MOYO USINIDANGANYE SEHEMU YA 03

MOYO USINIDANGANYE

NO :03

Marafiki wawili walifurahiana, wakipiga gumzo za hapa na pale, huku kwa namna fulani wakijaribu kutufanya mimi na yule mchumba wa jamaa tusijisikie wapweke. Kiukweli akili haikuwa hapo. Kila wakati nilimtupia Latiffa jicho la wizi, huku nikitamani azungumze. Kuna wakati alizungumza kidogo, basi nikamuitikia kwa shamra mpaka nikajistukia. Tuliendeleza zogo kwa muda, lakini nilijihisi nahitaji kwenda kupata pumzi, nikainuka kwenda uani. Yaani muda wote niliokaa pale mezani nilihisi hewa hainitoshi. Nilikuwa na hisia mchanganyiko, furaha ya kumuona mrembo wangu kwa mara ya pili, ambaye sikutegemea, lakini pia sikuwa na namna ya kumuiba mrembo huyo kwa jamaa hivyo niliishia kujisikitikia. Niliinuka na kwenda uani, nikajiangalia kwenye kioo, huku nikijiambia,”Ni sawa tuu Hammy, sio wako. Inatosha kumuona kwa mara nyingine na walau kukaa naye meza moja”.
Nilirudi, na haikuchukua muda tukaondoka. Kesho yake nilisafiri, nikimuwaza Lattifa akilini, lakini walau nilifanikiwa kumuona kwa mara nyingine, kujua jina lake na zaidi kujua anafanya wapi kazi. Akilini mwangu hakuondoka kuanzia wakati huo, japo nilijilazimisha kumtoa. Sijawahi kupenda hivi, wala kuhisi kama naweza kumpenda mwanamke ghafla kiasi hiki. Latiffa aliingia akilini mwangu, aliingia moyoni mwangu, alichukua nafasi ndani yangu kiasi ambacho sikutegemea. Sauti ya maneno machache aliyoongea usiku ule ilijirudia kichwani mwangu kana kwamba yalinihusu mimi. Sura yake haikuniacha akilini hata dakika moja. Hisia hizo zilinipa raha kiasi, kwani niliiruhusu akili yangu imuwaze, iwaze uzuri wake na kila kizuri kumuhusu yeye. Lakini wakati huo huo zilinipa mawazo, na huzuni pia kwani ni kama nilijaribu kujenga ghorofa hewani. Nilifarijika kwa kumuwaza tuu, hivyo safari nzima nilimuwaza binti huyu aliyeuteka moyo wangu kwa kasi

Maisha yaliendelea kwa miezi kadhaa, nikaendelea na biashara zangu. Kila nilipowasiliana na Obey nilimuuliza kuhusu rafiki yake. Sikutaka kumwambia kuwa Lattifa ndiye binti aliyenipagawisha siku ile kariakoo kwani Obey hata hakukumbuka ile sura. Nilijaribu kuulizia habari zake za kuoa, huku nikimdodosa kujua kama anamaanisha kumuoa Latiffa, japo sikutaka kudodosa sana kwani Obey angenistukia. Haikupita muda mrefu, nilitafuta tena safari ya Dar es Salaam, kama kawaida nikaenda kwa Obey ambaye hata baada ya kuoa hakuwa ananiruhusu nifikie hotelini. Siku moja usiku, mkewe akiwa amelala nasi tuko sebuleni kuzungumza kidogo, niliuliza tena habari za jamaa na kama ana nia kweli ya kuoa. Alistuka kidogo, akaniuliza kwanini nafatilia sana habari za huyo jamaa yake. Sikumwambia, lakini nilikazana kuuliza, akaniambia, “Jamaa si muoaji. Labda kama amebadilika sasa hivi, lakini kipindi chote namfahamu huwa, kila binti anayenitambulisha ni kama atamuoa mwezi ujao, lakini ukikutana naye wakati mwingine unamkuta na msichana mwingine”. Kwangu hiyo ilikuwa habari njema sana, hakujua tuu.
Niliacha kuuliza habari hizo tena kwa muda, lakini nikaamua kufanya jitihada zangu binafsi kumtafuta Lattifa. Kipindi hicho nilikaa Dar kama mwezi mzima, kiasi cha Obey kushangaa imekuaje, lakini sikumwambia nini hasa kimenikalisha. Kwa asili, sipendi kuonesha udhaifu wangu juu ya wanawake, hivyo japo Obey ni rafiki yangu wa ndani sana, sikutaka kumuonesha kiasi gani Lattifa aliiteka akili na moyo wangu, hasa kwa kuwa bado hakukuwa na mwanga wowote wa kumpata.
Endelea kufatilia.

COMMENTS

BLOGGER

[HOT NEWS]$type=blogging$count=4$source=random-posts

Jina

Afya Yako,101,AJIRA/JOBS,8,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,11,biashara mtandaoni,1,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),7,CHOICE OF MY HEART,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,131,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,96,FIFA.com - Latest News,4,Hadithi,72,HALIMA,2,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,Love Story,12,Mada,2,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,2,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,197,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,2,MUUZA MAZIWA,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,35,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,156,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,12,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
Bongo Life : MOYO USINIDANGANYE SEHEMU YA 03
MOYO USINIDANGANYE SEHEMU YA 03
Bongo Life
https://www.bongolives.com/2018/12/moyo-usinidanganye-sehemu-ya-03.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2018/12/moyo-usinidanganye-sehemu-ya-03.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy