$hide=mobile

ZIFAHAMU CHANGAMOTO 12 ZA UJASIRIAMALI

ZIFAHAMU CHANGAMOTO 12 ZA UJASIRIAMALI: Kila jambo lina changamoto zake, ujasiriamali nao unachangamoto zake nyingi. Ni wazi kuwa wajasiriam...

ZIFAHAMU CHANGAMOTO 12 ZA UJASIRIAMALI:

Kila jambo lina changamoto zake, ujasiriamali nao unachangamoto zake
nyingi. Ni wazi kuwa wajasiriamali wakubwa na wadogo, wote hukutana
na changamoto; tofauti ya chanzo cha changamoto hizo na njia wanazozitumia kuzikabili.
Wajasiriamali wadogo ndiyo
wamekuwa wakikabiliwa zaidi na changamoto hizo na hata kupelekea kupoteza biashara au miradi yao.

Inawezekana wewe ni mmoja wapo ya wajasiriamali wanaokabiliana na


changamoto. Karibu nikushirikishe changamoto 12 za ujasiriamali na jinsi ya kuzikabili;

1. Mtaji
Kila biashara inahitaji mtaji ili iweze kujiendesha na kujipanua.
Wajasiriamali wengi wanashindwa kuanzisha biashara au kupanua
biashara zao kutokana na kukosa mtaji.

Suluhisho:
Kumbuka! Siyo lazima upate mtaji wote unaouhitaji, unaweza kuanza na mtaji kidogo sana na ukaukuza taratibu. Zipo njia nyingi sana za kupata mtaji
kwa ajili ya biashara au umradi wako. Unaweza kutumia njia zifuatazo:
-Uza baadhi ya vitu vyako ambavyo si vya lazima sana. Kwa mfano; ikiwa una simu ya bei kubwa, mikoba, nguo au vifaa vya kielektroniki kama vile TV na Subwoofer ambavyo huvitumii sana, unaweza kuviuza na ukapata mtaji
wa kuanzisha biashara yako.

-Azima au omba pesa kwa rafiki au ndugu anayekuamini. Ikiwa una ndugu au rafiki anayekuamini unaweza kumwomba akupe kiasi
fulani cha pesa na utamrudishia
utakapopata faida.

-Jiunge na vikundi vya wajasiriamali. Vipo vikundi mbalimbali vinavyowawezesha wajasiriamali hasa wadogo kupata mitaji. Hakikisha kikundi unachojiunga nacho kinaaminika na kina masharti
unayoweza kuyafuata.

-Kopa pesa kutoka kwenye taasisi za kifedha. Njia hii nimeiweka mwishoni kwakuwa mara nyingi haifai sana kwa wajasiriamali wanaoanza. Ikiwa biashara yako au mradi wako umeshakuwa kwa kiasi
fulani, unaweza kukopa pesa
kwenye tasisi hizi na ukaongeza
mtaji wako.

-Soma pia: Jinsi ya Kuanza Biashara na Mtaji Mdogo.

2. Ushindani
Biashara au miradi mingi ya
wajasiriamali ina ushindani mkubwa kutokana na kufanywa na watu wengi. Hata hivyo bado wewe kama mjasiriamali unaweza kukabili changamoto ya ushindani.

Suluhisho:
Unaweza kukabili changamoto ya ushindani kwa kufanya haya
yafuatayo.

-Uza bidhaa inayoendana na muda wa sasa. Kwa mfano kama unauza redio, tambua kuwa watu hawanunui redio zinazotumia kanda tena, bali wanataka redio zinazotumia USB pamoja na CD. Kwa kuuza vitu kuendana na wakati
utaweza kukabili ushindani vyema.

-Uza kwa punguzo au bei ya chini kidogo tofauti na wengine.

-Lenga matatizo ya watu katika
bidhaa na huduma yako. Watu
wananunua bidhaa kwasababu
wanataka zitatue matatizo yao na si vinginevyo.

-Jitangaze jinsi ipasavyo. Watu
hawatanunua bidhaa yako kama
hawakufahamu, hivyo hakikisha
unajitangaza kwa wateja.

-Soma pia: Mbinu 10 za Kuvutia Wateja Kwenye Biashara.

3. Mzunguko wa pesa
Inawezekana una mtaji mzuri lakini mzunguko wa pesa unakuwa mgumu katika biashara yako. Hili linaweza
kusababishwa na maswala kama vile watu au taasisi zinazodaiwa na biashara yako kuchelewa kulipa madeni yao kwa wakati. Changamoto inatokea pale ambapo
wewe unataka kulipa wale wanaokupa huduma na bidhaa mbalimbali lakini unakuwa bado hujapata pesa kutoka kwa wadaiwa wako.

Suluhisho:
Unaweza kutumia njia zifuatazo
kukabili changamoto ya mzunguko wa pesa.

-Weka bajeti nzuri kwenye biashara au mradi wako. Kuweka bajeti nzuri
kutakuwezesha kuwa na pesa za akiba ambazo zitakusaidia
kuendesha biashara wakati
utakapokuwa na mzunguko duni wa pesa.

-Fuatilia na kumbusha malipo
yaliyoko nje. Ikiwa kuna watu au
taasisi ambazo unazidai, basi
wakumbushe na ufuatilie pesa hizo ili ziweze kulipwa na kukidhi
mahitaji ya biashara yako.

-Punguza matumizi yasiyo ya
lazima. Unapokuwa kwenye
changamoto ya mzunguko duni wa pesa, inakupasa kupunguza
matumizi yote yasiyo ya lazima ili upate pesa kwa ajili ya mambo ya lazima.

4. Kuchagua bidhaa ya
kuuza au wazo la kibiashara.
Wajasiriamali wengi hasa wale
wanaoanza, hushindwa kujua ni bidhaa gani wanayoweza kuuza au ni wazo gani la kibiashara wanaloweza kulitekeleza. Hili huwafanya kushika hiki na kile na kuacha au kufanya vitu
wasivyovipenda wala kuvimudu.

Suluhisho:
Unaweza kuzingatia haya yafuatayo
wakati wa kuchagua bidhaa ya kuuza au wazo la kibiashara.

-Chagua wazo au bidhaa
unayoipenda na kuimudu kuifanyia kazi.

-Angalia wakati na uhitaji wa bidhaa husika.

-Angalia upatikanaji wa mtaji.
Hakikisha unaweza kupata angalau mtaji mdogo wa kuanzia biashara unayotaka kuichagua.

-Soma pia: Mambo 5 ya Kuzingatia Kabla ya Kuchagua Wazo la Biashara.

5. Masoko
Hauwezi kupata faida na kukuza
biashara au mradi wako kama hutouza bidhaa zako. Kutokana na uelewa duni wajasiriamali
wengi hawajui kutafuta wala kuandaa mikakati ya kupata masoko. Hili linakuwa ni changamoto kwao kwani
bidhaa zao haziuziki.

Suluhisho:
Unaweza kufanya haya yafuatayo ili kukabili changamoto ya masoko.

-Tafuta mtaalamu wa masoko
akusaidie na kukushauri jinsi ya
kupata masoko ya bidhaa yako.
Siyo lazima utumie watu
wanaolipwa pesa nyingi, bali
unaweza kumtafuta rafiki au mtu wa karibu mwenye taaluma ya masoko akakusaidia.

-Hakikisha unafahamu soko na uhitaji kabla ya kutengeneza bidhaa. Hili litakusaidia kutengeneza bidhaa ambazo zinahitajika sokoni.

6. Ukosefu wa elimu.
Wajasiriamali wengi wanakwama kwenye shughuli zao kutokana na
kukosa elimu stahiki ya ujasiriamali. Wengi hawafahamu usimamizi wa miradi, pesa au hata biashara. Ikizingatiwa nchi nyingi za Kiafrika bado hazijaandaa mtaala au mfumo
mzuri wa kuwafundisha wajasiriamali.  Hili linakuwa ni changamoto kubwa
kwani hata yale mafunzo machache yanayopatikana hutolewa mijini tena
kwa gharama kubwa.

Suluhisho:


Ili kukabili changamoto hii ya elimu au maarifa ya ujasiriamali unaweza kufanya haya yafuatayo.

-Tumia maarifa kutoka kwenye
mtandao. Badala ya kutumia simu au kompyuta yako kwenye
mitandao ya kijamii, unaweza
kutembelea mamia ya tovuti
zinazotoa mafunzo mbalimbali juu ya ujasiriamali.

-Jiunge na wajasiriamali wengine kisha mumuite mtu aje
kuwafundisha. Kuita mwalimu wa ujasiriamali kama kikundi ni rahisi zaidi kuliko kumwita kama mtu binafsi.

-Hudhuria semina za ujasiriamali. Inawezekana unaogopa gharama au
umbali, lakini kumbuka hii ni njia
nyingine nzuri ya kukupa maarifa.

7. Sera duni za kiserekali.
Serekali zetu za kiafrika bado zina sera mbovu ambazo siyo rafiki kwa wajasiriamali.
Wajasiriamali hukutana na milolongo mirefu ya kupata vibali na nyaraka muhimu au kukabiliwa na mizigo mikubwa ya kodi. Hili huwakatisha
tamaa na kuwakwamisha wajasiriamali wengi.

Suluhisho:
Kwa hakika suluhisho kubwa na la kudumu ni serikali zetu kutengeneza mazingira na sera rafiki kwa wajasiriamali. Hata hivyo kuna mambo kadhaa unayoweza kufanya.

-Anza kidogo kidogo. Unapoanza na vitu vingi au mradi mkubwa
mwanzoni, ni wazi sera na kanuni mbovu vitakukabili moja kwa moja.

-Uliza waliokutangulia walifanyaje kukabili mazingira magumu yanayokukwamisha.

-Epuka njia za mkato. Kamwe
usianze mradi kwa mambo kama vile kukwepa kodi au kwa kutumia vibali bandia kwani utakapobainika utafilisiwa au hata kushitakiwa.

-Anza taratibu nawe utapata upenyo hata kama hali ni ngumu.

8. Kuajiri
Kuna wakati wewe kama mjasiriamali unahitaji kuajiri mtu ili akusaidie kutimiza jukumu fulani. Wajasiriamali wengi wanajikuta wakiajiri watu ambao
hawafai au wasioweza kuwamudu. Hivyo hili huwa ni changamoto kubwa kwa baadhi ya wajasiriamali.

Suluhisho:
Unaweza kufanya mambo yafuatayo kabla ili kukabili changamoto hii.

 -Tathimini kama ni wakati sahKuna Kuna wakati sahihi ambapo kweli unahitaji mtu mwingine; hakikisha unaajiri mtu unayemhitaji. Ajiri mtu mwenye sifa stahiki. Usiajiri mtu kwa kuwa ni rafiki, mpenzi au ndugu hakikisha mtu unayemwajiri
ataweza kutekeleza majukumu yake vyema na kuiletea biashara yako faida.

9. Matumizi ya muda.
Kuna mtu mmoja aliwahi kusema ukitaka kuoa usioe au kuolewa na mjasiriamali kwani hana muda. Ni kweli wajasiriamali wengi huzidiwa
sana kiasi cha kukosa muda wa
maswala yao binafsi.

Suluhisho:
Kuna mikakati kadhaa unayoweza kuifanya wewe kama mjasiriamali ili kukabili changamoto ya muda.

-Panga ratiba na uifuate.
Ondoa mambo yasiyo ya lazima
kwenye ratiba yako.

-Gawa majukumu. Kubeba
majukumu yote wewe mwenye
kunakufanya uzidiwe na ukose
ufanisi.

-Weka malengo na uyafuate.
Soma pia: Kanuni 9 za Kufanikiwa
katika Matumizi ya Muda.

10. Kupanga majukumu.
Hii ni changamoto inayowakabili
wajasiriamali wengi, kwani
wanashindwa kupanga majukumu  yao vyema; hawajui wampe nani jukumu lipi na lipi wafanye wao. Hili huwafanya kufanya kila kitu na
hatimaye kuharibu zaidi.

Suluhisho:
Unaweza kutumia njia zifuatazo
kukabili changamoto hii.

-Andaa mwongozo wa kufanya kila kazi. Huu utawawezesha wale unaowagawia majukumu kufanya kazi vyema.

-Panga majukumu kwa watu stahiki.

-Kagua kila kazi ili kuhakikisha
imefanywa vyema na mtu husika.

-Toa ushauri na mapendekezo pale ambapo utendaji haukuwa sawa.

11. Kuacha kazi ya awali.
Changamoto hii huwakabili
wajasiriamali wale wanaotaka kuacha kazi yao ya awali ili wawe wajasiriamali. Maswali mengi huibuka akilini mwao kama vile je nitapata faida? Nianzeje? Nani atanisaidia?
Nitafanya nini? Nikishindwa itakuaje? Na mengine mengi.

Suluhisho:
Hakuna kitu kinachoshinda nia na mipango stahiki. Usiogope kuwa mjasiriamali kama tayari una nia na mipango madhubuti. Kwa mfano kama una akiba ya kutosha na unampango
mzuri wa kibiashara, hakuna haja ya kuhofu.

-Soma pia: Mambo 7 ya Kufanya Kabla ya Kuanzisha Kampuni au Biashara.

12. Kukata tamaa na
kujilaumu.
Wajasiriamali wengi hukata tamaa au kujilaumu hasa pale wanapokutana na changamoto zinazotokana na maamuzi
au matendo yao.

Suluhisho:
Kumbuka kuwa hakuna mtu yeyote aliyefanikiwa bila kukutana na changamoto. Jipe moyo usikubali kupoteza sehemu ya kazi ambayo
tayari umeshaifanya.
Weka mikakati sahihi, usijilaumu bali jifunze kutokana na kosa ili lisitokee tena wakati mwingine.

-Soma pia: Nukuu (Quotes) Zitakazo Kuhamasisha Maishani Mwako.

Kwa hakika zipo changamoto nyingi za ujasiriamali, lakini kwa hizi kubwa chache nilizozibainisha sambamba na
njia za kuzikabili, naamini hutokwama tena.
Je kuna changamoto nyingine
inayokukabili? Tafadhali tuandikie maswali au maoni yako hapo chini kuhusu makala hii juu ya changamoto za ujasiriamali.

Usisahau kuwashirikisha wengine makala hii pamoja na kujiunga

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,149,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,196,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,110,FIFA.com - Latest News,15,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,11,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,207,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,39,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : ZIFAHAMU CHANGAMOTO 12 ZA UJASIRIAMALI
ZIFAHAMU CHANGAMOTO 12 ZA UJASIRIAMALI
BongoLife
https://www.bongolives.com/2018/12/zifahamu-changamoto-12-za-ujasiriamali.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2018/12/zifahamu-changamoto-12-za-ujasiriamali.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content