MWANAUME WA DAR SEHEMU YA 01 | BongoLife

$hide=mobile

MWANAUME WA DAR SEHEMU YA 01

MWANAUME WA DAR

Ni asubuhi na mapema, Hellen alikuwa akienda zake chuo, alikuwa na mawazo mengi sana sababu alizinguana na mpenzi wake Ibra, kwahiyo siku hiyo ilikuwa mbaya sana kwake ukizingatia alimpenda sana Ibra.
Akiwa kwenye daladala, alibahatika kukaa karibu na kijana mmoja mtanashati ambaye alikuwa akinukia sana marashi kiasi kwamba hata Hellen alipenda marashi yale na alitamani kuyajua ila alihofia kumuuliza kitu chochote.
Maongezi ya yule kijana na Hellen yalianza baada ya yule kijana kumwambia Hellen afungue kidogo dirisha la kwenye daladala, basi yule kijana akapitisha mkono wake na kufungua dirisha ambapo Hellen alishindwa kujizuia na kumuuliza,
"Samahani kaka, marashi yako yanaitwaje nimeyapenda"
Yule kijana alitabasamu na kumwambia Hellen,
"Unahitaji upate marashi kama haya?"
"Nimeyapenda kweli, nikiyapata nitafurahi sana"
"Nipatie namba yako, ili tuwasiliane halafu nitakupeleka wanapouza hivi vitu adimu"
Hellen hakuona tatizo kwani kwa muda ule ule alimpatia yule kijana namba yake, halafu yule kijana akamuuliza,
"Unaitwa nani? Mimi naitwa Baraka"
"Oooh na mimi naitwa Hellen"
"Tutawasiliana basi Hellen, ni vyema kukufahamu"
Kituo kilichofuata Hellen alishuka na kuelekea chuo moja kwa moja.

Ila kabla hajafika chuo, Hellen alikutana na mkaka mwingine ambaye alionekana kuvutiwa na urembo wa Hellen na kujikuta akimsimamisha na kumsalimia,
“Dada habari”
“Nzuri”
Hellen aliendelea na safari yake,
“Dada, samahani nina shida na wewe. Nina maongezi na wewe”
“Aaaah mimi nawahi chuo bhana nina kipindi”
“Basi naomba namba zako”
“Aaaah achana na mimi bhana”
Hellen aliondoka zake ila yule mkaka aliendelea kumfata nyuma, hadi Hellen anaingia kwenye geti la chuo yule mkaka alimfata hadi pale ambapo Hellen hakumjali wala nini kwani yeye alichokuwa akijali kwa muda ule ni kipindi tu alichokuwa nacho.

Hellen alipotoka chuo tu alitumiwa ujumbe mfupi na Baraka,
"Hellow Hellen"
"Poa tu, za wewe"
"Nimeshakumiss mwenzio"
Hellen alitabasamu tu kuona mwanaume kaonana nae siku hiyo hiyo na tayari amemisiwa nae, basi alitabasamu na moja kwa moja alihisi kuwa yule kijana anamtaka kimapenzi
Muda Hellen alipokuwa akitabasamu, alifatwa na rafiki yake Rehema ambaye walizoea kumuita Rey, kisha Rey akamuuliza Hellen,
"Unaonekana una furaha muda huu!!"
"Acha tu, nina furaha balaa"
"Ya nini tena!! Ibra kaomba msamaha?"
"Ibra wapi? Ibra wa nini, nishamsahau tayari"
"Kheee Hellen wewe wa kumsahau Ibra kwa jinsi unavyompenda!!"
"Wa kazi gani Ibra!! Nimekutana na mkaka leo, ni mtanashati hatari, ananukia huyo marashi yenyewe, ukimuona lazima uchenguke. Tena ananitaka, nahisi kumpenda pia"
Rey akamuangalia kwa makini Hellen na kumwambia,
"Hongera kwa hilo rafiki yangu ila ni mapema mno, yani kuachana jana sijui juzi na Ibra leo umepata mpya kweli!!"
"Mapenzi kiti cha basi, akishuka yule anakaa huyu"
"Haya hongera zako"
Muda ule ule kuna ujumbe mwingine uliingia toka kwa Baraka,
"Nakupenda sana Hellen"
Hellen akatabasamu na kufanya Rey amuulize tena,
“Eeeeh ni nini tena?”
“Yule mkaka kaniambia kuwa ananipenda”
“Mmmmh Hellen, mimi yangu macho tu. Haya leo, utarudi hosteli au utaenda kwenu?”
“Aaaah tunaenda wote hosteli”
“Haya twende basi”
Basi Hellen aliongozana na Rey huku akiendelea kuwasiliana na Baraka tu, wakati wakitoka pale chuo mlinzi alimuita Hellen na kumpa barua na kumwambia,
“Kuna mkaka ulikuwa umeongozana nae muda ulipokuwa ukiingia chuo, ameacha huu ujumbe”
“Mmmmh haya”
Hellen alipokea ule ujumbe na kuondoka zake na Rey.

Usiku wa siku hii, Hellen alikuwa makini kwenye kuwasiliana na Baraka kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno hadi wakati wa kula alikuwa akiwasiliana nae tu, Rey akamuangalia Hellen na kumwambia,
“Jamani, ndio mapenzi gani hayo ya kuwasiliana muda wote?”
“Chezea penzi jipya eeeh!!”
“Mmmh kweli penzi jipya, ndio hadi unakula huku unachat tu. Duh ni noma”
“Aaaah acha zako Rey, fanya mambo yako bhana”
“Haikuwa hivyo kwa Ibra lakini?”
“Usinichefue kuhusu huyu mtu, hata sitaki kumfikiria, kwa muda huu kichwa changu ni Baraka tu”
“Duh!! Haya bhana”
Hellen aliendelea kuwasiliana na Baraka kwa muda wote, hadi muda wa kulala ilionekana akiwa anawasiliana nae tu, hadi pale Hellen alipopitiwa na usingizi.
Kulipokucha tu, Rey alikuwa wa kwanza kumuuliza Hellen kuhusu ule ujumbe aliopewa na mlinzi,
“Hellen na wewe unalala sana, hebu fungua huo ujumbe bhana tuone unasemaje”
“Aaaah fungua mwenyewe”
Rey alifungua ule ujumbe na kukuta namba ya simu na noti ya shilingi elfu kumi, kisha akamwambia rafiki yake,
“Nimekuta namba ya simu, je utampigia?”
“Wa nini mimi? Tayari nina Baraka, tena kaahidi kunioa”
“Kheee mara hii ushaahidiwa ndoa!! Huyo Baraka ni noma. Kwahiyo huyu huna haja na namba yake, nimtafute mimi”
“Mtafute tu, kwanza mwanaume mwenyewe huyo sura mbaya”
“Kwahiyo Baraka ni mzuri?”
“Ndio, Baraka mzuri bhana. Ni mtanashati, mwanaume ananukia marashi”
“Mmmmh haya”
Rey aliiweka ile elfu kumi vizuri kabisa na kutunza zile namba za simu za yule mtu.

Zilipita siku mbili huku Hellen akiwa makini sana na mawasiliano yake na Baraka, walikuwa wakiwasiliana kwa kila muda, hadi Rey alikuwa akichukia sana.
Siku hiyo walipotoka chuo, Rey alikuwa akiongea na Hellen,
“Nimeonana na Ibra”
“Anasemaje?”
“Mmmmh hajasema chochote kile”
“Achana nae, mimi nipo busy na Baraka”
“Haya bhana”
Rey kuna mtu alipiga kidogo kwenye simu yake na kukata, basi Rey aliangalia namna ya kumpigia mtu huyo ila aliona kuwa hana salio na kufanya aombe simu ya Hellen ilia pate kumpigia, basi Hellen alimpa simu yake na muda huo huo kuna ujumbe uliingia kwenye simu ya Hellen toka kwa Baraka, sababu Rey alikuwa akibonyeza simu alijikuta amefungua ule ujumbe na kumwambia Hellen,
“Kheee kuna ujumbe wako umetumiwa na Baraka”
Basi Hellen akamwambia kwa kujiamini,
“Hebu nisomee, najua anasema kuwa ananipenda sana”
“Hapana, kaandika hivi samahani mpenzi naomba nisaidie vocha ya buku, nimeishiwa muda wa maongezi”
Rey alipomaliza kusoma alicheka sana kisha akasema,
“Mwanaume wa Dar huyu”
Hellen alibaki tu akimuangalia Rey bila kummaliza.

Itaendelea Jumatano usiku…..!!!!
Kwa mawasiliano 0714443433
By, Atuganile Mwakalile.

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : MWANAUME WA DAR SEHEMU YA 01
MWANAUME WA DAR SEHEMU YA 01
BongoLife
https://www.bongolives.com/2018/12/mwanaume-wa-dar-sehemu-ya-01.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2018/12/mwanaume-wa-dar-sehemu-ya-01.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy