SOMA SIMULIZI HII | BongoLife

$hide=mobile

SOMA SIMULIZI HII

“Wewe ni nani?”
“David! Mtu ambaye baba yako alimsaidia sana!” alisema David.
“David! Naomba unisamehe kaka!”
“Siwezi kutenda dhambi ya udanganyifu. Kukusamehe siwezi kabisa. Umembaka msichana wangu halafu unataka nikusamehe! Siwezi!” alisema David na kuondoka ndani ya chumba kile, baada ya dakika kadhaa akarudi huku akiwa na kisu mkono wa kushoto na shoka mkono wa kulia.
“Nitakuua! Ila nitakuua kifo chenye maumivu makali kidogo. Wewe ni mwanaume, jitahidi kuvumilia. Umenisikia?” alisema David huku akimwangalia Jericho aliyekuwa akipiga kelele. Wakati huo Cecilia alikuwa pembeni.
“Naomba unisamehe!”
“Nenda chumbani. Naomba uniache na hiki kiumbe,” alisema David na Cecilia kutoka humo ndani.
“Ratiba yangu ipo hivi! Leo nitakukata ulimi na kiganja cha mkono wa kulia, keshokutwa nitakukata vidole vya miguu na mkono wako mmja, siku mbilizi zitakazofuata nitakukata mfupa laini mguuni ambao unakufanya kusimama. Ila sina roho mbaya sana. Nitakapokuwa ninakufanyia hivyo, pia nitakupa matibabu mimi mwenyewe ili kukupunguzia maumivu. Na kila kiungo nitakachokikata, nitampelekea baba yako ajue kile kinachoendelea humu,” alisema David maneno yaliyomfanya Jericho kulia kupita kawaida.
“David! David! David kaka yangu naomba unisamehe! Nisamehe, ni shetani tu alinipitia, nisamehe! Sitorudia tena! Haki ya Mungu sitorudia tena,” alisema Jericho huku kijasho chembamba kikimtoka.
“Hata nikikuua najua hutorudia tena. Utapiga sana kelele kama alivyopiga Cecilia. Hilo usijali, unaruhusiwa kufanya hivyo kwani humu ndani sauti huwa haitoki nje hata ukipiga matarumbeta. Nitavikata viungo vyako vyote na kitu cha mwisho kabisa kukikata katika mwili wako kitakuwa ni kichwa chako ambacho kitakuwa kama zawadi kubwa kwa baba yako. Hilo litakuwa onyo dunia nzima kwamba hakuna mtu anayetakiwa kucheza na mpenzi wangu,” alisema David. Akamsogelea Jericho.
“Naomba unisam...” alisema Jericho lakini hata kabla hajamaliza sentensi yake, akaanza kulia.
“Jericho. Usijali. Ni kazi ndogo sana. Nakuahidi rafiki yangu, ndani ya sekunde tano tu, kiganja chako kitakuwa chini. Nakuahidi, haki ya Mungu sitozidisha dakika,” alisema David, akachukua shoka lake, akakiweka kiganja cha Jericho vizuri.
Kilichosikika baada ya hapo ni mlio wa kitu kukatwa. Jericho alipiga uyowe mkubwa, damu zikaruka mkononi mwake, kiganja kikadondoka chini na damu kuruakaruka.
“Pole sana Jericho! Subiri niweke hiki kitambaa kuzuia damu zisitoke kwa wingi. Subiri niweke na kitu cha moto kikate damu,” alisema David na kuanza kuzuia damu hizo kutoka katika mkono wa Jericho.
***
Mzee Armando alikuwa ndani ya chumba chake, kilikuwa na mwanga hafifu, alihitaji kukaa peke yake kwa kuwa kulikuwa na mambo mengi yaliyokuwa yakimchanganya, hakutaka kuwa na mtu yeyote chumbani humo, alihitaji kuwa peke yake kwa kuwa alitaka kupanga mipango yake kwamba ni kitu gani alitakiwa kufanya ili kumuokoa mtoto wake aliyekuwa ametyekwa na mtu aliyekuwa akimpenda sana.
Ndani ya chumba kile, kulikuwa na meza iliyokuwa na simu yake, alikuwa akifikiria mambo mengi ambayo yalimjia kichwani mwake mfululizo lakini akakosa kuamua uamuzi ambao aliamini kwamba ungekuwa sahihi kwake.
Hakutaka kumuua David lakini kwa kile alichokuwa amekifanya, hakutaka tena kumuacha mwanaume huyo, ilikuwa ni lazima kumuua kwa kuwa aliugusa moyo wake, alimgusa mtu ambaye alikuwa akimpenda kupita kawaida.
Alipotulia kwa dakika kadhaa, akachukua simu yake na kumpigia mwanaume aliyeitwa kwa jina la Sebastian na kuanza kuzungumza naye.
Sebastian alikuwa kijana wake machachari, mjanja aliyekuwa akimpambania kwa kipindi kirefu. Kabla ya kumpata David, alikuwa akimtumia kijana huyo ambaye alikuwa akiua badala yake mpaka pale alipoamua kuachana naye na kumchukua David.
Alimwambia kwamba alihitaji kuonana naye na kuzungumza pamoja. Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, haraka sana Sebastian akamwambia kwamba angekwenda nyumbani hapo na kuonana kama alivyokuwa ametaka.
Ndani ya dakika kadhaa, akapigiwa simu na mwanaume huyo na kumwambia kwamba alikuwa amefika. Akamwambia aende chumbani mule na ndani ya dakika moja, Sebastian akaingia ndani na kuanza kuzungumza naye.
Kwa jinsi mzee Armando alivyokuwa akiongea, ilionyesha kabisa kulikuwa na kitu kinausumbua moyo wake, alimwambia wazi kwamba mtoto wake alitekwa na mtu aliyemteka alimfahamu sana, aliitwa David.
“Unataka nifanye nini?” aliuliza Sebastian huku akimwangalia mzee huyo.
“Kwanza kumkomboa mtoto wangu, halafu umuuue huyo kijana,” alisema mzee Armando huku akimwangalia Sebastian ambaye akatoa tabasamu pana kwani kile alichoambiwa kilikuwa chepesi kama kuambiwa kwenda kumwaga maji nje.
“Yupo wapi kwa sasa?”
“Hapahapa Ujerumani japokuwa sijajua ni mahali gani,” alijibu mzee Armando.
“Hata kukisia?”
“Nahisi nyumbani kwake. Subiri kijana wangu akupeleke,” alisema Armando.
Hicho ndicho kilichofanyika, haraka sana kijana mmoja akaambiwa aelekee huko kwa lengo la kumtafuta Jericho ambaye alikuwa ametekwa na kufichwa sehemu. Armando hakutaka kuona mtoto wake akipata mateso zaidi, alikuwa tayari kufanya lolote lile liwezekanalo mpaka kuhakikisha mwanaume huyo anamkamata na kumuua kama njia ya kujipa furaha moyoni mwake.
Sebastian na kijana aliyepewa wakafika mahali ilipokuwa nyumba hiyo. Haraka sana akateremka, hakukuwa na mlinzi, nyumba ilikuwa peke yake, ukimya mkubwa ulikuwa umetawala mahali hapo. Kabla ya kuingia, Sebastian akachukuua bastola yake na kuingia ndani ya nyumba hiyo.
Alitembea kwa kunyata, akaufungua mlango na kuingia mpaka sebuleni. Akaanza kuangalia huku na kule, hakuona mtu wala dalili za kuwepo kwa mtu yeyote yule. Akaingia katika kila chumba lakini kote huko hakufanikiwa kumuona mtu yeyote yule.
Alipoona imeshindikana kufanyika siku hiyo, akarudi kwa mzee Armando na kumwambia kile kilichotokea kwamba mtu aliyekwenda kumtafuta huko, hakumkuta. Hilo halikuwa na tatizo, alimpa kazi hiyo, haikuwa lazima kufanyika siku hiyo, hata kama ingefanyika siku nyingine, ingekuwa sawa tu ilimradi mwisho wa siku David auawe kama alivyokuwa akitaka.
“Nitamtuma kwenda kumuua Alfonce, nitaongea na Alfonce na kumwambia kwamba kuna mtu anakuja kukuua, awe makini ili hata kabla ya kuuawa, yeye ndiyo amuue. Yeah! Hii kazi imekwishakuwa nyepesi sana, ngoja nizungumze na Alfonce,” alisema mzee huyo na kuchukua simu kumpigia mwanaume huyo.
Alifonce alikuwa mmoja wa marafiki zake aliokuwa akifanya nao biashara ya kuuza madawa ya kulevya. Alikuwa mwanaume mwenye sura ya upole, mtanashati, Mzungu wa unga ambaye alikuwa na uwezo wa kufanya kitu chochote kile.
Alikuwa akiishi nchini Hispania katika Jiji la Madrid. Akampigia simu na kumwambia kuhusu mpango wake kwamba kulikuwa na mwanaume angemtuma kwake kwa lengo la kumuua lakini upande wa pili yeye ndiye aliyetakiwa kuuawa.
Alfonce alivyoambiwa hivyo, alishtuka, hakutegemea kusikia akiambiwa hivyo na rafiki yake. Alijua kwamba kusingekuwa na mtu ambaye angekuwa na uwezo wa kumuua lakini nini kingetokea kama muuaji huyo angetumia bunduki ya mbali kumtungua.
“Unanitania. Akinipiga risasi?”
