MWANAUME WA DAR SEHEMU YA 02 | BongoLife

$hide=mobile

MWANAUME WA DAR SEHEMU YA 02

MWANAUME WA DAR: 2

Rey alipomaliza kusoma alicheka sana kisha akasema,
“Mwanaume wa Dar huyu”
Hellen alibaki tu akimuangalia Rey bila kummaliza.
Rey alizidi kucheka sana, ilibidi Hellen amuulize sasa kilichokuwa kikimchekesha ni kitu gani pia alimuuliza,
“Na kwanini useme Baraka ni mwanaume wa Dar?”
“Nina haki ya kusema hivi, hebu fikiria ni siku ngapi toka ufahamiane na Baraka? Ndio wa kukuomba vocha leo hii? Mwanaume wa kweli anajiheshimu bhana, hawezi kujishushia hadhi namna hiyo kwa mwanamke, hata wiki kwenye mahusiano hamna eti leo anaomba vocha ya buku loh!”
“Kwani tatizo likowapi Rey? Labda ameshindwa, kwani wewe hujawahi kuomba vocha?”
“Na wewe endelea na ujinga wako, kwahiyo unamtumia vocha huyu kiumbe? Nicheke mie, haya mtumie”
Hellen alimuangalia Rey na kuchukua simu yake kisha alimuuliza Baraka kuwa anataka vocha gani,
“Vocha ya mtandao gani Baraka?”
“Nahitaji ya mtandao huu huu ninaotumia mpenzi wangu”
Basi moja kwa moja walienda dukani kununua vocha na akamrushia Baraka, basi Rey akasema,
“Ukienda kumcheki hivyo utamkuta ana laini ya chuo huyo halafu anaomba vocha kweli jamani!! Pole sana rafiki yangu kwa kukutana na mwanaume wa Dar, halafu pole zaidi sababu hutaki kusanuka”
Hellen hakumjibu kitu Rey kwani moja kwa moja waliondoka tu na kurudi hosteli ambapo Hellen aliendelea tu kuwasiliana na Baraka kwa njia ya ujumbe mfupi.

Walipokuwa hosteli, Rey alimtania Hellen,
“Vipi mwanaume wako wa Dar hajaomba tena vocha?”
“Halafu Rey sipendi, mwanaume wa Dar ndio kitu gani sipendi kabisa hayo maneno yako”
“Haya yaishe, ila kakwambia sababu ya kuomba vocha?”
“Kwani tatizo liko wapi kwa mtu kumuomba mpenzi wake vocha? Hata mimi naweza kumuomba yeye vocha sit upo kwenye mapenzi? Mapenzi ni kusaidiaana”
“Unajiwekea dhana hiyo kwa mwanaume wa Dar!! Wallah utalia wewe, siku sio nyingi utaniambia tu, hakuna cha kusaidiana kwa mwanaume wa Dar yani wewe ndio utamsaidia yeye”
“Ndio kazaliwa hapahapa Dar, kwani kuzaliwa Dar ndio tatizo?”
“Sio tatizo, wengi tu wamezaliwa Dar ila mwanaume wako ni mwanaume wa Dar”
Kisha Rey alicheka tena na kuendelea na mambo mengine huku Helleni akiendelea kuwasiliana na Baraka na kuendelea kuambiana ni jinsi gani wanapendana.

Leo, Hellen na Rey walikuwepo tu hawakuwa na pesa leo maana hela ya boom ilichelewa kuingizwa, basi wakakaa na kujadiliana,
“Tutafanyaje sasa? Hela hamna”
“Aaaah usijali, kuna elfu kumi hapa, ngoja nikanunue chakula tule”
“Ndio hapo hapo ninapokupendea Rey yani wewe upo vizuri sana”
“Mmmh ungejua”
“Ningejua nini!!”
“Aaaah acha tu, ngoja nikanunue kitu tuweze kula”
Basi Rey alitoka ila Rey alikuwa akimwambia kuwa angejua ni hela aliyoipata kwenye ile namba ya simu ya yule mtu, yani Rey alikuwa akimuona mwenzie kama kapotea kufanya mawasiliano kiasi kile na Baraka.
Muda wote Hellen nae hakuwa na tatizo zaidi ya kuwasiliana na Baraka,
“Sijala mpenzi”
“Pole sana, ila kwanini hujala?”
“Sina hela”
“Pole sana mpenzi wangu”
Rey alikuwa amerudi kwa muda huo, na Hellen alimwambia,
“Yani Baraka namwambia sijala sina hela kashindwa hata kujiongeza, eti ananiambia pole”
“Ajiongeze nini na yeye ni mwanaume wa Dar!! Usikute hata yeye hajala pia”
“Ila na wewe Rey hadi unakera jamani, kwani mwanaume haishiwi?”
“Anaishiwa ndio ila huyo Baraka ni mwanaume wa Dar na hata sio mwanaume kuishiwa, siku akili ikikukaa sawa utakumbuka maneno yangu. Haya tule kiepe nimenunua na upige picha umtumie huyo Baraka kuwa ndio unakula”
Walikaa pale na kula huku wakipiga stori kidogo tu kwani Hellen alikuwa makini sana na simu yake.

Jioni ya siku hii, Rey alifikiria kitu na kuona kuwa wanazidi kutokuwa na hela basi aliamua kupiga ile namba ya yule mtu na kuanza kuongea nae,
“Mimi naitwa Rey, uliacha namba kwa mlinzi chuoni”
“Oooh yani mrembo ndio unanitafuta leo kweli?”
“Aaaah si unajua masomo yanabana sana. Kwani wewe unaitwa nani?”
“Mimi naitwa Dennis, je tunaweza kuonana ili kuongea mawili matatu?”
“Hakuna tatizo, niambie tu ni wapi tuonane”
Yule Dennis akamtajia mahali ambapo anahitaji akutane na Rey, na kweli Ile ile jioni Rey alijiandaa vizuri kabisa na kwenda kukutana na Dennis kisha alijitambulisha,
“Mimi ndio Rey tuliokuwa tunaongea kwenye simu ila mimi sio yule mtu uliyeacha namba kwaajili yake, ila mimi ni rafiki yake”
“Oooh jamani, asante sana kukufahamu inaonyesha ni mstaarabu sana maana angekuwa mwingine si angekazana kusema kuwa ndio yeye jamani, ila wewe ni mstaarabu sana nimependa. Mimi ndio Dennis”
“Nafurahi sana kukufahamu”
“kwakweli Rey nampenda sana rafiki yako”
“Hata mimi nimehisi hiko kitu ndiomana nikaamua kukutafuta ingawa yeye amegoma kukutafuta”
“Aaaah nashukuru sana ila kama ukinipatia namba yake utakuwa umefanya jambo la kheri kweli”
Rey alisita kidogo kutoa namba ya Hellen, ndipo Dennis alipotoa noti ya elfu kumi na kumkabidhi Rey, basi hapo Rey alimtajia namba ya rafiki yake bila kinyongo na kumwambia,
“Uwe na lengo kweli, sio kumchezea tu”
“Hapana, sitaki kumchezea, nahitaji awe mke wangu kabisa kama atataka amalize chuo kwanza ndio tuoane basi nitashukuru, ikiwa sasa hivi nitafurahi pia”
“Ooooh nafurahi kusikia hivyo”
Rey aliongea na Dennis ambapo Dennis alimfungia vitu vya Rey kwenda navyo hosteli kwaajili ya Hellen.

Rey alivyorudi tu, Hellen alifakamia kuvila ambapo Rey alimueleza ukweli kuhusu vile vitu,
“Aaaah Rey tabia mbaya hiyo, yani unaniuza rafiki yako sababu ya elfu kumi tu!”
“Kwa shida tulizonazo, elfu kumi ni kubwa sana shoga yangu. Tushukuru kuipata, kwani tatizo ni nini? Si unawasiliana nae tu!”
Muda huo huo Dennis alimpigia simu Hellen na kufanya Hellen aipokee baada ya kuona namba mpya ila badae Dennis alijitambulisha na kufanya waendelee tu na maongezi, basi Dennis alifanya kazi ya kumsifia Hellen jinsi alivyo mzuri na jinsi anavyompenda na jinsi anavyohitaji awe wake, Hellen hakutaka kuongea sana na Dennis kwanza hakumpenda wala hakumtaka kwahiyo aliona kama anapiga kelele tu, alikata simu na kuendelea kutumiana ujumbe mfupi na Baraka.

Baada ya Dennis kumsumbua kiasi Hellen kuwa anampenda basi Hellen aliamua kumueleza Baraka kuwa kuna mkaka anamsumbua sana kuhusu kumpenda,
“Yani mimi hata silitaki, lenyewe lisumbufu hilo hatari”
“Mpenzi wangu, hao ni wale wanaume wenye hamu ya kuchunwa, kwahiyo huyo ni wa kumchuna tu”
“Kivipi?”
“Kwanza mtumie ujumbe kuwa una shida na elfu ishirini, akikutumia niambie”
Basi muda ule ule Hellen alimtumia Dennis ujumbe,
“Nina shida na elfu ishirini”
“Aaaah jambo dogo hilo, subiri kama dakika tano tu muamala utasoma”
Hellen kazi yake ilikuwa ni kutuma tena zile jumbe anazojibiwa na Dennis kwa Baraka huku akitabasamu.
Muda kidogo hela iliingia kwenye simu ya Hellen, basi Hellen akatuma tena kwa Baraka ile meseji ya hela hiyo iliyoingia kwenye simu yake huku akitabasamu sana, Rey alitokea na kumuona rafiki yake jinsi anavyotabasamu basi alimuuliza,
“Mbona una furaha hivyo?”
“Kwanza sina hela, hilo nadhani unalijua ila huwa siwezi kumuomba hela mwanaume. Sasa nimemueleza Baraka kuhusu Dennis, basi Baraka kaniambia kuwa Dennis anataka kuchunwa, nimuombe elfu ishirini, nimemuomba muda sio mrefu na muda huu huu amenitumia”
“Duh!! Hebu tuone hiyo meseji kama kakutumia kweli?”
Hellen alimpa Rey simu yake ilia aone meseji ya muamala wa hela, ila muda huo huo ujumbe wa Baraka unaingia, ambapo Rey anaufungua na kusoma kwa sauti,
“Mpenzi, naomba nisaidie hiyo elfu 20 maana kuna shida imetokea gafla”
Rey anacheka sana na kusema,
“Yani huyu ni mwanaume wa Dar kabisa hata sio utani”

Itaendelea Ijumaa usiku…..!!!
Kwa mawasiliano 0714443433
By, Atuganile Mwakalile.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : MWANAUME WA DAR SEHEMU YA 02
MWANAUME WA DAR SEHEMU YA 02
BongoLife
https://www.bongolives.com/2018/12/mwanaume-wa-dar-sehemu-ya-02.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2018/12/mwanaume-wa-dar-sehemu-ya-02.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy