YEMEN IMEHARIBIWA NA SAUDI ARABIA | BongoLife

$hide=mobile

YEMEN IMEHARIBIWA NA SAUDI ARABIA

YEMEN IMEHARIBIWA NA SAUDI ARABIA!

Machafuko nchini Yemen yameyofikia kiwango cha kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe yanatokana na misuguano mingi lakini sababu kuu ni vile 'watawala' walivyokuwa wameigeuza kuwa 'shamba la bibi' kwa hasara ya wananchi kiasi cha kuzidi kufukarishwa sana huku viongozi hao wakinona maradufu (sasa hakupo kunona), sababu zingine ni matokeo ya kukabiliana na kadhia hiyo na hivyo kupatikana kwa upenyo wa kubomoana kimadhehebu yaani sunni na shia kushikana mashati. Kwa habari ya umadhehebu, mataifa mengine yalianza kujikita zaidi kishabiki na kimasilahi kama vile United Arab Emirates, Bahrain, Morocco, Kuwait, Qatar, Jordan, Sudan, Egypt, na Pakistan kwa kuegemea zaidi upande wa Serikali ya Mansur yenye mlengo wa kisunni; USA na Israel na wapo ktk mzozo huu kwa madai ya kuona tawi la kundi la kigaidi la Alqaeda halipati pumzi ya kujiimarisha kama sio kuona likitokomezwa..
Kuwepo kwa Jamhuri ya kiislam ya Iran kunaeleweka maana huyo hawezi hasiwepo mahala ambapo jamii ya kishia inatishiwa amani kama tunavyoona huko Syria na Iraq pamoja na Lebanoni kwa kundi la wanamgambo wa kipalestina la Hizbullah ambao ni washia dhidi ya Israel inayoelezwa kupora ardhi yao kimabavu.

Lakini kwanza ebu tuitazame Saudi Arabia ambaye ndiye mzizi mkubwa wa kadhia hii kiasi inafikiriwa kwamba kuuawa kwa mwandishi wa habari Jamal Khashogi kunaweza kufifisha mambo ingawaje haieleweki itakuwa kwa faida ya makundi gani yakiwemo ISIL na Alqeada, kabila la houthi lenye mlengo wa kishia, bila kuwaacha pembeni Muslim brotherhood, al ansar, nk.
Ndio, kimsingi Saudi Arabia ni mali ya marehemu Muhammad bin Saudi aliyegeuza eneo hilo kuwa taifa kwa kuliwekea mifumo yake ya kiutawala wa kifalme yenye kuliendesha mpaka leo, kwamba, marehemu huyu ndiye alifanya taifa hilo kuendeshwa kwa mujibu wa kiislam kwa mlengo wa sunni huku raia wake zaidi ya 80% wakiwa ni dhehebu la sunni na idadi inayobakia ikijumuisha dhehebu la shia pamoja na madhehebu mengine ya kiislam, na wachache sana wakiwa wakristo wanaozuiwa kujipanua kupitia mburuzo mkali wa kisheria. Ni Taifa tulivu kwa alama kubwa na lisilo ruhusu sensa rasmi yenye kubainisha idadi ya wanadini mbalimbali na hivyo kuzidi kuliweka ktk udhibiti mambo mzuri huku likiwa mstari wa mbele kutetea na kukuza usunni ktk majirani zake kama inavyojieleza huko Yemen inavyosaidia kijeshi kuhakikisha shia haipati nafasi ya kushika hatamu za kuongoza nchi.

Sasa tuwepo kwenye jambo lenyewe maana ndicho tunachojadili - ni kwamba, Yemen ya awali iliyojumuisha maeneo ambayo leo hii yanafahamika kama Ethiopia na Eritrea ilikuwa inakaliwa na watu wanao nasibishwa na jamii kutoka utawala wa malkia wa sheba anayetajwa katika vitabu vitakatifu vya Quran na Biblia yaani wasabaean waliokuwa wanazungumza lugha ya kiarabu waliojazana kwa maelfu ya miaka huku wakiliweka eneo kuwa la kibiashara zaidi.
Kuanzia mwaka 275 CE, eneo hilo lilitawaliwa na Dola la Himyarite lililovutiwa sana na uyahudi kiasi cha kuwaiga namna zao za utawala na pengine ndio ilirahisisha kupenya kwa ukristo katika karne ya nne; hatahivyo, uislam ulitokeza na kupanuka kwa haraka sana na hivyo kuwa wenye nguvu zaidi kuanzia karne ya saba na hivyo kukiweka kipande kinachoitwa Yemen ya leo kuwa chenye wenyeji wa kiarabu kwa zaidi ya asilimia 95 waliokuwa waislam wanaongozwa kwa miondoko ya dini hiyo juu ya maisha ya kila siku.
Tawala mbalimbali za kifalme ziliibuka kuanzia karne ya 9 hadi ya 16 huku ile ya Dola ya Rasulid ikiwa ndio yenye nguvu zaidi na iliyopata mafanikio makubwa kwa misingi na taratibu za kiislamu; lakini kufikia mwanzoni mwa karne ya 20, nchi hiyo iligawanyika na kuwa vipande viwili ambapo upande wa kaskazini ulikuwa chini ya mamlaka za Dola la Ottoman, huku kusini ikiwekwa chini ya mamlaka za Ufalme wa Uingereza.

Jamhuri ya Kiarabu ya Yemen ilianzishwa mwaka 1962 katika eneo la kaskazini ambalo lilikuwa limefanywa ufalme baada ya vita vikuu vya kwanza vya dunia huku ile ya kusini ikibakia chini ya Uingereza ikijulikana kama 'Aden Protectorate hadi mwaka 1967 ilipokuwa Taifa huru ambalo baadaye lilifanyika kuwa la kijamaa (Marxist state); lakini ilipofika mwaka 1990, nchi hizo mbili ziliungana na kuwa taifa moja lililojumuisha zaidi ya visiwa 200.
Yemeni moja ilianza kuongozwa na Rais Ali Abdullah Saleh katika mfumo usiokuwa rasmi wa kisiasa ambapo mamlaka za kitawala ziligawanywa kwa watu watatu, kwanza Rais mwenyewe aliyekuwa mtawala na mdhibiti mkuu wa Taifa kwa habari ya mambo yote, Major General Ali Mohsen al-Ahmar aliyekuwa anadhibiti Jeshi la ulinzi kwa kiwango kikubwa, na wakati Abdullah ibn Husayn al-Ahmar alikuwa kiongozi mwenye ushawishi mkubwa wa chama cha Islamist Islah huku halikadhalika akiwa wakala mteuliwa wa ufalme wa Saudi Arabia uliokuwa unamtumia kutembeza 'mlungula' kwa viongozi muhimu wa kisiasa pamoja na wale wa kidini katika makabila kwa lengo la kuwapa nguvu za kiuchumi ili waweze kusaidia kuyadhibiti makabila yao yaendelee kuwa watiifu mbele ya serikali ya Rais Saleh aliyekuwa kibaraka wa falme hiyo akiwa amepewa dhamana ya kuhakikisha Yemen inabakia kuwa Taifa la kiislam kwa mlengo wa kisunni na kutakiwa kuwadhibiti washia wasiweze kuwa kikwazo cha usalama.

Lakini kwa bahati mbaya sana kupitia utawala mbovu usiozingatia masilahi ya wananchi, nchi hiyo ilitumbukizwa katika umaskini wa kupitiliza kupitia uongozi wa Rais Ali Saleh kudhihirisha kutopania kushughulikia maovu mbalimbali vikiwemo vitendo vya rushwa na ukosefu wa ajira; na kama haikutosha, katika mwaka wa 2011, Rais huyo alijikuta badala ya kuimarisha udhibiti mambo alikuwa amezidisha hasira za wananchi dhidi ya uongozi wake kiasi cha kuwafanya waingie mitaani na kuandamana kwasababu walipinga maamuzi ya kupanga na kubadilisha sheria iliyomruhusu Rais kuwa wa maisha.
Kuanzia hapo, hali ilizidi kuwa mbaya maana machafuko yaliendelea kupitia maandamano na migomo yenye vurugu iliyokuwa ikifanyika mara kwa mara hadi kufanya polisi kujikuta wakitumia silaha za moto kujaribu kuwatuliza wananchi wenye hasira wakiwa katika makundi ya kimapigano ya kikabila na kimadhehebu ya kidini; ndivyo wakati mmoja zaidi ya watu 50 waliuawa jijini Sana'a na ikawa kawaida polisi kuua waandamanaji waliopania kuona nchi haitawaliki kama Rais asipoachia ngazi.
Ndivyo Rais huyo alijikuta amejitumbukiza katika wakati mgumu sana maana alianza kupoteza uungwaji mkono nje ya nchi, kama vile matokeo ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kupitisha azimio la kulaani machafuko hayo ikiwa ni pamoja na kutaka uongozi wa juu kubadilishwa katika kipindi cha mpito ili kuiweka nchi chini ya misingi bora ya demokrasia na utawala; kwa mitokezo hiyo na misukumo yake kutoka ndani na nje ya nchi, na ikiwa imepita mwezi mmoja toka Mwanaharakati wa Yemen wa kutetea haki za binadamu Tawakul Karman apate tuzo ya amani ya Nobel Peace Prize (Oktoba 2011), ndipo pengine kupitia mbinyo mkali kutoka kwa viongozi wenzake ilimlazimu Rais huyo kwenda Riyadh nchini Saudi Arabia kusaini mkataba wa mpango wa baraza la ushirikiano katika nchi za ghuba kwa ajili ya kuanzisha na kuweka kipindi cha mpito cha kisiasa kuelekea utawala wa kidemokrasia wenye masilahi ya wananchi wote katika haki, umoja, kweli, na amani.
Katika hali isiyotarajiwa, mara baada ya kumaliza kusaini nyaraka hizo husika, Saleh alikubali kisheria kumkabidhi madaraka yote makamo wake yaani Abdrabbuh Mansur Hadi na hivyo Yemen ikawa inaingizwa katika hatua ingine iliyodhaniwa ingerekebisha mambo.

Ikiwa imetarajiwa kuwa siku muhimu sana yenye furaha kwa masilahi ya ustawi mwema wa Taifa hilo wakati Makamo wa Rais Abdrabbuh Mansur Hadi alipokuwa anaapishwa kuwa Rais mpya wa Yemen katika mwezi huo wa Februari 2012 kutokana na kushinda uchaguzi wa Rais ambapo hakuwepo mpinzani wa kupambana naye, lakini badala yake ikiwa ni hukohuko Ikulu lilitokea shambulizi la la kujitolea mhanga lililoua walinzi 26 na kufuatia kukiri kuhusika kwa tawi la kundi la kigaidi la Al Qaeda la nchini humo (AQAP); hatahivyo, tukio hilo halikurudisha nyuma ratiba za serikali hiyo mpya ambayo ilikuwa ya kipindi cha miaka miwili ya mpito huku ikitakiwa kuyarisha katiba mpya kwa ajili ya kuelekea katika uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge wa mwaka 2014.
Miezi mitatu baadaye, tawi hilo la Al Qaeda lilidai kuhusika na shambulizi jingine la kujitolea mhanga ambapo wanajeshi 96 jijini Sana'a walipoteza maisha; shambulizi jingine la kuripua gari lilifanyika mwezi wa tisa na kuua watu 11 katika jiji hilohilo, na  hivyo alama kujieleza Nchi ya Yemen ilikuwa inaimarika kuwa pango madhubuti la kuzalisha magaidi ikiwa ni pamoja na kuwa hifadhi salama kwa ajili ya kuendesha harakati mbalimbali duniani za kiovu kwa masilahi yao. Siku iliyofuatia ya shambulio hilo la kuripuliwa gari, mmoja wa viongozi wa tawi hilo la al-Qaeda yaani Said al-Shihri aliripotiwa kuuawa maeneo ya kusini; na wakati huo, katika mwaka huo wa 2012, ilidaiwa kuwepo operesheni ndogo za chinichini za Marekani kupitia kikosi chake maalumu kwa lengo la kukabiliana na ongezeko la Al Qaeda kushambulia wananchi ili kujiimarisha kimkakati kwa hasara.
Baadhi ya wachambuzi katika kuitazama Yemen kwa jicho la kina wanaeleza alama za uwepo wa Marekani katika masuala ya ndani ya Taifa hilo ulitokana na kuubaini utawala wa zamani wa Ali Abdullah Saleh (alikuwa amerejea nchini humo baada ya bunge kumuwekea kinga kamili ya kutoshitakiwa) kuhusika kwa namna nyingi kuyajenga na kuyaweka kwa makusudi mazingira rafiki mbele za ukuaji wa shughuli za kigaidi nchini humo ili wawatumie dhidi ya wananchi na wanaharakati walioonekana kuwa kinyume nao kama sio hasa kuwatumia kupambana dhidi ya harakati za waislama wa kishia kutaka kupata sauti katika maamuzi ya uendeshaji wa shughuli za kila siku za taifa hilo.
Pengine kuingia madarakani kwa Abdrabbuh Mansur Hadi na kule kupata msaada kutoka Marekani kuliwezesha kuwarudisha nyuma waasi wa Ansar al-Sharia kutoka kabila la Houthis ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kumkamata mtawala wao wa kijimbo Shabwah; lakini hatahivyo, bado serikali ya jiji la Sana'a ilikuwa dhaifu maana vurugu za mitaani ziliendelea kuleta usumbufu na hofu huku waasi wa kishia wakizidisha uadui dhidi ya serikali wakiongozwa na mkuu wao wa kikabila Abdul-Malik Al-Houth ambapo kundi la kidini la kimapigano la Ansar al-Sharia lilikuwa linamuheshimu sana, makundi mengine yalikuwa ya kisunni kama vile al-Islah na al-Qaeda.

Waasi wa kishia wa kabila la Houthi hawakukubali kukata tamaa kwa kule kurejeshwa nyuma, bali walijiimarisha zaidi hadi kufikia Septemba 2014 walitumia wingi wao wa kikabila kuuvamia mji wa Sana'a na kutaka kumlazimisha Rais Mansur kukubali kuunda serikali moja iliyowahusisha maana Waziri Mkuu hakutoka kwenye kundi lao; lakini walipopewa nafasi za uongozi ndani ya serikali kwa kuwaomba wajumuike kwenye mazungumzo ya kulitenda na kulikamilisha jambo hilo, walishangaza kwa kugoma kushiriki huku wakiendelea kuuweka mji katika hali ya hatari kila mahali maana walikuwa wametapakaa viunga vyote ikiwepo kuyazunguka makazi binafsi ya Rais na kufanikiwa kumfanya ashindwe kutoka (the president was under house arrest). Ndipo ilipofika tarehe 6/2/2015, serikali kwa ujumla wake ilijikuta ikilazimika kutoa tamko la kuachia ngazi zote za uongozi wa nchi na hivyo kuwa 'ushindi wa kimapinduzi' kwa kundi hilo kama alivyouita Abdul-Malik al-Houthi katika kujitapa kwake akiamini walikuwa wamefanikiwa kukamilisha ndoto zao za muda mrefu za kuliweka taifa hilo chini ya uongozi wa kiislam kwa mlengo wa kishia na hapo wakiapa kuendeleza harakati za kupanua dhehebu hilo hasimu mkubwa wa Sunni kwa njia za amani na kuvumiliana na imani zingine. Ila inaelezwa kuwa nyuma ya mafanikio hayo licha ya kuwepo kwa udhahiri msaada mkubwa wa kivifaa kutoka Jamhuri ya Kiislam ya Iran, halikadhalika, ulikuwepo msaada kutoka kwa Ali Abdullah Saleh na ikiwezekana kwa kumuhusisha mwanawe General Ahmed Ali Abdullah Saleh aliye endelea kuwa na madaraka makubwa katika baadhi ya maeneo katika Jeshi la Ulinzi na Usalama kwani Rais huyo wa zamani alidai alilazimishwa na wenzake kuachia madaraka.

Mapinduzi hayo yakionekana yamekamilika kwa upande wa jiji la Sana'a, Abdrabbuh Mansur Hadi alifanikiwa kukimbilia kusini mwa nchi hiyo katika mji wa Aden ambapo palikuwa nyumbani kwao kiasili na kupafanya kuwa ngome yake ya kutumainia akitumia watu wa kabila lake pamoja na usunni uliokuwa mkubwa sana huko; na moja kwa moja katika siku hiyo iliyokuwa tarehe 21 katika mwezi huohuo wa pili wa kutendeka kwa mapinduzi hayo haramu, alihutubia Taifa kupitia chombo cha habari cha televisheni na kufuta tamko lake la kujiuzuru na kutaka aendelee kutambuliwe kama Rais halali wa Taifa pamoja na serikali yake na kuishia kuyalaani vikali mapinduzi hayo.
Akiendelea kuupigania uongozi wake, Mansur aliutangaza mji wa Aden kuwa makao makuu ya muda ya serikali katika mwezi uliofuatia; jambo ambalo lilipuuzwa na waasi hao wa kishia walioanza kupeleka majeshi yao kusini mwa nchi hiyo huku wakiendelea kupuuza kelele za upinzani ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kutoyatilia maanani maamuzi ya baraza la ushirikiano la nchi za ghuba dhidi yao.
Waasi walipigilia msumari kwa kuvunja bunge na kutangaza kamati ya mapinduzi iliyowekwa chini ya kiongozi wa mpito Mohammed Ali al-Houthi.

Mambo yalivyozidi kuharibika kwa habari ya kuongezeka kwa machafuko ambayo sasa yalikuwa yamechukua sura mpya ya kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe huku mataifa ya nje yakiingilia mzozo huo kwa namna za kishabiki na hivyo kuzidi kuvuruga mambo, Rais Mansur alilazimishwa kukimbilia nchini Saudi Arabia maana wapiganaji wa uasi walikuwa wameingia mjini Aden huku Marekani ikiondosha wafanyakazi wake katika ubalozi na wengine kutoka ofisi zake za taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwataka raia wake kuondoka kwa ajili ya usalam wao; na ilipofika tarehe 26/3/2015, Saudi Arabia iliitangaza operesheni mahsusi iliyopewa jina la 'Kimbunga cha al-Hazm' na kuanzisha mashambulizi ya ndege dhidi ya waasi wa kishia ikiwa ni pamoja na kuanza kujenga na kuongoza muungano wa kijeshi kutoka nchi zilizojiita marafiki wa Yemen wakati ukweli ulikuwa muungano wa nchi za kiislam kwa upande wa sunni ili kuwafurumusha washia waliopania kuiweka Yemen mikononi mwao (muungano huo ulijumuisha nchi za United Arab Emirates, Kuwait, Qatar, Bahrain, Jordan, Morocco, Sudan, Egypt, na Pakistan.)
Wakati huo Marekani ilieleza ingetoa msaada wa kitelijensia, takwimu, teknolojia na misaada katika ulengaji shabaha wa maeneo mahsusi kama vile katika ngome za adui ingawaje yenyewe ilijikita zaidi katika kupambana na magaidi wa Al Qaeda.

Mvua za mabomu kutoka ndege za kivita huko Aden, ziliwezesha majeshi ya Rais Mansur kuudhibiti mji wa Aden kutoka mikononi mwa wapiganani wa Houthis waliokuwa wameanza kuudhibiti na hivyo kurudi nyuma hadi jiji la Sana'a iliyogeuka kuwa ngome yao kuu maana huko walikaa kikabila zaidi wakiwa sambamba na wananchi wengi waliokuwa kabila hilo lenye idadi ndogo sana ya wasunni; lakini kwa upande wa pili, wanaharakati wa kidini wenye misimamo mikali waliongezeka kuwa tishio kupitia kuzaa vurugu za kigaidi katika mji huo huku Taifa likionekana kumeguka na kuwa vipande viwili vikubwa.

Mnamo Decemba 2017, Rais wa kwanza wa Yemen Ali Abdullah Saleh aliuawa kwa kupigwa risasi na mtu asiyejulikana (sniper) jijini Sana'a; yapo madai yanaeleza kuwa waasi wa Houthi aidha ndio walitekeleza jambo hilo baada ya kuona hakuwa na faida na hivyo zile chuki zao dhidi yake toka akiwa Rais kuibuka na kumalizikia kumuondoa duniani, lakini yapo madai mengine kuwa aidha aliuawa kwa amri ya utawala wa Mansur kwa msaada kutoka Saudia Arabia kwa kuonekana msaliti kwa kitendo chake cha kuwasaidia waasi wa kishia kupambana na serikali.

Pamoja na matokeo hayo ya kufurumushwa kwa waasi wa kishia mjini Aden na kisha kuundwa kwa baraza la mpito la kusini mwa Yemen mnamo Februari 2018 linalopata uungwaji mkono kutoka United Arab Emirates, bado sura ya ujumla wa Taifa la Yemen imeendelea kuwa mbaya sana kama vile mitokezo ya kufariki kwa baa la njaa kwa zaidi ya watoto 50,000 kwa hesabu za mwaka jana tu peke yake huku zaidi ya watu milioni moja kudaiwa kukumbwa na maradhi ya kipindupindu; matatizo haya yanazidi kuiweka Saudi Arabia katika shutuma namba moja kutokana na vitendo vyake vya kuingilia mambo ya ndani ya taifa hilo toka mwanzo wa kuundwa kwake ikiwemo kuweka vikwazo kiasi maeneo mengine yanashindikana kufikika ili taasisi za kutoa misaada ya kibinadamu ziweze kutimiza majukumu yao.
Licha ya Saudi Arabia kuonekana wazi ndiye mbomozi wa Taifa hilo kwa kuhakikisha Taifa hilo haliwi mikononi mwa washia kwa masilahi yake, lakini Marekani naye anashutumiwa kuhusika katika ubomozi huo kupitia harakati zake za kupambana hasa na tawi la kundi la kigaidi la Al Qaeda lililoweka makazi nchini humo kwa lengo la kutenda ugaidi dhidi ya masilahi ya Taifa hilo yanayojumuisha masilahi ya nchi kama Israel nakadhalika.

Lakini mzozo huu kwa uhalisia wake ni alama ya uhasama uliopo baina ya usunni na ushia unaoelezwa kuanzia rasmi katika matokeo ya kuuawa kwa mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) yaani Hussein bin Ali bin Mutalib katika mwezi wa Ashura; madhehebu haya yanapaswa kukaa na kuzika tofauti zao ili yaweze kuwa jambo moja kwakuwa wote ni waislam; kwamba, shia hapaswi kuwa na uadui na sunni ambaye pia hapaswi kuwa adui wa shia maana kuendelea kuwa hivyo wanawapa mwanya adui wao halisi katika kuwadhohofisha.

Ndio, Yemen ikijitazama kama taifa la waarabu, hiyo itakuwa nguvu tosha katika kuwaunganisha kuwa jambo moja lenye mshikamano wa kizalendo maana wao ni asilimia 92.8 ya Raia wote huku asilimia zilizobakia kuondoa asilimia 1.4 ni waarabu wenye asili ya Afrika pamoja na asilimia moja wakiwa wahindi wa kipakistani; lakini nguvu halisi ni kwamba, wao ni waislam wenye majibu ya matatizo yote katika kuwafanya waishi wakiwa jambo moja lenye kupendana na kushirikiana katika haki, usawa na amani.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : YEMEN IMEHARIBIWA NA SAUDI ARABIA
YEMEN IMEHARIBIWA NA SAUDI ARABIA
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/01/yemen-imeharibiwa-na-saudi-arabia.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/01/yemen-imeharibiwa-na-saudi-arabia.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy