KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 13

RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA KUMI NA TATU

MTUNZI : ALEX KILEO..

______________
ILIPOISHIA..
______________

"ooh, karibu babu, vipi
mbona umekuja bila taharifa" Babu
akauliza huku akimpa mkono Omary
na Kayoza.

"ni matatizo babu,
nitakusimulia tu babu" 0mari akamwambia babu yake huku
akifurahi babu yake kumtambua,

"Naona umekuja na mwenzako?"
Babu akamuuliza Omary,

"ndio babu" 0mari akajibu,

"karibu kijana" Babu akamwambia
Kayoza huku
akimpa mkono, ila kitu cha ajabu,
babu aliung'ang'ania mkono wa
kayoza kwa dakika mbili nzima huku
akiwa amemkazia macho,

"kijana una mzigo mzito sana wa matatizo" Babu alimwambia Kayoza
huku machozi yakimtoka..

_____________
ENDELEA....
_____________

kayoza akashtuka,

"hapana babu, mimi
niko sawa tu" Kayoza akamjibu babu
huku akijilazimisha kutabasamu,

"kijana jaribu kuwa mkweli,
vinginevyo utapata matatizo zaidi ya hayo
yaliyokukuta" Babu akamsisitiza
Kayoza,

"babu tutakusimulia baadae" Omary akaingilia kati baada ya kuona Kayoza hawezi kukubali.

Babu yake na Omary
anaitwa Mzee Salum Said Omari
Shekindile Mkwiji, ila jina maarufu
lililozoeleka kwa watu wa pale
kijijini, wanamuita Mzee Mkwiji,
huyu mzee katika maisha yake ya
ujana alioa wanawake saba na
kuwazalisha watoto zaidi ya hamsini,
na ana wajukuu wasio na idadi, ila
kitu ambacho kilichokuwa
kinawachanganya watoto wake, ni
kuwa huyu mzee hakuitaji kabisa
msaada wao, wakimpelekea pesa,
anawarudishia.

Kuna kipindi watoto wake walijipanga
wamjengee nyumba nzuri, akakataa,
ila watoto wake hawakujua sababu
ya yote hayo, ila sababu aliijua
mwenyewe mzee Mkwiji, na sababu
yenyewe ni kuwa na mizimu ya
kiganga aliyorithishwa na baba yake,
ambayo yenyewe inataka anayeimiliki
awe anatoa tu misaada, na asiwe
anapokea, anaishi peke yake, wake
zake watano walishafariki, na wawili
aliwapa talaka.

Ni mganga
anayependwa sana katika eneo
analoishi.

Baada ya kupata chai na
mihogo, Omary na Kayoza walimsaidia
kazi ndogo ndogo babu yao, baada
ya shughuli za hapa na pale kuisha,
wakatindika mkeka nyuma ya
nyumba, wakaanza kumsimulia Mzee
Mkwiji, kuanzia mwanzo hadi
mwisho, Mzee Mkwiji aliwasikiliza
kwa makini, kisha akaingia ndani
kwake akatoka na kibuyu kidogo,
alafu akamwambia Kayoza ateme
mate chini, Kayoza akatema, Mzee
Mkwiji akamimina dawa kidogo
kutoka kwenye kibuyu alafu
akaichanganya na mate ya kayoza,
ukatokea moshi mweusi, ukawa
unapanda juu kuelekea mashariki,

"mh, kazi ipo" Mzee Mkwiji
akajisemea huku akitingisha kichwa kwa masikitiko, kisha akarudia tena
kufanya kama mwanzo, sasa hivi ule
moshi ulipotoka, ukaingia puani kwa
mzee Mkwiji, kisha akapiga chafya,
akawa kama kasinzia, alikuwa katika
hali hiyo kwa muda ya dakika tatu, kisha
akafungua macho na kusema,

"pole
sana kijana, ningekusaidia ila
mizimu yangu imeingiwa na uoga
kupambana na mzimu ulionao" Mzee Mkwiji aliongea huku akimuangalia Kayoza kwa jicho la huruma,
Kayoza akapoteza matumaini, ila
babu akaendelea kumwambia,

"mama yako ndio anaweza kuwa
msaada mkubwa kwako" Mzee Mkwiji alitoa kauli ilijenga swali kwa Kayoza,

"Samahani babu, umesema nina mzimu?" Kayoza aliuliza kanakwamba hakumsikia Mzee Mkwiji,

"Tena wa hatari sana" Mzee Mkwiji alijibu,

"Sasa unaposema mama yangu ndio anaeweza kuwa msaada kwangu hapo unanivuruga kidogo, kwa maana mama yangu sio mganga, kwa hiyo ni vipi atakuwa msaada kwangu?" Kayoza alimuuliza Mzee Mkwiji,

"Kwa kweli hilo swali nitashindwa kukujibu, ila mizimu yangu ndio imeniambia hivyo" Mzee Mkwiji alijibu huku akimwaga yale maji yake aliyofanyia uganga,

"Ila naweza kupona, si ndio?" Kayoza alimuuliza tena Mzee Mkwiji,

"Kama mizimu imesema msaada upo, basi unaweza kupona" Mzee Mkwiji alitoa jibu lililompa matumaini Kayoza,

"Sasa inabidi kesho tu nisafiri, niende kwa mama" Kayoza aliongea huku akimuangalia Omary,

"Ungepumzika kwanza mjukuu wangu, yaani jana umekuja alafu uondoke kesho? Shinyanga ni mbali kutoka hapa" Mzee Mkwiji aliongea na kumfanya Kayoza ashtuke,

"Umejuaje Nataka niende shinyanga?" Kayoza aliuliza huku akishangaa,

"Si ndio mama yako yupo uko?" Mzee Mkwiji nae aliuliza badala ya kujibu,

"Ndio, sasa umejuaje yupo uko?" Kayoza aliuliza tena huku akistahajabu maono ya Mzee Mkwiji,

"Sina uganga wa kubahatisha, mizimu yangu uwa inaniambia ukweli" Mzee Mkwiji alijibu huku akitabasamu,

"Aisee wewe mzee ni kiboko" Omary aliongea huku akicheka,

"Kama nilivyosema hawali, kesho naondoka" Kayoza alirudia Kutoa taharifa,

"Itabidi twende wote" Omary aliongea,

"Wewe baki tu ndugu yangu, msaada ulionipa ni mkubwa sana. Nakushukuru sana" Kayoza alimwambia Omary,

"Hapana siwezi kubaki, kama kutafutwa ni mimi ninayetafutwa kwa maana picha yangu ndio ipo katika vyombo vya habari, kwa hiyo ni bora niwe na wewe popote niendapo kwa maana wewe pekee ndiye unaweza kuniokoa mikononi kwa polisi" Omary aliongea kwa huzuni,

"Omary unafuata kifo uko" Mzee Mkwiji alimwambia mjukuu wake,

"Kivipi babu?" Omary aliuliza,

"Mnapoenda mtapata utatuzi wa tatizo lenu, ila kurudi salama ni kazi sana" Mzee Mkwiji aliwaambia na kufanya vijana waogope,

"Kwa hiyo tukienda uko shinyanga tunakufa?" Omary aliuliza kwa taharuki,

"Shinyanga hamtokufa, ila kazi isipofanikiwa shinyanga, basi mtakuwa na safari nyingine itakayoambatana na kifo" Mzee Mkwiji alizidi Kutoa taharifa mbaya kwa vijana,

"Kwa hiyo tusiende au?" Kayoza aliuliza,

"Usipoenda itakuwa umeridhika na Maisha ya kuua, cha muhimu ni uende, ila kuweni makini na maamuzi yenu uko muendako" Mzee Mkwiji aliongea huku akijinyanyua mkekani,

"Mbona umakini tunao tu babu" Kayoza alijibu wakati babu akiingia ndani,

"Pamoja na umakini wako, kifo chako kitakuwa cha kujiua mwenyewe" Babu aliongea kwa utani huku akipotelea ndani,

"Babu mzinguaji kweli, kaongea vya maana wee, ameona amalizie na utani" Kayoza aliongea huku akicheka,

"Ndivyo alivyo huyo, akiona maswali yanakuwa mengi uwa anayapotezea kwa utani" Omary aliongea huku wakikunja mkeka kwa lengo la kuingia ndani.

**********

Sajenti Minja alienda hospitali na kufanyiwa vipimo katika jeraha lake na hakukutwa na tatizo lolote,

"Daktari rudia kunipima, haiwezekani nikutwe sina kitu" Sajenti Minja aliongea na pia akishangaa majibu ya vipimo,

"Ridhika na majibu, au kama hutuamini nenda kajaribu kucheki kwenye hospitali nyingine, labda jibu linaweza kuwa tofauti" Daktari alimjibu kistaharabu Sajenti Minja,

"Sio kama nadharau huduma zenu, kinachotisha ni kiumbe kilichoniachia hizo alama, kiko kama zombi, nahisi na mimi naweza kubadilika na kuwa kama hicho kiumbe" Sajenti Minja aliongea kwa upole huku akishika eneo la jeraha lililokuwa na bandeji,

"Acha kuamini movie au masimulizi ya kizombi, zile uwa ni habari tu za kusadikika zisizo na ukweli wowote" Daktari alijibu huku akicheka,

"Hayajakukuta wewe na ndio maana unasema hivyo" Sajenti Minja aliongea huku akinyanyuka katika kiti,

"Usiondoke, bado hatujamaliza" Daktari alitoa kauli iliyomrudisha Minja kwenye kiti,

"Bado nini?" Sajenti Minja aliuliza,

"Kuna dawa unatakiwa ukanunue kwa ajili ya kukausha jeraha lako" Daktari aliongea huku akimpatia Sajenti Minja kikaratasi chenye maandishi yaliyoandikwa kwa mkono, Sajenti Minja akapokea na kuondoka.

***************

Baada ya Kayoza na Omary kumaliza mambo yao madogo madogo, ilipofika jioni Kayoza akachukua
simu ya Omari akampigia mama yake,
baada ya salamu,

"mama keshokutwa
nitakuja huko" Kayoza akamwambia
mama yake.

"chuo mmeshafunga?"
mama yake akauliza.

"Sio mda mrefu
sana toka tufunge, mama" kayoza akamjibu,

"uko wapi, au kwa shangazi yako?" mama yake akamuuliza.

"nipo Tanga kwa rafiki yangu" Kayoza
akajibu.

"Kuna nini uko Tanga, au matembezi tu?" Mama Kayoza aliuliza,

"Ni safari tu ya bahati mbaya mama" Kayoza alijibu,

"Kwanini iwe ya bahati mbaya?" Mama Kayoza akauliza kwa shahuku,

"Ngoja nije, tutaongea vizuri mama" Kayoza alimwambia mama yake,

"Lakini wema upo au?" Mama Kayoza alimuuliza mwanaye,

"Nikija tutaongea mama" Kayoza alijibu,

"Sasa si inabidi kwanza nijue kama kuna wema au lah?" Mama Kayoza alitilia mkazo msimamo wake,

"Wema upo" Kayoza alijibu ili kumridhisha mama yake, kwa maana anamjua jinsi alivyo na maswali mengi,

"haya, karibu mwanangu"
Mama yake akamwambia, kayoza akaitikia kisha akakata simu.

********

Hiyo siku ya Safari ilipofika ikabidi waondoke
pamoja na Omari kama walivyokubaliana. Mzee Mkwiji akawafanyia tambiko dogo kwa ajili ya usalama wao, kisha
wakaagana nae kwa ahadi ya kurudi
tena baada ya kutoka uko waendako.

Wakaenda mpaka mjini, wakaingia
kwenye mashine ya kutolea pesa (ATM), wakachukua
pesa ya kuwatosha wao, wakatafuta
mabasi ya Shinyanga wakapanda, safari ya kuelekea shinyanga ikaanza..

******ITAENDELEA******

COMMENTS

BLOGGER
Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,166,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,210,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,125,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,165,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 13
KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 13
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/03/kijijini-kwa-bibisehemu-ya-13.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/03/kijijini-kwa-bibisehemu-ya-13.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content