Iklan Billboard 970x250

MAPISHI YA SUPU YA KUKU NA VIAZI/MBATATA

MAPISHI YA SUPU YA KUKU NA VIAZI/MBATATA

SUPU YA KUKU NA VIAZI/MBATATA

SUPU YA KUKU NA VIAZI/MBATATA

MAHITAJI YA KUPIKA SUPU YA KUKU NA VIAZI/MBATATA
 • Kuku - 4 LB
 • Viazi/mbatata - 3
 • Kitunguu maji - 1
 • Kitunguu saumu(thomu/galic) - 5 chembe
 • Pilipili mbichi - 2
 • Nyanya ya kusaga - 1 kijiko cha chai
 • Pilipili manga ya unga - ½  kijiko cha chai
 • Haldi/tumeric/bizari ya manjano - ¼  kijiko cha chai
 • Mafuta ya zaytuni - 2 vijiko vya supu
 • Kotmiri (coriander freshi) - 1 msongo
 • Ndimu/siki - 2 vijiko vya supu
 • Chumvi - kiasi

JINSI YA KUPIKA SUPU YA KUKU NA VIAZI/MBATATA

 1. Osha kuku na ukate vipande vipande kiasi
 2. Menya viazi/mbatata, katakata vipande kiasi.
 3. Menya kitunguu maji ukate vidogodogo
 4. Weka mafuta katika sufuria, kisha tia vitunguu vikaange kidogo tu hadi viwe laini.
 5. Kisha  tia vipande vya kuku, chumvi, pilipili manga, thomu ilochunwa (grated) au kukatwakatwa vipande vidogodogo.
 6. Tia nyanya,  haldi, na maji kiasi.
 7. Tia viazi/mbatata na iache ichemke hadi kuku na viazi/mbatata ziive.
 8. Katakata kotmiri na pilipili mbichi ndogo ndogo utie mwishoni.
 9. Tia ndimu au siki ikiwa tayari kuliwa  na mkate au upendavyo

Related Posts
SHARE
Subscribe to get free updates

Related Posts

Chapisha Maoni

Post Central Advertising