SIFA ZA MJASIRIAMALI

1. ANAPENDA KUJIFUNZA

Hahahahaa hapa ndipo ugonjwa wa watu wengi
ulipo mtu anajiita mjasiriamali lakini muulize kasoma
vitabu vingapi vya ujasiriamali au kahudhuria
semina ngapi za ujasiriamali. Watanzania wengi
tunapenda sana vitu vya urahisi hatupendi
kujifunza kama kweli unataka kuwa mjasiriamali au
ni mjasiriamali lazima uwe na sifa hii upende
kujifunza kutoka kwa watu wengine na uhudhurie
semina au mafunzo mengi ya ujasiriamali la sivyo
utabaki kuwa mfanyabiashara.

2. MBUNIFU

Mjasiriamali yeyote ni mbunifu, ninapozungumzia
ubunifu nina maana je unapata kitu tofauti kila siku
ambacho jamii yako itapendezwa nacho au
umeng'ang'ania aina moja siku zote? lazima kama
mjasiriamali uwe mbunifu kila siku kuhakikisha
unapata njia mpya ambazo zitakufanya upanue
soko lako, au kazi yako ni kuona mwenzako
kafungua boutique na wewe unaenda kufungua
boutique...!!

3.MTU MWENYE KUTAMBUA SEHEMU YA KUPATA
USHAURI

Hapa ndio watu weengi wanafeli kwenye biashara,
anahitaji kuwa mjasiriamali au ni mjasiriamli lakini
anapoenda kuomba ushauri ni kwa mtu ambaye
hata hajui ujasiriamali au kafanya kashindwa we
unafikiri unaenda kumuomba mtu ushauri
aliyeshindwa atakupa jibu gani? atakwambia huwezi
matokeo yake na wewe utashindwa.

4.MTU MWNYE MAHUSIANO NA WATU MBALIMBALI
YA KIBIASHARA

Watu wengi hawaamini katika nguvu ya mtandao
(power of network) kama kweli wewe ni mjasiriamali
lazima uwe na mahusiano mazuri na watu wengi
ya kibiashara lakini ukiangalia wajasiriamali wengi leo
hii hawana mahusiano mazuri na watu wengine
kibiashara hutaweza kukua kibiashara kama
hutaweza jifunza kutoka kwa wangine jifunze
kutoka kwa wengine rafiki na hutaweza jifunza
kama hutakuwa na mahusiano mazuri na watu
wengi kibiashara

5.ANAYEPENDA USHINDANI

Siku zote kama mjasiriamali usipende kukwepa
ushindani shindana ili product yako iwe bora, watu
wengi hushindwa kufanikiwa katika biashara
kwa sababu ya kuogopa ushindani, anashindwa
kufanya biashara fulani kwa sababu washindani
wengi, unapokutana na washindani wengi ndio
unafahamu mapungufu yako na yao ukijirekebisha
unafanya product yako kuwa bora.

6.ASIYEOGOPA KUSHINDWA NA KUKATA TAMAA

Watu wengi hushindwa katika biashara kwa kuogopa
kushindwa anataka kuanzisha kitu lakini cha kwanza
anawaza nikifirisika je watu si watanicheka? acha
mawazo mgando rafiki kama kweli wewe ni
mjasiriamali au unataka kuwa mjasiriamali kamwe
usiogope kushindwa kwani ninasema mjasiriamali
ni mtu ambae yuko tayari kushindwa na kujaribu
tena(risk taker), matajiri wote unaowaona duniani
wamefeli mara nyingi na ndio wakaja kufanikiwa
sasa kama unataka kuwa mjasiriamali usiogope
kushindwa na wala usikate tamaa ukishindwa
unaanza tena na tena na tena hiyo ndio sifa ya
mjasiriamali.

7.MTU ANAYETUMIA MUDA WAKE WA ZIADA
KUFANYA KITU CHA ZIADA

Siku zote mjasiriamali ni mtu ambaye ana uwezo
wa kufanya biashara zaidi ya moja yuko tayari
kutumia muda wake wa ziada kufanya kitu ambacho
japo kimuingizie hata elfu kumi kwa siku mtu
ambaye ana uwezo wa kutumia muda wake wa
ziada kufanya kitu cha ziada huwa anafanikiwa
sana maana huwa hapotezi muda.

Acha kuzubaa rafiki maisha yamebadilika
unatumiaje muda wako wa ziada wakati vipo vitu
ambavyo unaweza fanya na kujiongezea
kipato, usisubiri kesho anza leo kutumia muda wako wa ziada kuingiza kipato cha ziada.

