KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 18 | BongoLife

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 18

RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA KUMI NA NANE.

MTUNZI : ALEX KILEO..

_______________
ILIPOISHIA..
________________

Kile kiumbe kikasema,
kitu kitakachotokea asubuhi
tutakapoamka tusishangae, Kisha
upepo mkali ukakibeba na paa la nyumba yetu likarudi kama mwanzo, tukabaki tunashangaa huku kila mmoja akiwaza lake, ila mwisho
tukajadiliana na kukubaliana
tusubiri mpaka kesho ili tuone hicho
kitakachotokea, tukalala.

Kesho tulipoamka ndipo
tukapata kitu kilichotupa mshtuko, kiasi kwamba nikapoteza fahamu...

____________
ENDELEA..
____________
tulimkuta mtoto wetu wa pekee
amekufa kwa mtindo ule ule aliokufa
nao mtoto wetu wa kwanza.

Ndugu wa mume wangu walikuwa wanajua
chanzo cha vifo vyote vya
wanangu,baada ya mazishi kuisha na
watu kutawanyika, ndugu wa baba
yako wakamuita pembeni na
kumshawishi aurudie ule mzimu na
kuuomba radhi ili mambo yake
yarudi kama awali, ila baba yako
akakataa.

Baada msiba kuisha, ule
mzimu uliendelea kumuandama
baba yako, mi kuona umezidi ikabidi
nimwambie baba yako aukubali ili
aulee kama mwanzo.

Baada ya kauli ile, usiku mzimu ulitutokea tena tukiwa tumelala kitandani na kuongea maneno makali na ya kutisha juu ya msimamo wa baba yako, na kisha mzimu ukaongea maneno mazuri na kunisifia sana juu ya ushahuri niliompa baba yako, kwa ushauri ule niliompa baba yako, kuanzia hapo
ule mzimu ulinipenda mimi na
kuahidi kuwa kamwe hautanidhuru
mimi na mtu yeyote yule ambae ana
damu au nasaba moja na mimi, yaani mwanangu
na ndugu zangu wote tuliochangia wazazi wote, au baba tu, au pia mama tu.

"ndio maana Sajenti Minja haukumdhuru eee!?" Omary akauliza huku akimuangalia Kayoza,

"inawezekana
mwanangu, labda Minja hakudhurika kutokana na ahadi aliyonipa mzimu" Mama kayoza akajibu,

"Duh, hii habari inazidi kunisisimua, inawezekanaje mimi nikawa mzimu?" Kayoza aliuliza huku akijishangaa,

"Je unaamini kuwa nabii Musa aliweza kuipasua bahari ya shamu na akapita na wanaisraeli?" Mama Kayoza alimuuliza mwanae,

"Hiyo naamini" Kayoza alijibu huku akimuangalia mama yake,

"Sasa kwa nini huamini kuwa hata wewe unaweza kuwa mzimu?" Mama kayoza alimuuliza mwanae,

"Sasa utafananishaje mambo ya Mungu na uchawi?" Kayoza alimjibu Mama yake huku akionekana kutofurahia hilo swali,

"Huo uchawi uliumbwa na Mungu na manabii waliutumia ila waliuita muujiza na si uchawi" Mama Kayoza alimfafanulia mwanae,

"Endelea na simulizi yetu mama bwana" Kayoza akamuambia mama yake,

"Ngojeni kidogo" Mama kayoza aliongea kisha akainuka na kuelekea msalani.

****************

Sajenti Minja alienda mpaka nyumbani kwake, akaingia mariwatoni na kuanza kusafi mwili.

Alipomaliza alienda mpaka katika meza na kuanza kuandika barua ya kuacha kazi. Aliindika kwa ufanisi mkubwa kwa kutumia ile nakala ya barua aliyopewa na yule Dada polisi.

Alipomaliza kuandika aliirudia tena na tena kuisoma na kuona haina makosa.

Akaiweka vizuri katika bahasha na hakuona haja ya kuchelewa kuiwasilisha ofisini kwa mkubwa wake ingawa muda ulikuwa umeenda sana.

Akatoka nje na kuchukua gari iliyomfikisha katika kituo cha kazi, na kwenda moja kwa moja mpaka kwa yule dada aliyempa maelekezo hawali, kwa bahati nzuri alimkuta,

"Umerudi tena? umemaliza nini kuandika?" Yule dada aliuliza huku akiwa anaamini Sajenti Minja kuna kitu kingine kafuata na wala sio kuwasilisha barua ya kuacha kazi,

"Ndio nimeileta barua hivyo" Sajenti Minja alijibu huku akimpatia ile bahasha yenye barua ndani,

"Kha! Wewe mtoto mbona umeandika haraka hivyo, hujajipa hata muda wa kufikiri?" Yule dada alimuuliza huku akimshangaa Sajenti Minja,

"Mpaka nimefikia hatua hii, ujue nimefikiria sana" Sajenti Minja alijibu huku akionekana kutofurahishwa na maswali ya yule dada,

"Wenzako wanatafuta kazi, wewe unaacha" yule dada alimuuliza Sajenti Minja huku akipokea ile bahasha,

"Ni bora nikae bila kazi kuliko kupambana na kiumbe cha ajabu" Sajenti alijibu kijeuri,

"Na kwenye barua umeandika sababu ya kuacha kazi ni kiumbe cha ajabu?" Yule dada aliendelea kuuliza huku akijua anamkera Sajenti Minja,

"Ifungue uisome, ukimaliza utairudishia kwenye bahasha nyingine" Sajenti Minja alijibu,

"Unaona huo ndio utakuwa ustaharabu?" Yule dada nae alimuuliza,

"Nadhani ndio itakuwa nzuri zaidi kuliko kuniuliza maswali ilihali majibu nimekupa ndani ya hiyo bahasha" Sajenti Minja alijibu,

"Okey, unaweza kwenda" Yule dada aliongea huku akiwa amekasirishwa na majibu ya Sajenti Minja,

"Kuna hivi vitu pia" Sajenti Minja alimpa bahasha nyingine ila ilikuwa kubwa zaidi ya ile ya mwanzo na pia haikufungwa,

"Na humu kuna nini?" Yule dada aliuliza huku akiipokea ile bahasha,

"Ipo wazi hiyo bahasha, unaweza tu kuangalia vilivyomo ndani" Sajenti Minja alijibu kisha yule dada akaingiza mkono na Kutoa kitu kimoja moja, ilikuwepo bastola, namba ya uaskari na kitambulisho cha Sajenti Minja mwenyewe.

"Sasa hivi unaniletea vya nini?" Yule dada aliuliza huku akimshangaa Sajenti Minja,

"Unapoacha kazi si unatakiwa kurudisha hivi vyote?" Sajenti Minja aliuliza,

"Hivyo utamkabidhi mkubwa wako, tena atakapokubaliana na maombi yako" Yule dada alijibu huku akivirudisha vile vitu katika mfuko ambao vilikuwepo hawali,

"Sasa kama nimeshawasilisha barua, hivi nikae navyo vya nini" Sajenti Minja aliuliza,

"Zingatia nilichokwambia, tusibishane hapa. Tena ulete mkanda, kofia na buti" Yule dada alimalizia,

"Sikupewa magwanda mimi, narudisha nilichopewa" Sajenti Minja alijibu huku akivipokea vile vitu vikiwa ndani ya ile bahasha,

"Sawa, kesho mchana nenda kwa mkuu, nadhani atakuwa ameshaipitia barua yako" Yule dada alimpa maelekezo Sajenti Minja.

Baada ya hapo Sajenti Minja akaondoka.

*****************

Mamá kayoza alipotoka msalani, akanywa maji kisha akaendelea,

"kuanzia siku ambayo mzimu aliniahidi hatonidhuru mimi na kizazi changu, nikawa najihisi niko tofauti na
mwanzo, kila nilichofanya
nilifanikiwa, nadhani mzimu aliamua kunionesha namna anavyonijali.

Baada ya miezi mitatu toka kaka yako wa pili amefariki, kwa bahati nikashika
mimba.

Siku ambayo niligundua nina mimba, mzimu alitutokea tena usiku na kuniomba sana niendelee na msimamo wangu wa kumshahuri baba yako juu ya kuujali huo mzimu, nami nikaitikia kwa kukubaliana nao.

Mimba ilipofikisha miezi tisa ndipo nilikuzaa wewe,
tena hapo ni baada ya kukaa mwaka mmoja tangu nilipompoteza
mwanangu wa pili.

Baada ya wewe kuzaliwa, sasa hapo yule
mzimu alichachamaa, alitutokea usiku na kusema kuwa anataka
kuingia kwenye mwili wa baba yako, Baba yako hakukubali hilo jambo,
hata baba yako alipokataa yule
mzimu hakuwa na cha kufanya kwa
sababu nilimuomba ampe baba yako muda wa kufikiri kwanza, na kwa kuwa mzimu aliniahidi kutonidhuru mimi
na ndugu zangu na damu yangu kwa
hiyo kazi yake ilikuwa kunilinda mimi
na nasaba zangu, mzimu akaondoka.

Miaka ikasogea na
mzimu haukuchoka kumsumbua
baba yako, ulitutokea kila siku na kuongea maneno ya vitisho juu ya Maisha ya baba yako, ila Baba yako aliendelea kushikiria msimamo wake.

Ikafika kipindi baba yako
akaanza kuumwa, aliumwa wiki
nzima na tulipoenda hospitali ugonjwa ukawa hauonekani, ghafla hali yake ikawa mbaya
zaidi, mwili ukadhohofika na hakuweza hata kuamka
kitandani.

Ule mzimu kuona Baba yako yupo katika hali ile, ukabadilisha
maamuzi ya kumuingia baba yako,
ukawa unataka kuingia ndani ya
mwili wako, ila baba yako
akapinga tena jambo hilo, tena alilipinga kwa nguvu zote ingawa alikuwa mgonjwa.

Kwa mila za kijijini kwa
baba yako mtu anapokuwa anaumwa
sana anatenganishwa na mke au
mme wake. Huduma zote muhimu anakuwa anahudumiwa na
mama yake au ndugu zake, kwa hiyo
baba yako alikuwa anahudumiwa na
mama yake ambaye ni bibi yako.

Sasa siku moja wakati niko nje
nakunyonyesha huku natayarisha
chakula, ghafla upepo ulivuma kwa
nguvu sana, kisha ukaingia katika
chumba alichokuwepo baba yako ambaye pia ndani alikuwa bibi yako.

Baada ya dakika tano za ukimya katika chumba kile, nikasikia mabishano yamezuka kati
ya bibi yako na baba yako, mara ghafla bibi yako akaja kukuchukua
mapajani kwangu, kwa ahadi ya kwamba kuna kazi anaenda kuifanya na
anakurudisha mda si mrefu.

Akaingia na wewe kwenye chumba alichokuwepo
baba yako, kisha yale mabishano
yakaendelea, baada ya muda kidogo
nikaskia baba yako analia kwa sauti
ya juu sana, ndipo nikatoka mbio hadi
katika chumba alichokuwepo Baba yako na
mama yake ambaye ni bibi yako, nikakukuta wewe Kayoza
unamnyonya damu baba yako" Mama kayoza aliongea
maneno haya huku machozi yakianza kumtoka....

******ITAENDELEA******

COMMENTS

BLOGGER

VISA NA MIKASA $type=THREE

Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,171,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,212,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,126,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,7,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 18
KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 18
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/03/kijijini-kwa-bibisehemu-ya-18.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/03/kijijini-kwa-bibisehemu-ya-18.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content