$hide=mobile

AFRIKA KATIKA ULIMWENGU WA CHINA

AFRIKA KATIKA ULIMWENGU WA CHINA. MIKOPO INAVYOZIDI KULIPELEKA BARA LA AFRIKA KATIKA SHIMO LA UMASIKINI. Na Mpoki Buyah Kaminah.  Baada ya D...

AFRIKA KATIKA ULIMWENGU WA CHINA. MIKOPO INAVYOZIDI KULIPELEKA BARA LA AFRIKA KATIKA SHIMO LA UMASIKINI.

Na Mpoki Buyah Kaminah.

 Baada ya Donald Trump kuingia madarakani mambo mengi yamebadilika katika maeneo tofauti tofauti Duniani. Marekani ya sasa haijaipa kipaumbelee sana Afrika, Marekani ya sasa imejikita katika barani Asia  na  kupunguza uhusiano wake kwa kiasi fulani katika na mataifa ya Afrika ndani ya miaka 2 ya Republican na kujikita kwenye ideology yake ya Make America Great again(America First the rest will follow). Bwenyenye huyo amekuwa akiyanyoshea vidole mataifa ya Afrika kwa uongozi usio thabiti na alienda mbali zaidi kwamba mataifa ya Afrika yananuka kama choo. Hapa alikuwa analenga uongozi mbaya na usiojali wananchi wake (Kleptocrats Government).

Hata hivyo mke wa Trump (Melanin Trump) ametembelea nchini  Kenya tarehe 4/10/2018 akitokea Ghana lakini pia Misri ambapo ameenda mpaka katika mji wa Giza kuangalia Pyramids  bila kusahau kwamba alitembelea pia  Malawi, mataifa yote haya ni wanufaika wakubwa wa Marekani hususani kenya na Misri wamekuwa na Uhusiano wa karibu sana ndani ya miaka hii ya karibuni kupungua kwa ushawishi wa Marekani kumeifanya Afrika ikimbilie China katika kujiendesha ila usisahau kwamna mfadhili mkubwa wa bara la Afrika bado ni Marekani na siyo China.

Afrika katika Ulimwengu wa China, ni muda wa miaka 20 sasa tangu bara la Afrika kuanza kupokea mikopo na msaada kwa kiasi kikubwa kutoka China, Bara la Afrika linafungua ukurasa mpya katika kujiingiza katika shimo la madeni kutoka China pasipo kujua namna gani wataweza kurejesha mikopo hiyo. China imehusika katika miradi mbalimbali ya barani Afrika, kujenga viwanja vya ndege, barabara za kisasa, madaraja makubwa, uwekezaji katika nishati ya umeme na katika uwanja wa mawasiliano  kurahisisha ukuaji wa uchumi na huduma za kijamii lakini unakuwa ni mzigo mzito katika kulipa madeni hayo miaka 10-30 ijayo.

Kwa upande wa Afrika mashariki pekee mpaka sasa kulingana na taarifa kutoka CARI (China Africani Research Initiatives) China imekopesha Zaidi ya $29.42 Billion huku Kenya wamechukua kiasi kikubwa kuliko mataifa mengine Afrika mashariki na kati. Wasiwasi umeibuka miaka ya karibuni juu ya mikopo isiyokuwa na riba kutoka china na hili sakata la Zambia kuingia katika mkwamo na kutawaliwa upya kwa mara ya pili na serikali ya China, China ndiyo muwekezaji mkubwa Nchini zambia, China amejenga vituo vya police nchi nzima, 90% ya barabara zimejengwa na mchina, kwenye upande  wa ujenzi wa Viwanja vya mpira, Uwanja wa Ndege na pia kwenye upande wa nishati mchina mdiyo amewekeza huko.

Zambia ametawaliwa na China, Zambia hakuna  wanachoweza kufanya pasipo kupata maamuzi kutoka China, Zambia siyo taifa huru tena kama zamani, mpaka sasa Zambia wamekopa $13 Billion lakini pia Taifa hilo limekuwa likificha uhusiano na China kuna taarifa zinaenda mbali zaidi kwamba kuna uwezekano mkubwa wakawa wanadaiwa $30 billion ambazo kwa lugha nyepesi Zambia hawawezi kuIipa mali pesa Zote hizo hivyo kupelekea mashirika na mali nyingi za Zambia kiwa chini ya China. Mikopo ya China inaenda kuliingiza Bara la Afrika katika umasikini wa kudumu endapo viongozi wetu hawatachukua hatua za mapema katika kuandaa mazingira ya ulipaji madeni hayo.

Afrika pia imetembelewa tayari na  Rais wa China Xi Jipping  Rais huyu wa milele kutoka China ambaye anapewa heshima sawa na Mao Tse Tung (Mao Zedong) mwasisi wa taifa hilo. China amewekeza sana Afrika kuliko sehemu nyingine yotote ile duniani na mataifa ya  Afrika yananufaika sana na China katika miundombinu na teknolojia miaka ya karibuni hilo halina ubishi hususani katika mikopo isiyokuwa na riba ambapo mpaka sasa mikopo ya China imeanza kuogopesha na kutia wasiwasi maana mataifa ya Afrika yanazidi kujitumbukiza kwenye shimo la umasikini. Maana wanakopa lakini namna ya kurudisha mikopo hiyo imekuwa changamoto maana mataifa ya Afrika yanachukua mikopo kutoka China huku wakitegemea kurudisha mikopo hiyo kwa kodi za watu masikini.

 Afrika Kusini ni moja ya taifa linalopekea msaada mkubwa wa mikopo usiyokuwa na riba  kutoka China bila kusahau Ethiopia ambao kulingana na China African Research initiatives ndani ya miaka ya karibuni Ethiopia pekee imekopa  $13.73 katika ujenzi wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa reli za kisasa (SGR), ambayo pia ujenzi unaendelea kutoka mji mkuu wa Adis Ababa kwenda Djibouti. Na ujenzi huo utagharimu $4 billion pekee, taifa la Ethiopia liliweka records ya kuwa taifa la kwanza kuchukua mkopo mkubwa ndani ya mwaka 2013 .

Miradi mingi inayofanyika Ethiopia ni pamoja na mikopo kutoka China ila wachuuzi wa mambo wanadai kwao wao wanaweza kulipa mikopo hiyo pasipo shida yoyote ile na hii ni kutokana na aina ya uchumi walionao tofauti na mataifa mengine kama Uganda, Sudani, Zambia na Tanzania. China imehusika katika kujenga miradi mikubwa ya umeme chini humo  hata hivyo taifa litalazimika kuwabana watu wake katika kulipa kodi ili kurudisha madeni hayo lakini bado kuna wasiwasi kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kushindwa kulipa madeni hayo kwa China ndani ya miaka 10-20  ijayo na kujitumbukiza kwenye mkwamo wa madeni.

Lakini pia Kenya hawako nyuma kwenye mikopo ya China wanadaiwa zaidi ya $9.8 Billion na hizo ni zile ambazo wamechukua miaka ya karibuni kwa ajili ya miundombinu ya kisasa pamoja na nishati lakini sana katika ujenzi wa reli (SGR) mpya za kisasa mfano wa ile inayojengwa kutoka Naivasha kwenda Kisumu ambayo itagharimu zaidi ya $3.8 billion kutoka China. Na hata hivyo kulingana na uchumi wa taifa hilo wamejigamba kwamba wanaweza kulipa deni kwani wana uwezo huo pia ila bado pia Kenya na Ethiopia wana wasiwasi kama wataweza kulipa madeni hayo kutoka China ambayo yanaonekana kuliingiza bara la Afrika umasikini mkubwa maana  kuna wasiwasi mkubwa kama miundombinu hiyo itaweza kukukusanya mapato ya kutosha na kumlipa mchina punde baada ya kukamilika .

Uganda pia hawako nyuma sana katika kukopa kutoka China ambapo ndani ya miaka 3 tangu mwaka 2015/2018 Uganda wamechukua mkopo kutoka China kiasi cha $2.96 Billion kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kisasa inayotoka Entebe Kwenda Kampala ambayo kwa kiwango kikubwa imekamilika na inaonekana kuanza kifanya kazi. Na wao pia yameibuka maswali kama Uganda itaweza kukusanya mapato ipasavyo na kurejesha mkopo huo maana imeonekana wazi kwamba Uganda ni moja ya mataifa ambayo yapo nyuma sana katika ukusanyaji wa mapato Afrika mashariki na kati ukiachilia mbali  DRC na Sudani Kusini ambao na wao wamekopa katika kujenga barabara ambao na kuwekeza kwenye nishati ambapo  mpaka sasa wapo vitani sasa sijui watalipa lini hizo hela za Wachina. Ndiyo kwanza wanachinjana kila kukicha (paranoid and paradox in Afrika).

 Kuongezeka kwa ushawishi wa China barani Afrika hakuna ubaya wowote ila kumekuwa na faida kubwa kwenye sekta ya miundombinu na nishati tangu mwaka 2000 mpaka sasa, mikopo ya china imetufuta machozi kwa kiasi fulani katika nyanja mbalimbali ila pia ni vyema kutambua kwamba mikopo hii tusipojitambua vyema itakuja kutuletea shida kubwa na kuendelea kuwa watumwa hapo baadae. Viongozi wa Afrika wahakikishe kwamba Waafrika wananufaika pakubwa na uwepo wa China barani Afrika lakini pia wahakikishe wanachukua mikopo ambayo watakuwa na uwezo wa kulipa nje ya hapo wajiandae kuwa watumwa wa China kifikra na kiuchumi miaka 20 baadae na dalili zimeanza kuonekana Zambia.

Tusifurahie mabilion ya pesa yanayamwagika Afrika kutoka China ila ni vyema pia mikopo hiyo lazima iwe na faida kwa pande mbili maana kinachoonekana mikopo ya China ambayo haina riba imeanza kuwa tishio kwa Afrika na hii inatokana na kuwa na mikakati mibovu juu ya ulipaji madeni hayo na China ukishindwa kurejesha pesa zao wanatabia ya kushika miundombinu kama Viwanda, viwanja vya ndege, migodi, barabara ama kitu chochote kitakacho rudisha hela yao. Haya yametokea Burma (Mynmar), Malysia, Sri Lanka na kwa upande wa Afrika Zambia wamewashiwa taa nyekundu hawawezi kufanya chochote pasipo kuihusisha China bila kuwasahau Angola.

Tutaendelea kukamuliwa mpaka ibaki mifupa endapo hatutakuwa makini na mikopo ya China na mataifa makubwa. Uwepo wa China Afrika umeonekana kutiliwa shaka miaka ya karibuni tofauti na miaka ya 1990s,  mataifa mengi yamemkaribisha Mchina Afrika kwa sababu mikopo yake isiyokuwa na riba na amekuwa msaada mkubwa katika miundombinu lakini mikopo hiyo imeonekana kuzielemea nchi nyingi za Ki-Afrika. Xi ametembelea mataifa mengi zaidi Afrika kuliko taifa lolote lile kubwa duniani miaka ya hivi karibuni.   Kuanzia mwaka 2012- 2018, Xi ametembelea Senegal, Afrika kusini, Rwanda, Sudan kwa Ali-Bashir na mataifa makubwa mengine na yote hiyo ni katika kuimarisha biashara na uhusiano wa kidiplomasia.  China amekuwa na msaada mkubwa katika maendeleo ya Afrika ila mikopo yake isiyokuwa na riba pia imekuwa kikwazo maana mataifa mengi ya Afrika yanakopa lakini hayazalishi chochote na hii kujikuta wana malimbikizo ya mikopo isiyokwisha.

 Afrika Institute Researh kutoka chuo kikuu Marekani John Hopkins kwamba China kuanzia mwaka 2000 mpaka 2018 imekoposha dolla zaidi ya billion 143 katika bara la Afrika. Mikopo imekuwa kutoka Billion 5 hadi Billion 30 ndani ya mwaka 2016-2017, mikopo yote hiyo imekuwa ikikua kila siku na mataifa ya Afrika yameonekana kutokuwa na uwezo wa kurudisha mikopo hiyo na hiyo hupelekea mataifa ya Afrika kuwa vibaraka na watumwa wa mikopo. Angola pekee ndiyo limekuwa taifa ambalo linanufaika pakubwa na mikopo kutoka China, kwa muda wa miaka 17  kuanzia mwaka 20-2018, taifa hilo limekopa dolla billion 42 na hii ni kulingana na CARI (China African Research Iniatiative). Huku Zambia wakiwa wamekopa dolla Billion 13 japokuwa inasemekana Zambia inadaiwa zaidi ya  $20 bilion ila wanaficha na Serikali hiyo ipo katika mkwamo wa kulipa madeni hayo na hivyo kupelekea baadhi ya mali za Serikila kushikiliwa lakini Zambia Imekanusha juu hilo. Lakini huo ndiyo uhalisia wa Afrika katika mkwamo wa madeni kutoka nje.

Mnamo tarehe 3/09/2018 mataifa zaidi ya 50 yalikwenda China kushiriki mkutano mkuu baina ya China na Afrika FOCAC ( Forum China-Afrikani Co-operation), kulingana na Jarida la Afrika  Fundamental kwamba China ameahidi  mataifa ya Afrika  kutoa mkopo wa  dolla billion 60 katika mataifa zaidi ya 50 kuanzia sasa na kuendele, bado tunaendelea kukopa na hapo ndipo wazungu wanasema Xi has played his Card Right. Mataifa karibia 50 ya Afrika yanategemea msaada kutoka mataifa wahisani,  60% ya bajeti nyingi za mataifa ya Afrika hutegemea pesa kutoka njee, huo ndio ukweli. Tunakaa bungeni na kupanga bajeti kubwa lakini unakuta hatuna hela tunapanga sawa lakini hela hatuna ni mpaka tuanze kuomba msaada kutoka Uingereza, mpaka tuombe msaada kutoka Ujerumani au Ufaransa na Marekani na kwa sasa Mataifa ya Afrika hawajamaliza mikopo ya Marekani wameamia China, tunapanga mambo mengi na kutoa ahadi nyingi wakati hela zenyewe za mikopo.

Asanteni sana .

Ulikuwa nami Mpoki Buyah kaminah
Contacts:0762155025
Contacts:0624027362
Email:mpokibuya@gmail.com

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,149,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,196,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,110,FIFA.com - Latest News,15,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,11,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,207,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,39,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : AFRIKA KATIKA ULIMWENGU WA CHINA
AFRIKA KATIKA ULIMWENGU WA CHINA
BongoLife
https://www.bongolives.com/2019/01/afrika-katika-ulimwengu-wa-china.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2019/01/afrika-katika-ulimwengu-wa-china.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content