8.ANAYEITUMIA JAMII INAYOMZUNGUKA KUINGIZA
KIPATO

Watu wengi hushindwa kulitambua hili na kujiita
wajasiriamali lakini hawajui jinsi ya kuwatumia watu
wanaowazunguka katika kuingizia kipato, rafiki
unawatumiaje watu ambao mmekutana kwenye
kikao cha harusi, kikao cha kitchen part au kikao
cha familia au kwenye kahawa katika kuitambulisha
biashara yako au unajua kazi kupiga umbea tu na
kulalamika biashara yako haitoki, unategemea
wateja unawapata wapi kama sio hao..!!!

AMKA SASA UFANYE
Naamini umeshajielewa uko wapi sasa
unaweza anza biashara karibu uungane nami kama
unapenda kumiliki biashara yako mwenyewe na
uwe bosi ili uachane na adha za mishahara.

Napatikana kupitia:

0719 696004- whatsapp

COMMENTS

BLOGGER: 2
 1. Zijue sifa za Mjasiriamali

  [img] https://entrepreneurs.or.tz/wp-content/uploads/2016/08/IMAG8597-2-300x168.jpg [/img]

  Nidhamu binafsi – Hakuna mjasiriamali anayependa kuona biashara yake inakufa, kila mmoja analenga kuhakikisha biashara inafanikiwa na huondosha kila jambo linaloweza kuhatarisha ustawi wa biashara husika. Wajasiriamali waliofanikiwa wana nidhamu ya kuchukua hatua kila siku kuelekea kwenye kufanikisha malengo yao. Hakikisha unanidhamu ya kutunza mda na nidhamu ya kutumia pesa zinazopatikana kutokana na biashara yako.

  Kujiamini – Mjasiriamali hupaswi kuwa na wasiwasi kuwa unaweza kufanikiwa au la, unapaswa kujiamini mda wote kuwa utafanikisha biashara yako. Jitahidi kudhihirisha kujiamini huko kwa kufanya kazi kwa bidii ili kifikia malengo uliyojiwekea.

  Muwazi wa fikra – Mjasiriamali anatambua kuwa kila tukio au hali ni fursa ya kibiashara. Mawazo mapya yanaibuliwa kila mara kuhusu mtiririko wa kazi na ufanisi, ujuzi, na biashara mpya. Mjasiriamali ana uwezo wa kutizama kila jambo [hali/ tukio] linalomzunguka na kulitumia kufanikisha lengo lake.

  Muanzilishi – Mjasiriamali anafahamu kuwa kama kuna jambo linalopaswa kufanyika basi yeye mwenyewe ndiye anayepaswa kulianzisha. Hujiwekea vigezo na kuhakikisha biashara inafuata kuelekea kutekeleza/ kukidhi vigezo hivyo. Wako makini katika kutwaa fursa bila kuhitaji kusubiri mtu mwingine awape fursa

  Mshindani – Chanzo cha biashara nyingi ni mjasiriamali mmoja kutambua kuwa anaweza kufanya biashara hiyo kwa ubora kuliko mwingine/ wengine. Wajasiriamali wanahitaji kufanikiwa katika biashara wanazoanzisha mithili ya mchezaji anavyohitaji kushinda katika mchezo anaocheza. Mjasiriamali ni mwepesi kuonesha namna taasisi yake ilivyofanikiwa katika hatua mbalimbali.

  Mbunifu – mojawapo ya mambo muhimu katika ubunifu ni kumudu kuunganisha mambo ambayo hayaonekani kuwa na uhusiano katika kutengeneza fursa. Wajasiriamali huja na suluhisho baada ya kuchambua na kutengeneza uhusiano wa hali/ matukio mbalimbali. Huweza hata kubadili malengo ya bidhaa fulani na kuiuza katika soko tofauti.

  Kutokata tamaa – Wajasiriamali hawakatishwi tamaa na kushindwa. Kila anaposhidwa huichukulia kama fursa ya kujifunza na kufanikiwa. Wanatamani kila wanalofanya lifanikiwe, hivyo hujaribu tena na tena hadi wafanikiwe. Hawaamini kuwa kuna jambo lisilowezekana

  Ujuzi binafsi – Mjasiriamali ana ujuzi mzuri wa kuwasiliana katika kuuza na kuwapa motisha waajiriwa wao. Wajasiriamali wengi waliofanikiwa hufahamu namna ya kuwapa motisha waajiriwa wao hivyo kukuza biashara zao. Ni wazuri katika kuelezea faida za hali mbalimbali na kuwafundisha wengine katika kufanikiwa.

  Mwenye kuheshimu maadili ya kazi yake – Mjasiriamali hufanikiwa kwa kufuata/ kutii kanuni na taratibu zilizowekwa na mamlaka husika. Mifano ya wajasiriamali wasio na maadili ni: Muuzaji wa matunda anayeokota matunda kutoka kwenye shimo la taka kwa ajili ya kuwatengenezea wateja wake sharubati (juisi), au mjasiriamali anayeuza nyama isiyokaguliwa au iliyokatazwa kwa matumizi ya binadamu.

  Mwenye kupenda kazi yake – Kupenda na kuthamini kazi yake ni sifa muhimu kuliko zote anayohitaji mjasiriamali ili kufanikiwa. Mjasiriamali ana mapenzi ya dhati kwa kazi yake. Yuko tayari kufanya kazi saa za ziadakuhakikisha biashara yake inafanikiwa, maana hupata furaha kuona biashara inafanikiwa. Mjasiriamali anayefanikiwa ni yule ambaye hujifunza bila kuchoka na kutafiti namna mbalimbali za kufanya biashara yake iwe bora zaidi.

  Wajasiriamali wanaofanikiwa hutizama biashara zao kama mtu aliye juu ya kilima na kuona biashara yake ilivyo. Akishaiona, anataka kwenda mbali zaidi. Wanafahamu namna ya kuzungumza na waajiriwa wao, na buashara zao hutanuka kwa sababu hiyo.

  JibuFuta
 2. Mteja ni nani?

  Mteja ni mtu au tasisi yoyote ambaye tuna uhusiano naye katika biashara. Si lazima mteja awe ni yule anayenunua bidhaa au huduma kutoka katika biashara yako leo.

  Hata yule mtu anayekuja kuulizia au kutembelea biashara yako ni mteja vilevile.

  Vidokezo vya kujenga uhusiano mwema na wateja.

  Kila mara msalimie mteja na kisha muulize “ Naweza kukusaidia”?

  Kwanza jifunze kuwa msikilizaji mzuri. Sikiliza na kuelewa.

  Kama hujaelewa, uliza ili kukidhi haja ya mteja.

  Kuwa mkarimu kwa wateja wote. Wahudumie kwa tabasamu. Watimizie wanachotaka kwa utaratibu ulio wazi.

  Wahudumie wateja kwa makini.

  Ruhusu wateja wazijaribu bidhaa zako (inapobidi).

  Kubali malalamiko na ujibu kwa uangalifu.

  Zungumza kidogo, onyesha zaidi.

  Uza manufaa, siyo bidhaa pekee.

  Kila mara jaribu kuwa na subira, kwasababu wateja wengine ni wazito kuamua.

  Mambo Yasiyofaa

  Usibishane na mteja

  Usimchanganye mteja kwa maelezo mengi mno.

  Usimuuzie mteja zaidi ya kile anachoweza kutumia

  Usikate tamaa mteja anaposema kwamba bei ni kubwa mno. Badala yake mweleze manufaa atakayopata

  Usimlazimishe mteja kununua, bali mshawishi.

  Usimkatize mteja anapozungumza, yeye ndiye mfalme.

  Usinywe, usivute, wala usile unapokuwa unauza, hivi ni vitendo vinavyoweza kumkera mteja.

  Mambo ambayo huweza kuharibu uhusiano na mteja

  Uso wenye hasira

  Uso unaoonyeha kusononeka au kuchoka.

  Kutojali mteja anapokuja

  Kutoa huduma kwa upendeleo

  Kuonyesha kutokuwa na ujuzi katika utoaji huduma

  Kutoa huduma pole pole sana

  Lugha isiyofaa

  Kukejeli wateja

  Kumdai mteja kitu kilicho nje ya utaratibu ndipo huduma itolewe

  Kutotekeleza ahadi

  Kupokea zawadi kutoka kwa wateja (zenye nia ya kutoa upendeleo)

  Kujenga mahusiano ya kimapenzi na wateja

  Kutowatimizia wateja mahitaji yao

  Kupiga soga wakati wateja wanasubiri

  Kutoa huduma huku umelewa.

  Kushindwa kutoa faraja kwa wateja wakati inapobidi wasubiri huduma.

  JibuFuta
Use [video]youtube-or-vimeo-video-link[/video] to insert video in comment
Use [img]image-link[/img] to insert image in comment

Jina

Affiliate Marketing,1,AFTER DEATH (BAADA YA KIFO),4,Afya Yako,151,AJIRA/JOBS,8,ANGA LA WASHENZI,1,ASIA DIGITAL,2,Baba Kiumbe Wa Ajabu,20,BAKING,1,BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA,7,betting,1,Biashara,12,biashara mtandaoni,2,BIKIRA YANGU,1,BIKRA YANGU HAKI YA BABU,25,BISCUITS,2,BLACK AMERICA,33,BONGO MOVIES,12,Bora ungekufa kesho,1,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),16,CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu),1,CHOMBEZO,56,CHOZI LISILOFUTIKA,1,Chunusi,1,CHUPI MKONONI,4,CITY LIGHT,5,Classified,10,DARASA LA MAHUSIANO/MAPENZI,69,Darasa la mapenzi na ndoa,203,DEREVA TAXI,18,DUDU WASHA,4,Elimu na ushauri wa maisha,114,FIFA.com - Latest News,17,Hadithi,73,HALIMA,2,HOUSE GIRL WA DADA,8,I WILL BE BACK,15,I'M NOT A BOY,1,Jam,1,JAMANI BABA,8,JAMBAZI MTAMU,3,JAMII MEDICAL AWARENESS(JMA),1,JASTINA,7,JIBU,2,JIKONI,1,JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU,5,Jobs,19,Joke,5,Kampuni,2,Kanyago,8,KEKI YA CHAI,1,kibamia,9,KIFO MKONONI (BIKIRA YA BIBI HARUSI),20,Kijijini kwa bibi,19,Kilimo,2,kofia za steaming,2,loans,1,LOVE BITE,10,Love Story,12,Mada,3,Mada ya Leo,7,Mahusiano,126,Makala,12,make money online,3,Mapenzi,2,Mapenzi na ndoa,3,MAPENZI YA KICHAWI,6,mapenzi/Ndoa,115,Mapishi,208,Mfalme Gilbert,4,Micro loans,1,MOYO ULIOJAA MAUMIVU,46,Mpiga Picha,3,MTOTO WA MAAJABU,44,MUME WANGU SHUJAA WANGU,3,MUUZA MAZIWA,10,MWAJUMA UTAMU,11,MWALIMU MKUU,10,MWANACHUO,5,Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ),9,NAITAFUTA FURAHA YANGU,3,NAMTAKA MPENZ WANGU ARUDI,8,Natural hair,4,Ndoa,1,News,40,Ngozi,1,Ngumu Kumeza,11,Nguvu za kiume,2,NILIKUWA NA MPENZI,4,NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA,2,NILIYOYAONA DARFUR YANATISHA,1,NIPE KIDOGO,2,NISAMEE RATIFA,25,Noti Bandia,6,Nyama,1,Nywele,3,ONLY YOU,10,PENZI KABLA YA KIFO,5,PENZI LA MME WA MAMA,3,PENZI LANGU LINAVUJA DAMU,10,PENZI TAMU,6,PENZI ZITO,7,Riwaya,107,Roast,1,ROSTI YA MBUZI,1,SAFARI YA KUZIMU,19,SALA YA SARAH,1,SANGARE,25,Shahiri,1,SIFA ZINAUWA,3,Simulizi,161,SIMULIZI - ULIKUWA WAPI,8,SITO ISAHAU,8,Soup,1,SPHAGETTI BOLOGNESE,1,Sports News,4,SUBIRA HUVUTA HERI,21,Tangazo,4,U KILL ME,3,Ujasiriamali,13,UKURASA WA 56,10,ULIKUWA WAPI,2,ULIMWENGU WA MBWA MWITU,1,UNBREAKABLE LOVE,1,UTAM WA KITUMBUA,2,UTAMU WA JIRAN,1,UTAMU WA MAMDOGO,3,Videos,46,VISA NA MIKASA,2,Young paster,40,YouTube,74,
ltr
item
BongoLife : SIFA ZA MJASIRIAMALI
SIFA ZA MJASIRIAMALI
kujifunza kama kweli unataka kuwa mjasiriamali au ni mjasiriamali lazima uwe na sifa hii upende kujifunza kutoka kwa watu wengine na uhudhurie semina au mafunzo mengi ya ujasiriamali la sivyo utabaki kuwa mfanyabiashara.
BongoLife
https://www.bongolives.com/2018/09/sifa-za-mjasiriamali.html
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/
https://www.bongolives.com/2018/09/sifa-za-mjasiriamali.html
true
170677852813010960
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS PREMIUM CONTENT IS LOCKED STEP 1: Share to a social network STEP 2: Click the link on your social network Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy Table of Content