MTAA WA TATU SEHEMU YA 09 | BongoLife

$hide=mobile

MTAA WA TATU SEHEMU YA 09

*MTAA WA TAT EP 09*


usijali shemu wangu twende ukachukuwe ghetto”
Wakaongozana mpaka kwa Hafidhi akafungua mlango na kumkuta
Amina kalala chini ya sakafu huku kavaa lile bagi
Mwanaume akashtuka na kumwita
Mpendu si ndio Dada wa Amina
“Mpenduu!!!
“abee unasemaje shemu?
”embu njoo”….
Mpendu akaja mbio hakuweza kuamini kumkuta mdogo wake hajitambui kabisa akaita
“Aminaa!!! Amka tafadhali fanya hivyo
Mwanaume hakutaka kuzubaa akambeba na kutoka nae nnje wakakodi bajaji na kumuwahisha hospitali.
“kwani imekuwaje shemu mbona Amina yuko vile?”

“mimi hata sijui kabisa nilimuacha akiosha vyombo nikatoka zangu kuingia kwenye mishemishe na muda ule ndio narudi nakutana nawe kuingia chumbani ndio namkuta kalala chini
Sijui nini kimemkuta”
Ghafla sauti ya kilio ikasikika kutoka wodini
wote wakashtuka

Niachee nakufaa!!! Huyoo anakuja”….huyoo mshikeni nakufaa”….
Zote zilikuwa kelele za Amina yani alipiga kelele na kuitaji kukimbia. Ikabidi Madaktari wajitahidi kumshika kwa kumzuia asiweze kuondoka,
Sema ikashindikana hakika alikuwa na nguvu za ajabu,
Hafidhi akiwa na Mpendu wakaingia wodini humo na kupishana na Amina akitoka mbio
Mpendu akapigwa kipushi na kudondoka chini, ikabidi
Hafidhi amnyanyuwe na kuanza kumkimbilia Amina kelele za mshike mshike mkamate huyo ndizo zilizosikika nnje ya hospitali hiyo
Amina akizidi kukimbia na kuvuwa nguo moja baada ya nyingine.
Binafsi tayari amekuwa chizi sijui aligongwa na kitu gani.
Mwanaume ikabidi atumie akili na kuongeza kasi ya kumkimbiza.
Lakini kabla hajamfikia ghafla bin vuu Amina akagongwa na gari.
Dahaa ilikuwa ajali mbaya sana maana baada kupigwa mzinga akarushwa hewani huku kichwa kikipasuka, hakuwa tena Amina zaidi ya kuwa marehemu,
Mpendu akabaki kulia tu huku watu walioweza kushuhudia tukio lile wakibaki kujishika vichwa na kuacha vinywa wazi,
Hafidhi nae hakuweza kuamini aisee Dereva wa gari hakusimama akaondoka kwa speed ya ajabu.
Basi ilikuwa ni siku ya hudhuni kwa familia ya marehemu ndugu jamaa na marafiki walifika,
Ikiwa imepita kama wiki moja hivi tokea kifo cha
Amina kitokee siku hiyo
Hafidhi alikuwa yupo chumbani kwake akitafakali mustakabari mzima kuhusu kipenzi chake, kwanza alimkuta kalala sakafuni hajitambui kabisa, kingine kalivaa hili bag sasa nini kilitokea juu yake.
Akazidi kuumiza kichwa akashtuka baada kuhisi kuguswa begani na kitu kama cha moto hivi, kitendo cha kuangalia tu ndio akashtuka zaidi baada macho yake kugongana na sura ya kiumbe cha ajabu alikuwa ni kiumbe cha kutisha yani sura yake imebaki fuvu tu haina ngozi.
Hayo macho yake kama vile makaa ya moto yanawaka na kufuka moshi.
Hiyo pua yake kama vile shimo la choo
Mdomo wake una minjino miwili imechongoka na kuwa mikubwa
Ulimi kama mjusi kenge,
Hafidhi akarudi nyuma kwa uwoga kile kiumbe kikaanza kucheka kwa kusema
“hahahaha kijana hutakiwi kuogopa kabisa tambua kitu kimoja mimi ndio
Surtani wa makata niliyetumwa na
Baba yako kukulinda wewe.
Ndio ninaefanya kazi ya kuibadirisha sura yako watu wasikutambuwe.
Sasa basi yule binti amekufa kutokana na kuingiwa na tamaa tu”….
Hafidhi akabaki kimyaa kijasho kikimtoka na kupiga mahesabu ya kukimbia kwanza aliona kama ndoto tu anazootaga kila siku atakuja kushtuka muda si mrefu.
Kiumbe kikaendelea kusema
“usikimbie wala usiogope mimi ndio bodyguard wako mkuu”
Ghafla akatoweka ndipo Hafidhi akakurupuka na kukimbia.
Ndani ya mtaa wa tatu tunamuona bwana Dennis akiwa na vijana wake wapo katika mawindo ya kumsaka Hafidhi moja kwa moja wakafikia kwa Ankor wake”
“Kessy kijana wangu wewe itabidi uishi ndani ya nyumba hii ipo siku Hafidhi atakuja hapa”

“sawa mkuu usijari kabisa maadam nimepata chumba sio mbaya nitaishi hapa,

Basi taratibu zikafanyika Kessy akahamia hapo wakati Muna au Boyka akipata chumba maeneo ya mtaa wa kwanza,
“Boyka kuwa makini kama jina lako lilivyo tambua ya kwamba tumekuja kufanya kazi si kingine”
“sawa mkuu nimekuelewa kuhusu hilo swala nitalifanyia kazi vilivyo,
Basi bwana Dennis akaondoka na yule kijana mwingine mpaka maeneo ya
Mabibo hostel kijana yule anaekwenda kwa jina la Taqawa nae akapanda chumba kwenye nyumba ya kina Amina
maana baada
Amina kufariki chumba kilikuwa hakina mtu wa kukaa ikabidi wapangishe tu,
“hivi mama ni upuuzi wa kiasi gani mnaufanya huu”
“upuuzi gani tena?
“yani hata arobaini ya marehemu bado watu tukiwa na machungu ya kufiwa leo hii mnakipangisha chumba chake”…
Hafidhi akauliza hivyo.
“sasa wewe ulitakaje inamaana unauchungu sana kuliko mimi niliyembeba Amina tumboni miezi tisa nikaenda Reba
Wewe unaongea tu hujui jinsi moyo wangu unavyojisikia”….

“hata kama ulimbeba ulimtema kitendo cha kupangisha chumba chake sio kabisa
Sasa natoa amri huyu mpangaji
Mwambie atoke ndani ya chumba kile”

“sasa utoe amri hiyo wewe kama nani ndani ya nyumba hii ujachangia hata shilling kumi
Kingine sikutambui kama ni mkwe wangu”
Hafidhi baada kuambiwa vile akasema
“thamani ya Amina kwangu ilikuwa kubwa sana sasa basi
Kama hutaki kumtoa yule mpangaji ndani ya kile chumba subiri na uwone”
Hafidhi akaondoka zake akimuacha mama mkwe wake akiduwaa tu.
“huyu kijana mwehu nini naona anataka kunipanda kichwani hanijui ehee haya tutaona.
Taqawa siku hiyo alikuwa anafua nguo zake watoto wa mama mwenye nyumba kina
Asha-Aisha- Mpendu washaanza shobo za kumshobokea kidume
“hendsome mambo vipi?”
Alikuwa Aisha kwa sauti ya kichokozi akatoa salamu.
“ahaa powa tu sister niambie”
“nikwambie nini tena nawe mmbea nakuona unafua mwenyewe”….
“ha!ha!ha!ha!
Nani mmbea tena?
“si wewe hapo nakuona unafua mwenyewe kwani wifi yuko wapi?”
“ahaa wifi yako atokee wapi usawa wenyewe huu pangu pakavu tia mchuzi,
Yani tutabanana hapahapa ukijikuna unanuka kwapa!”

“ha!ha!ha!ha!
Una maneno wee mkaka unaonaje nikufulie, wakati huo bibiye ameshainama na kuishika nguo moja wapo na kuanza kuifua.

“hapana sister usifanye hivyo nitafua tu mwenyewe”
Sema bibiye akang’ang’nia kufua basi akamuachia kisha
Taqawa akaingia chumbani kwake
Huku nnje ghafla beseni likapigwa teke nguo na mimaji kule,
Aisha akapiga kelele
“jamani nakufaa!!! Taqawa akatoka ndani faster na kukuta kikundi cha watu kama nane hivi wameshika dhana mwenye nondo mwenye panga,
Aisha asikimbilie chumbani mchezo
“vizuri sana wewe bwege umetoka mwenyewe kwa taarifa yako
Itabidi uchaguwe vitu viwili tu
Uhame au tukuuwe jibu faster”…
Taqawa akacheka kwa dharau na kusema
“hahahaha nanyie jichagulieni vitu viwili niwachape au muwe wake zangu?”
Masela baada na wao kuulizwa hivyo wakaona usitutanie wee nyau mmoja kati yao akaenda mbio kwa nia ya kumpiga nondo ya kichwa kitendo cha kukaribia tu akajikuta akipigwa teke na kurushwa kule
Ukawa mwendo wa mateke yani
Taqawa alikuwa yuko fiti kwenye kupiga mateke ya hatali
“ndio baby wapige hao watoto wa mama tu!!!
Yani Aisha akashangilia mpaka aita baby ni kauli iliyomchefua Mpendu kwani yeye mwenyewe anamuwinda Taqawa.
Na vile anaonekana mkali wa mapigo mbona balaa, haikuchukuwa dakika nyingi
Vijana nane kwa mtu mmoja wako chali
“bila shaka huyu atakuwa Eddy ndio kawatuma hawa”
Mama mwenye nyumba akasema hivyo.
Taqawa akauliza
“huyo Eddy ndio nani na kwanini kawatuma hawa vijana?”

“Eddy alikuwa mpenzi wa mwanangu ambae kwa sasa ni marehemu amefariki kwa ajali ya gari baada kugongwa huyo
Eddy hakutaka hiki chumba nikipangishe ndio akaniapia kufanya kitu.
Nahisi ndio hiki”
Yani mama mwenye nyumba kwa umbea akaongea hivyo,
“kwasasa yuko wapi huyo Eddy?”
“mi sijui labda uwaulize hao kuku wake,
Taqawa akashika mmoja sikio akafanya kumfinya na kumuuliza
“huyo aliewatuma yuko wapi?”
Kijana yule kwa sauti ya kubabaika akataja
“yuko kulee kwa fundi viatu”
“haya ongoza njia unipeleke,
Safari ya kwenda kumfata Hafidhi ikaanza.
Assss,,,,,,ahaaaaaa,,,,,uwiiiiiiiii,,,,
Ammmmmmm
Ilikuwa sauti ya raha utamu baina ya
Salma na kijana Kessy yani ana wiki tu tokea ahamie ndani ya nyumba hiyo
Ameshachukuwa demu,

ITAENDELEA

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : MTAA WA TATU SEHEMU YA 09
MTAA WA TATU SEHEMU YA 09
BongoLife
https://www.bongolives.com/2018/12/mtaa-wa-tatu-sehemu-ya-08_17.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2018/12/mtaa-wa-tatu-sehemu-ya-08_17.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy