BORA ANGEKUFA BABA KULIKO MAMA

Juzi nilihudhuria msiba wa rafiki yangu mmoja na mkewe. Yeye na mkewe walifariki kwa ajali ya gari, wameacha watoto wawili mmoja wa miaka kumi na mwingine wa miaka minne wakike, mkubwa ni wakiume.


Sasa tukiwa kwenye ule msiba, mimi kama rafiki nilikua karibu sana na wale watoto kwani wananifahamu kama Baba mdogo, kusema kweli nilichokishuhudia kilinifanya nije nimpende mke wangu mara mia zaidi.


Kweli nampenda sana mke wangu lakini kuna wakati namchukuliaga poa nikiwa na mambo yangu najifanya kidume na ninamuudhi. Kwa siku tatu zote nilikua karibu na ile familia tukimalizia msiba, katika kipindi chote hicho watoto walikua wakimlilia Mama yao.


Yaani wakilala wakiamka ni kuniuliza, wananiita anko, Mama yuko wapi (Mara nyingi wnaaniita anko), wanamauuliza Bibi yao Mama yuko wapi. Sasa kilichonifanya nilie nipale ambapo mtoto mkubwa wa miaka kumi ambaye anaelewa kitu kidogo alikua anampembeleza mdogo wake alikua anamuambia.


“Usilie Mama kaenda sehemu nzuri, kaenda kupumzika kwa Mungu na Malaika…” Mdogo wake ndipo alipouliza Baba na yeye, akasema “Amemsindikiza Mama watakaa huko na mimi ndiyo nitakulinda, usiogope nipo hapa. Unakumbuka siku ile Mama alivyotuambia twende kwa Bibi kukaa wenyewe…”


Alimuuliza… “Mimi si nilikulinda…nitakulinda na sasa…Mama anatuangalia lakini sisi hatumuoni….” Kama hapo umelia basi subiri majibu ya yule mdogo wake. Huku akijaribu kujizuia kulia alimuuliza Kaka yake.


“Sasa kama Baba ameenda na Mama si atampiga tena, mimi sitaki Mama apigwe, kwanini asingeenda baba peke yake….???”


Nilianza kuwaza namna ambavyo rafiki yangu yule alikua akimnyanyasa mkewe, namna alivyokua akimpiga na kumsimanga, nilishaongea naye mara nyingi lakini hakujali.


Lakini alikua anawapenda watoto wake na kila siku aliwadekeza ila hawakumkumbuka. Jibu la kijana wake ndiyo lilinifanya niamini kuwa wanadamu si chochote. “Huko hawezi kumpiga, Mama ameenda kwa Mungu, huyo ana nguvu zaidi kuliko Baba. Akimsogelea tu atamchanachana kamakaratasi! Mungu ana upendo hapigi watu wema kama Mama!”


Hapo yule mtoto alikua akiongea kwa uchungu lakini kwa hasira na kwa imani kabisa. Sikuweza kuendelea kuvumilia kuwasikiliza, niliwaacha na kwenda kumuangalia mke wangu, nilimkumbatia na kumuuliza “Mke wangu hivi na mimi nakunyanyasa?”


Aliniangalia kwa mshanagao, aliniuliza kwanini unasema hivyo, nilimuambia hapana niambie tu. Niambie kama kuna kitu nakifanya kinakukwaza ambacho watoto wangu watakiona. Nilimuambia


 “Nataka wanangu waniulizie nikifa, sitaki wanangu wafurahie kifo changu.”


Mke wangu alinikumbatia huku akitokwa na machozi aliniambia “Hakuna mume wangu, wewe ni mume bora, sema uache tu kuweka soksi kwenye makochi na kuacha sahani kitandani.” Nilijikuta natabasmau kidogo, kwani mke wangu alikua na furaha.


Sasa hivi najifunza nisiache soksi kwenye makochi wala sahani kitandani. Najua alikua anatania ila kama kinamkera nitaacha, maisha hapa duniani ni mafupi, watoto ndiyo kitu tunaacha kwaajili ya kututambulisha, sitaki wnaangu wanaitambue kama Baba mkatili.


Lengo la ujumbe huu ni kuwakumbusha wanaume wenye tabia za kuwanyanyasa wake zao.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,151,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,203,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,114,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,12,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,208,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,40,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : BORA ANGEKUFA BABA KULIKO MAMA
BORA ANGEKUFA BABA KULIKO MAMA
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/04/bora-angekufa-baba-kuliko-mama.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/04/bora-angekufa-baba-kuliko-mama.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content