BIKRA YANGU HAKI YA BABU SEHEMU YA 26

___BIKRA YANGU HAKI YA BABU___
                    (Love Story......... Part 26.)

"MTUNZI:Geofrey Mustafa,©Jafa: mkali mpya"
                  (WhatsApp: 0713024247)
©Jafa
TULIPOISHIA....⏪⏪
Basi wakiwa bado wanapiga story za hapa na pale mala Shangazi ikasikika ikiita:
Shangazi; "Rechoooo jamani jali muda wewe..!"
Recho; "Sawa Shangazi dakika moja tu"
Baada yakumaliza kupiga story zao Recho akamkumbatia Ndundame kisha akampa ulimi kidogo alafu akamwambia:
Recho; "Huwezi amini nakupenda Sana Ndundame tena Sana, una sura nzuri alafu ni mpole na unaye jituma kwa kila jambo"
Ndundame; "Asante Sana nami nakupenda pia ila Ndio ivyo wewe tayari ni mali ya mtu, ila usijali kuna mpango naufuatilia ukikamilika nitakuja kwa usafiri wangu kisha nitakuchukua."
Recho; "Niambie mpango gani uo Jamani Ndundame, inamaana na wewe una usafiri wako hee kumbe una gari...!!??"
Ndundame; "Usijali nitakwambia nikisha fanikiwa wala usijali, saizi mapema Sana.!
Basi jamaa alipogoma kusema huku Shangazi naye kakazana kumwita Recho mpaka akawaambia wale vijana wawa luhusu punda waondoke maana muda ulikuwa umeisha.
Yeye Recho alipo hana habari na kelele za shangazi yake, alikuwa Ndio kwanza kambania pua yule Ndundame akimbembeleza amwambie uo mpango anao usubiri:
Recho; "Niambie  bwana nakuomba Jamani"
Ndundame; "Nakwambia ila naomba iwe siri yako tafadhali usiseme ovyo, ni kwamba mizimu ya ukoo imenichagua Mimi kuwa mmiliki wa shughuli zote za ukoo wenu, na babu yako atakuwa Kama mshauri tu..!"
Recho; "Haa! Jamani unakabidhiwa kiti lini..?"
Ndundame; "Bado mpaka ilizi yangu ikamilike pamoja na usafiri wa kwenda kwenye vikao sehemu mbali mbali duniani, usijali kila kitu kitakuwa Sawa tu Ndio maana ata mzee alipo nipa ile adhabu yake Mimi sikuwa na wasiwasi wowote niliona anapoteza muda wake tu.
"Weeeee Recho sisi tunaenda utakuja Kwa miguu, maana naona uoni jua lilipo"
Alikuwa Shangazi yake awamu hii aliongea Kwa hasira huku akiwaambia vijana waondoe mkokoteni wasijali wala nini.
Basi wale vijana wakawapiga fimbo punda kisha punda wakaanza kuondoka taratibu..!
Basi Recho kwa woga akaanza kumwambia Ndundame watafanyaje maana ndio ivyo mkokoteni unamuacha..! Ndundame akamwambia asiogope awe na amani tu mkokoteni hauwezi kufika popote pale......!!!
                ENDELEA KUSOMA⏩⏩
Basi taratibu mkokoteni ukawa ukiondoka huku Recho naye akizidi kuonyesha ofu maana palikuwa ni porini Sana, sauti za ndege na nyani Ndio zilikuwa zimetawala pale. Ndundame yeye hakuonyesha wasiwasi wowote kabisa zaidi aliendelea na story za kawaida tu:
Ndundame; "Vipi Recho unaniangusha bwana"
Recho; "Nakuangusha...kivipi?"
Ndundame; "Una wasiwasi sana, inamaana hujiamini kuwa na Mimi hapa"
Recho; "Sio ivo tatizo mkokoteni umeniacha alafu pili Hapa ni porini Sana"
Ndundame; "Usiogope ukitaka unaweza kufika kabla ya Shangazi yako aliye jifanya kukuacha"
Recho; "Mhhh...! Maneno ya kweli ayoo...?"
Basi waliendelea kupiga story za hapa na pale kisha Ndundame akaanza kupiga ngoro kwa kutumia mikono yake, najua wengi hamuwezi kuelewa ila wale waliochunga ng'ombe tutakuwa pamoja kabisa....
Ndundame akaendelea kupiga ngoro kwa sauti huku mashavu yakiwa yametuna misiri ya mimba ya fuko.... Recho akawa anamuangalia huku akitabasamu...kisha akaamua kumuuliza maana ya iyo ngoro porini pale:
Recho; "Jamani Ndundame mbona unapiga kelele wakati tupo katikati ya msitu...?!"
Ndundame; "Weee tulia bibie nikufanyie surprise ya maana mpaka ushangae"
Kisha akaendelea kupiga ngoro yake iliyokuwa ikiimba ivi: "Poliiii poliii polilolilo polii poliloooo"
Hakuacha wala hakupunguza mpaka Recho akaanza kumuona Kama mjinga sasa, maana wakati Ndundame anapiga iyo ngoro yeye Recho macho yalikuwa hayatulii anaangalia kila kona aone kama kuna iyo surprise aliyoambiwa. Alipoona hakuna kinacho endelea akaamua kukaa zake pembeni kidogo chini ya mti wa mkwaju aliona kitu Kama gogo ivi basi akalikalia kisha akawa anamuangalia Ndundame kwa jicho swali zito.
Kwa upande wa Shangazi na wasindikizaji wao safari ilikuwa ikiendelea vizuri tu huku Shangazi akiwasiliana na John nakumsihi amwambie rafiki yake awasubiri hapo mbeya, John hakuwa na neno kesha penda  atafanyaje sasa. Yani kila baada ya dakika kadhaa John anampigia simu Shangazi nakumuuliza safari yenu vipi, mala nko wapi saizi, mala Recho anasemaje.
Wakiwa wameanza kusikia sauti za redio na azana za misikitini ndipo punda wakagoma kwenda wale vijana wakajitahidi kuwa chapa lakini walitulia tu kabisa, kitendo cha wale vijana kushuka juu ya mkokoteni ili wawachape vizuri duuuh..!! Ilikuwa Kama wamewaamsha toka usingizini maana waligeuka wote wawili kwa ghafla mpaka Shangazi akajipigiza kwenye lile bodi la mkokoteni na simu yake kuleee...!!
Basi hawaja kaa sawa waliamsha liadha speed ya Bugatti  yani mkokoteni ulikuwa unakimbia hakuna mfano, Shangazi akainua kichwa ili aone kinacho endelea maana mwendo ulibadilika sana alafu ni ghafla. Basi akatoa kichwa maana alikuwa ndani kabisa ya mkokoteni huku akiwa kafunikwa na tulubai, alipotoa kichwa hakuamini macho yake akashangaa kuona wale punda wanaludi walikotoka akiwaangalia wale vijana hakumuona hata mmoja..! Kwaiyo alibaki peke yake na mkokoteni upo kasi kinyama ata kuluka hawezi, maana kuangalia tu nje upepo ulikuwa mkali mpaka macho yake yalianza kutoa machozi Sio yakulia ila ni kasi ya mkokoteni.
Shangazi akawaza moyoni mwake; "Jamani uyu Babuuu.. Yani ameamua maisha yetu yaishie huku porini kweli... Kweli mchawi sio rafiki"
Kisha akaludisha kichwa ndani ya mkokoteni akatulia kimya huku akiwa ameishiwa pozi kabisa maana hakujua hatima yake.
Basi Shangazi akiwa katulia huku mawazo yake yakiwa mbali Sana ndipo akaona mkokoteni umesimama na sauti za watu zikisikika nje, sasa ile achungulie akashangaa kuona akiwa pale pale alipomuacha Recho na Recho pia alikuwa pale pale yule Ndundame.
Yule Ndundame akawapa wale punda majani Fulani ivi kisha akamwambia Recho sasa unaweza kwenda.. Nakutakia safari njema, mala na wale vijana wakawa wamefika pale huku wakihema sana maana walikuwa wanaukimbizia mkokoteni wao. Basi walipofika tu yule Ndundame akawaambia wale vijana:
Ndundame; "Nyinyi mliona Kama mpo sahihi Sana, mkajifanya mna haraka aya mmefika wapi sasa zaidi mmeludi pale pale"
Vijana; "Twapela, (Tumekosa)"
Ndundame; "Niko na awa punda zaidi ya miaka. Kitano sasa wananijua mpaka jina, acheni kujiamria amria ovyo sawa yameisha."
Baada yakumaliza kuwapa onyo wale vijana akawaluhusu punda kisha punda wakageuka tayari kwa kuanza  liadha upyaaa...mala Recho akaita; "Ndundame.. Ndundame.. Naomba njoo mala moja tu" basi bila kulemba jamaa akajongea karibu na mkokoteni upande wa nyuma basi Recho akafunua tulubai kisha akavua mkufu wake aliopewa na John Kama zawadi siku ile ya ndoa yao, basi yeye leo akampa Ndundame Kijana ambaye Recho ametokea kumpenda ghafla tena kwa upendo wa kweli kabisa.
Wakati yote hayo yakiendelea Shangazi alikuwa hana jipya maana alikuwa katulia Kama kuku aliye lowa vile macho tu Ndio yalikuwa yakigeuka geuka na kopa basi.
Baada ya Recho kumaliza kumvisha ule mkufu wa ghalama ndipo yule Ndundame mwenyewe kwa mdomo wake akawaamulu wale punda kwa lugha ambayo hakuna aliyeitambua:
Ndundame; "Mwani nyame mwani lwahato shimbila pa shivumbi sha lwelo"
Aisee walipomaliza kutamka herufi ya mwisho..Nakwambia ilikuwa mala tatu ya kasi ile ya mwanzo, mkokoteni ulikwa zaidi ya treni ya umeme yani Shangazi na Recho mle ndani ilikuwa patashika kamata shati chanika. Punda wao walikuwa wakiona kikolongo wanakiluka tu, sasa mziki unabaki kwenye bodi pamoja na waliolipanda Ndio kulushwa lushwa balaa..! Mwendo wa dakika kadhaa tu tayari wakaanza kusikia honi za magari na kelele nyingine nyingi za watu wakiwa kwenye pilika pilika zakujenga taifa si unajua ilikuwa asubuhi Sana.
Baada yakufika wakaelekea mpaka stand ya hapo bahati nzuri wakalikuta gari ambalo lilikuwa tayari kuondoka maana abiria walikuwa wengi basi bila kupoteza muda wakajiunga na ilo gari ambalo linapiga luti za lukwa mjini kwa kijijini kwa bei nafuu kabisa.
Saa tano kamili asubuhi walikuwa tayari Lukwa mjini mabus mengi yalikuwa yameondoka, ikabidi Shangazi ampigie simu tena John ili ajue Kama rafiki yake bado anawasubiri pale mbeya..maana usafiri umekuwa mgumu. Lakini ile anataka kuchukua simu tu mala ikafika cost moja amabayo ni private ikiwa na watu wachache sana, kisha kondakta akawa ana tangaza aya wale wa Dar  wale wa dar ya haraka hii hapa twende...wale wa mbeya, Iringa, Moro, mpaka Dar ya haraka hii hapa... Haina foleni hii.
Basi Recho akamwambia Shangazi yake, kuwa bora waende tu na hii gari kuliko kuendelea  kusubiri mpaka John awaambie.
Ndipo wakapanda ile costa ambayo ni private na safari yakuuanga mkoa wa Lukwa ikaanza, saa chache baadaye walikuwa tayari ndani ya jiji la mbeya. Ilikuwa tayari saa 8:25 mchana wakatelemka kwenye ile costa jambo ambalo recho hakulipenda. Basi wakaiacha ile costa ikiendelea na safari wao wakabaki pale mwanjelwa ili wawasiliane na John awaelekeze na kuwakutanisha na rafiki yake aliye kuwa akiwa subiri tangu asubuhi, lakini baada ya Shangazi kujaza vocha nakumpigia John akashangaa kuambiwa namba ya mteja unayempigia haipatikani kwa sasa.
Wakaamua kuingia kwenye moja ya mgahawa uliokuwa pale jilani na stand ya mwanjelwa ili wapate chakula maana ilikuwa saa nane alafu ata chai hawakunywa kule kwa Babu.
Basi wakati wanakula mala simu ya wakabaki ikaita alipoitazama namba ilikuwa ngeni, basi ikabidi apokee tu:
Shangazi; "Halloo habari yako....?"
Simu; "Safi, bila Shaka naongea na shangazi yake Recho, au nimekosea...??"
Shangazi; "Haujakosea babaangu ndio Mimi"
Simu; "Sasa ukwapi Shangazi maana nimesha chelewa Sana, kiasi kwamba siwezi kuwa subiri Kwa kweli mtanisamehe kwa ilo...!!"
Shangazi; "Mbona sisi tumeshafika mbeya muda mlefu Sana, na saizi tupo hapa mwanjelwa tunampigia simu John hapatikani"
Simu; "Aha, basi nakuja sasaivi maana Mimi nilikuwa hapa Iyunga namalizia kubook mizigo yangu ya viazi kwenye treni"
Shangazi; "Sawa, utatukuta kwenye huu mgahawa ulioandikwa Mwafilombe Cafe"
Simu; "Sawa Shangazi, sasaivi ntakuwa hapo"
Baada yakumaliza kuongea na ile simu sasa ata tabasamu likaanza kuonekana usoni mwa Shangazi maana alikuwa tayari kavulungwa, ndani ya ule mgahawa mlikuwa na vijana kadhaa ambao walikuwa busy kumuangalia Recho jinsi alivyokuwa na uzuri wa asili.
Dakika kadhaa baadaye simu ya Shangazi ikaita tena alipoipokea sauti ikamwambia chungulia huku nje, basi akatoka nje, akaiona gari aina Alteza ikiwa bado mpya kabisa..........!!
"SAMAHANI KWA KUCHELEWA KIDOGO, ILA NDIO MAMBO YA UTUNZI YALIVYO"
               .....ITAENDELEA TENA.....
Mtunzi: Geofrey Mustafa, ©Jafa, mkali mpya
          (WhatsApp Group: 0713024247)

COMMENTS

BLOGGER
Jina

Affiliate Marketing,1,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,151,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,203,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,114,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,12,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,208,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,40,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : BIKRA YANGU HAKI YA BABU SEHEMU YA 26
BIKRA YANGU HAKI YA BABU SEHEMU YA 26
BongoLife
https://www.bongolives.com/2018/12/bikra-yangu-haki-ya-babu-sehemu-ya-26.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2018/12/bikra-yangu-haki-ya-babu-sehemu-ya-26.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content