PUNGUZA KULALAMIKA. | BongoLife

PUNGUZA KULALAMIKA.

Kuna wakati unajikuta unajishughulisha na kulaumu mazingira yanayokuzunguka kama sababu za kushindwa au kufanikiwa. Yaani unajisemesha.


🏿 "mie ningesoma mie, nisingekua hapa"


🏿mie ningekua mtoto wa bakhresa, ningeishajenga ghorofa.


🏿ningezaliwa ulaya mie, nisingekua hivi.


🏿ningekua na mtaji mkubwa, ningeishatoka

Yaani, hufikirii kama WEWE ni tatizo. Unaamini kabisa mazingira uliyopo ndio chanzo cha kushindwa kwako. Unaiambia akili yako kila siku kuwa tatizo ni mazingira na sio WEWE.

Usichojua (au usichotaka kuamini) ni kwamba, 


🏿kuna watu wamesoma na wana mafanikio kidogo


🏿Kuna watu wamezaliwa Ulaya na hata hawasomeki.


🏿kuna watu wamezaliwa na wazazi matajiri na hata hawana lolote la kujivunia. 


🏿kuna watu wamekua na mitaji mikubwa na hawajafika popote.


Maisha haya yanajengwa na imani uliyo nayo. Yanaongozwa na kile kilichopo katika kichwa chako. maisha unayoishi leo ni matokeo ya mawazo yako ya jana. Sasa maisha yako ya kesho ni matokeo ya mawazo yako ya leo.


🏿Unajiambia nini mwenyewe?


🏿Unaamini kipi kutoka katika kile unachoambiwa na wenzio?


🏿Unaruhusu mawazo gani yakutawale? Hasi au chanya?


Kile unachojiambia mara kwa mara hata kama sio kweli ndicho akili yako inakitengeneza na kuruhusu utende kama imani yako ilivojijenga.

Ukijiambia huwezi hesabu. Yaani wewe kila mara unajisemesha tu "mie hesabu siwezi" basi akili yako itaamini na hivyo utatenda kama akili yako inavyokutuma. Utajikuta husomi vitabu vya hesabu...kwa kua ukisoma utafaulu na hiyo ni kinyume na imani yako.


Utajikuta huendi kwenye discussions za hesabu kwa kua ukienda, utafaulu na hiyo ni kinyume na imani yako.


Vivyo hivyo katika biashara na kazi. Ukijiambia mara kwa mara kuwa "mimi hii kazi siwezi" "mie biashara siwezi kabisa hii", hicho ndicho kitakachotokea.


Napoleon Hill anasema "whatever the mind of man can conceive and believe, it can achieve.." yaani, chochote kile ambacho akili ya binadamu inajazwa kwacho na inaamini basi itafanikiwa kukipata.


🏿Jaza akili yako na mawazo ya kukujenga.


🏿Soma, sikiliza na angalia mambo yanayokupa nguvu na sio ya kukutisha na kukukatisha tamaa.


🏿wapotezee marafiki vimeo ambao kila kukicha stori zao ni jinsi ilivyo ngumu kufanikiwa katika jambo fulani iwe , kazi, biashara au mahusiano.


Ambatana na wale walioko kwenye njia ambayo wewe unaiendea, HALI YA MAISHA HAITOKAA IWE NZURI PASIPO WEWE KUIRUHUSU IWE IVO.  Kumbuka wewe ndio umeshika usukani wa maisha yako, chagua njia sahihi itakayokufikisha salama kule unakokwenda. 

Jiamini, Vumilia, na wala husikate tamaa.💪 UNATAMANI KUOLEWA?

Badilisha Mwenendo wako


Kisha kuwa na Hofu ya Mungu


DADA mrembo kama wengi wanavyo kuita na huenda kweli we mrembo.lakini mvuto wako unakusaidiaje kufikia malengo yako??


Unatamani siku moja upate KUOLEWA lakini utawezaje ikiwa mda mwingi una utumia kushinda kumbi za starehe...

Vipi utafanikiwa wakat macho yako yanawaza pesa tu hivyo unawapanga waume za watu kisa tu wana pesa...


Kweli PESA inahitajika ili maisha yaende lakin isitumike kama siraha ya kuyadumisha mapenz. Siku zote pesa haitoshi na wala haiwez kukosekana mkifanya juhud kuitafuta.


NDOA ni kuridhika kwa upendo na tabia mengine in jitihada kupata. Toka upo shule msingi mpaka chuo au kazin kichwan mwako unawaza 


"Mwanaume WA kutoka nami sharti awe na pesa afu pia mvuto WA sura na mrefu..awe mjanja WA kunitoa OUT kila ntapo hitaj..awe na gari na nyumba nzuri."


Wangap wenye pesa.nyumba na magar wamekutumia na kukuacha??, wameishia kukunua simu nzuri na mavaz kisha kukuzalisha na wengine magonjwa kukuwchiaa


Toka ume anza Mahusiano umetembea na WA aume wangapi wenye sifa hizo ? Miongoni mwao kuna aliye kuja kwenu na kutoa posa?   ma X wako wangapi ambao Leo hii wamesha Oa Na wana watoto afu wewe bado unashikwa Makalio na wazee ambao huna uhakika na afya zao kisa tu wana pesa ??


Wanaume wangapi walio taka kukuoa ila ulikataa kwa mada sio TYPE Yako.?? Hao walio Type yako kipi kizuri wamekufanyia zaid ya kukutumia na kukuacha?  Afu ulio wakataa leo wana maisha mazur na familia zao


. Mwanamke MWENYE hofu ya MUngu anaomba apate Mwanaume MWENYE upendo WA dhati na kujiheshimu  kuhusu pesa  anaamin waki jibidiisha watapata'


 kuhusu kupendeza nguo atamchagulia..   

Sasa we we endelea  kuwa na. Mawazo ya KAHABA ambae anasubir Giza liingie ili akawinde wenye pesa. Wanawake weenzako wanajituma ktk  masomo na biashara ili wajikwamue kiuchumi we msubir Mume WA Fulani utaona ukifika miaka  30 soko likishuka..


Binti mrembo msomi ila unaona  mwanaume mweenye kuvalia suruali chini ya makalio ndo type yako.akinyoa kiduku na kuvuta masigara kulewa pombe unaona ndo kidume afu mchanga mungu wamuona mshamba.. Utaishia kujaza kaddi za mwaliko WA harusi toka kwa marafiki zako ikiwa hukui kiakil. Pesa ikitafutwa hakunaa MTU mbaya ..


Wanaume  wengi watanashati na wenye pesa sio WAOAJi ila huzalisha na kutoweka.  Jifunze kutokana na makosa ya nyuma. Unaweza kuwa mzuri WA sura ila tabia ikakunyima nafasi ya kuolewa.


Mwanaume hasifiwi sura ila kutafuta pesa Ili watoto  wale na kusoma vizuri.  Magonjwa meeengi tulia utapata  WA kukufaa au Fanya biashara  .pesa ya. Kuhongwa hainaga malengo  utaisshia kula na kuvaa vizuri  lakini vipi ukiwa na miaka 40  utahongwa tena?


Piga magoti sali mwombe MUngu ;huenda kuna mwanaume alikuuumiza ndo maana Leo hii umekata tamaa na kuamua kujichanganya na yeyote. bado unayo nafasi kuutulia kama zamani na utapendwa.hata kama ulisha zalishwa bado unayo nafas kuolewa kaama Mungu alipanga 


Bado we mrembo

Bado unayo nafas kujaribu tena

Jifunze kujitegemea

Uzur wako haukupi mume 

Uuzur wako utakufanya tu unywe bia na kununuliwa supu


UJANA UNA MWISHO WAKE Ukibahatika kupata Mwanamke anayejielewa, atakupa *Amani* na utalala usingizi mnono. Hili la kupewa Amani ni pana sana...... ila itoshe kusema kuwa ukipata mwanamke _“pasua kichwa_” unaweza ukajikuta unatamani kuwa baharia ili muda mwingi ushinde baharini na samaki.


2. Pia Tendo la Ndoa (pamoja na kutiwa moyo nk) ni *dawa nzuri sana* ya mwanaume Mwenye msongo wa mawazo. Stress za kazini, kwenye biashara nk. Zote hizo haziwezi kumsumbua mwanaume aliyebahatika kupata mke sahihi. 


Hivyo mwanamke *anayejielewa* anampa mume wake haki hii bila choyo wala masharti ili mradi mazingira na hali vinaruhusu na hawaendi kinyume na utaratibu. 


3. Na hayo mawili (na mengineyo yenye muelekeo huo) yakifanyika kwa *usahihi*, mafanikio yatamiminika mpaka mshangae. 


Ndio maana nitasisitiza tena na tena, Kwa wale wanaume wenye wito wa kuishi maisha ya NDOA, hawawezi kuishi maisha yenye mpangilio mzuri bila kuwa na mwanamke sahihi pembeni yake - achilia mbali mafanikio.

COMMENTS

BLOGGER

VISA NA MIKASA $type=THREE

Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,171,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,212,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,126,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,7,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : PUNGUZA KULALAMIKA.
PUNGUZA KULALAMIKA.
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/03/punguza-kulalamika.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/03/punguza-kulalamika.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content