HAYA SASA SHUHUDA HIZO, WALE WAMAMA MSIOPENDA KUPIKA WALA KUFUA, MPO BIZE KAZINI TU NA BIASHARA TUU

HAYA SASA SHUHUDA HIZO, WALE WAMAMA MSIOPENDA KUPIKA WALA KUFUA, MPO BIZE KAZINI TU NA BIASHARA TUU MNAPENDA DEZO TUUU. DADA AKIKUBEMBELEZA UNAJUA ANAKUPENDA KUMBE ANA LAKE.

NIMEITUMIWA USIKU HUU NA NIMEIPOST USIKU HUU HUU.

MANA LOOH MTU ANAJENGA KWAO NA KWENU KIJIJINI MAMA YAKO HANA HATA RUMU MOJA.

HAYA MSOME HILO MJIONEE.


Habari Devotha, nimekuja inbox ila lengo ni kutoa ushuhuda na kukupongeza kwa kazi nzuri ya kuelemisha jamii.

Ulifundisha kuhusu kufulia mume na kumpikia.

Mimi nilikua msichana wa ndani kwenye familia moja huko dar miaka nane iliyopita ndo niliacha kazi.

Naomba sitaitaja.

Nilipoenda kufanya kazi nilikua na mtoto wa miaka minne ila nilimwacha na mama yangu kijijini.

Nilipofika pale nilikaa kama miezi mitatu hivi nikisoma ramani. Yule mama katika hiyo miezi mitatu kama aliingia jikoni basi ni mara moja. Kama aliwahi mfulia mumewe sikumbuki. 

Nikaona hii fursa. Niliaga naomba niende kumwona mwanangu anaumwa, nikaenda. Nilikaa wiki moja. Nilipofika nyumbani, niliongea na mama, nikaenda kwa mganga, nikapewa dawa za kumnasa yule baba. Lengo langu halikua kuolewa nae wala sikua nampenda, lengo langu lilikua nipate pesa za kumsomesha mwanangu na kumjengea mama yangu. 

Nikapewa dawa. Ya kuweka kwenye chakula, na ya kumfulia nguo zake. Kila nikiweka nanuizia anipende mimi na kila ninachotaka nipewe.


Dada baada ya wiki nikarudi. Nilikuta nguo rundo.

Niliomba samahani kwa mama kuchelewa akanielewa. Kesho yake kazi ikaanza. Kila nikipika, dawa yangu naweka. Kila nikifua dawa yangu naweka. Nyingine hadi nadekia.

Heeeh yule baba akaanza mwenyewe kunitongoza, nikakubali. Ila nikamwambia mweshimu mkeo.

Na asijue. Yule baba alinunua simu nyingine na line nyingine akasajili jina la kike. Akifika  ofisini ndo tunawasiliana nayo.

Yani nilikua namfulia yule baba, napasi vizuri nguo zake na mkewe ili mke asijue. Naziweka sebuleni, mama akija namkabidhi kwa adabu. Anafurahi, 

Mama akifika nambembeleza pole mama, namchana nywele, namwekea maji ya kuoga nk asinishtukie.

Chochote nikiomba kwa yule baba ananipa, mara nyingi anarudi kabla ya mkewe, akifika namwambia mwanangu shule hana pesa na mama hana pesa napewa hata laki 2 nakimbia mpesa fasta namtumia mama nunua tofali, 

Akiwa kazini namuuliza anataka kula nini usiku? anasema. Namwambia mwambie basi mama unataka kula kitu fulani  mwambie dada apike. Mama ananipigia ananiuliza unaweza kupika kitu fulani namwambia ndio mama,

Huyo baba anamtuma mtu wa tax analeta vitu napokea.

Napika.

Siku tunataka kutoka namwambia mama nina ndugu kafiwa naomba niende nawahi kurudi. Natoka asubuhi tunaenda hoteli na huyo baba, nakuja kuchukuliwa na tax. Tunalala, tunafanya yetu narudi nyumbani natulia. Sikua nampenda huyu baba ila nilifanya hivyo mana huyo mama hakua na muda na nyumba yake nikatumia upenyo kujifaidia nilijenga kijijini nikamaliza, nikapata mchumba, nikawaaga nikaenda kuolewa sasa nipo kwangu. Ila nilijenga na mwanangu akasoma shule nzuri. 


Wamama wasiwe bize kupita kiasi. Na wasishindane na wanaume. Waangalie ndoa zao pia.

Wamama hasa wanaofanya kazi na biashara, hawapiki wengi wao, hawafui, hawaangalii watoto.

Kama huyo mama alikua akirudi wanae wamelala, asubuhi wanaenda shule mapemaaaa wala hata haamki hata siku moja kuwaandaa. Chochote kikiliisha mi ndo niseme,

Na nilikua nachapa kazi kama terekta.

Wenzake wakija anawaadithia yani dada ni huyu ni Mungu kanipa, anajua kila kitu, yani hata nikisafiri kikazi nakuta nyumba safi hakuna shida. Najichekesha pale huku moyoni najua yangu.

Ila sasa namshukuru Mungu nimeokoka, nipo na ndoa yangu na nipo makini.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,151,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,203,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,114,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,12,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,208,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,40,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : HAYA SASA SHUHUDA HIZO, WALE WAMAMA MSIOPENDA KUPIKA WALA KUFUA, MPO BIZE KAZINI TU NA BIASHARA TUU
HAYA SASA SHUHUDA HIZO, WALE WAMAMA MSIOPENDA KUPIKA WALA KUFUA, MPO BIZE KAZINI TU NA BIASHARA TUU
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/04/haya-sasa-shuhuda-hizo-wale-wamama.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/04/haya-sasa-shuhuda-hizo-wale-wamama.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content