“Atakupigaje? Kweli na ulinzi wote huo ataweza kukusogelea?”
“Sasa mimi nitamuuaje? Nitamjuaje? Una picha yake?” aliuliza Alfonce.
“Hapana! Ila nitamtuma kwako.”
“Nitamjuaje?”
“Kwani una urafiki na watu weusi?”
“Kiasi! Yeye ni mweusi?”
“Ndiyo!”
“Basi ishia hapohapo. Nitaifanya kazi hiyo. Nitamuua kwa mkono wangu na kukutumia kichwa chake,” alisema Alfonce.
“Nashukuru sana.”
Mzee Armando hakutaka kumwambia kama mtu aliyekuwa akienda huko alikuwa Mzimu Unaotabasamu kwa kuhofia kukataa kusogelewa na mtu huyo. Dunia nzima hakukuwa na mtu aliyekuwa akogopwa kama yeye, alitafutwa kila kona lakini hakukuwa na dalili zozote za kuonekana sehemu yoyote ile.
CIA na mashirika mengine ya kijasusi yalihangaika dunia nzima kumtafuta mwanaume huyo lakini walishindwa. Hawakujua aliishi wapi, hawakujua ni mtu gani alikuwa akimdhamini kwani kila alipokuuwa akienda, alifanya mauaji na kuufanya ulimwengu ujue kwamba yeye ndiye aliyefanya mauaji hayo.
Alimpa taarifa kwamba alikuwa mtu mweusi hivyo kwa mtu wa aina hiyo ambaye angelazimisha ukaribu kwake basi alitakiwa kujua ndiye huyo na alitakiwa kumuua haraka sana. Alichokifanya mzee Armando ni kumwambia Sebastian naye aelekee nchini Hispania kwa Alfonce ili kufuatilia ni mtu gani mweusi ambaye angeekuwa karibu na mwanaume huyo na kumuua.
Hilo halikuwa tatizo, haraka sana Sebastian akasafiri na kwenda nchini humo huku akiwa na uhakika wa kufanikisha lile alilokuwa ameambiwa. Ili kumfanya Alfonce asihofu chochote, akamwambia kuhusu Sebastian, kwamba mwanaume huyo alikuwa safarini kwenda huko na kufanya mauaji. Alfonce akakubaliana naye bila tatizo lolote lile.
***
Hiyo ilikuwa siku ya kwanza ya mateso makali ambayo Jericho hakuwahi kukutana nayo wala kuhisi kwamba kuna siku angekutana nayo. Alipiga kelele lakini sauti haikuwa ikitoka kabisa kutokana na chumba cha chini alipokuwa amehifadhiwa na hata jinsi alivyofumbwa mdomo wake kwa kuwekewa kitambaa.
David alijua kabisa kwamba ni lazima mzee Armando amtafute kijana wake, na sehemu ya kwanza kabisa kwenda ingekuwa nyumbani hapo. Akatoka na kumwambia Cecilia kwamba walitakiwa kuondoka kuelekea hotelini, alitakiwa kubaki huko kwa kuwa kuna kazi kubwa alikuwa akiifanya.
Wakaondoka na kwenda hotelini, akamuacha hapo na yeye kurudi nyumbani, akaelekea katika kile chumba cha chini na kuendelea na kazi yake.
Jericho alikuwa akilia, hakuweza kuongea, ulimi ulikatwa, alikuwa kwenye maumivu makali kupita kawaida. David hakuonekana kuwa na presha hata kidogo, kila wakati uso wake ulikuwa ukitabasamu tu.
Alichokifanya ni kuchukua kamera na kuanza kumrekodi Jericho pale alipokuwa. Ilikuwa ni video ya dakikka kumi, yenye kutisha. Baada ya kuhakikisha amempiga video ya kutosha, akachukua kitambaa, akakivaa na kuacha macho tu kisha kuendelea na mateso yale.
“Nilipanga nivikate viungo vyako kimoja baada yya kingine. Ila nimeghairi, sasa nitakukata viungo vyote kwa pamoja, leo hiihii,” alisema David.
Hakuwa mtu wa kuzungumza sana, alikuwa mtendaji zaidi. Akachukua kisu chake na kuanza kumkata masikio. Alianza na sikio la upande wa kushoto, kisu kilikuwa kikali kiasi kwamba alipokipitisha mara moja tu, sikio lilikuwa chini.
Hakuishia hapo, akalifuata sikio la pili na kulikata. Kila kitu alichokuwa akikifanya, alikuwa akijirekodi kama kawaida. Jericho alilia lakini David hakutaka kujali, alifanya ukatili mkubwa kiasi kile kwa sababu tu mwanaume huyo alikuwa amembaka mpenzi wake.
Alipomaliza, akamlaza chini na kumwambia kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wake, angemkata kichwa chake na kisha kumtumia baba yake. Alizungumza kama utani, tena huku tabasamu likiwa usoni mwake lakini moyoni mwake alimaanisha, alikuwa mtu hatari ambaye kusingekuwa na mtu yeyote duniani ambaye angetamani kukutana naye.
Akakishika vilivyo kisu chake na kuzishika nywele za Jericho na kilichotokea baada ya hapo ni kumchinja kama kuku. Jericho alikuwa akihangaika, alitamani kujitoa pale alipokuwa lakini alishindwa kabisa. Kilikuwa ni kifo chenye uchungu, David akakichukua kichwa cha Jericho na kukiweka juu ya meza.
Alipohakikisha kwamba amemaliza kila kitu, akatoka na kuelekea juu, wakati akiwa amefika sebuleni, akasikia mlango wa geti ukifunguliwa, alipoangalia, akamuona mwanaume mmoja akiingia na bastola.
Hakutaka kujiuliza, akajua kabisa kwamba huyo alikuwa mmoja wa vijana wa mzee Armando, alichokifanya ni kurudi ndani na kuingia katika kile chumba cha chini kwa kuamini kwamba mwanaume yule asingeweza kufika kule.
Akakaa mule kwa dakika thelathini ndipo akatoka, hakukuwa na mtu yeyote, mwanaume yule, Sebastian alikuwa ameondoka zake. Hakutaka kubaki mahali hapo, akaondoka zake, alipofika hotelini, akapumzika na mpenzi wake mpaka asubuhi ambapo akamtumia ujumbe mfupi mzee Armando kwa njia ya WhatsApp na kumwambia kwamba kulikuwa na maiti ya mtoto wake nyumbani kule katika chumba cha chini hivyo alitakiwa kwenda kuichukua na kuizika hata kabla haijaharibika.
“Nashukuru! Inamaanisha huu ndiyo utakuwa mwisho wa kufanya kazi na wewe?” aliuliza mzee huyo kwa njia ya ujumbe mfupi.
“Nakusikiliza wewe. Ukisema mwisho, utakuwa mwishi, ukisema tuendelee, tutaendelea,” alisema David.
“Naomba tuendelee! Kifo cha mtoto wangu hakiniumizi kwa kuwa nilimwambia kile alichokifanya sikupenda. Na hata kama usingemuua wewe, ningemuua mimi mwenyewe,” aliandika mzee Armando, David alipousoma ujuumbe huo, akacheka sana kwani aliuona kabisa uongo wa mzee huyo.
“Basi nimekurahisishia kazi. Kuna mtu unataka auawe?”
“Wapo wengi. Nataka tuanze na mmoja anaitwa Alfonce.”
“Yupo wapi?”
“Hispania. Nitakupa maelekezo. Nitataka umuue na nitakulipa kama kawaida.”
“Haina shida,” alijibu David pasipo kujua kwamba huko alipotakiwa kwenda, tayari mipango ilisukwa kwa leengo la kuuawa yeye.
***
David hakujisikia amani moyoni mwake, alijua kabisa kwamba ilikuwa ni lazima mzee Armando afanye kila linalowezekana kuhakikisha anammaliza. Hakutaka kuona akifa kizembe na hata huko alipokuwa akielekea alijua kabisa kwamba kulikuwa na kitu nyuma yya pazia.
Akawasiliana na Lee na kumwambia kwamba alihitaji sura nyingine ya bandia ambayo ilitakiwa kupelekwa mpaka nchini Hispania ambapo kulikuwa na kazi ilitakiwa kufanyika haraka sana.
Hilo halikuwa tatizo, sura ikatengenezwa na kama kawaida kijana mmoja kutumwa kuelekea nchini humo katika Jiji la Madrid ambapo ndipo kazi ilitakiwa kufanyika.
Alipofika, akachukua chumba katika Hoteli ya Gran Melia Palacio de Los Duques ambayo gharama yake ilikuwa ni zaidi ya milioni moja kwa usiku mmoja tu.
Akapewa kadi ya kufungulia chumba chake na kuanza kwenda nayo juu. Alikaa kitandani huku akifikiria mambo mengi yaliyokuwa yakiendelea katika maisha yake. Alikumbuka jinsi alivyokuwa mpole, alivyotamani sana kuwa mchungaji wa kimataifa katika maisha yake ya mbele lakini ghafla, kila kitu alichokuwa amepanga kiliharibika.
Hakuacha kumpa lawama baba yake, alimchukia kwa kuwa yeye ndiye aliyemfanya kuwa na roho mbaya na ya kikatili kama aliyokuwanayo kipindi hicho. Mikono yake ilijaa damu, kila alipokuwa akiua, moyo wake ulifarijika na hivyo kutamani kuua zaidi na zaidi.
Huko, alilala siku hiyo na jioni ya siku iliyofuata akaonana na kijana aliyetumwa na Mchina, Lee ambaye alimpelekea sura yake na kuondoka zake. Alichokifanya, siku hiyohiyo katika hoteli hiyo akapanga tena chumba kingine kwa kutumia sura hiyo ya bandia, akapewa kadi na kuelekea chumbani.
Ilikuwa ni lazima huyo Alfonce afe haraka iwezekanavyo. Katika hilo, alitakiwa kuwa makini mno kwani moyo wake haukuwa na amani na mzee Armando kwa kuhisi kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia.
Hakutaka kufanya mambo kirahisirahisi sana, alihakikisha ni lazima afanye vitu kisiri sana na ndiyo maana aliamua kumuingia mwanaume huyo huyo kwa staili nyingine kabisa.
Alitaka kujua kuhusu huyo mwanaume, aliambiwa kwamba alikuwa na pesa, ulinzi mkubwa, alitaka kufahamu mengi kuhusu mwanaume huyo hivyo alichokifanya ni kumuulizia mhudumu kuhusu huyo Alfonce.
Mhudumu alimjua vilivyo, hakukuwa na mtu asiyemjua mwanaume huyo. Alijulikana Madrid nzima kama mtu aliyekuwa akipenda sana starehe. Kwake, kunywa pombe ndiyo ilikuwa furaha yake, alipenda kutembea na wanawake wazuri na alikuwa akimiliki jumba moja kubwa lililokuwa huko Calle del León.
“Everybody knows him!” (kila mtu anamfahamu) alijibu mhudumu wa hoteli hiyo.
“How can I meet him?” (nitaweza kuonana naye vipi?) aliuliza David.
“Do you like soccer?” (unapenda mpira?)
“Yeah!”
Mhudumu huyo alimwambia kwamba sehemu pekee na ya urahisi kumuona mwanaume huyo ilikuwa ni kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu ambapo kesho yake kulikuwa na mechi kati ya Real Madrid na Real Sociedad.
David akashukuru na kumuahidi yule mhudumu kwamba angekwenda kuonana naye, na ili kuonyesha kwamba kweli alisaidiwa, akatoa kiasi cha euro elfu moja na kumkabidhi.
Pesa ile ni kama ilimchanganya msichana huyo, aliona yale maelezo aliyomwambia hayakuwa yakitosha na hivyo kumuongezea kwamba kulikuwa na msichana ambaye kama angemtumia vizuri basi angefanikiwa kumpata mzee huyo kiurahisi zaidi, msichana huyo hakuwa mwingine bali Jolinda Rodriguez.
“Ndiye nani huyo?”
“Ni rafiki yake. Ni msichana mcheshi sana, kama kweli ukionana naye! Utafanikiwa kuonana na huyo Alfonce,” alisema mhudumu yule.
“Sasa nitampata vipi Jolinda?”
“Atakuja klabu! Nitakushtua!”
“Ahsante!”
Baada ya kupewa maelekezo yote, David akaondoka kuelekea chumbani kwake. Alipofika huko, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuandika jina la msichana huyo katika tovuti ya Google na kuanza kumwangalia.
Alimpata. Aliziangalia picha zake, alikuwa msichana mrembo mno, nywele ndefu na kwa jinsi alivyoonekana, alionekana kuwa msichana wa maisha ya juu. Alimwangalia zaidi, picha zake nyingine alipiga na mwanaume aliyeandikwa kama Alfonce, japokuwa hakuwa ameambiwa na mzee Armando kuhusu mwanaume huyo wala kutumiwa picha, akawa na uhakika kwamba alikuwa mwenyewe.
Siku hiyo usiku akapigiwa simu na mhudumu yule na kuambiwa kwamba Jolinda alikuwa amefika katika klabu iliyokuwa katika hoteli hiyo. Hakutaka kubaki chumbani, akaondoka na kuelekea huko, akakutana na mhudumu ambaye alimwambia mavazi aliyokuwa amevaa na hivyo kwenda klabu.
Akapitiliza mpaka VIP, huko akakutana na wanaume wengi walioonekana kuwa na pesa zao, kwenye kochi kuubwa jekundu alikuwepo msichana mrembo aliyevalia kimini na nywele zake alizifunga kwa nyuma huku mkononi akiwa na chupa ya pombe ya Ciroc, akazugazuga na kumsogelea msichana yule.
Alipokaa karibu naye tu, wanaume wawili wakamfuata na kumwambia kwamba alitakiwa kuondoka, hakutakiwa kukaa na msichana huyo, wanaume hao walikuwa walinzi.
David alishangaa, alichokifanya ni kumwangalia msichana yule kwa macho yaliyomwambia kwamba alitaka kuzungumza naye hata kwa dakika kadhaa. Msichana huyo aliutambua mtazamo wa David hivyo kuwaambia vijana wake kwamba walitakiwa kumruhusu kukaa pale.
“U mzuri sana,” alisema David kwa sauti kwani sauti kubwa ya muziki ingeimeza sauti yake.
“Ahsante sana!”
“Bila shaka wewe ni Jolinda!”
“Yeah! Wewe?”
“Naitwa Emmanuel Kom, ni Muingereza, nimekuja kutembea huku. Nacheza katika Klabu ya Newcastle! Unaifahamu?” alisema David huku akimwangalia msichana huyo.
Jolinda akastuka kidogo, hakuamini kusikia kile alichoambiwa, ni kweli alikuwa akipenda sana mpira na kitendo cha kukutana na mwanaume huyo kilimaanisha kwamba angeweza kwenda hata Uingereza kutembea, moja ya nchi alizokuwa akizipenda sana.
“Ooh! Kumbe wewe ni mwanasoka?”
“Yeah! Mimi ni rafiki mzuri wa nyavu. Nazisalimia sana,” alisema David na wote kuanza kucheka.
“Hongera sana. Hivi hujatamani hata kuja kucheza Real Madrid hata siku moja?”
“Ninatamani kila siku lakini natakiwa kupambana sana,” alisema David.
Walibaki wakizungumza mambo mengi tu, baada yya hapo, wakabadilishana namba za simu na kuanza kuwasiliana kwenye simu.
Kwa kuwa mwezi huo ulikuwa ni wa sita, David alimwambia kwamba alikuwa likizo na baada ya siku kadhaa angerudi nchini Uingereza ambapo huko angemkaribisha msichana huyo japo kukaa kwa siku kadhaa nchini humo.
Kutokana na uchangamfu mkubwa aliokuwanao David, Jolinda akatokea kumpenda, kila siku, tena mara kwa mara alikuwa akimpigia simu na kumsalimia. Urafiki ukadumu huku mara nyingine wakiwa wanatoka na kwenda sehemu kutembea.
David alikuwa na pesa, alitaka kumuonyeshea msichana huyo kwamba kweli alikuwa mwanasoka aliyekuwa na kipato kizuri. Kila kona, yeye ndiye aliyekuwa akilipia kwa kila kitu kiasi kwamba Jolinda akaamini moja kwa moja kwamba mwanaume huyo alikuwa na pesa.
“Huyu nakwenda naye hivihivi! Mwisho wa siku, nitataka nikutane na huyo Alfonce na kumfanyia kazi,” alijisemea David huku akiwa na uhakika wa kukamilisha kazi kubwa iliyokuwa mbele yake.
***
Dunia ilishtuka, hakukuwa na aliyeamini kile alichokuwa akikiona, video za unyama aliokuwa amefanyiwa mtoto wa bilionea Armando. Hakukuwa na mtu aliyeamini kama kungekuwa na mtu aliyekuwa na uwezo wa kufanya unyama mkubwa kiasi kile, wengi walioona, hawakuamini macho yao na mbaya zaidi, muuaji huyo ndiye yuleyule alijitambulisha kwa jina la Mzimu Unaotabasamu.
Watu wakachanganyikiwa, hawakuamini kilichokuwa kikiendelea. Muuaji huyo alionekana kuwa tishio, kila kona jina lake lilikuwa likivuma kupita kawaida. Maofisa wa CIA walihangaika usiku na mchana kumtafuta lakini kitu cha ajabu kabisa, alikuwa akifanya mauaji kwa kuhamahama huku akituumia sura za bandia.
Video hiyo ikawa gumzo duniani, Jericho alionekana akiteswa kwa mateso makubwa mno, alilia na kuomba msamaha sana lakini muuaji hakutaka kumuacha, aliendelea kumtesa mpaka kumkata kichwa na kumtumia baba yake.
Dunia ni kama ilitikisika, watu walichanganyikiwa, matajiri waliogopa na kuona kwamba kama wangeendelea kuwa na maadui basi wangeweza kuuawa au kutekwa kama ilivyokuwa kwa mtoto wa bilionea Armando.
CIA hawakutulia, dunia nzima ilikuwa ikiwazungumzia wao kwamba kwa nini mpaka kipindi hicho walishindwa kumkamata mtu huyo na wakati alikuwa akiendelea kufanya mauaji kila kona?
Hakukuwa na mtu aliyejibu lolote, kwao, lile likaonekana kuwa kama kashfa, walijitahidi kwa nguvu zao nyingi kumtafuta mwanaume huyo lakini hawakufanikiwa na mbaya zaidi, hata kwa kutumia simu hawakuweza kumpata.
“Huyu ni nani?” lilikuuwa swali lililokuja kichwani mwa kila mtu, swali ambalo lilikosa majibu.
“Swali si yeye ni nani! Ila ni kwa nini anaua?”
“Hilo nalo la msingi. Hivi kweli mtuu anaweza kufanya unyama kama huu? Sidhani! Nahisi kuna kitu, inawezekana huyu mtu hana akili,” alisema jamaa mmoja.
Kila kona ni Mzimu Unaotabasamu tu ndiyo uliokuwa ukizungumziwa, magazetini, aliandikwa sana, kwenye televisheni alizungumziwa sana.
Watu wengi waliogopa kwa kuhisi kwamba baada ya matajiri muuaji huyo angeweza kuhamia kwao kwani alifanya mauaji pasipoo kuangalia huyu ni nani, kulionekana kutokuwa na sababu maalumu bali alipenda kuua pasipo kuangalia mt yeyote yule.
Kampeni kubwa ikawekwa duniani, kampeni ya kumtaka muuaji huyo aache kufanya mauaji hayo. Watu wengi wakajitokeza barabarani katika nchi mbalimbali kuandamana, walipinga mauaji hayo na kila mtu alitaka dunia iwe sehemu ya amani na si ya mauaji kama ilivyokuwa.
“Stop killings! Love each other,” (Acha mauaji! Tupendane) yalikuwa ni baadhi ya mabango yaliyokuwa yameshikwa na watu mbalimbali. Hakukuwa na mtu aliyejua kwamba katika kipindi hicho kulikuwa na mauaji mengine yalitakiwa kufanyika nchini Hispania.
***
David hakutaka kuacha kuwasiliana na msichana huyo, alimtumia muda wake mwingi kumpigia simu na hata kuwasiliana kwa kuandikiana meseji. Kitu alichokigundua ni kwamba msichana huyo alipenda sana Waingereza na kikubwa zaidi alitamani sana kutembelea nchi hiyo.
Alipoligundua hilo, akaanza kumwambia mambo mengi kuhusu Uingereza, jinsi watu walivyokuwa wakila bata na hata wengine kusafiri kwa umbali mkubwa kwenda kutazama mpira wa miguu. Jolinda alichanganyikiwa, alitamani kumfuata David usiku huohuo na kumwambia ampeleke nchini humo na kwenda kuangalia kila kitu kilichokuwa kikiendelea huko.
“Na daraja?” aliuliza Jolinda.
“Lile la London?”
“Ndiyo! Huwa watu wanajaa sana kupiga picha?” aliuliza msichana huyo.
“Sana. Watu wengi huja pale. Yaani kwa kifupi Uingereza ni sehemu nzuri sana, kama itawezekana naomba keshokutwa twende huko,” alisema David.
“Mmh!”
“Unaogopa?”
“Hapana! Haina shida. Naomba unipeleke,” alisema Jolinda huku akionekana kuwa na furaha tele.
Hilo halikuwa tatizo, hakuwa na shida ya pesa, kwenye akaunti yake kulikuwa na kiasi kikubwa cha pesa, alichokifanya siku hiyo ni kupanga mikakati ya safari na kuelekea huko Uingereza kwa lengo la kula raha tu.
Hawakuwa wamefahamiana kwa kipindi kirefu lakini Jolinda akatokea kumkubali David kupita kawaida. Kesho yake, wakaonana na kupiga stori. Muda wote msichana huyo alionekana kuwa na furaha isiyo kifani, aliufurahia ukaribu wake na David pasipo kugundua kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia.
Jolinda akawa na kazi ya kuulizia safari ya kuelekea Uingereza. Japokuwa aliambiwa kwamba kesho ndiyo ilikuwa safari yenyewe lakini hakutulia, kila wakati yeye alikuwa mtu wa kuulizia safari tu.
Alizaliwa kwenye familia iliyokuwa na pesa, wanaume aliokuwa akitembea nao walikuwa ni Wahispania tu, kwa nchi za Ulaya, Waingereza walionekana kuringa kupita kawaida, hawakupenda kuwa na wanawake wa mataifa mengine na ndiyo maana Waingereza wengi wameoana wenyewe kwa wenyewe.
Kwa Jolinda, alitaka kuonja mwanaume wa Kiingereza, alifananaje na alikuwa na kitu gani cha ajabu kitandani. Wakazungumza mambo mengi siku hiyo na siku iliyofuata wakaondoka na kuelekea nchini humo.
Ndani ya ndege, Jolinda alichanganyikiwa, aliona ndege ikienda taratibu sana, kila wakati alimuuliza David kuhusu Uingereza, alitaka kufahamu mambo mengi kuhusu nchi hiyo.
Hawakutumia saa nyingi, ni ndani ya saa moja na nusu wakaingia nchini humo. Wakati ndege ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heathrow jijini London nchini Uingereza, macho yake yalikuwa dirishani huku akiangalia mandhari ya jiji hilo jinsi lilivyokuwa.
Walipoteremka, alikuwa beneti na David, hakutaka kumuacha, ili kumzuga msichana huyo, alivalia kofia na miwani kwa kumwambia kwamba hakutaka kugundulika kwani angesumbuliwa na mashabiki zake na hivyo kulilia kupiga picha.
Hilo likamfanya Jolinda kuona alikuwa na mtu maarufu sana nchini Uingereza, wakaondoka na kuelekea hotelini, wakakaa katika hoteli ya kifahari na kutanua sana.
Usiku huohuo akamuaga Jolinda kwamba alikuwa akienda kuzungumza na meneja wake aliyekuwa chini hotelini. Hilo halikuwa tatizo hasa kwa msichana kama Jolinda ambaye aliyajua maisha ya masupastaa.
Alipoteremka, akamtafuta mhudumu na kumwambia awatafutie vijana ishirini ambao angewalipa vizuri kwa kufanya kazi yake. Hilo halikuwa tatizo, akatafutiwa vijana hao na kuanza kuzungumza nao.
Aliwaambia kwamba alitaka kujifanya supastaa kwa hiyo usiku huo kama angetoka chumbani na kwenda hotelini basi wote walilie kupiga naye picha. Ili kufanya kazi hiyo vizuri, akamlipa kila mmoja dola elfu mbili na kuwapeleka mgahawani na kuanza kunywa.
Akarudi chumbani na kumwambia Jolinda kwamba alimalizana na meneja wake hivyo walitakiwa kushuka mgahawani kwa lengo la kula chakula.
“Kwa nini usiagize chakula kije hukuhuku?” aliuliza Jolinda.
“Twende tu mgahawani mpenzi!”
“Kule kuna watu, huogopi kugombaniwa?”
“Usijali! Ni maisha yetu. Twende tu,” alimwambia msichana huyo.
Wakaondoka na kuelekea mgahawani. Walipofika, alipoingia na kukaa, watu wote wakaanza kumwangalia kwa mshangao. Wengine wakamsogelea, walionyesha kushtushwa na kumkuta mahali hapo, wakamkumbatia na kukata kupiga naye picha.
Ilikuwa ni kama fujo, kila mtu alitaka kupiga naye picha kama alikuwa amekutana na mtu maarufu. Jolinda akaamini kwamba alikuwa na mtu maarufu mno nchini Uingereza, akastaajabu yale yaliyokuwa yakiendelea.
“Emmanuel! Wewe ni maarufu sana jamani!” alisema Jolinda huku akimwangalia mwanaume huyo.
“Kawaida sana. Ukiwa unafunga mabao mengi ni lazima uwe maarufu kwa kuwa unawafurahisha watu wengi,” alisema David huku akimwangalia msichana huyo.
Kwa kile kilichofanyika pale mgahawani kilimfanya Jolinda kuzidi kuamini kwamba mwanaume huyo alikuwa supastaa. Wakala na kunywa kisha kurudi chumbani.
Walifanya mambo mengi kama wapenzi na siku iliyofuata wakatembea sehemu mbalimbali na siku hiyohiyo kurudi nchini Hispania huku Jolinda akiwa na uhakika wa asilimia mia moja juu ya kile alichoambiwa na David kwamba alikuwa staa mkubwa.
“Kuna siku nitachezea Real Madrid, ni ndoto yangu japokuwa sijajua nitaanzia vipi,” alisema David huku akijifanya kutia huruma.
“Mbona rahisi sana!”
“Kivipi?”
“Nina rafiki yangu ambaye ni kama ndugu yangu, anafahamiana na bosi wa klabu hiyo, anaitwa Alfonce. Yaani nikizungumza naye, hakuna tatizo,” alisema Jolinda, alijibebisha kwani tayari aliona mwanaume huyo alikuwa na pesa sana.
“Basi nikutanishe naye!”
“Haina shida. Nitafanya hivyo! Ngoja nimpigie simu kwanza,” alisema Jolinda, akachukua simu yake na kumpigia Alfonce ambapo akahitaji kuonana naye, hilo halikuwa tatizo, wakapanga muda wa kukutana katika mgahawa wa KFC uliokuwa hapo Madrid.
***
Alfonce alikutana na Sebastian na kupanga mipango mingi, walijua kwamba kwa namna moja au nyingine ilikuwa ni lazima David afike nchini Hispania kwa lengo la kufanya mauaji kama alivyokuwa ameambiwa.
Walipanga mipango mingi na kukubaliana kwamba siku ambayo mwanaume mweusi angekuja kwake na kuzungumza naye kuhusu jambo lolote lile basi huyo ndiye alikuwa David na hivyo alitakiwa kuuawa mara moja.
Wakati wakiwa wamepanga, baada ya siku mbili akapigiwa simu na Jolinda na kuambiwa kwamba alitaka kuzungumza naye, hilo halikuwa tatizo, wakapanga mahali pa kuonania na kuonana huko.
Jolinda akaonana naye huku akiwa na David. Mawazo ya Alfonce kugundua kwamba mwanaume huyo ndiye alikuwa David yalipotea kabisa mawazoni mwake kwa kuona kwamba David angetumia nafasi ya kuonana naye kupitia yeye na si vingine, hakujua kama huyo David alikuwa akifikiria mbele zaidi yake.
“Huyu ni mpenzi wangu!” alisema Jolinda huku akimwangalia Alfonce.
David akasalimiana na Alfonce na kuanza kupiga stori. Muda mwingi wa mazungumzo yao Jolinda alikuwa akimsifia David kwamba alikuwa mwanaume mzuri aliyejua kupenda na alimjali kupita wanaume wote aliowahi kuwa nao.
“Na mna muda gani tangu muwe kwenye uhusiano?” aliuliza Alfonce.
“Miezi miwili,” alijibu Jolinda kwa harakaharaka kwani alihisi kwamba kama angemwambia Alfonce ni siku chache zilizopita angeshangaa kwa kutokea kumwamini mwanaume kwa kasi namna hiyo.
“Sawa. Nimefurahi kusikia hivyo! Umetoka wapi?”
“Uingereza. Ninaishi Newcastle na ninachezea timu hiyo pia,” alisema Alfonce.
“Ooh! Sawa. Karibu Hispania!”
“Haina shida mkuu!”
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kufahamiana, David alijua kwamba kama angejifanya kuwa beneti na mwanaume huyo basi inawezekana kabisa angemgundua kwamba yeye ndiye aliyetumwa kwani tayari alikuwa na hofu kwamba inawezekana mwanaume huyo alikwishapewa taarifa kuhusu yeye.
David alikuwa huru kufanya mauaji siku yoyote ile, alichokuwa akikitafuta ni nafasi ya kufanya hivyo tu. Siku ziliendelea kwenda mbele, alipokuwa akiwasiliana na mzee Armando alimwambia kwamba bado hakuwa ameonana na Alfonce hivyo alikuwa akijipanga kuhakikisha anafanya kila liwezekanalo kumuua.
Alipokuwa akipewa taarifa, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumpigia simu Alfonce na kumwambia kila kitu alichokuwa ameambiwa na david.
“Kwa hiyo bado hajaonana nami?” aliuliza Alfonce.
“Yeah! Bado! Nimezungumza naye, ila amesema atakufuata!”
“Hatoweza kunipata. Na siku ambayo atanifuata, naomba uniambie,” alisema Alfonce.
“Kwa hilo usijali hata kidogo.”
Mpaka kufikia hapo, Alfonce hakuwa na shida na David ambaye kwake alijitambulisha kwa jina la Emmanuel. Alimwamini mwanaume huyo na muda mwingi alikuwa akizungumza naye kwenye simu kama shemeji yake kwa msichana Jolinda.
Ukaribu wao ukaongezeka, wakawa wanatembeleana huku muda wote ambao alikuwa akienda kuonana naye aliongozana na Jolinda. Kutokana na kuwa karibu na mwanaume huyo, Alfonce akaamua kumtambulisha David kwa rafiki yake, Sebastian ili kujenga ukaribu kwani aliamini kwa kuwa mwanaume huyo alikuwa mweusi, basi kusingekuwa na tatizo kama David atakapokuja na kumtumia mwanaume huyo kummaliza kwa urahisi.
“Una uhakika huyu si mtu wetu tunayemtafuta?” aliuliza Sebastian.
“Hakuna. Huyu ni shemeji yangu, mpenzi wa Jolinda.”
“Una uhakika?”
“Ndiyo! Walianza uhusiano miezi miwili iliyopita, juzijuzi ndiyo alinitambulisha rasmi,” alisema Alfonce.
“Hapo sawa. Nahisi hakuna tatizo,” alisema Sebastian.
Bado David alivyokuwa akizungumza na mzee Armando alimwambia kwamba bado hakuwa ameonana naye na kwa jinsi mwanaume huyo alivyokuwa akijificha alionekana kuwa mgumu sana kupatikana.
Hilo halikuwa tatizo, alichokifanya mzee huyo ni kumuongezea kiasi cha pesa na kumwambia kwamba afanye kila linalowezekana mpaka ahakikishe Alfonce anakufa kama wengine.
“Sawa. Nitamfuatilia mpaka kuhakikisha namuua.”
“Haina shida. Nakutegemea.”
***
Wiki ya kwanza ikakatika tangu Sebastian awe nchini Hispania kwa kazi ya kummaliza David lakini mpaka muda huo hakukuwa na dalili zozozte za kumuona mwanaume huyo na kumuua.
Alichanganyikiwa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, mara kwa mara alimpigia simu mzee Armando na kumwambia kuhusu kilichokuwa kikiendelea lakini mzee huyo alimwambia atulie kwani David angemfikia Alfonce na kufanya harakati za kumuua.
Hakukuwa na aliyejua kama mtu aliyekuwa akisubiriwa ndiye yule ambaye walikuwa wakiongea naye na kumfahamu kwa jina la Emmanuel, kila siku walikutana naye na kula bata huku kila mmoja akijua kwamba mwanaume huyo alikuwa mpenzi wa Jolinda hivyo walitakiwa kumuheshimu.
David hakutaka kuonekana mtu wa kawaida, alikuwa akitumia pesa vibaya huku akiwaambia wanaume hao kwamba alikuwa mwanasoka aliyekuwa akilipwa vizuri tu nchini Uingereza.
Walimwamini, matumizi yake yalikuwa makubwa mno kiasi kwamba kila mmoja aliamini kwamba kweli mwanaume huyo alikuwa mwanasoka kwa sababu watu hao walilipwa vizuri sehemu mbalimbali barani Ulaya.
Kadiri siku zilivyozidi kwenda mbele ndivyo Jolinda alivyozidi kuchanganyikiwa kwa David, kila siku alikuwa pamoja naye huku akimuahidi kwamba ni lazima siku moja wafunge ndoa kwani kati ya ndoto ambazo aliwahi kuwa nazo katika maisha yake kwa kipindi kirefu ni kuolewa na Muingereza.
David akaaminika, Alfonce akazidi kuwa karibu naye kiasi kwamba hata walinzi wake wakamzoea na kumuona kama ndugu wa bosi wao kitendo ambacho kilikuwa kosa kubwa sana.
David hakutaka kumwambia mzee Armando alipokuwa ameishia, kila alipokuwa akiwasiliana naye kwenye simu alimwambia kwamba hakuwa ameonana na mwanaume huyo na ilionekana kuwa na ugumu mkubwa kuonana naye kwani kwa jinsi alivyofuatilia ilionyesha kabisa mtu huyo alikuwa akilindwa sana.
“Analindwa sana?” aliuliza mzee Armando.
“Ndiyo! Nimesikia analindwa sana, yaani hata ukiwa mdunguaji, kumpiga risasi vigumu sana,” alisema David alipokuwa akiongea naye kwenye simu.
“Kwa hiyo tufanye nini?”
“Sijajua! Yaani nimejaribu kumtafuta lakini hali imekuwa ngumu sana. Kuna kipindi nasikia yupo sehemu fulani, nikienda huko, naambiwa ametoka, yaani imekuwa ni usumbufu na usumbufu,” alisema David.
“Kwa hiyo kazi itafanikiwa kweli?”
“Bila shaka itafanikiwa. Nipe muda.”
Hivyo ndivyo alivyokuwa akimwambia mzee huyo kila siku, hakutaka kumwambia ukweli kile kilichokuwa kikiendelea kwani alihisi kama kulikuwa na mpango ulikuwa umefanywa na ndiyo maana mzee huyo alikuwa akimuulizia kila siku tofauti na kazi za watu wengine ambazo alimpa kabla.
Huko Hispania, David alikuwa mtu wa bata tu, aliendelea kumuonyeshea Jolinda kwamba alikuwa akipenda starehe na alijua hasa kutumbua pesa. Kila siku jioni alikuwa akienda naye kutembea baharini kwa boti ya kifahari ya kukodi na kurudi naye usiku wa manane.
Jolinda alijiona kufika, alijiona kupendwa kuliko msichana yeyote katika dunia hii. Penzi lilimchanganya kiasi kwamba wakati mwingine alijiona kama akielemewa nalo kwani yalikuwa mapenzi ambayo hayajawahi kutokea katika dunia hii.
Baada ya kukaa nchini Hispania kwa mwezi mmoja huku akiwa amezoeleka na kila mtu ndipo akamwambia Jolinda kwamba alitakiwa kurudi nchini Uingereza kwenye kambi ya timu yake kwa kuwa mechi za maandalizi ya msimu mpya zilitakiwa kuanza haraka sana.
Jolinda akamwangalia mpenzi wake, maneno aliyoambiwa yalimuumiza sana, alitamani kuendelea kubaki na mpenzi wake huyo kwa siku zaidi kwani alimzoea na alijua kabisa kwamba kama angerudi nchini Uingereza angekuwa bize sana na mpira kiasi cha kulifanya penzi lao lianze kuisha.
“Ninataka unipende milele mpenzi, naomba usiniache,” alisema Jolinda huku akimwangalia david usoni.
“Nitakupenda maisha yangu yote. Nilikwambia hilo kabla na nitaendelea kukwambia kwamba penzi langu kwako ni la kufa na kuzikana,” alisema David huku akimwangalia msichana huyo na kumtolea tabasamu pana.
Wakakumbatiana, alichomwambia ni kwamba walitakiwa kwenda sehemu kusherehekea hata kabla ya kurudi nchini Uingereza na sehemu ambayo aliichagua ni kwenye Kisiwa cha Canary sehemu iitwayo Las Palma.
Hiyo ilikuwa ni sehemu moja nzuri ambayo ilitembelewa na watu wengi. Ilikuwa ni moja ya majimbo ya Tenerife ambapo watu wengi walikuwa wakienda huko kwa lengo la kufurahia na familia zao.
Kulikuwa na uoto wa asili, mahali kilipokuwa kisiwa cha Canary hakukuwa mbali na Morocco. David alimwambia Jolinda kwamba alikuwa akisikia sana kuhusu kisiwa hicho na hivyo alitamani kwenda huko kujionea kwa macho yake uoto wa asili uliokuwa huko ambapo sehemu kubwa ilikuwa ni misitu na milima mikubwa.
Hakutaka kwenda huko wawili bali alichomwambia ni kwamba angekwenda na Alfonce kwani kwake, mwanaume huyo alikuwa kama rafiki yake mkubwa nchini humo.
Jolinda akapewa kazi ya kuzungumza na Alfonce, alichokifanya msichana huyo ni kumpigia simu na kuanza kuongea naye. Alimshawishi sana kuhusu kwenda huko huku akimwambia kwamba huo ndiyo ungekuwa mtoko wake wa mwisho pamoja na David ambaye alitarajiwa kuondoka kurudi nchini Uingereza.
“Nakuomba. Naomba twende tukafurahie pamoja, anatuaga, anaondoka, nakuomba twende wote,” alisema Jolinda kwa sauti ya kubembeleza.
“Kweli?”
“Ndiyo!”
“Niambie utaniandalia nini!”
“Wanawake. Nitakuwa na marafiki zangu, wanawake wazuri ambao hutoyaamini macho yako,” alisema Jolinda na kutoa kicheko cha chini kwani alijua jinsi rafiki yake huyo alivyopenda wanawake.
Mpaka kufikia hapo hakutakiwa kutumia nguvu kubwa kumshawishi, alipoambiwa kuhusu wanawake, akakubaliana naye na hivyo kumwambia kwamba naye angekwenda kusherehekea pamoja naye.
“Amesemaje?” aliuliza David.
“Amekubali!”
“Kweli?”
“Yeah! Huamini?”
“Nakuamini mpenzi. Ahsante sana,” alisema David.
Moyo wake ukawa na furaha tele kwa kuamini kwamba huko ndipo ambapo angekwenda kumalizia kazi yake iliyomfanya kusafiri mpaka nchini Hispania. Akapiga simu katika hoteli nzuri iliyokuwa kisiwani huko na kuwaambia kwamba alihitaji vyumba vinne kwa ajili yake, Alfonce na marafiki wa Jolinda, hilo halikuwa tatizo, alipolipia, vyumba vikaandaliwa.
Baada ya siku mbili tayari watu hao walikuwa kwenye boti ya kifahari aliyokodi David na kuanza kuelekea katika kisiwa hicho ambacho kilikuwa kilometa kadhaa kutoka katika Jiji la Madrid.
Njiani, walikuwa wakizungumza kwa furaha, walikunywa na kula huku muda wote David akiwa bize na Jolinda aliyekuwa amemkumbatia na kulishana kama njiwa.
Kwa jinsi alivyoonekana, ilikuwa vigumu kugundua kwamba yote hayo aliyokuwa akiyafanya kwa msichana huyo hayakutoka moyoni bali aliyafanya kwa kuwa kulikuwa na kazi kubwa aliyotakiwa kuifanya.
Alfonce hakutaka kupoteza muda wake kwenda na walinzi wake, alijiamini na kuwaambia vijana wake wabaki nyumbani kwani kule alipokuwa akienda, hakutaka kuingiliwa na mtu yeyote yule, na kwa kuwa aliambiwa kwamba kulikuwa na wanawake, aliamini kwamba kama angekuwa peke yake ndiyo ungekuwa muda mzuri wa kustarehe na wanawake hao kuliko vile ambavyo angekuwa na walinzi wake.
Kwenye boti ilikuwa ni fujo, walifanya uchafu wa kila aina, walipiga kelele, waliimba na kuruka huku na kule. Ili kumzuga Alfonce, David hakutaka kuwa naye beneti, alijifanya kujiweka bize na Jolinda ili kumfanya mwanaume huyo kutokuhisi kitu chochote kile jambo lililomfanya Alfonce kutokuhisi kitu chochote kile kibaya.
Walichukua dakika arobaini, wakafika katika kisiwa hicho na kuteremka. Kutoka baharini mpaka ilipokuwa hoteli ilikuwa ni mwendo wa gari wa dakika kumi hivyo wakapanda magari ya hoteli waliyokuwa wameweka oda na kuanza kwenda huko.
Wakati wakiwa wamefika hotelini, Alfonce akawachukua wasichana wawili, marafiki wa Jolinda na kwenda nao chumbani kwake, alipofika huko, akawatupa kitandani, akavua nguo zake na kuanza kuwapapasa huku na kule. Wakati zoezi lake likiendelea, mara simu yake ikaanza kuita, akaichukua na kuangalia kioo, mpigaji alikuwa Sebastian.
“Kuna nini?” aliuliza Alfonce kibabe kwani alipokuwa akistarehe na wanawake, hakuhitaji usumbufu wowote ule.
“Upo wapi?” ilisikika sauti ya Sebastian.
“Nakula bata!”
“Wapi?”
“Kisiwani!”
“Kisiwani! Mbona hukuniambia? Hata kunipigia simu mshikaji wangu!”
“Ilikuwa ghafla sana.”
“Poa. Upo na nani?”
“Maswali yamekuwa mengi sana Seb! Unaonaje tukaonana nikirudi?”
“Ila si nimekuuliza!”
“Nipo na Jolinda, mshikaji wake yule Muingereza na mademu kibao!” alijibu Alfoncce na kutoa kicheko.
“Upo nao wote hu...” aliuliza Sebastian lakini hata kabla hajamaliza swali lake, akamkatia simu na kuizima kabisa.
Upande wa pili Sebastian alishangaa, haikuwa kawaida kumpigia simu rafiki yake huyo na kumkatia kama alivyofanya. Aliumia moyoni mwake lakini akaamua kupuuzia kwani aliamini kwamba inawezekana kabisa Alfonce alimfanyia hivyo kwa kuwa tu alikuwa na mademu.
Akatulia. Bado kichwa chake kilisumbuka kuhusu David, aliambiwa kwamba mwanaume huyo angefika nchini Hispania kwa kazi kubwa ya kumuua Alfonce lakini cha kushangaza mpaka muda huo hakuwa amepata kitu chochote kile na hakujua kama mwanaume huyo tayari alianza mipango yake ya kumuua Alfonce au la.
Kila alipomwambia mzee Armando, alimwambia kwamba alikuwa akiwasiliana na David na kumwambia kwamba kazi haikuwa imefanyika kwa kuwa hakuwa amepata nafasi ya kumuona mtu huyo hivyo alitakiwa kusubiri.
Muda ulizidi kwenda, ilipofika majira ya saa mbili, Sebastian akachukua simu yake na kumpigia Alfonce. Simu haikuwa ikipatikana, hakutaka kujali sana, alihitaji kuzungumza naye hivyo kumpigia simu Jolinda.
Simu ilianza kuita na baada ya dakika chache ikapokelewa huku kukisikika kelele nyingi upande wa pili, lakini katika kelele hizo, aliyasikia mazungumzo vizuri kabisa.
“Tell me what happened, where is my brother. Tell me, where is my brother?” (niambie nini kimetokea, kaka yangu yupo wapi. Niambieni kaka yangu yupo wapi?) ilisikika sauti ya Jolinda kutoka upande wa pili ambapo simu ilipokelewa lakini pasipo mtu yeyote kuongea.
“Halo! Halo!” aliita Sebastian huku akianza kuwa na hofu.
“Halo!”
“Who is this?” (nani wewe?)
“Emmanuel!”
“Emmanuel! What is going on there?” (Emmanuel! Nini kinaendelea huko?) 
“I have killed him!” (nimemuua!)
“What?” (nini?) aliuliza kwa mshtuko.
“I have killed him!” (nimemuua) alijibu david kisha kukata simu kitu kilichomfanya Sebastian kuchanganyikiwa.
***
David hakutaka kujifanya yupo bize na Alfonce, muda wote alikuwa bize na mpenzi wake wa muda, Jolinda na kujifanya akimpenda na kumpa mapenzi ya njiwa.
Kichwa chake kilikuwa kikipanga mipango kabambe, ilikuwa ni lazima amuue Alfonce na kitu kizuri ambacho alihitaji kukifanya ni kuonyesha kwamba hakujali sana kuhusu yeye hivyo kuendelea na mambo yake.
Walikula na kunywa, kwa Alfonce alifanya starehe za kila aina mpaka kufanya mapenzi na marafiki wa Jolinda ambao walikwenda nao katika kisiwa kile.
Siku hiyo walilala huko mpaka siku iliyofuata. David hakutaka kuona wanaondoka kisiwani hapo pasipo kumuua Alfonce ambaye aliambiwa kwamba ni lazima ahakikishe anakufa ndiyo aondoke nchini Hispania.
Asubuhi ilipofika, yeye ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuamka na kuelekea jikoni ambapo akaandaa kahawa na kumpelekea mpenzi wake kitandani pale. Kwenye sahani hakukuwa na vitafunwa tu, bali pia kulikuwa na ua zuri ambalo aliamini kwamba mpenzi wake huyo angelifurahia.
Hilo likampagawisha Jolinda na kuona kwamba katika dunia nzima hakukuwa na mwanamke aliyekuwa akipendwa kama yeye. Palepale kitandani, akawekewa kahawa ile na kuanza kunywa.
“Ninakupenda sana,” alisema David huku akimwangalia Jolinda kwa macho yaliyoonyesha mapenzi yote na wakati moyoni mwake hakukuwa na lolote lile.
“Ninakupenda pia. Umebadilisha maisha yangu, hakika ninajivunia kuwa na mwanaume kama wewe. Naomba unioe,” alisema Jolinda huku akimwangalia David.
“Hakika nitakuoa. Nakuhakikishia tukiondoka kisiwani, nitakuvisha pete ya uchumba,” alisema David.
“Kweli?”
“Unatakiwa kuniamini katika hilo,” alisema David maneno yaliyomfanya Jolinda machozi kumlenga.
Hakutaka kukaa sana chumbani, akamwambia Jolinda kwamba alitaka kwenda kuzunguka na boti ndogo baharini pamoja na rafiki yake, Alfonce. Hilo halikuwa tatizo, kwa Jolinda lilionekana kuwa jambo jema kwa kuwa tu hilo lingewafanya wawili hao kuwa karibu zaidi.
David akaondoka na kuelekea katika chumba cha Alfonce na kugonga, baada ya dakika moja mlango ukafunguliwa na mwanaume huyo aliyetoka huku akiwa na boksa tu. Macho yake yalipotua kwa David, uso wake ukajawa na tabasamu pana, kwake, David alionekana kuwa mwanaume sahihi kwa rafiki yake, Jolinda.
David akamwambia kwamba alitaka kuondoka naye kuelekea baharini kwa boti ndogo kwa ajili ya kula raha tu. Kwa Alfonce ambaye alizoea maisha ya starehe, hilo halikuonekana kuwa jambo baya, kwake, David alionekana kuwa mtu muhimu sana, japokuwa alikuwa na pesa lakini David hakutaka atumie, kila kitu kilikuwa kwake jambo lililomfanya Alfonce kuona kwamba mwanaume huyo alistahili kuwa shemeji yake.
Alfonce akakubaliana naye, akarudi ndani, akawabusu wanawake aliolala nao kisha kujiandaa kwenda huko baharini. David akarudi mpaka chumbani, akaunganisha mpaka katika sehemu ya jiko na kuchukua kisu.
Alikificha kwa kukiweka kwa nyuma na kukibana na suruali yake ya jinsi na kukifunika na fulana, alipoona kwamba kimekaa sawa, akamuaga Jolinda na kuondoka zake huku akiwa na kadi yake ya benki.
Tayari roho ya mauaji ikamuingia, siku hiyo alitakiwa kufanya mauaji hayo kwa kuwa tu muda ulikuwa ukienda na hakutaka kushtukiwa kwamba hakuwa mchezaji mpira kama alivyokuwa amewaambia watu hao.
Akakutana na Alfonce, wakaingia kwenye boti na pombe kali na kuondoka mahali hapo. Walikuwa wakipiga stori mbalimbali huku kila mmoja akiwa ameshikilia chupa iliyokuwa na pombe.
Alfonce hakuuhisi kabisa ubaya wa David, kwake, mwanaume huyo alionekana kuwa mpole, mwenye huruma nyingi kwani hata maneno aliyokuwa akiyazungumza yalionyesha kabisa kwamba kama si kucheza soka basi angeweza kuwa hata padri.
David akahakikisha wamekwenda mpaka mbali na kisiwa kile, akasimamisha boti na kumgeukia Alfonce na kuendelea kunywa huku wakipiga stori mbalimbali.
“Hivi unaonaje kama utanitafutia nafasi pale Real Madrid?” aliuliza David.
“Real Madrid?”
“Ndiyo! Ninatamani sana kucheza katika klabu ile,” alisema David.
“Kiukweli ni vigumu sana, labda ufanye kitu kimoja,” alisema Alfonce.
“kitu gani?”
“Unaonaje ukaachana na wakala uliyekuwanaye na ukanichukua mimi?” aliuliza Alfonce, japokuwa David alionyesha kama kusaidiwa lakini mwanaume huyo akaingiza mambo ya biashara kabisa kuonyesha kwamba hakuwa tayari kusaidia bali alitaka kufanya biashara na kuingiza pesa.
“Uwe wakala wangu?”
“Ndiyo! Yaani ukikubaliana nami, nakuhakikishia mwaka kesho utacheza pale. Huku Beckham, kule Zidane, pale Ronaldo, hapa Figo, wewe utasimama popote pale,” alisema Alfonce na wote kuanza kucheka.
Walizungumza mambo mengi huku David akijaribu kumuondoa hofu mwanaume huyo ili aone kwamba alikuwa mtu mwema. Alipoona amejisahau, akaishikilia chupa yake vizuri, wakati Alfonce akiwa amejisahau na kucheka sana, akashtukia akipigwa kwa nguvu kichwani na chupa kubwa ya pombe, kwa kuwa lilikuwa tendo la ghafla sana, hapohapo akaanguka na kupoteza fahamu.
Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi aliyokuwa akiitaka David, akamsogela, akatoa kisu chake na kuanza kumchomachoma mwili mwake na mwisho kabisa kumalizia kwa kumchinja shingoni.
Damu zikatapakaa katika boti ile, Alfonce akatulia, hakutingishika, na baada ya sekunde kadhaa, mapigo ya moyo yakasimama na kufariki dunia ndani ya boti hiyo.
Kwa kuwa kule hakwenda na kitu chochote kile, hakutaka kubaki huko, alichokifanya ni kuondoka mahali hapo na boti ile na kusonga mbele. Hakutaka kurudi Madrid, alijua kabisa kama angerudi huko mambo yangekuwa magumu, alichokifanya ni kuunganisha kuelekea katika kisiwa cha Lanzarote ambacho hakikuwa mbali kutoka kwenye kisiwa hicho.
Mwendo wake ulikuwa ni wa dakika ishirini, alipokaribia kama mita mia moja kutoka mahali kisiwa hicho kilipo, akaiacha ile boti, akatumbukia ndani ya maji na kuanza kuogelea kuelekea huko.
Hakuchukua dakika nyingi, akafika, akapiga hatua ufukweni ambapo aliwakuta baadhi ya vijana na kuwauliza mahali ambapo angeweza kupata msaada wa boti kwa lengo la kupelekwa jijini Madrid.
Hilo halikuwa tatizo, akapelekwa sehemu iliyokuwa na boti nyingi, akakodia kwa makubaliano ya kulipa baada ya kufika Madrid, hilo halikuwa tatizo, akaingia na kuanza kupelekwa huko ambapo baada ya dakika arobaini, wakafika, akachukua kadi ya benki, akatoa pesa katika mashine ya ATMna kumkabidhi mwanaume yule na kuondoka zake.
***
Muda ulizidi kwenda mbele, Jolinda na marafiki zake walikuwa wakiwasubiri David na Alfonce warudi ili waendelee kufanya mambo mengine. Muda ulisogea lakini watu hao hawakuwa wamerudi kisiwani hapo.
Mara ya kwanza walichukulia kawaida lakini baada ya kuona saa nne zimepita pasipo watu hao kuonekana mahali hapo, wakaanza kuingiwa na wasiwasi.
Kitu cha kwanza walichokifanya ni kuongea na uongozi wa hoteli waliyofikia na kuwaambia kile kilichotokea. Meneja wa benki akapiga simu polisi na kumwambia Jolinda asimulie kama alivyokuwa amemsimulia.
Jolinda akafanya hivyo. Polisi walimsikiliza na kugundua kwamba inawezekana kulikuwa na tatizo limetokea baharini hivyo walitakiwa kufuatilia. Wakachukua boti zao na kuingia baharini.
Walizunguka huku wakiangalia huku na kule, hawakufanikiwa kuiona boti waliyoambiwa. Hilo likawaongezea hofu kwa kuhisi kwamba inawezekana wageni hao walikuwa wameuawa na watu waliokuwa wakizunguka baharini kutafuta watalii ili wawaibie.
Walizunguka kwa saa mbili, hawakufanikiwa kuwaona kitu kilichowapelekeakurudi hotelini na kuwaambia kwamba katika kila kona waliyokwenda baharini, hawakuweza kuwapata watu hao.
“Mliangalia kila kona?” aliuliza Jolinda huku machozi yakimtoka kwani tayari picha mbaya ilikwishajengekea kichwani mwake.
“Ndiyo!”
“Na hamkuwaona?”
“Kabisa mama! Umejaribu kuwapigia simu?”
“Ndiyo! Lakini simu zao waliziacha, waliondoka bila simu,” alijibu Jolinda.
Hakukuwa na mtu aliyekuwa na amani tena, kila mmoja alikuwa akihuzunika kwani kitendo cha kupotea kwa watu hao kilimaanisha kuvurugika kwa mipango yao.
Japokuwa polisi waliwatafuta kwa nguvu zote, hawakutaka kuacha, wakaingia tena baharini na kuendelea kuwatafuta watu hao. Walipoona kwamba wamewakosa baharini wakapanga kutembelea kila kisiwa kilichokuwa huko ili kuona kama wangeweza kuwakuta.
Kisiwa cha kwanza kilichokuja kichwani mwao kilikuwa ni Majorca. Wakaelekea huko, walipofika, wakawauliza wakazi wa huko kama walifanikiwa kuwaona watu waliokuwa wakiwatafuta ambao walikwenda kwa boti lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyewaona watu hao.
Hawakuishia kwenye kisiwa hicho tu, wakaondoka na kuelekea katika Kisiwa cha La Gomera lakini majibu yalikuwa yaleyale. Huku ikiwa imefika jioni kabisa ndipo wakaamua kumalizia katika Kisiwa cha Lanzarote.
Wakati wakiwa njiani kukisogelea kisiwa kile, kwa mbali wakafanikiwa kuiona boti ambayo waliambiwa kwamba watu hao ndiyo waliyoichukua. Kasi ya boti yao ikaongezwa kuisogelea boti ile.
Ilikuwa ni kama imetelekezwa, walipoifikia, wakachungulia, kwa mbali wakaona damu, hilo likawatia hofu na hivyo kuisogelea zaidi na kuangalia kilichokuwa ndani.
Hawakuamini macho yao baada ya kuishuhudia maiti ya Alfonce ikiwa imelala chini huku akiwa amezungukwa na damu zilizoganda. Hilo liliwachanganya polisi hao, hawakujua ni kitu gani kilichotokea hivyo kuanza kumtafuta na David kwani waliambiwa kwamba watu hao walikuwa wawili.
“Rafiki yake yupo wapi?’ aliuliza polisi mmoja.
“Hatujui! Sasa sijui yeye ndiye aliyemuua au wamemuua huyu na rafiki yake kumchukua!” alisema polisi mmoja.
Hawakutaka kubaki huko, wakaondoka mahali hapo huku wakiichukua ile boti iliyokuwa na maiti ya Alfonce na kuanza kurudi nayo katika Kisiwa cha Las Palma walipokuwa marafiki zake.
Njiani, bado polisi walikuwa wakijiuliza maswali mengi kuhusu maiti hiyo, hawakujua ni nani hasa aliyemuua, kama aliuawa na rafiki yake, aliondokaje kwenye boti na kama aliuliwa na watu wengine, je, walimteka huyo rafiki yake? Kila walichojiuliza wakakosa jibu kabisa.
***
Moyo wa David ukaridhika, kwake, kufanya mauaji ya Alfonce kilionekana kuwa kitu muhimu kupita kawaida. Alijua kwamba Sebastian alikuwa nchini humo, ujio wake haukuwa na maswali mengi, alijua kabisa kwamba alikuwa mahali hapo kwa lengo la kumuua na ndiyo maana kila alipokuwa akiwasiliana na mzee Armando alimwambia kwamba hakuwa amemuona Alfonce ili kumpa ugumu Sebastian.
Hapo jijini Madrid, hakutaka kuzurura sana, alichokifanya ni kwenda katika choo kimoja cha jumuiya na kisha kuitoa sura ile ya bandia na kuitupa chooni, akabaki na sura yake kisha kuondoka kuelekea katika hoteli moja na kuchukua chumba.
Huko, kitu cha kwanza kilikuwa ni kuwasiliana na Cecilia, alimwambia kwamba alimkumbuka mno na kulikuwa na kazi alikuwa akiifanya na kwa kuwa alikuwa amemaliza alitakiwa kurudi haraka nchini Ujerumani. Msichana huyo aliposikia hivyo, moyo wake ukafurahia kwani kila wakati alihitaji kuwa na mpenzi wake huyo ambaye alionekana kuwa na mambo mengi mno.
“Nimekukumbuka sana mpenzi,” alisema Cecilia kwenye simu.
“Nimekukumbuka pia. Nitakuja huko, tutakuwa pamoja kabla ya kurudi Nigeria kuendelea na maisha,” alisema David maneno yaliyomfanya Cecilia kushtuka.
“Kurudi Nigeria?”
“Ndiyo!”
“Hapana! Siwezi kurudi, ninatafutwa mno.”
“Najua, ila hautorudi huko kama Cecilia, utarudi kwa jina jingine kabisa. Labda Martha, lakini utatakiwa kurudi nchini humo kuendelea na maisha yako,” alisema David.
Walizungumza mambo mengi usiku huo na kukubaliana kwamba kama inawezekana Cecilia alitakiwa kurudi nchini Nigeria alipokuwa akitafutwa kwa udi na uvumba.
Walipomaliza kuzungumza, David akakata simu na kupumzika. Mawazo yake bado yalikuwa katika kazi kubwa iliyokuwa mbele yake, alijua dhahiri kwamba mzee Armando hakuwa rafiki tena, alikuwa adui ambaye alitakiwa kupambana naye kimyakimya.
Hilo likafanyika na aliamini kwamba angeweza kufanikiwa kwa kila kazi ambayo angepewa na mzee huyo. Ilipofika majira ya saa mbili usiku, akaondoka na kwenda mtaani katika maduka makubwa yaliyokuwa wazi na kununua simu.
Akarudi hotelini, akachukua laini yake na kumpigia Sebastian. Simu ilianza kuita, haikuita muda mrefu, ikapokelewa na sauti ya mwanaume huyo kusikika kutoka katika upande wa pili wa simu ile.
Alimpa taarifa huku akicheka, alimwambia kwamba alifanya kazi aliyotumwa na kipindi hicho tayari Alfonce alikuwa amekufa kama ilivyotakiwa kuwa.
Sebastian hakuamini alichokisikia, akakata simu na mtu wa kwanza kabisa kumpigia Jolinda ambapo huko akapokelewa na sauti ya kilio, msichana huyo alikuwa akimuulizia kaka yake huku akilia kama mtoto.
Sebastian alichanganyikiwa, alichokifanya ni kumpigia simu mzee Armando kwa lengo la kumpa taarifa. Simu hiyo haikuita sana, ikapoelewa na sauti ya mzee huyo kusikika.
“Mzee kuna tatizo,” alisema Sebastian.
“Tatizo? Tatizo gani?”
”Alfonce ameuawa!” alisema maneno yaliyomfanya mzee Armando kushtuka.
“Unasemaje?”
“Alfonce ameuawa!”
Hilo lilimchanganya mzee Armando, hakuamin alichokisikia kwamba mtu aliyekuwa ameagiza auawe kwa lengo la kumuua muuaji ambaye ni David alifanikiwa kutekeleza kile alichokihitaji.
Moyo wake ukamuuma mno, hakuamini kama kweli David angefanikiwa kummaliza mwanaume huyo na wakati yeye ndiye aliyetakiwa kuuawa.
“Imekuwaje?”
“Bosi! Yule mwanaume ni hatari!” alijibu Sebastian.
“Hatari gani? Yaani inamaana hamkumtambua?”
“Mzee yule kijana ni mtu hatari! Hapana, sitaki kuendelea kumtafuta, anaweza akaniua!” alisema Sebastian.
“Kwa nini?”
“Hapana! Nimeshindwa. Hapana! Nimeshindwa,” alisema Sebastian na kukata simu.
Baada ya dakika kadhaa, Jolinda akapewa taarifa ya mauaji yaliyokuwa yamefanyika, moyo wake uliuma kupita kawaida, hakuamini kama kweli mtu ambaye alimchukulia kama kaka yake alikuwa ameuawa kinyama.
Mbali na kaka yake huyo pia akaanza kumfikiria mpenzi wake aliyemjua kwa jina la Emmanuel, akawauliza polisi, wao wenyewe hawakuwa wakijua mahali alipokuwa David aliyejiita Emmanuel kwani kule walipokuwa wamekwenda, walikuta boti ikiwa na maiti ya Alfonce lakini David hakuonekana.
“Yupo wapi? Mpenzi wangu yupo wapi?’ aliuliza Jolinda huku akilia.
“Hatujui! Mama! Bado tunaendelea na uchunguzi, tutakupa majibu,” Alisema polisi mmoja maneno yaliyomfanya Jolinda kulia kupita kawaida.
Taarifa za kifo cha Alfonce zikaanza kusambaa kila kona nchini Hispania, kila mtu aliyeisikia taarifa hiyo alishangaa, walishtuka baada ya kusikia kwamba mwanaume huyo aliuawa katika boti yake.
Hakukuwa na watu walioamini, wengine walihisi kwamba ulikuwa ni mchezo uliopangwa kwa lengo la kufanya jambo fulani baya. Haikuwa rahisi kuaminika kwamba mwanaume huyo, muuza madawa ya kulevya aliuawa na wakati alikuwa na ulinzi mkubwa.
Watu wakapigiana simu na kuulizana kuhusu mauaji hayo, taarifa ziliendelea kusema kwamba mtu ambaye alimuua Alfonce alikuwa mtu wa karibu, shemeji yake aliyetoka nchini Uingereza huku akiwa mwanasoka katika Klabu ya Newcastle.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : SOMA SIMULIZI HII
SOMA SIMULIZI HII
BongoLife
https://www.bongolives.com/2018/12/soma-simulizi-hii.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2018/12/soma-simulizi-hii.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy