MOYO USINIDANGANYE SEHEMU YA 01 | BongoLife

$hide=mobile

MOYO USINIDANGANYE SEHEMU YA 01

MOYO USINIDANGANYE

NO :01

Mara yangu ya kwanza kuja Dar es Salaam, rafiki yangu Obey alinizungusha kariakoo. Zanzibar pamechangamka lakini mji huu ni hatari. Kuna kila aina ya bidhaa, na nyingi hupatikana kwa bei rahisi kuliko Zanzibar, hasa za madukani. Tulipita sehemu moja, kununua nguo za ndani maarufu kama boxer, mtaa wa DDC. Niliona boxer nzuri zilizouzwa kwa bei nafuu, nikachanganyikiwa kidogo lakini Obey akanipeleka duka ambalo alidai ni mteja hapo. Nilitegemea angemchangamkia muuzaji, ama kuonesha anamfahamu, lakini ilikuwa tofauti. Walisalimiana kama watu wasiojuana kabisa, huku mimi nikiwa nimetoa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango.

Nilishindwa kujizuia kumkodolea yule dada muuzaji, kiasi cha yeye mwenyewe kujistukia, hivyo akanitazama na kutabasamu, na kunipa salamu ambayo kwa mara ya kwanza ni kama sikuisikia japo niliisikia. Mara ya pili akanistua tena kwa kuniita, “Kaka, habari yako?”. “Oh, nzuri, za kwako mrembo?”, nilijibu kwa aibu.
Obey alimuulizia mwenye duka, nikaelewa kumbe yule mrembo hakuwa mwenye duka au muuzaji wa awali.”Ametoka kidogo, ameenda kuniulizia boxer fulani kwa rafiki yake, hapa zimeisha. Lakini naweza kuwauzia chochote mnachohitaji, hakuna shida, pia kama hamniamini, jirani yake huyo anamlindia”. Alizungumza huku akionesha tabasamu mahiri. Hakujua muonekano wake usingefanya mtu yeyote kutomuamini. Kusikia hayo maelezo, moyo wangu ulisononeka kidogo, kwani maelezo yake yalionesha aidha ameolewa ama yuko kwenye mahusiano imara. Baada ya muda mfupi, alikuja muuzaji, aliyezoeana vizuri na Obey, akampa yule dada mzigo wake, kisha binti akaondoka.

Tulinunua tulichohitaji kununua, tukaondoka, akilini nikiwa na mawazo utadhani nimepoteza hela. Obey alianza kunicheka, jinsi nilivyomshangaa yule binti ambaye kwa bahati mbaya hata jina au namba ya simu yake sikufanikiwa kuuliza. Obey ananijua kuwa mimi si kijana ninayezuzuka na mabinti, na nina misimamo yangu fulani kuhusu mahusiano. Hata kwangu pia ilikuwa ni ajabu kuvutiwa na msichana kiasi kile, kwa mara ya kwanza tuu namuona. Miezi miwili iliyopita tuliachana na aliyekuwa mpenzi, bila sababu ya msingi naweza sema, kwani chanzo cha kukosana kilikuwa kidogo sana, kikapelekea kukorofishana mpaka kuachana. Nadhani ni kama nilimsukuma aliyechuchumaa, kwani kabla ya hapo viliwahi kutokea visa kadhaa kuniashiria kuwa Fatmah, mpenzi wangu huyo, hakuwa ananipenda tena. Hata hivyo si lengo langu kuelezea sana uhusiano wangu uliopita.
Nilirudi Zanzibar, wiki mbili baadaye. Nikaendelea na biashara zangu za kusambaza bidhaa za kula kwenye maduka na supamaketi mbalimbali pale Zanzibar. Huwezi amini, akili yangu ilishindwa kupuuza sura ya mrembo niliyekutana naye kariakoo, kwa muda wa miezi kadhaa. Siku ile nilipomtazama kwa kuduwaa, niliona uzuri wa ajabu kwa binti yule. Rangi yake ni ya kahawia, si nyeusi lakini si mweupe pia. Ngozi laini kama ya mtoto, yani utadhani hajawahi hata kung’atwa na mtu. Alipotabasamu meno yake meupe sana yalionekana, na kama pengo dogo upande wa kushoto wa kinywa chake pia nililiona kwa mbali nalo liliongeza mvuto. Zaidi ya hayo, mrembo huyu aliongezewa kionjo cha dimpoz katika uumbaji wake, mashalaah, Mungu fundi jamani! Macho yake meupe, makubwa kiasi, niliwaza akilini mwangu, akiwa ndio yuko mikononi mwangu ananitazama kwa mahaba itakuaje? Sitaki kuongelea umbo lake kwani sikupata fursa kulitazama kwa ufasaha, lakini kwa sekunde chache nilizomtizama akiondoka pale dukani, naweza sema ile ni namba sita ndefu, nadhani unanielewa.

Kwa jinsi alivyoiteka akili yangu, haikuwa ajabu kumuota mara kadhaa. Niliota nimekutana naye tena, na mara hii nikamuomba namba yake. Lakini mara ya pili niliota niko naye eneo zuri, kama wapenzi, huku tukifurahia kila mmoja wetu hiyo fursa. Asubuhi kuamka, Kumbe! Ni mawazo na hisia zangu hunipeleka mahala ambapo hakuna matumaini ya kufika. Kumuwaza yule mrembo mara zote kulinisaidia kumsahau kabisa Fatma, kwani mpaka wakati huo nilikuwa nikijaribu kumbembeleza kwa simu turudiane, huku nikiambulia vichambo na matusi. Basi maisha yaliendelea hivyo, kwa miezi kadhaa, nikamkatia tamaa Fatmah kabisa, nikawa mpole, nikifarijiwa na hisia zangu hewa za binti mrembo, ambaye hakuna matumaini hata tone ya kumuona tena.
Usikose SEHEMU YA 2


COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,Afya Yako,137,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,155,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,107,FIFA.com - Latest News,8,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,202,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,38,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,160,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : MOYO USINIDANGANYE SEHEMU YA 01
MOYO USINIDANGANYE SEHEMU YA 01
BongoLife
https://www.bongolives.com/2018/12/moyo-usinidanganye-sehemu-ya-01.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2018/12/moyo-usinidanganye-sehemu-ya-01.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy