Iklan Billboard 970x250

NGUMU KUMEZA;(18+) Sehemu ya 04- Muandishi: Jclassic boy (Next level Author)

NGUMU KUMEZA;(18+) Sehemu ya 04- Muandishi: Jclassic boy (Next level Author)

NGUMU KUMEZA;(18+)    Sehemu ya 04:

NGUMU KUMEZA;(18+)    Sehemu ya 04

ILIPOISHIA
“Nini?”
“Ahaaa nimekuletea kitabu”
“Kiweke hapo mezani”
 Mariam alipo yatupa macho yake mezani na kuona
noti za dola mia mia, nikaona kama amepagawa
fulani. Akakiweka kitabu hicho mezani na kubaki
amezikodolea macho noti hizo hadi nikamstua kwa
 kumuongelesha.
“Unashangaa nini?”
“Dany kumbe na wewe unamiliki dola?”
“Ndio kinacho kushangaza”
 “Ndio, kwenye maisha yangu sijawahi kuigusa hii
 pesa zaidi ya kuiona kwa watu au kwenye tv”
“Iguse kisha utoke”
 “Jamani Dany, hunipi hata moja?”
“Nikikupa utanipa nini?”
 Nilimuuliza Mariam kwa utani, kwa maana tangu
nifike kwenye hii nyumba, Mariam ametokea
 kunizoea na mara kadhaa huwa tunataniana sana.

“Mmmmmm nitakupa my pussy”
“Kwenda huko, una ubavu huo?”
 “Aaah Dany unahisi ni utani, nipe uone kama
sikuvulii nguo hapa”
Nikamtazama Mariam kuanzia chini hadi juu, mwili
wake wenye urefu kama futi tano hivi, umeumbwa
kwa mfumo ambao kama ningekuwa ni injinia wa
kuunda magari basi ningeuundia magari, makalio
makubwa na hispi nene zilizo chomoza pembeni, huwa zinampa maksi kubwa sana ya uzuri wake,
ukiachilia rangi ya weupe wa sura yake pamoja na
kifua chake kilicho bebe chuchu ndogo. Kitu
 ambacho kinauzuia uzuri wa Mariam kuonekana ni
matunzo, hali duni ya ufukara ndio inayo mfanya
hadi kuonekana kuwa hivi.

“Mama yako ameenda wapi?”
“Amekwenda kwenye vikoba vyao si unajua leo ni
jumapili”
“Ahaa sawa, chukua noti moja uende saluni sasa
hivi”
 “Kweli Dany”
 “Nitaghairi sasa hivi, chukua moja tu”
 Maria akachukua noti moja kwa haraka kisha
akanikumbatia kwa nguvu na kuanza kunipiga
mabusu mfululizo mashavuni mwangu, busu la
 mwisho lililo nisisimua ni busu la mdomo. Lipsi
zake ndogo kiasi ila zenye unene kiasi,
zilipogusana na zangu, nikajihisi kitu cha tofauti
 sana hadi ndani ya moyo wangu. Ni wanawake
wengi sana ambao ninawabusu ila huku Mariam
 amenipa msisimko ambao umenishangaza kwa
kiasi kikubwa. Mariam akaniachia akataka
kuondoka, ila nikamdaka mkono na kumtazama
kwa macho ya matamanio nikatamani arudie japo
kwa sekunde kadhaa kunipa busu kama hilo.


ENDELEA..
“Nini tena mbona unanizuia? ”
Mariam alizungumza huku akitabasamu,
nikamtazama Mariam usoni mwake, nikazidi
 kugundua mambo mengi sana, hususani wa uzuri
 wake.
 “Aaaha…. hakuna kitu”
 “Haya niachie nikaichenchi kwanza”
“Unajua zinapo chechiwa?”
“Ndio nachukua bodaboda hadi Mlimani City”
 “Ahaaa sawa niletee zawadi basi?”
“Unataka zawadi gani?”
“Yoyote”
 “Yoyote kweli?”
“Ndio”
 “Sawa ngoja niende”
Nikamuachia Mariam, aliye anza kunipagawisha,
akatoka chumbani kwangu na kuufunga mlango.
Nikawasha feni langu na kupanda kitandani. Kila
 nilipo jaribu kuyafumba macho yangu, picha ya
 Mariam ikanijia kichwani na kukumbuka busu alilo
nipatia.

“Huyu mtoto ana nini?”
 Nilijiuliza huku nikijigeuza geuza kitandani kwa
maana sio kawaida ya mimi kuweza kupagawishwa
na busu tu, tena la msichana kama Mariam
 ambaye anaishi maisha ya kawaida tu. Kila nilipo
jaribu kulala sikuweza mwisho nikaamua
kunyanyuka kitandani na kuwasha tv kufwatilia mechi
za mpira zinazo onyeshwa kila mwisho wa wiki.
Masaa yakazidi kwenda na kukatika. Hadi inatimu
 saa tatu kasoro, ndipo nikakumbuka kwamba
sijaweka kitu chochote tumboni mwangu tangu
 nilipo kula na K2 asubuhi. Nikanyanyuka,
nikachukua tisheti yangu kabatini, kabla sijatoka,
mlango wangu ukagongwa.

“Nani?”
Sikujibiwa zaidi ya mtu huyo kugonga mlango
 tena, ikanibidi kupiga hatua hadi mlangoni
 ambapo, nikaufungua kwa tahadhari, nikamkuta
Mariam amesimama huku mkononi ameshika
mfuko mweupe wenye maandishi ya kijani
 ‘NAKUMAAT’
“Tantaraaaaaaa suprizee”
Mariam alizungumza huku akiingia ndani,
nikamtazama jinsi alivyo pendeza, hapo sasa
asilimia za msukumo wa kimapenzi zikazidi
 kupanda moyoni mwangu. Suruali nyeusi aliyo
ivaa, imeyabana makalio yake vizuri na kuzichonga
hispi zake nene kiasi. Kijinguo cha juu alicho kivaa,
kiliyabana maziwa yake yaliyo simama vizuri, huku
 nywele zake alizo ziongezea na vigi lenye rangi ya
 dhahabu zilishuka hadi mgongoni.

“Nimekufanyia shoping ya vitu vya ndani”
 “Wacha wee”
 “Ndioooo. Kwa maana natambua mabachela siku
zote huwa hawanunui vitu, nikifungua friji naweza
nikakuta halina kitu”
 “Wewe umejuaje?”
 “Nimejua tu”
 Mariam akaweka mfuko juu ya meza, akapiga hatua
hadi kwenye kafriji kangu ambako si karefu kwenda
 juu. Akainama na kutazama ni vitu gani ambavyo
 vipo kwenye friji langu. Kitendo cha yeye kuinama
huku makalio yake akiwa ameyaelekezea kwangu,
nikabaki nikiwa nimekodoa macho. Akasimama
huku akiwa ameshika sahani, akaniongelesha ila
 kusema kweli nikabaki nikiwa nimemkodolea tu
 macho wala nisielewe ni kitu gani ambacho
 anakizungumza.

“Dany si nakuongelesha”
 Mariam alizungumza huku akiwa amenishika
mkono, ndipo nikarudisha kumbukumbu zangu na
kumtazama usoni vizuri.
 “Ulikuwa unasemaje?”
“Ahaaa ina maana umesimama hapa na hapa
hujanisikia?”
 “Akili yangu nahisi haikuwa hapa”
“Mmmmm kwa hiyo ilikuwa wapi?”
“Tuachane na hayo, sema ulikuwa unasema…..?”
“Hizi soseji kakupikia nani?”
 “Nimepika mwenyewe”
 “Mbona kama sahani ni ya kwetu hii?”
“Acha utoto unataka kusema kwamba sahani hizo
zipo kwenu tu”
 “Zimefanana”
 Mariam alizungumza huku aking’ata soseji moja,
 akaaiweka sahani mezani, akaanza kupanga vitu
 alivyo leta huku vingi vikiwa ni vinywaji. Alipo maliza
 akalifunga friji na kunigeukia.

“Sasa hiyo ndio zawadi yako”
“Asante”
“Kuna matunda, soda, juisi za kopo, maziwa ya
kopo. Ila niliogopoa kukununulia bia nikajua wewe
si mnywaji”
 “Na kweli mimi sio mywaji. Ila nina njaa nataka
kwenda kununua chakula”
 “Ohoo nilitaka nikujie na piza, ila nikaona uvivu
 kubeba mboksi wake”
 “Haina shida”
 “Basi twende wote”
 “Wapi?”
 “Si huko unapotaka kwenda kununulia chakula”
 “Mama yako yupo?”
 “Bado hajarudi”
 “Poa” Nikazima Tv, tukatoka ndani Mariam akatangulia
nje na mimi nikamalizia kuufunga mlango wangu
 kisha nikaanza kutembea kwenye korido ndefu,
vyumba viwili kabla sijatoka nje kabisa nikasikia
kilio katika chumba cha kushoto kwangu, huku
 sauti ya mwanaume ikigomba sana.
‘Wanagombana nini hawa nao?’
 Nilijisemea kimoyo moyo huku nikipiga hatua mbili
mbele kabla sijafika hata mlango wa kutokea
nikastukia kumuona Asma akitoka mbio ndani
kwake huku akiwa amejifunga kanga moja, akilia
akionekana kukimbia kipigo cha mume wake.

Sija
kaa sawa mume wake naye akatoka kasi akiwa
 ameshika kisu mkononi mwake akielekea uwani
 ambapo ndipo alipo kimbilia Asma.
Bila hata ya kutaka kupoteza muda na mimi
 nikakimbilia uwani kwa kasi nikamkuta Juma
akimfwata Asma kwa hasira haku kisu akiwa
amekinyanyua juu. Kwa haraka nikamuwahi Juma
na kumdaka mkono alio shika kisu.
“Jumaa unataka kufanya nini wewe”
 “Niachie nitamuua huyu malaya”
“Mwanamke hapigwi hivyo Jumaa”
 “Toka hapa na wewe **, ina kuhusu nini?”
“Nashukuru kwa matusi yako ila usifanye hivyo
 Jumaa”
 Nikastukia Juma akinipiga kisukusuku cha kifua
 na kunifanya nimuachie mkono wake alio shika
 kisu, kitendo hicho kikanifanya nikasirike,
nikamuangalia Asma aliye jibanza kwenye ukuta wa
 fensi ya nyumba yetu, asijue ni wapi atakimbulia.

Kwa haraka nikamuwahi tena Juma, mkono wake
ule ule ulio shika kisu. Nikaukunja kwa haraka na
kumgeuza Juma, nikampiga mtama mmoja mkali
 ulio muangusha chini kama zigo la kuni.
Nikavikunja vidole vya viganja vya mkono wake
 ulio shika kisu na kumfanya Juma kutoa ukelele
mkali.
“Utarudia tena kumpiga mkeo?”
Nilimuuliza Juma kwa ukali huku nikizidi
kuvikunja vidole vyake kwa kuvirudisha nyuma.
 Asma na Mariam ambaye sikujua hata ameingia
saa ngapi huku uwani walibaki wakiwa
 wamesimama huku wametukodolea macho. Juma
kwa jeuri hakujibu kitu chochote na kunifanya
 nizidishe kuvikunja vidole vyake, hapo ndipo Juma
 alipo zidi kupiga kelele kwa maumivu makali.

“Simpigi, Simpigi”
 Jumaa alizidi kulalama kwa maumivu.
“Muombe msamaha mke wako”
“Ehee”
Nikazidi kumkunja kiganja chake na kumfanya
 Juma aanze kumuomba msamaha Asma aliye
jikunyata kwa woga.
“Dany msamehe bwana”
 Mariam alizungumza huku akinitazama usoni.
Nikamuachia Juma huku nikimkazia macho
makali. Taratibu Asma akamfwata mume wake na
 kumnyanyua chini nilipo mlaza. Juma akanitazama
na macho makali kisha wakaondoka na mke wake
na kuelekea chumbani mwao.
“Twende zetu”
 Mariam alizungumza, sikumjibu kitu chochote zaidi
ya kutoka nje huku akinifwata kwa nyuma.
 Tukakatiza mitaa miwili na kufika kwenye
kimgahawa kimoja ambacho wanauza vyakula
mbalimbali.

“Agizia unacho hitaji”
“Ndio unazungumza na sauti nzito hivyo, au bado
una mahasira yako?” Mariam alizungumza huku akinitazama usoni
mwangu, nikashusha pumzi na kurudi katika hali
ya kawaida. Akaja muhudumu, akatuuliza
tutatumiua nini.
“Nahitaji nyama choma ya ng’ombe na bia”
“BIA…..!!?”
Mariam aliniuliza kwa mshangao, hadi muhudumu
 akastuka.
 “Ndio kwani vipi?”
 Mariam hakujibu kitu zaidi ya kuagiza kitu
 ambacho ana hitaji. Haikuchukua muda sana
chakula kikaletwa pamoja na vinjwaji.
“Dany kumbe unajua kupigana eheee?”
 “Kwa nini?”
“Nimeona jinsi ulivyo mkaba Juma, yaani yule
kaka kila siku anakazi ya kumpiga mke wake”
 “Hivi chanzo kinakuwa ni nini?”
 “Wivu tu wa ajabu, yaani Jumaa hataki hata mke
wake awe na marafiki wa kike. Ni ndani nayeye”
“Mpuuzi, nikisikia tena nitamlaza ndani”
“Utamlaza ndani?”
“Aahaa tuachane na hayo”

Jinsi Mariam anavyo kula chakula chake, nikawa na kazi ya kumchunguza uzuri wake. Kitu ambacho
hakikuwahi kutokea kwenye maisha yangu ni
kushindwa kumtongoza mwanamke ambaye nina
muhitaji, ila kwa Mariam nikajikuta ninakuwa mzito
 sana kutamka kitu chochote. Kadri muda na masaa
 yanavyo zidi kwenda ndivyo jinsi nilivyo zidi
 kuzigida pombe kushindana na hisia, nikiamini
 kwamba nikiwa nimekunywa sana nina weza
kumtamkia Mariam kwamba nina mpenda.
“Dany inatosha bwana, usinywe tena pombe” “Kwa…kwani hii ni bia ya ngapi?”
“Bia ya tisa”
“Ahaa tisa mbona chache”
 Sauti yangu ilibadilika kabisa na kuwa sauti ya
kilevi.

Mariam akaninyanyua kwenye kiti nilicho
kalia. Nikasimama wima, na kutoa noti za shilingi
elfu kumi zipatano nane na kumkabidhi
muhudumu, sikuhitaji kujua anatudai bei gani kwa
maana kiasi nilicho mpa ni kikubwa kuliko
kiasi ambacho tumetumia eneo hilo.
“Dany tuchukue bajaji” “Bajaji….!! Bajaji ya nini sasa?”
“Umelewa wewe huwezi kutembea njia nzima na
sasa hivi muda umekwenda”
“Kwani sasa hivi ni saa ngapi?”
Mariam akatoa simu yake mfukoni mwa suruali na
kuangalia saa.
“Ahaa saa sita na nusu usiku”
“Sasa unasema usiku kwani sioni giza”
 “Dany acha masihara bwana, tazama hapa
 umesimama tu unayumba yumba”
“Ahaa kwanza sihitaji kurudi nyumbani kwa sasa”
 “Ahaa!!”
 “Unashangaa nini sasa. Mimi sihitaji kurudi
 nyumbani”
 “Sasa unataka kwenda wapi jamani Dany, kumbe
ukilewa unakuwa na vituko kiasi hichi”
“Ahaa achana na mimi nataka kwenda kulala
 kwenye hoteli moja nzuri”
 “Mungu wangu, sasa Dany unataka kwenda hoteli
 gani?”
 “Wewe rudi nyumbani, mimi nakwenda kulala
hotelini”
 “Siwezi kurudi mwenyewe kama vipi nikodishie
bajaji inipeleke nyumbani”
Mariam akaita bajaji moja, akaingia kwenye bajaji
na mimi nikaingia kwenye bajaji.

“Ahaaa wewe si umesema unataka kwenda kulala
hoteli nzuri vipi tena na huku?”
 “Hei dereva tupeleke KC Hoteli”
“Sawa kiongozi”
 “Dany mimi nakwenda nyumbani, nataka nikalale
 mapema kesho nina mtihani asubuhi chuoni”
 “Unataka kulala mapema gani, wakati saa hizi
inakwenda saa saba. Dereva endesha bajaji”
 “Dany kumbe ukilewa upo hivi”
 “Nipoje”
“Mmmm haya, ukifika hotelini dereva ananirudisha
nyumbani”
 Bajaji ikafika katika hoteli niliyo hitaji kufika.
 Nikamlipa kiasi anacho kihitaji. Nikashuka na
 Mariam naye akashuka.
“Unakwenda wapi?”
“Sirudi mwenyewe nyumbani”
 “Rudi wewe, mama yako atakuchapa”
“Ahaa nimekuwa mtu mzima nirudi nisirudi hilo
halimuusu”
 Sikuwa na cha kuzungumza huku moyoni mwagu
 nikiwa na furaha sana kwa maana naona Mariam
 anaingia kwenye kumi na nane zangu.
Nikalipia
chumba kimoja wala Mariam hakuzungumza
 chochote zaidi ya kukaa kimya akaanza kunifwata
kwa nyuma, tukapandisha hadi gorofa ya pili kisha
 tukaingia katika chumba ambacho nimelipia.
 Kitendo cha kufunga mlango kwa funguo,
nikamuwahi Mariam kwa nyuma na kumshika kiuno,
kwa haraka Mariam akakurupuka mikononi
 mwangu na kunigeukia. Akanitandika kofi moja zito
 la shavu huku akiachia msunyo mkali na mzito.
“Mimi sio malaya wa kujirahisisha kwa mwanaume,
na sijakuja hapa unitom**, lala zako kitandani
 mimi nitalala hapa kwenye kochi”
 Mariam alizungumza huku akiwa amekunja sura,
akapiga hatua hadi lilipo sofa akajirusha na kukaa, huku akinikazia macho makali. ITAENDELEA
SIMULIZI HII NI KWA WASOMAJI WENYE UMRI ZAIDI YA MIAKA 18. HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA. USIKOSE SEHEMU YA 05 YA KISA HICHI CHA KUSISIMUA. INAPATIKANA PIA KWENYE GROUP ZA WHATSAPP NA FACEBOOK. 
Related Posts
SHARE
Subscribe to get free updates

Related Posts

Chapisha Maoni

Post Central Advertising