UJUMBE WANGU KWA DADA ZANGU | BongoLife

$hide=mobile

UJUMBE WANGU KWA DADA ZANGU

*UJUMBE WANGU KWA DADA ZANGU...*

Na Mwalimu Isaya
0686310306☎
0672427474☎

My dada, mchungaji kule church alikutabiria utapata mume mwaka 2018, na uliamua kufanya maombi ya kufunga kwamba MUNGU akupe mme kabla mwaka huu haujaisha... lakini sasa tumebakiwa na siku chache sana kabla hatujaumaliza mwaka bado upo single na muujiza wako ulioomba huuoni ukitendeka.
~
Lakini my dada, kabla hujaanza kulalamika kwamba unabii wa mchungaji haukuwa wa kweli, kwamba yale maombi yako ya kufunga huoni yakijibiwa, hebu pitia upya inbox yako ya facebook ama Whatsapp. Kuna vijana wengi huko walikupa Hi lakini ulikuwa unabagua text za kujibu, kuna mwingine hata hujamjibu mwezi wa nane sasa. Mwingine anakusalimia mara kwa mara mtaani lakini kumuitikia tu tabu! Mie nashawishika kuamini kabisa, katika wimbi la wanaume wote waliokusalim mtaani kwenu ama kule inbox, kuna mmoja alikuwa ni fungu lako halisi but ulipuuza. My dada, mume hua haji na bango kichwani lililoandikwa *"NIMEKUJA KUKUOA".* Uliza yeyote yule mwenye ndoa yenye furaha, atakueleza mmewe alikujaje!
~
Lakini my dada, kitu kingine unachonishangaza ni kwamba, mchungaji anakuombea kweli kwa jina lako halisi la *"Mwajuma Mabula",* lakini wewe umebadilisha jina fb unajiita *"Nancy Davidson"* a.k.a *"De cute lady"*. My dada, wadhani mme alie serious kuoa huvutiwa kwa uzuri wa majina? Mitandaoni unapost picha umejiopodoa podo na kuvalia nguo za nusu uchi ukiwa umesuka ule msuko wa kisasa na kujitegesha kwenye magari ya kuazima ili kwenye picha uonekane unatoka familia ya kitajiri kumbe ni fundi cherehani, kumbe ni kibarua tu wa kile kisaloon cha mama Jesca, kumbe ni mama ntilie tu pale mtaa wa pili. Kumbe ni baamed tu wa ile baa ya pale mtaani kwenu. My dada mme wa kuoa havutiwi na picha kama hizo. Mtandaoni post picha za maisha yako halisi, mme wa kweli utamuona.
~
Dada yangu Penina alinisimulia jinsi rafiki yake alivyopata mme kimasihara tu humu Facebook. Penina anasimulia; *"Yaani mwalimu huu ni ukweli mtupu; kuna rafiki yangu alipataga mume humu fb lakini ilikua ni masihara sana. Rafiki yangu aliwekaga picha ya kawaida tu na Jina lake la ukweli. Yule kaka akaombaga kuonana nae, mimi nikamwambia, 'Kubali wito kataa maneno' akaenda ilikuwa jioni. Yule kaka akaja na gari yake, ila akawa amepaki mbali, akaja kwa miguu tena amechafuka ile mbaya. Basi yule rafiki yangu akaona hapa hamna kitu, akahisi labda mvuta bangi. Wakaongea akaja kunihadithia kwamba hata hajampenda, nikamwambia, 'haiwezekani mchunguze tu taratibu'. Siku nyingine akamuita Buguruni, rafiki yangu akajiremba mwenyewe akajua labda watakutana Mahali penye hadhi looh ilikua ni chini ya mwembe tena kaja afadhali ya siku ya kwanza. Basi wakaongea akaja nihadithia tena,  'ooh Peny mimi yule simtaki, kwanza anaonekana muhuni' ila nilivyokua naona mimi na yeye tofauti, nikawa namtia moyo asikate Tamaaa. Jamaa akiulizwa wafanya Kazi gani anasema 'gereji'. Basi buana, ikaendelea wakaanza uhusiano hivyo hivyo mwaka ukaisha, yule kaka akamwambia 'nataka nikuoe' binti akaja niambia tena. nikamjibu, 'hilo sasa best liko juu ya moyo wako, moyo ukikubali, olewa naye tu'. Akakubali kuolewa nae. Basi eeh mwishoni yule kaka akaanza kumwambia ukweli sasa yule binti, 'Mimi nafanya kazi TANESCO nisamehe kwa kukuficha muda mrefu, nilikuwa nikikupima imani yako kwangu ikiwa u mwanamke shujaa kuweza kuishi na mme si kwa sababu anacho, nimekuamini sasa u shujaa'. Rafiki yangu hakuamini kusikia vile. Alifurahi zaidi na kunishukuru kwa ushauri niliokuwa nikimpa. Yule kaka ana 'Degree' ya 'electrical&electronic, ana gari mbili, na ana biashara zake binafsi na nyumba alikua ndo anaimalizia kipindi hicho. Pia huyo kaka kwao wazazi wake ni watu wakubwa serekalini, wakarimu na wachamungu. Basi yule rafiki yangu hadi leo kasahau ilovyokuaga, ameolewa na yule mkaka na sasa ana mtoto, wanaishi maisha mazuri tena wachamungu. Mwalimu humu fb wanaume wapo kabisa ukibahatisha..."*
~
Hivyo ndivyo alinisimulia dada Penina jinsi rafiki yake alivyopata mme fb. Naamini umejifunza mengi my dada.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : UJUMBE WANGU KWA DADA ZANGU
UJUMBE WANGU KWA DADA ZANGU
BongoLife
https://www.bongolives.com/2018/12/ujumbe-wangu-kwa-dada-zangu.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2018/12/ujumbe-wangu-kwa-dada-zangu.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy