KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 08 | BongoLife

KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 08

RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA NANE.

MTUNZI : ALEX KILEO.

_______________
ILIPOISHIA...
_______________

"taxi hiyo imeingia sasa hivi, ongea
na dereva
akupeleke" mwenzake alimjibu huku
akinyooshea kidole gari waliomo
ndani
wakina kayoza,

"poa basi, tutakutana kesho ili tujue
ofisi itasema nini kuhusu hili tukio"
Sajenti Minja aliongea Kisha
akapeana mikono na mwenzake ikiwa
ni ishara ya kuagana.

Alafu akawa anaelekea kwenye gari
ambalo ndani wapo wakina Kayoza....

____________
ENDELEA...
_____________

Sajenti Minja aliendelea kuisogelea ile taxi waliyokuwamo wakina kayoza,

"Au mkuu..." Dereva wa kwenye ile gari ya Polisi aliita na kumfanya Sajenti Minja asimame,

"Unasemaje tena Timo?" Sajenti Minja aliuliza huku akisimama,

"Njoo nikukimbize mara moja, maana nahisi waliopo ndani hawatatoka sasa hivi" Dereva wa gari la polisi aliongea,

"Ni jambo la kheri, ila wakitoka alafu wakakukosa?" Sajenti Minja aliuliza,

"Wewe twende tu, hata usijali" Dereva wa Gari ya polisi alijibu na kumfanya Sajenti Minja aache kuifuata gari waliyokuwepo wakina Kayoza na kurudi kuipanda gari ya Polisi, kisha ikaondoka.

Wakina Omary walikuwa katika taxi walishuhudia kila hatua iliyokuwa inafanywa na Sajenti Minja, na kila mmoja tumbo lilikuwa na joto,

"Umeshakuwa mkosi huu, hamna ya kushuka, bora tuondoke tu" Omary aliongea huku akitetemeka,

"Na hivyo vidonda vyako vitapona vipi bila kutibiwa?" Denis alimuuliza Omary,

"Tutajua mbele ya safari" Omary alijibu,

"Usije ukaoza mgongo" Denis alimtahadharisha Omary,

"Dereva ebu tupeleke Lodge yoyote iliyo karibu na Stendi ya mabasi ya mikoani" Kayoza aliongea baada ya ukimya wa muda mrefu na kuwafanya wenzie wamuangalie,

"Vipi, unajisikiaje bab?" Omary alimuuliza kayoza huku akimshangaa,

"Tutaenda kuulizana mbele ya safari" Kayoza alijibu huku akijishangaa alivyochafuka kama alilala kwenye vumbi.

Dereva wa taxi aliindoa gari eneo la hospitali na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye eneo ambalo aliamini zinapatikana nyumba za wageni na pia ni jirani na stand ya mkoa wa Dodoma, na kuwashusha hapo,

"Shilingi ngapi unatudai?" Omary alimuuliza Dereva baada ya kushusha mabegi yao,

"Kwa mizunguko tuliyofanya, uwa nafanya shilingi elfu kumi na tano, kwa kuwa nyinyi Mi washkaji, nitawafanyia elfu kumi" Dereva taxi aliongea huku akitabasamu,

"Punguza bwana, sisi tuna elfu saba" Omary aliongea kwa kulalamika,

"Suka shika pesa yako" Kayoza aliongea huku akimpa noti ya shilingi elfu Dereva taxi,

"Ungesubiri kwanza nimsaundishe" Omary aliongea huku akimlaumu Kayoza,

"Hakuna kusaundishana hapa, unapoteza muda tu" Denis aliongea huku akibeba begi lake na kuingia ndani, Kayoza akamfatia.

"Niachie namba yako, kesho asubuhi tunaweza kukupigia utufuate ili utupeleke stand" Omary alimwambia Dereva taxi,

"Stand si hapo nyuma tu, mnaweza kwenda hata kwa mguu" Dereva taxi alimjibu Omary,

"Wewe nipe tu hizo namba, unakuwa kama sio mfanyabiashara bwana" Omary aliongea na kumfanya Dereva taxi ampe namba zake za simu na kisha wakaagana.

Omary akachukua begi lake na kuingia nalo ndani, kwa bahati nzuri aliwakuta wenzake wakimsubiri mapokezi,

"Jamaa unatuyeyusha sana" Denis alimwambia Omary huku wakielekea sehemu vyumba vilipo,

"Nawayeyusha na nini sasa?" Omary alihoji huku akiwafuata wenzake,

"Sasa muda wote ulikuwa unaongea nini na Dereva?" Kayoza alimuuliza Omary,

"Nilikuwa nachukua namba ya simu ya Dereva" Omary alimjibu kayoza,

"Sasa namba ya simu ya nini wakati stand ipo karibu?" Denis aliuliza,

"Hamuwezi jua, kama sio kesho anaweza kuwa msaada siku nyingine" Omary alijibu wakati Denis akiufungua mlango wa chumba walichotakiwa kulala,

"Alafu huo ujinga wako uachage. Kwanza jana ilikuwaje mpaka ukakamatwa?" Denis aliuliza wakati akikaa kitandani,

"Dah, ilikuwa kama movie yaani" Omary aliongea huku akicheka utadhani anasimulia jambo zuri,

"Hivi utakua lini wewe?" Kayoza aliuliza kwa hasira,

"Kwani nimefanyaje boy?" Omary aliuliza huku akimshangaa Kayoza,

"Wewe si umeulizwa ilikuwaje ukakamatwa jana? Badala ya kujibu unaleta utoto" Kayoza aliongea huku akivua suruali,

"Sasa si ndio nilikuwa naanza kujibu?" Omary aliongea,

"Jibu sasa, acheni kulumbana" Denis aliongea huku akimuangalia Omary.

Omary akaelezea mwanzo mpaka mwisho wa kukamatwa kwake na mpaka Mipango ilivyosukwa na Sajenti Minja ili kuwaingiza mtegoni Kayoza na Denis.

"Sajenti Minja ndiyo nani?" Denis aliuliza,

"Yule polisi aliyetaka kuja kwenye taxi tuliyokuwepo" Omary alimjibu Denis wakati huo Kayoza alikuwa ameingia bafuni kuoga,

"Alafu tumuulize Kayoza ni kwa nini alikuwa katika umbo la kutisha namna ile kule lodge?" Omary alimshauri Denis,

"Kweli aisee, ila tutaanzaje sasa? maana anaogopesha" Denis aliuliza kwa mashaka,

"Hawezi kutufanya kitu bwana, kama angekuwa na lengo la kutudhuru, angetudhuru toka zamani" Omary aliongea kwa kujiamini,

"Kama ni hivyo ni sawa, ila utamuuliza wewe" Denis alimwambia Omary,

"Sawa, mimi nitamuuliza" Omary alijibu kisha nae akavua suruali kwa lengo la kwenda kuoga Kayoza akitoka bafuni.

********

Baada ya saa moja, wote watatu walikuwa tayari wameshaoga na kila mmoja alikuwa akiwaza jambo lake,

"Jamani eeh, wote tumebeba mabegi lakini hatujahambiana kila mmoja wapi anaelekea" Denis aliuliza baada ya ukimya wa muda mrefu,

"Sasa si tulikuwa na matatizo, unadhani huo muda wa kuambiana ungepatikana vipi?" Kayoza nae aliuliza,

"Mimi naenda Tanga, hadi hapo tayari nimeshawajibu" Omary alijibu huku macho yakiwa kwenye simu yake,

"Tanga kufanya nini? Wewe kwenu si ni kondoa wewe?" Denis alimuuliza Omary huku akicheka,

"Kule kuna babu yangu, sijamuona siku nyingi na inabidi nikamuone kwanza kama wiki mbili hivi" Omary aliwaelezea wenzake,

"Na wewe Kayoza unaenda wapi?" Denis alimuuliza kayoza,

"Mimi nitaenda Bukoba" Kayoza alijibu,

"Mimi kama kawaida, Dar hiyo" Denis aliongea kwa furaha,

"Nadhani tutaondoka pamoja ingawa tutapanda mabasi tofauti" Omary aliwaambia wenzake,

"Wazo zuri sana hilo" Denis aliongea kukubaliana na Omary,

"Ila ndugu yetu, ebu tueleze nini tatizo?" Omary alimuuliza Kayoza,

"Tatizo lipi?" Kayoza nae akamuuliza Omary na kufanya washangaane,

"Hujui au?" Omary aliuliza kwa upole,

"Sio sijui, ebu liweke swali lako vizuri ili nijue nianzie kujibu wapi" Kayoza nae alijibu kwa upole,

"Sawa. Ilikuwaje ukawaua wakina Stellah kule Guest?" Omary aliuliza huku akiwa na wasiwasi kidogo,

"Dah, sijui nianzaje kujibu, ila kifupi Stellah naweza kusema sijamuua ila Tausi nilimuua bila kutegemea" Kayoza alijibu huku machozi yakimtoka kuonesha kujutia kile alichokifanya,

"Sasa kama hukumuua Stellah ni nani alimuua wakati mlikuwa peke yenu chumbani?" Denis aliuliza,

"Mimi sijui ndugu zangu, niliamka asubuhi nikamkuta katika hali ile na sijui nini kilitokea" Kayoza alijitetea,

"Na Kwanini ulimuua Tausi?" Omary aliendelea kuuliza,

"Tausi nilimuua bahati mbaya baada ya kumziba mdomo asipige kelele alipouona mwili wa stelah, Kumbe wakati namziba mdomo nilimziba na pua akajikuta anashindwa kupumua" Kayoza aliwaeleza wenzake,

"Hiyo hali ya kubadilika na kuwa kiumbe cha kutisha inatokana na nini?" Denis alimuuliza Kayoza,

"Mimi?" Kayoza aliuliza huku akijioneshea kidole,

"Sasa kwani naongea na nani?" Denis nae aliuliza huku amemtolea macho Kayoza,

"Mnanishangaza mjue, mimi sijaiona hiyo hali initokee" Kayoza alitoa jibu lililofanya wenzake waangaliane,

"Tulivyoingia kwenye chumba alichoruelekeza Omary tumfuate, ulifanya nini?" Denis alimkumbusha Kayoza,

"Si tuliwakuta polisi watatu, alafu sikumbuki kitu zaidi ya kujikuta nimelala barabarani" Kayoza alitoa jibu jingine lililowashangaza wenzake,

"Makubwa basi, Ngoja nilale mie" Omary aliongea kisha akajifunika shuka na kuwaacha wenzake wakiendelea kuongea.

Saa kumi na moja alfajili waliamka na kuanza kujitayarisha kwa ajili ya safari.

Ilipotimia saa kumi na mbili kila mtu alikuwa tayari na wakatoka mpaka mapokezi, wakakabidhi chumba na kuondoka kuelekea stand ya mabasi, walitembea kwa miguu tu kwa maana haikuwa mbali na lodge waliyoichukua.

Walipofika karibu na Stand walishangaa kuona Askari wakiwa wengi, wamejitawanya eneo lile la Stand ya mabasi,

"Nadhani wako Pale kwa ajili yetu" Kayoza aliongea huku akisimama na wenzake pia wakasimama,

"Dah, kweli imeshakuwa tabu" Denis aliongea kwa kukata tamaa,

"Tunafanyaje sasa?" kayoza aliuliza,

"Turudi tukajipange" Denis alijibu,

"Hapa hakuna kurudi, ngojeni kwanza" Omary aliongea huku akiitoa simu yake na kumpigia Dereva taxi,

"Kwa hiyo akishakuja ndio tunafanyaje?" Kayoza aliuliza,

"Anatupeleka mpaka nje ya mji, alafu uko mbele tutashuka kuyasubiri mabasi" Omary aliwaambia wenzake,

"Hapo umefanya vizuri" Denis alimpingeza mwenzake kisha wakasubiri dakika kadhaa na taxi ikaja kuwachukua,

"Mpaka nzuguni utadai shilingi ngapi?" Omary alimuuliza dereva taxi,

"Elfu kumi na tano tu bosi wangu" Dereva taxi alijibu kwa unyenyekevu,

"Twendeni wanangu" Omary akawaambia wenzake ambao waliingia ndani ya gari.

Safari ikaanza, ubaya ilikuwa ni lazima upite karibu na Stand, wakati wanapita eneo hilo kulikuwa na gari ya polisi imeegeshwa pembeni huku likiwa na Askari wamekaa pembeni yake.

Gari waliyopanda wakina kayoza ikasimamishwa na wale Askari,

"Usisimame wewe" Omary alimsisitizia Dereva taxi ambaye alikuwa anataka kusimama,

"Kwanini nisisimame? Au nyie waarifu?" Dereva taxi alijibu huku akisimama,

"Acha upumbavu wewe" Denis aliyekaa kiti cha mbele aliongea huku akimsukumia Dereva nje na yeye akakaa kwenye kiti cha Dereva na kuiondoa gari kwa kasi.

Polisi kuona hivyo nao wakawasha gari yao na kuanza kuifukuza ile gari waliyokuwemo wakina Kayoza.

"Umefanya jambo la maana sana. Kumbe nawe ni jasiri hivyo?" Omary aliongea kumpongeza Denis kutokana na tukio alilolifanya,

"Ilikuwa haina namna" Denis aliongea huku macho yakiwa mbele,

"Lakini umeona wako nyuma wanatufuata?" Kayoza aliongea huku macho yake yakiwa nyuma,

"Nimeshawaona, hapa tuombe tu gari iwe na mafuta ya kutosha, vinginevyo hawatupati" Denis aliongea huku akizidisha mwendo wa gari,

"Kuwa makini lakini, usije ukatumwaga" Omary aliongea huku akitetemeka.

Gari zilifukuzana kwa mwendo wa dakika thelathini mpaka kwenye barabara moja nyembamba iliyo juu juu na chini kulikuwa na mabonde.

Kufika eneo lile, Denis akapunguza mwendo kwa kuwa barabara ni mbaya.

Gari ya polisi ikaongeza mwendo na kuwafikia kisha ikaigonga kwa nyuma gari waliyokuwemo wakina Denis na ile gari ikapoteza muelekeo na kupinduka kuelekea kwenye korongo huku ikibiringita zaidi ya mara kumi na kusimama ikiwa haitamaniki kwa jinsi ilivyopondeka baada ya ile ajali.

Gari ya polisi baada ya kuigonga gari waliyokuwamo wakina kayoza, nayo ilipoteza muelekeo na kuanza kubiringita kuelekea kwenye korongo na mwisho ikaenda kuokita ile gari waliyopanda wakina Denis na baada ya hapo ni damu tu zilitawala eneo lile......

+++++ITAENDELEA+++++

COMMENTS

BLOGGER

VISA NA MIKASA $type=THREE

Name

Affiliate Marketing,3,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,171,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,16,biashara mtandaoni,5,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,blogging,1,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,11,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,212,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,126,FIFA.com - Latest News,18,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,13,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,241,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,MPENZI CHEUPE | WHITE LOVER.,8,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natura shampoo,2,Natural hair,6,Ndoa,1,News,41,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nyumba ya maajabu,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,209,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Sumu Mwilini,1,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,USO WA FEDHA | FACE OF MONEY,35,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,7,WAPANGAJI WENZANGU,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 08
KIJIJINI KWA BIBI SEHEMU YA 08
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/03/kijijini-kwa-bibi-sehemu-ya-08.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/03/kijijini-kwa-bibi-sehemu-ya-08.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content