Iklan Billboard 970x250

DEAR MY WIFE TO BE!

DEAR MY WIFE TO BE!

Sijui unafanya nini kipindi hiki ila  tangu nimejitambua sijaacha kukuombea, wala kuacha kumwambia Mungu akutunze, kweli ninajua unaniombea pia, japo  hujawahi kuniona, nataka nikusisitize Maisha ya ujana nayajua nilipita  nikavuka na kwa umri nilio  nao nimeona mengi, sitamani kurudia ujinga wowote niliofanya, kwa sababu inawezekana nikakutana na wewe hata Leo ukanikuta na ujinga huo nikakupoteza, najitunza nakuheshimu, najiheshimu, mwili wangu nautunza kwa ajili yako na kwa ajili ya Bwana maana Mimi ni hekalu takatifu,...


Ninafanya  bidii ya kusoma, na kufanya Kazi kwa bidii pia katika shughuli zangu zote, zaidi nawekeza mbinguni katika kumtumikia Mungu sijachoka kusali, kwenda kanisani na kuwa na ushirika na watu, huo ndio Upendo Wa Ki Mungu, nakutengenezea mazingira mazuri  ili tuweze kumtumikia Mungu pamoja, ..


Usikate tamaa ukiona wenzako wanatangulia kuolewa waambie yangu inakuja, tumia muda huu kumtumikia Mungu, Fanya Kazi zako kwa Bidii, ishi na watu vizuri, tafuta amani na watu, wazazi Ndugu pia, rekebisha tabia zisizofaa natamani nitakapokuja kukuchukua  rasmi kwa heshima tupewe Baraka na wazazi wako na Ndugu zako pia,


Nakukumbusha kujitunza, usijitupe kwa wanaume Wa mjini wanapojifanya kutaka kukuoa, kuwa makini mpenzi, ni bora unisubiri hata kama nikichelewa  kwa sababu ya Mipango ya Mungu, ila  usiharakishe kumuamini mtu akakuumiza moyo wako, maana utakapokutana nami utanipa shida sana kukupoza moyo itakupa  shida pia kuniamini, utasema wanaume ni walewale NYOKA! usipende kuwa karibu na wanawake wasiojua THAMANI ya wanaume utajiingiza kwenye tabia chafu, na hutojua umuhimu wangu kama mume wako hapo baadae.....


Mke wangu mtarajiwa jifunze neno la MUNGU sana, ili uje unibebe kwenye maombi nitakapohisi kupitishwa au kushindwa, jifunze kuomba, uje usimame kwenye nyumba yetu kama mama SHUJAA! jifunze HEKIMA, UPENDO MSAMAHA, Nina familia Nina wazazi Nina walezi, Nina kaka Dada na wadogo ambao utawaita wakwe wifi  na mashemeji, bila vitu hivyo nilivyosema  hutoweza kuishi nao, sio wao tu Mimi pia utanikuta Nina madhaifu Yale mazuri  yako yatafiti kwenye madhaifu yangu na Yale mazuri  yangu yatafiti kwenye mazaifu yangu ndio maana ukaitwa  MSAIDIZI/BALOZI nitafurahi ukinijua zaidi ya mwanamke yoyote duniani itakujengea uaminifu na imani juu yangu lakini pia utapata Raha maishani na hatokuwepo mwanamke Wa kukupa presha Maisha yako yote, maana moyo wangu nimeamua  kukupa wewe na sio mwingine.


Hakuna siku nayoisubiria kama ya kukutana na wewe, na hakuna siku naingojea kwa hamu kama ya wewe kusema YES I DO kwangu, ayeeeeh na siku ninayoisubiria ni ile natoa mahari kwenu kama asante kwa wazee wako, nakuvika Pete ya uchumba kanisani, na ile siku ambayo nitakosa usingizi ni ile siku nayoamka na kuvaa suti na wewe ndani ya shela nikikuvika Pete na kukubadilisha jina  lako la ukoo na kukuita MKE WANGU WA MAISHA! Sipati Picha familia tutakayoitengeneza  hapo baadae!!!!! sasa mama haya yatatokea kama utasali huko ulipo sali  kwa katika njia za MUNGU na Mimi nimemwambia MUNGU nikikuona tu moyo wangu upate amani sana nawe, omba hivyo pia.


Can't wait to meet you beautiful!!


Ni Mimi wako mtarajiwa mume kutoka kwa Bwana.


SHARE!!!

Related Posts
SHARE
Subscribe to get free updates

Related Posts

Chapisha Maoni

Post Central Advertising