$hide=mobile

NDOA INAANZA BAADA YA HARUSI

(BINTI YANGU YAJUE HAYA) NDOA INAANZA BAADA YA HARUSI. Mwanangu nisikufiche, watu wengi huchangia sherehe ili waje kula na kunywa na kuonesh...

(BINTI YANGU YAJUE HAYA)
NDOA INAANZA BAADA YA HARUSI.

Mwanangu nisikufiche, watu wengi huchangia sherehe ili waje kula na kunywa na kuoneshana fahari, ukoo wa  Mume na ukoo wa mke nao wanaoneshana umwamba hawa kwenye Send-off na hawa wanajibu kwenye harusi.

Na ule usiku baada ya reception sijui ndio mnaita hivyo mnaingia kwenye gari kuelekea kwenye fungate(honey moon).

Hapo hata wanakamati huwa wanakimbiana ninyi mkishaondoka kwani shughuli yao imeishia pale.

Hata wasimamizi watawasindikiza mpaka chumba mnacholala kisha wanawaacha hapo. Lakini kazi yako ndio inaanzia hapo.

Wewe humalizii siku ya harusi. Hapa ndio unaosha make up na kubandua hizo kope artificial na kucha na kuingia kwenye mapambano kupigania Ndoa yako.

Ukweli ni kwamba wanaotarajia NDOA itakushinda ni wengi nikiwemo Mimi, na tunapokupigia simu kuuliza "Mnaendeleaje? " huwa tunatarajia jibu lolote kutoka kwako. Kwa sababu NDOA Inaanza baada ya harusi. Usiingie huko ndani kwenda kucheza.

Naomba nikwambie kauli ngumu na ndio ukweli kwa sababu nakupenda. Hicho cheti ni karatasi tu yenye nembo ya Taifa ili kukutambulisha kisheria kama mke wa Mtu. Shetani hakiogopi wala wanawake wa nje hawakiogopi.

 Na hizo Pete ni kama urembo vidoleni mwako, usidhani kuwa zimemfunga mume wako kufanya maamuzi magumu ikiwa utamvuruga kichwa.

Ukweli ni kwamba sijaona mwanaume anayeogopa cheti, labda wapo ila Mimi sijaona. Nakushauri binti yangu usikose adabu ukajivunia Pete na cheti. Hata kama mtajenga nyumba kwa majina yenu, mwanaume anapokosa amani anaweza kuacha ghorofa akaenda kupanga chumba kimoja uswahilini.

Usidhani wote wanaopaki magari huko kigogo huku wameacha nyumba zao bahari beach, zenye Jacuzzi na wanaenda kuoga kwa ndoo na kopo uswahilini, sio wote wamefungwa na uchawi. Wapo wengi wamekimbia makelele na ugomvi usiokoma.

Mdomo wako unapaswa kuleta faraja kwa Mumeo na sio maumivu ya kupasua moyo wake.

Sheria ya maisha ni kuvuna unachopanda na asilimia kubwa ya wanaume hawasemi wanapoumia kupitiliza. Ila huingia kwenye mapango ya mioyo yao na kutunga sheria, akitoka huko hata uje na jeshi la malaika wa mbinguni na baragumu hutarudisha nyuma maamuzi atakayofanya.

Usijibweteke. Nyumba inajengwa na Mwanamke mwenye akili au kubomolewa na Mwanamke Mpumbavu. Yote yako mikononi mwako. Ukitaka kupendwa pendeka, ukitaka kukalia kaa la moto, jifanye pasua kichwa.

Asili ya mwanaume ni games, ukianza kushindana naye na wewe unataka kibesi ligi haitaisha. Ila ukishuka na kukaa nafasi yako utadekezwa kama yai.

Namalizia na hili binti yangu usimnange Mumeo, amekuamini mpaka kukufanya mkewe. Anashambuliwa na kila kitu kwenye maisha yake. Hebu msaidie nyumba yake iwe sehemu ya makimbilio. Usimfanye moyo kupasuka kila anapowaza kurudi nyumbani utajitengenezea tabu ambazo kuzituliza itakuwia vigumu.

Hii NDOA ni yenu, usitumie mfumo wa mashost zako kuendeshea nyumba yako, wanaume hawafanani. Ushauri mwingine uishie kwenye magroup usilete nyumbani.

Nimekwambia haya ili NDOA yako ikadumu. Zaidi sana katika adhabu zote unazoweza kumpa Mumeo usimnyime tendo la Ndoa. Huo mwili ni mali yake. Hizo moods zako ziishie sebuleni, kule chumbani wasilisha rejesho la siku.

Hayo ukiyazingatia duniani utaitwa heri.

Nakupenda sana binti yangu.

Kama imekugusa ewe mwanandoa mtarajiwa au mwanandoa tayari
Share na wenzako

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,149,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,196,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,110,FIFA.com - Latest News,15,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,11,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,207,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,39,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : NDOA INAANZA BAADA YA HARUSI
NDOA INAANZA BAADA YA HARUSI
https://encrypted-tbn0.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcQM6RbmOkNDqhjijOgKmKVi__tb29kSfvkSmAwVOpNHzBwwo4HS
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/01/ndoa-inaanza-baada-ya-harusi.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/01/ndoa-inaanza-baada-ya-harusi.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content