MUDA WA KUMUONESHA TRAFIKI LESENI NI MPAKA SIKU TATU KAMA UMESIMAMISHWA NA HUNA | BongoLife

$hide=mobile

MUDA WA KUMUONESHA TRAFIKI LESENI NI MPAKA SIKU TATU KAMA UMESIMAMISHWA NA HUNA

*MUDA WA KUMUONESHA TRAFIKI LESENI NI MPAKA SIKU TATU KAMA UMESIMAMISHWA NA HUNA.* ​

*Na Bashir Yakub*
+255784482959

Kusimamishwa na trafiki barabarani, na ukawa huna leseni mfukoni kwa muda huo sio kosa. Mwambie huyo trafiki kuwa hilo sio kosa. Sheria inatutaka kutembea na leseni tunapoendesha vyombo vya moto, lakini pia haisemi kuwa utakapokuwa hauna pale unapoombwa na trafiki basi ni kosa.

Tunaongelea Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168. Wapo watu wameandikiwa faini kisa wameombwa leseni wakasema hawana, au wakasema wamezisahau majumbani. Hawa waliotozwa faini katika mazingira kama haya wameonewa. Na wanastahili kurudishiwa fedha walizotoa haraka.

Ni kweli kifungu cha 77 cha Sheria ya Usalama Barabarani kinamtaka kila mwendesha chombo cha moto kutembea na leseni barabarani. Ni kweli askari anayo mamlaka kumsimamisha mwendesha chombo cha moto. Na ni kweli pia kuwa askari anayo mamlaka ya kumtaka mwendesha chombo cha moto aoneshe leseni yake. Lakini sio kweli hata kidogo kuwa mwendesha chombo cha moto asipoonesha leseni kwa wakati huo basi tayari ametenda kosa. Sio kweli.

Kifungu cha 77(1) cha Sheria ya Usalama Barabarani kinasema kuwa mtu hatatiwa hatiani, kwa maana ya kulipa faini au kuandikiwa kosa au kuadhibiwa na chombo chochote ikiwamo mahakama, kwasababu tu hakubeba, au hakutoa/kuonesha leseni pale alipotakiwa kufanya hivyo, isipokuwa ana siku tatu za kutoa au kuonesha leseni hiyo tokea siku hiyo aliposimamishwa.

Tafsiri iko wazi kuwa unaposimamishwa, ukaombwa kuonesha leseni, ukawa huna kwa mda huo, unazo siku tatu mbele za kutakiwa kuleta na kuonesha. Anachotakiwa kufanya askari sio kukuandikia kosa, laa hasha, bali ni kukutaka umuoneshe leseni hiyo ndani ya siku tatu tokea siku hiyo. Ukishindwa kufanya hivyo ndani ya siku hizo hapo ndipo linaweza kuwa kosa.

Watu wasionewe. Wapo askari wengine pia hawajui hizi sheria. Hawa sisi madereva tuwaelimishe.Unaweza kudhani askari anakuonea kumbe naye hajui. Kwahiyo kazi unayo wewe kuhakikisha unamweleza huyo askari kuhusu kifungu hiki na namna kinavyotaka. Wewe ndiye mtetezi wa kwanza wa haki yako kabla ya kutetewa na mtu mwingine.

Na kama itatokea ukaandikiwa adhabu kwa lazima kwa kitu kama hiki, basi unayo haki ya kukataa kulipa na kuomba kufikishwa mahakamani ili sheria ikatafsiriwe.Mwambie “sitalipa nataka sheria ikatafsiriwe mahakamani”. Kukataa kulipa sio kosa au ukorofi na hivyo huna haja ya kukhofu.Kukataa kulipa ni haki katika haki ulizonazo ukihisi umeonewa. Na kama umeshalipa au ulilipa huko nyuma katika mazingira ya jambo kama hili na unao ushahidi basi unayo haki ya kudai hela uliyolipa. Unaweza kuidai huko ulikotozwa au mahakamani.

Sheria imetoa ahueni hii ikizingatia mazingira ya ubinadamu. Huwezi kila unapoamka asubuhi ukakumbuka leseni. Huwezi kila unapokuwa na safari ukakumbuka leseni. Safari nyingine ni za ghafla na za kushtua, mfano kuitiwa msiba,ugonjwa,matatizo kazini,bila kusahau msongo/stress za ada na kodi. Atapata wapi muda wa kukumbuka leseni mtu huyu.

Mwingine amebadilisha nguo na hivyo leseni kubaki kwenye nguo iliyovuliwa, mwingine amebadilisha gari na hivyo leseni kubaki kwenye gari jingine. Na mazingira mengine kama hayo. Zote hizi ni dharula za kibinadamu zilizowafanya watunga sheria kuweka muda wa siku tatu kwa ajili ya kutoa au kuonesha leseni.

Basi wote tubadilike, madereva na askari wasimamia usalama barabarani.Dereva asiwe mkorofi, kadhalika askari asimwonee dereva

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : MUDA WA KUMUONESHA TRAFIKI LESENI NI MPAKA SIKU TATU KAMA UMESIMAMISHWA NA HUNA
MUDA WA KUMUONESHA TRAFIKI LESENI NI MPAKA SIKU TATU KAMA UMESIMAMISHWA NA HUNA
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/01/muda-wa-kumuonesha-trafiki-leseni-ni.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/01/muda-wa-kumuonesha-trafiki-leseni-ni.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy