KISA  CHA MAFUNZO

NI KISA  CHA MAFUNZO

Mfugaji mmoja alikuwa anafuga farasi na kondoo, alimtumia farasi kwa usafiri wake.
 Siku moja farasi wake aliugua akaamua kumtafuta daktari wa mifugo amtibu haraka. Daktari wa mifugo akajaribu kumpatia dawa, akamwambia mfugaji kuwa ile dawa lazima iwe imemtibu farasi ndani ya siku 5 na kama zitafikia siku 5 hajapona basi itabidi achinjwe maana ni ishara tosha kuwa hatapona tena sababu ya mashambulizi makubwa ya bakteria. Daktari Akaondoka kwa ahadi ya kurudi tena kuangalia maendeleo ya farasi.

 Kondoo alikuwa pembeni akisikiliza kwa makini mazungumzo yao.
 Siku ya pili ilipofika, kondoo akamfuata farasi akamwambia "jitie nguvu rafiki yangu amka kama sivyo watakuchinja."
Lakini farasi hakuwa na nguvu, alishindwa kabisa kuamka.
Ikafika siku ya tatu, kondoo akarudia tena kumwambia : "Amka rafiki. yangu, sitaki kuona unachinjwa, jikaze na mimi nitakusaidia kukushika usianguke, haya twende! Moja mbili tatu….." Jitihada za kondoo zikawa bure maana farasi hakuweza hata kusogea.

Ilipofika siku ya nne daktari akaja kumuangalia tena farasi, akasema kwa bahati mbaya bakteria wamekomaa sana hivyo uwezekano wa farasi kupona haupo, itabidi kesho farasi achinjwe.
 Mfugaji akakubali akaanda vifaa vyote vya machinjio. Kondoo akaumia sana kujua kuwa kesho ndio siku ya mwisho ya rafiki yake farasi, akadhamiria kumsaidia kwa gharama yoyote ile ili asichinjwe.
 Ilipofika asubuhi ya siku maalumu kondoo akamfuata farasi kwa huzuni akasema: "sikiliza rafiki yangu, wakati wa kujaribu ni sasa au hutakaa ujaribu kamwe maana hutakuwa na nafasi nyingine ukishachinjwa.

 Akaanza kumtia moyo kwa maneno ya matumaini "Amka, simama, kaza miguu, Kuwa na ujasiri, polepole tembea, tembea rafiki, Haya njoo, moja , mbili, tatu... Good, vizuri. Sasa kwa kasi tembea..tembea.. endelea kutembea ..." Kondoo akazidi kumtia moyo farasi, " Haya kimbia, kimbia zaidi! Ndiyo! Yeah! Ndiyo! Unaweza, wewe ni bingwa!!!!!"... Kondoo akazidi kumtia moyo farasi, Kwa mbinu alizompa na maneno yale ya kutia moyo ya kondoo yule farasi akapata nguvu akaanza kukimbia.

Ghafla mfugaji akatokea, akamwona farasi wake anapiga mbio uwanjani huku pembeni yupo kondoo, mfugaji akafurahi sana kupita kiasi, akaanza kupiga kelele: "Jamani njooni muone muujiza! farasi wangu kapona. Anakimbia jamani!!, alikuwa hawezi hata kusimama, njooni muone Leo anakimbia! Lazima nifanye sherehe kubwa! haraka sana mchinjeni kondoo tule tusherekee!!! Watu wote njoonii!!!!!"..Majirani wakajumuika kushiriki furaha ya mwenzao, kondoo akakamatwa akachinjwa, sherehe kubwa ikafanyika.... Huo ukawa mwisho wa kondoo. Maskini Kondoo!!

FUNDISHO:
Kuna watu huchangia sana mafanikio ya watu wengine, lakini mwisho wa siku hawa watu hawatambuliki wala mchango wao huwa hauonekani katika jamii. Sifa na pongezi zinamuendea mtu mwingine bila kujua kuwa kuna mtu nyuma ya pazia aliumia na kutumia gharama nyingi katika kumsapoti huyu anayeoneka leo kuwa amefanikiwa.

Inauma sana tena sana, lakini hiyo ndiyo hali halisi tangu zamani.

YA ILAHI TUJaalie.

COMMENTS

BLOGGER

[HOT NEWS]$type=blogging$count=4$source=random-posts

Jina

Afya Yako,101,AJIRA/JOBS,8,ASIA DIGITAL,2,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,Biashara,10,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),7,CHOICE OF MY HEART,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,131,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,96,FIFA.com - Latest News,4,Hadithi,72,HALIMA,2,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,18,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),10,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,Love Story,12,Mada,2,Mada ya Leo,6,Mahusiano,126,Makala,10,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,197,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,2,MUUZA MAZIWA,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,35,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,156,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,12,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,1,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
Bongo Life : KISA  CHA MAFUNZO
KISA  CHA MAFUNZO
Bongo Life
https://www.bongolives.com/2018/12/kisa-cha-mafunzo.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2018/12/kisa-cha-mafunzo.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy