tumbo likichemka kadiri tulivyokuwa tukiusogelea uwanja wa ndege wa Jijini Muscut nchini Oman.


Dakika chache badaye, ndege ilikuwa ikiserereka kwa kasi kwenye ardhi ya nchi ya hiyo. Baada ya kusimama, tulianza kuteremka abiria mmoja mmoja.


Nilipoikanyaga aridhini, nilijiona nikiwa kiumbe mdogo mithili ya sisimizi, utitiri wa magorofa yaliyojichomoza kama uyoga sambamba na barabara za flyover zilinifanya nijione kama ndiyo nakwenda kupotelea katikati ya Jiji hilo.


“Are you Agripina?” nilisikia sauti moja akinisemesha, nilipogeuka nilimwona mama mmoja mnene wa umbo, aliyevaa baibui sehemu yote ya mwili wake isipokuwa machoni pekee, mkononi akiwa na bango lililoandikwa jina langu.

“Yes. I’m Agripina, who are you?” nilimjibu nikimuuliza, mimi ndiye Agripina na yeye alikuwa ni nani. 

“Naitwa Mariamu Rashidi, ninataarifa za ujio wako, mimi ndiye nitakuwa mwenyeji wako hapa Oman.” 

Yule mama alisema kwa Kiswahili huku akipokea begi langu la nguo.

“Kumbe unazungumza Kiswahili?” Niliuliza kwa wahaka

“Ndiyo, mimi ni Mbongo kama wewe, tena ni Msambaa wa Milimani, natokea maeneno ya huko Lushoto kijiji cha Mlalo,”alisema.


Kwa kweli nilifurahi kukutana na mwanamke yule anayezungumza Kiswahili kwenye taifa lile la Kiarabu tena akiwa anatokea kijiji jirani na chetu.


Hata hivyo, kwa muda mchache sana niliotumia kutambuna na yule mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Mariamu Rashidi, kuna mambo niliyoyagundua kutoka kwakwe, mambo ambayo yalinitisha vibaya mno.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,151,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,203,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,114,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,12,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,208,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,40,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : MAMBO NUMBER 5 - YALIYONIKUTA OMAN - SEHEMU YA 01
MAMBO NUMBER 5 - YALIYONIKUTA OMAN - SEHEMU YA 01
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/04/mambo-number-5-yaliyonikuta-oman-sehemu.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/04/mambo-number-5-yaliyonikuta-oman-sehemu.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content