Iklan Billboard 970x250

MAMA MKWE NAYE NI MAMA

MAMA MKWE NAYE NI MAMA

Ilikuwa wakati wa mchana ambapo mume alirejea nyumbani akiwa na habari mbaya.


MUME: Mpenzi, nimepigiwa simu: Mama hajisikii vizuri. Tunaweza kwenda kumnunulia baadhi ya mahitaji kwa ajili ya kumtembelea? Tafadhali andika orodha ya mahitaji kisha tuondoke.


MKE: Orodha ya vitu hivyo sio muhimu, tutanunua tu kabichi 2 na lita 2 za mafuta ya kupikia.


MUME: Vitatosha kweli?


MKE: Ndiyo mpenzi, hakuna haja ya kupoteza pesa, vitatosha.


Walielekea mjini na kununua kabichi 2 na lita 2 za mafuta ya kupikia. Wakati wakinunua mume alimuuliza mkewe tena kama vitu hivyo vingetosha.


Mke alisisitiza zaidi kuwa hawatakiwi kutumia pesa nyingi kwenye ziara ya kushtukiza.


Walianza safari kuelekea kijijini, na walipofika kwenye eneo la njia panda yenye barabara zinazoelekea vijiji mbalimbali, mume alikata kona kuelekea kwao na mke.


MKE: (Kwa mshituko) tunaelekea wapi mpenzi?  Nilidhani tunaenda kumtembelea mama yako.


MUME: Ndiyo, ndiko tunakuelekea. Ni mama yako (mama yetu) ndiye anayeumwa.


MKE: (kwa mshituko na kilio), lakini mahitaji haya hayatoshi. Turudi tuongeze vitu vingine.


MUME: Hapana! Nilikuuliza tena na tena kama mahitaji hayo yanatosha, ukaniambia “NDIYO”. Hakuna kurudi…..


FUNZO:


Wafanyie wenzako kile unachotaka ufanyiwe!!


Tunawatakia ndoa maridhawa isiyokuwa ya mwendo kasi!!

Related Posts
SHARE
Subscribe to get free updates

Related Posts

Chapisha Maoni

Post Central Advertising