MTAA WA TATU SEHEMU YA 03

*MTAA WA TATU EP 03*


Kwanza kwake aliona kama ni ndoto hakuweza kuamini kabisa kama
Baba yake kipenzi kapoteza maisha
akakumbuka tukio zima la janaake usiku
kisha akazidi kulia na kusema
“hapana baba yangu hajafa mnamsingizia tu,
hii si kweli kabisa ni ndoto tu”
Kwa kifupi alidata ghafla akadondoka chini na kupoteza fahamu.
Ni msiba uliovuta hisia za watu wengi sana hasa kwa watu masikini
wasiojiweza
walijazana vilio vyao vikasikika kila kona
“hiiiiiiiiiihaaaa mkombozi wetu
umeondoka na kutuacha peke yetu ni nani wa kutusaidia baba
Yahaaaaaaaaa!!!
Hafidhi nae hakuwa mbali kwenye msiba huo ni mmoja kati ya watu waliokuja kutoka Keko
bwana Khatibu ambaye ndio
Baba yake Habiba alitoa gari zake kama nne aina ya Coaster ziwapeleke
Wakazi wa maeneo hayo kwenye msiba wa rafiki yake kipenzi
Hafidhi akaitumia nafasi hiyo kwenda.
“Mke wangu kipenzi mbona
Habiba sijamuona hapa nyumbani yapata wiki sasa, yuko wapi?”

“ehee tena imekuwa vizuri kumuulizia huyo mbwa wako, kwa kifupi tu kachoka
kulinda hapa kisa tunamlisha machicha
Matokeo yake kaenda kulinda kule kwa mama
Asia”
“unasemaje wee mwanamke inamaana
Habiba aishi hapa tena?”

“ndio maana yake”
“ok! wacha nikamfate mbwa wangu huyo mama atanitambuwa
tunataka kwenda msibani hakuna mbwa wa kulinda nyumba”….
bwana Khatibu akatoka njia nzima akitukana
kitendo cha kufika tu, akamkuta
Habiba anachambua mchele akaupiga teke ungo wenyewe kule mchele ukamwagika
Habiba akapiga kelele
“yalaaa!!! uwiiiiiii, nisaidieni
mama Asia akatoka ndani mbiombio na kumkuta
Habiba akipigwa mateke ngumi zilituwa kila maeneo”….
Akashindwa kufanya chochote baada kumuona yule ni baba yake.
Akarudi ndani na kuchukuwa simu ampigie
Hafidhi si kaenda msibani.
Simu ikawa haipatikani dahaa akatoka tena nnje na kukuta
Habiba kabebwa, akabaki kulia tu
na kurudi ndani”
siku hiyo Habiba alijuta kuzaliwa kwani alipigwa vibaya sana
mdomo ukapasuka damu zilimtoka huwezi kuamini kama anaye fanya yote hayo ni
Baba yake mzazi.
Salome akapaza sauti kwa kusema
“baba muache inatosha utampigaje hivyo kama mnyama, tambua nae ni binaadamu
anaumia”
Ni kauli iliyowashangaza familia nzima
hata Habiba mwenyewe akashangaa.

Maana katika watu waliokuwa wakishabikia pindi akipigwa Salome alikuwa number moja,
Kingine ashawai kumpiga na chupa ya chai kichwani.
Chai ya moto ikamuishia mwilini, kwa kifupi
Salome hakuwa na huruma hata kidogo, iweje leo
Awe hivi

“Wife imekuwaje mbona Salome leo kawa hivi?”

“mmh mi mwenyewe nashangaa yani Salome huyu mwanangu leo hii kamtetea huyu mbwa”
Baada Salome kusema vile akaingia chumbani kwake huku akilia hakika alitokea kuingiwa na huruma sana.
Siku zote mtu anaweza kubadilika ghafla
mtu mbaya akawa mtu mwema.
Akaichukuwa simu yake na kukumbuka tukio la jana yake usiku
“Salome hakika wewe ni binti mzuri sana tena sana.
Lakini uzuri wako unautumia vibaya, yani roho yako haifananii kabisa”…

“kwanini unasema hivyo my baby Chanduka?”
Hafidhi kama anavyojiita eti Chanduka akaendelea kumwambia
“nasikia una roho ya kinyama sana juu ya mtoto wa baba yako wa kambo.
Salome please nisikilize kwa umakini sana tambua kitu kimoja kile usichopenda kufanyiwa basi na wewe usimfanyie mwenzako. Hivi unapenda kupigwa au kuteswa kunyimwa chakula?”

“hapana baby sipendi kufanyiwa hivyo hata siku moja”….

“ok! kama hupendi hata Habiba hapendi anaumia kusema tu anashindwa hata akisema hakuna wa kumsikiliza, anabaki kuwa mnyonge kilio chake
Mungu pekee anakisikia.
Salome”….

“abee baby”
“je unanipenda?”
“ndio nakupenda japokuwa tumekutana ndani ya usiku huu nimetokea kukuamini kwa kila kitu, yani umenibadilisha kwa kiasi kikubwa nakuapia
Wallah tena kuanzia dakika hii nitakuwa mtu mwema”
Aliongea hivyo Salome akiwa kajiegemeza kifuani kwa Hafidhi
“baby nikuombe kitu je unaweza kunifanyia ndani ya usiku huu?”

“baby mi niko tayari kwa lolote bwana embu niambie kitu gani hicho? Au unataka nikalale kwako mpaka asubuhi?”
“hapana baby sio hicho nataka uwende ndani ya chunba chenu kuna picha sijui katokea Buraki yani kichwa cha mtu mwili wake wa farasi.
Naomba ukaniletee hiyo picha”…..
Salome akanyanyuka na kutoka mbio kuifata hiyo picha.
Akashtuka kutoka kwenye dimbwi la mawazo akajifuta machozi na kubofya simu yake.
Akaweka sioni kusikilizia simu ikawa inaita……..”
Na kupokelewa
Sauti ya Hafidhi ikasikika japokuwa sauti ya vilio nayo ikasikika
“halloo my dear my love my sweat mambo vipi niambie”…..
Salome akaangua kilio na kicheko
“hiiiiiiiiihaaa, hahahaha,
Hafidhi akabaki kushangaa na kuuliza
“vipi Salome huko sawa kweli?”

“Chanduka kipenzi changu nacheka kwa furaha kwa kuniita majina matamu kama hayo.
Nalia kwa hudhuni baada Habiba kukamatwa na kupigwa vibaya mno kabla hajaongea zaidi simu ikakatwa akaishia kusema
Halloo…..halloo
hakufahamu kama
Kutanuka dakika si nyingi kidume kitafika hapo.

Hafidhi baada kupigiwa simu na kuambiwa
Habiba kapigwa akajihisi kama vile kutoneshwa kidonda,
akamwita dereva bodaboda na kuongea nae kisha akapanda na kuondoka.
“sikia wewe mbwa siku ukitoroka tena
nitakata miguu yako mtoto
wa malaya wewe”

“kila muda najiuliza nilipi kosa langu ewe baba yangu, mara nyingi najiuliza hivi wewe ndio yule baba
uliyemkimbiza mzee Mkwanga na panga kisa alinichapa mimi, ni wewe
kweli ulikuwa ukimgombeza mama na kumwambia asithubutu kunitia hata singi.
Baba yangu ni kipi kimekubadilisha
leo hii unanichukia hivi
Kabla ya kuongea zaidi akapigwa teke la mdomo na yule mama
tena kavaa sukuna basi damu tu ajabu
Habiba akacheka na kusema
“ha!ha!ha! Baba hii ndio damu yako leo hii inamwagika mbele ya macho yako.
Umekaa tu”
“wee mwanamke embu kaletu pasi
tumfunge mdomo huyu mbwa yani kazidi kunichefua”,,
Yule mama akaenda mbiombio chumbani na kutoka na pasi ikachomekwa kwenye umeme
Kisha akaambiwa
“mshike hicho kichwa kisha upanuwe huo mdomo wake Salome akatoka chumbani kwa kasi ya ajabu akaenda kuibeba ile pasi na kukimbia nayo chumbani kwake,
Mama yake akamuacha
Habiba na kumkimbilia
“wee Salome embu lete hiyo pasi wee mtoto mbona umekuwa hivi”…


ITAENDELEA......

Comments

Use [video]youtube-video-link[/video] to insert video in comment
Use [img]image-link[/img] to insert image in comment